Header Ads

TAMBWE HIZZA 'TAJIRI WA MANENO ' UMEKWENDA


Na Happiness Katabazi

KWA wafuatiliaji wa masuala ya siasa nchini tangu Miaka 1998 ni wazi kabisa masikioni mwao jina la mwanasiasa maarufu nchini,Richard Tambwe Hizza ambaye amefariki Leo asubuhi siyo geni masikioni mwao.

Tambwe Hizza alikuwa ni miongoni mwa Chanzo changu cha Habari muda mrefu Enzi zile za mwishoni mwa Mwaka 1999 hadi 2000-2005 Enzi hizo Mimi nikiwa Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi na Kisha Gazeti la Mtanzania na Tanzania Daima.

Hizza ambaye Enzi hizo alikuwa akitamba Katika medani ya siasa za upinzani Kwani alikuwa ni  Katibu Mwenezi  wa Chama cha Wananchi (CUF) ,chenye ofisi zake Buguruni ,Dar es Salaamu ,enzi hizo CUF kilikuwa ni chama cha upinzani chenye nguvu,ushawishi na mara kwa mara Jeshi la Polisi lilokuwa chini ya Inspekta Jenerali (IGP) , Omar Mahita lilikuwa likieleza nguvu zake kwa wafuasi wa chama hicho hicho cha CUF ambao walikuwa wakikaidi amri za jeshi hilo ambazo zilikuwa zikipiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara iliyokuwa inapangwa kufanya na Chama hicho siku ya Ijumaa baada ya ibada ya waumini wa dini kumalizika ,Mara nyingi CUF maandamano Yale ambayo yalikuwa yamepigwa marufuku na Jeshi la Polisi yalikuwa yakianzia Buruguru kuelekea Uwanja wa Kidongo Chekundu Dar Es Salaam.

Nikiwa kama Mwandishi wa Habari wa siku nyingi ambaye nilipata fursa ya kuripoti Habari za vyama Vingi Vya siasa Katika mikutano ,maandamamo ya halali, haramu kisheria toka 1998-2014 , lazima nikiri wazi CUF ya Enzi zile ya 1999-2005  kilikuwa ni Chama Chenye wanachama ambao walikuwa na umoja na ujasiri na walikuwa na baadhi Yao walikuwa na ujasiri wa kukaidi amri za Jeshi la Polisi na kuamua kuingia barabarani kuandamana , mikutano na Matokeo yake walikuwa wakiambuliwa kupokea vipigo ,kurushiwa mabomu ya Machozi na Jeshi l Polisi na wengine kufunguliwa Kesi za jinai mahakamani.

Nadiriki Kusema hadi sasa bado akijitokea hapa nchini Chama cha upinzani Chenye wafuasi wenye misimamo usiyoyumba kama waliyokuwa nayo wafuasi wa CUF wa zama zile .

Binafsi Hizza nawe kumweleza ni mwanasiasa aliyekuwa na ushawishi wa maneno yaani kwa maana Kuwa Hizza awapo jukwaani au Mbele ya vyombo Vya Habari alikuwa ni Hodari sana wa kupangilia maneno aliyokuwa akiyaongoza ambao yanamzaa ndani yake ,misimamo na ujasiri ndani yake.

Mwanasiasa Huyo pia aliwahi kugombea ubunge Jimbo la Temeke alikuwa akipenda kutumia siasa za kurusha vijembe kwa wapinzani wake wa kisiasa hadi ikafikia Hatua akapachikwa Majina yafuatayo ( TAJIRI WA MANENO YA KISIASA ) , ( MTOTO WA TEMEKE) .

Maandamano mengi ya CUF ambayo Jeshi la Polisi ilikuwa iliyapiga marufuku kupitia aliyekuwa Msemaji wa Jeshi la Polisi Enzi za IGP -Mahita, Aden Mwamunyange na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar Es Salaam Enzi hizo , Alfred Gewe,Hizza ndiyo alikuwa akituita sisi waandishi wa Habari licha Jeshi la Polisi kuwazuia maandamano hayo ,yeye anajitokeza anasema maandamano hayo lazima yafanyike na Anawataka wafuasi wa CUF washiriki maandamano hayo bila kukosa na kweli walikuwa walishiriki kikamilifu na Kuishia kupata kipondo kutawanywa kwa mabomu ya Machozi na Jeshi la Polisi.

