Header Ads

WAZIRI KIGWANGALA HIVI UNA AKILI TIMAMAMU?


Na Happiness Katabazi

JANUARI 25 mwaka huu, Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamis Kigwangala ametoa siku saba kwa Jeshi la Polisi kuwakamata wahusika wakuu wa Mtandao wa Ujangili wa nyara za serikali na kupanga Mauaji ya aliyekuwa Mkurugenzi wa kampuni Palms Foundation na Mtetezi wa wanyama pori, Wayne Lotter ,Augosti  Mwaka 2017.

Waziri Dk. Kigwangala alisema  hayo mjini Dodoma alipokuwa Akizungumza na waandishi wa Habari na kulitaka Jeshi la Polisi kutekeleza agizo la kuwakamata majangili Hao ndani ya siku Saba ili Hatua nyingine zichukuliwe na Jeshi Hilo likishindwa kufanya hivyo ataenda kuwashitaki kwa  Rais John Magufuli.

Baada ya kusikia agizo Hilo lilotolewa na Waziri Kigwangwala nimeishia kujiuliza hivi huyu Waziri Kigwangwala Ana akili timamu?

Na Je Mbona mwanaume mzima anaonyesha anatabia za umbea umbea za Kupenda kuchongeachongea wenzake kwa Rais wa nchi?

Nimefikia uamuzi wa kujiuliza hivyo kwasababu ukilitafakari agizo Hilo Katika jicho la Sheria ni wazi Waziri Huyo Hana mamlaka ya kisheria ya kulipa Jeshi la Polisi lililioanzishwa kwa The Police Force And Auxiliary Service Act  Cap 322 ,  aimpi Waziri Huyo mamlaka ya kutoa amri kwa Jeshi Hilo.

Nakuuliza wewe Waziri Kigwangala hayo mamlaka ya kulipa Jeshi la Polisi siku Saba Umeyapata kwa mujibu wa Sheria hipi?

Maana Tanzania ni dola linaloongozwa kwa mujibu wa Sheria na siyo hizo porojo zako ambazo mtu mweye hadhi ya Waziri awezi kuziongea Mbele ya umma kupitia vyombo Vya Habari.

Umesema eti unayo Majina ya Hao waliopanga Njama na kumuua Huyo mwanaharakati Wayne Lotter na ushahidi unaona.

Yaani we Waziri Kigwangala Umepewa taarifa za Mauaji ya Wayne na ma Infoma wako tena ukute wamekulisha TANGOPORI yaani taarifa za uongo basi na wewe unaenda katika vyombo ya habari kana kwamba wewe ulikuwepo katika mauaji hayo wakati ukuwepo .

Mimi kama Mwanasheria wewe kupitia hayo maelezo yako wewe ushahidi  wako ni ushahidi wa kusikia ambao autapokelewa  mahakamani.

Kwa mujibu wa kifungu cha 10 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai(CPA) ,kinatoa madaraka kwa Polisi kufanyia uchunguzi taarifa za Uhalifu.

Kwa vifungu hivyo kisheria mtakubaliana na mamimi Kuwa Polisi ndiyo wenye mamlaka ya kuchunguza ,kukamata na pindi wakijiridhisha wana vielelezo Vya kuweza kumfungulia Kesi mtu wanayemtuhumu Kutenda kosa Fulani basi Polisi wakapeleka vielelezo hivyo Katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka ( DPP).

Kwa mujibu wa Ibara ya  59 B ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 .

Na Kifungu  cha 9 cha National Prosecution Service Act ,2008 , Mkurugenzi wa Mashitaka ( DPP) ,ndiyo mwenye mamlaka ya Kufungua Kesi za jinai mahakamani Kwaniaba ya Serikali .

Kifungu cha 5   The Police Force Force And Auxiliary Service Act , kimeanisha wazi  majukumu ya Jeshi la Polisi ambapo Moja majukumu yake kulinda Amani ,Sheria ,Kuzuia Uhalifu usitendeke,kulinda Raia na Mali zao

Ndiyo maana namuuliza huyu waziri hayo  mamlaka ya kutoa amri ya kushinikiza Polisi wachukue Hatua ndani ya siku Saba ameyapata wapi?

Nani kakupa hayo mamlaka ?Atueleze ili Tujue maana Tanzania ni dola lililoanzishwa na kinaongozwa kwa mujibu wa Sheria na wewe Kigwangala Uliapa kulinda Sheria za nchi?

Jeshi la Polisi limeanzishwa kwa mujibu wa The Police Force and Auxiliary Services Act Cap 322 .

Na ni chombo kinachotakiwa kifanyekazi kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu au wanasiasa.

Sasa kwanini wewe unatoa amri hizo za ovyo ambazo kwanza Huna mamlaka ya kutoa amri kwa Jeshi la Polisi kukamata watu Hao ambao wewe kupitia matamshi yako umeonyesha umeishawahukumu watu Hao Kuwa ni wauaji wakati Chombo Chenye mamlaka ya mwisho yautoaji Haki ni Mahakama kwa mujibu wa Ibara ya 107A ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.

Kwani Mahakama ndiyo Chombo Chenye mamlaka ya Kumtia hatiani mshitakiwa Fulani kwa makosa aliyokuwa Akishitakiwa nayo.

Hivi unasema unayo Majina ya watu waliomuua Huyo mtu. Nakuuliza hayo Majina uliyapata lini? Na kutoka Katika mamlaka zipi?

We Waziri Kigwangala hivi ulikuwepo wakati hao watu wanne ambao majina yao umasema unayo wakimuua Huyo Raia wa kigeni?

Au ulivyoona Kamera zinakumuulika basi ukaamua kujiongelea mambo ambayo mwisho wa siku umechekesha walionuna?

Dk.Kigwangala hivi Jeshi la Polisi likija Kuibuka na Kusema hayo  Majina uliyonayo hayafanani na waliyonayo  utasema nini?

Au Jeshi la Polisi likisema waliomuua Huyo Raia wa kigeni ,Jeshi la polisi lilivyokwenda  kuwakamata washitakiwa wale walipambana  na Polisi na polisi likaamua kutumia silaha likawaua   utasema nini?

Maana kama walikufa katika majibishano na polisi , polisi wataendaje kwa DPP kutaka marehemu washitakiwe? Chunga mdomo wako nakushauri.

Uoni hilo agizo lako la siku saba kwa polisi ulilolitoa kwa umma linaweza kusaidia baadhi walioshiriki kutenda mauaji hayo kukimbia,kuvuruga ushahidi na hivyo kulipa wakati mgumu Jeshi la polisi kuendelea kufanya upelelezi wake katika tukio hilo la mauaji ya huyo Mwanaharakati ?

Kwanza  minakushangaa sana sijui wewe ni Waziri wa aina gani .Basi tufanye nikweli hayo Majina unayo kweli na Hao watu wamelimua kweli Huyo Rai wa kigeni hivi nafasi yako ya Uwaziri ulishindwa nini kwenda kimya kimya kwa Waziri wa Mambo ya Ndani na kueleza hayo ili yeye awasiliane na Mapolisi ?

Lengo Lako hasa lilikuwa ni Kujenga au Kubomoa?

Minaona Lengo Lako hapa ni Kubomoa kwasababu kupitia Hilo agizo Lako ni wazi umelipaka matope Jeshi letu la Polisi na Taifa kwa ujumla Kuwa Raia wakigeni aliyeuawa hapa kwetu  Tanzania ,Jeshi letu la Polisi linafumbia macho wauaji.

Hivi kupitia agizo Lako ambalo halina  hadhi ya kisheria umepeleka ujumbe gani kwa serikali ya Huyo Raia aliyeuwawa kikatiri hapa nchini?

Kigwangala hivi unajielewa kweli wewe ni nani na una wadhifa upi na matamshi yako Katika Jamii ya achukuliwa kwa uzito gani na Jamii na hiyo serikali ya kigeni aliyotokea Huyo Raia aliyeuwawa? Una matatizo sana .

Halafu Kumbe mwenzetu unajitapa utaarifa za uhakika za Mauaji ya mwanaharakati Huyo sasa kwanini usiende Polisi kuwapatia taarifa na ushahidi wa Mauaji hayo?

Maana Kifungu  cha 7 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai, kinamtaka Mtu yoyote mwenye taarifa za kutendeka au kutaka Kutenda kwa Uhalifu ikiwemo Mauaji akatoe taarifa Katika mamlaka husika ikiwemo Jeshi la Polisi na akishindwa kufanya hivyo atashitakiwa .

Sasa na usomi wako na uwaziri wako ni kwanini umeshindwa kutimiza matakwa ya Kifungu hicho cha Sheria kwenda kutoa taarifa Katika Jeshi la Polisi unakimbilia Katika vyombo Vya Habari ?

Vyombo Vya Habari sikuhizi ndiyo vimekuwa Jeshi la Polisi la kupelekea taarifa za kihalifu?