Kifo Tambwe Hizza Leo kimenifaya nimkumbuke Mwandishi wa masuala ya siasa marehemu Joyce Mmasi aliyefariki usiku wa kuamkia 6/12/2017 baada ya kuugua kwa muda mrefu , Kwasababu Joyce ambaye nilikuwa nafanya naye Kazi Katika Gazeti la Mwananchi ndiyo Mara kwa Mara nilikuwa naenda naye pamoja na Mpiga picha Leah Samike au Marehemu Joseph Senga kuchukua Habari za CUF na Katika maandamano Yao haramu ambayo mwisho wa siku vurugu zikianza tulikuwa tukikaa upande wa madefenda ya Polisi kwaajili ya Usalama wetu .

Kuna siku Niliwahi kumuuliza Hizza ni Kwani amekuwa Kinara wa kuhamasisha  watoto wawatu  washiriki maandamano yaliyoharamishwa na Jeshi la Polisi Enzi hizo CUF ilikuwa ikiitwa CUF NG'ANG'ARI halafu yeye hapokei Katika maandamano hayo haramu ?alinijibu kwa kifupi Kuwa bado anaitaji kuishi.

Nilimtazama Hizza baada ya kunipa Jibu Hilo na kuanza kuwasikitikia wafuasi wa vyama Vya siasa wanaondamana Katika maandamano haramu na wengine niliyokuwa karibu Yao nilikuwa naninaendelea kuwashauri wasikubali kutii amri za baadhi ya viongozi wa kisiasa zinazowataka washiriki maandamano haramu Kwani mwisho wa siku watakaoumia ni wao siyo viongozi wao wa kisiasa.

Kuelekea kampeni za Mwaka 2005 , upepo wa kisiasa Ulianza kuvuma vibaya upande wa Hizza ndani ya CUF Hali iliyosababisha kuanza kusuasua kisiasa .

Na kwakuwa sisi waandishi wa Habari ' Wachokonozi' tulikuwa tukipata taarifa hizo toka ndani ya Vyanzo vyetu CUF . Na binafsi Hizza alipoondoka CUF Nilimhoji Hizza ameondoka  CUF amatarajia kwenda kujiunga na Chama gani cha upinzani Kwani hapo awali akiwa CUF alishajiapiza Kuwa hawezi kujiunga na CCM Kwani  'YEYE KUHAMIA CCM NI SAWA NA KUZINI NA MAMA YAKE MZAZI'?

Hizza alinijibu hivi ; " Amehama  ghorofani  ataenda kuhamia ghorofani'. Kwa maana anatoka Katika Chama kikubwa yaani CUF anaenda kujiunga na Chama kikubwa ambacho hakukotaja kwa siku hiyo.

Baada ya uchaguzi Mkuu 2005 kumalizika na Dk.Jakaya Kikwete kushinda kuapishwa Kuwa Rais wa awamu ya nne na Mwenyekiti wa CCM, Hizza na aliyekuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha TLP, Leo Lwekamwa walitangaza kujiunga na CCM .

Na muda mchache baada ya Hizza kujiunga na CCM, CCM ilimpa Cheo Mkurugenzi wa Kitengo cha Propaganda Katika Idara ya Itikadi na Uenezi Makao Makuu ya CCM nchini ya Katibu Mkuu wa CCM wa Enzi hizo, Mzee Yusuf Makamba.

Hizza aliweza kufanyakazi hiyo ndani ya CCM licha alikuwa akinieleza alikuwa akifanya Kazi Katika mazingira magumu Kwani wale CCM  kindakindaki walichukia yeye kupewa nafasi ile Kwani yeye Hizza alivyokuwa CUF alikuwa akiisumbua CCM sana .

Lakini hata hivyo Hizza akufumu ndani ya CCM aliamua kuhama Chama hicho cha CCM na kwenda kujiunga na Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA)  ambapo hadi Leo hii umauti unamkuta ghafla alikuwa akikitumikia Chama hicho kikamilifu.

Na ushahidi wa Hilo ni Katika kampeni za uchaguzi Mdogo jimbo la Kinondoni, Hizza ndiyo amekuwa akisimama Katika majukwaa kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo Hilo kwa tiketi ya Chadema, Mwanahabari  Salum Mwalimu.