Hivi ukienda kushitaki kwa Rais Magufuli ndiyo Magufuli yeye atakusaidia kuandaa Jalada la Kesi kufunguliwa mahakamani hata kama vielelezo bado haijapatikana Vya kutosha Vya kuwafungulia Kesi washitakiwa au ndiyo unaenda kuwashitaki awafute Kazi?

Maana sikuelewi kabisa ,maana hata ukienda kuwashitaki polisi kwa Rais mwisho wa siku Huyo Rais Hana mamlaka ya kuchunguza Kesi wala Kufungua Kesi mahakamani .

Naninalishangaa sana Jeshi la Polisi hadi sasa alijatoa amri ya kumuita na kumhoji Waziri huyu ili awapatie hizo taarifa na Majina ya Hao washukiwa?

Ni Jeshi hili hili uwa linafanya  haraka sana kuwakamata viongozi wa upinzani pindi wanapotoa matamshi mbalimbali na Kudai zinawahoji kwa kutoa Kauli za uchochezi?

Ajabu ni kwamba hadi Leo hii huyu Waziri ,Jeshi alijamuita kumhoji na awapatie ushahidi hayo maelezo aliyoyatoa  maana inaonenaka anajua mengi kuhusu Mauaji hayo.

Hivi Kigwangwala Mbona unapenda sana kuingilia Uhuru wa kufanyakazi wa taasisi zingine kama Polisi wewe nani kukuingilia Katika Wizara nayoiongoza?

Nani anakutuma kuingilia Uhuru wa Utendaji Kazi wa Jeshi la Polisi?

Kesi za jinai hazina  ukomo wa muda ( Limitation of Time) ya Kufungua Kesi mahakamani hata kama mtu  katuhumiwa kufanya kosa leo  anaweza kuja kushitakiwa hata miaka 40 ijayo tofauti na Kesi za  Madai  ( Civil Case) ambapo zinaukomo wa muda wa kuzifungua mahakamani.

Sasa  kwanini wewe Waziri Dk.Kingwangala unashinikiza Polisi ambao ndiyo wenye taaluma ya upelelezi wa Kesi za jinai wafanyekazi  kwa mashinikizo yako wewe badala ya taaluma? Una maslahi gani na hayo Mauaji ya Huyo Raia wa kigeni ?

Kuna watu wangapi hapa wanauwawa Katika mazingira yanayoaacha maswali, maiti zinaokotwa Kwenye fukwe za Bahari ya Hindi atujakusikia ukitoa siku saba kwa Jeshi la Polisi kukamilisha uchunguzi?

Nakuasa   Dk.Kigwangala punguza sana kutumia vyombo Vya Habari Katika Utendaji wako wa Kazi Kwani siku zote Kizuri kinajiuza Kibaya  kinajitembeza.

Ndiyo wewe maana kupitia hivyo vyombo Vya Habari unavyovitumia tena wakati mwingine siyo  unatumia kutaja majina ya watu  Katika tuhuma ambazo tukikusikiliza mwisho wa siku tunaona unaweza kuja Kumpa Kazi bure DPP  mahakamani .

Heshimu mgawanyo wa madaraka , fanyakazi na Taasisi zingine za serikali kwa ushirikiano wa kweli siyo kwa kuwavizia kama hivi unavyolivizia Jeshi la Polisi ambayo Kimsingi wao ndiyo wapelelezi ,wakamataji.

Waziri Kigwangala  siku zote unapoamua kudili na Wapelelezi  ' Makachero' nakushauri  udili nao kwa akili sana siyo njia hii ya kitoto unayotumia kudili nao , ukijifanya  Mjuaji dhidi yao watoto wa mjini tunasema  Wapelelezi  'WATAKUFURAHISHA  ' na UTAFURAHII  .Yaani watakushangaza .

Mtangulizi wako Katika Wizara hiyo ya Maliasili , Balozi Sued Kagasheki naye alijaribu kufanya kama hili ulilofanya ambalo aliituhumu ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Mkoani Arusha Mwaka 2014   Kwamba aipelelezi ipasavyo Kesi za Ujangili lakini mwisho wa wasiku Jeshi Hilo lilifanya uchunguzi wa Madai ya Kagasheki nakubaini alikuwa akisema uongo dhidi ya Ofisi ya RCO - Arusha .

Mwandishi wa Makala ni Mwandishi wa Habari Mwandamizi nchini na Mwanasheria.

Mungu ibariki Tanzania

CHANZO: www.blogger.com
Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
27/1/2018

No comments:

Powered by Blogger.