Hizza tume fahamu nae Miaka mingi sasa Aliniona wakati Nina mwili mdomo na baadae uzito uliongezeka sana .Ilipofika Mwaka 2013 nilikuwa na uzito wa Kg.130 Niliamua kuanza kufanya mazoezi ya viungo kupunguza uzito ambapo hadi sasa Nina Kg.80 .

Kwa tunaomfahamu Hizza hapo zamani akuwa na uzito mkubwa kama huu aliyokuwa nao hadi Leo anafariki Duniani. Amefariki akiwa na uone Kano wa uzito mkubwa( Mnene sana) na hata Nilipokuwa nikikutana naye na kukaa naye tunajadili masuala ya siasa alikuwa akionekama akihema kwa tabu na ule uzito mkubwa unamnyima raha.

Mara Kadhaa nilikuwa kumshauri apunguze huo uzito ,uzito umemuelemea na umemualibia mwonekano wake alikuwa akiniambia amesikia ushauri wangu atakufanyia Kazi ila akawa anania kama kweli nataka nimsaidie apunguze ule uzito nikubali anioe ili GYM tuwe tunaenda nae.

Hata hivyo Mara kwa Mara amekuwa akinieleza ugonjwa wa PUMU umekuwa umkimsumbua sana na kuamini ipo siku utakuja kukatisha Maisha yake.Nilikuwa nikimpa pole Sana.

Mara ya mwisho Kuwasiliana naye ilikuwa wiki  iliyopita kupitia namba yake 0755 263798, Tulijadili Hali ya siasa zinavyokwenda na akasema anakerwa na serikali ya awamu ya nne kupiga marufuku mikutano ya vyama Vya siasa na kwamba anashangazwa na Uongozi wa Chadema sijui ni Kwani hawampi nafasi ya use maji wa Chama hicho na kwamba endapo angepewa basi kila kukicha serikali ingekuwa inamfungulia Kesi za uchochezi. Nilicheka sana.

Poleni familia, wanasiasa wenzake, Chadema ,CCM,ndugu na jamaa na marafiki kwa kuondokewa na Mpendwa wetu Hizza ambaye  alikuwa aishiwi mzaha ,,kurusha vijembe kwa mahasimu wake wa kisasa hasa CCM , na kukosoa pale anapoona mambo ayaendi  sawa.

Kila binadamu Ana madhaifu yake , na Hakuna ubishi Kuwa Hizza ameweka rekodi ya kuhama Hama vyama na kuhama vyama siyo kosa Kwani Ibara ya 20 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ,inatoa Haki Mtanzania yoyote kujiunga na Chama chochote akipendacho.

Pia Hizza Katika siasa hasa siasa katika vyama vya upinzani ameacha harama na kwasisi tuliopataga fursa ya kumshuhudia  akifanya siasa Enzi zile akiwa CUF,CCM na sasa CHADEMA.

Na Hizza alitumia kikamilifu Haki yake hiyo ya Kikatika alikuwa CUF akaondoka akahamia CCM akatoka akajiunga na CHADEMA hadi umauti ulivyo mkuta Leo asubuhi.

Tajiri wa Maneno ya Kisiasa Tambwe Hizza, sisi  tulikupenda ila  Mungu amekupenda zaidi.

Utakumbukwa sana na waandishi wa habari tuliokuwa karibu yako kwa miaka mingi nikiwemo mimi (Happiness Katabazi), Martin Malela ( Tanzania Daima ) ,Ezekiel Kamwaga na wengine wengi.Tutakukumbuka .
Imenichukia muda kaumini Hizza kama amefariki kwasababu hadi Jana Hizza alishiriki mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni, Salum Mwalimu .

Na  kila nikikumbuka vibweka vyake majukwaani Leo Nikawa naangua kicheko na Kuishia  kukubaliana na ule Msemo usemao ' HAPA DUNIANI SISI TUNAPITA' Kweli Hizza umefariki ,nitakukumbuka  Kwani nilimpenda sana aina yako ya siasa uliyokuwa ukiifanya majukwaani ya kurusha vijembe kwa maasimu wa Chama Chako cha siasa.

Mungu aiweke roho yako Mahali panapostahili.Amina.

CHANZO: www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
8/2/2018

No comments:

Powered by Blogger.