Header Ads

DPP ANYANG'ANYWA TENA MAMLAKA YA KUZUIA DHAMANA


Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA Ya Rufani nchini imeifukuza kwa gharama   rufaa ya Kesi ya Madai iliyokuwa  imekatwa  na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya mjibu    Rufaa, Jaremia Mtobesya iliyokuwa inaiomba  Mahakama hiyo itengue uamuzi  uliotolewa  na Mahakama Kuu Kanda Dar es Salaam ambayo ulisema  Kifungu cha 148 (4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai sura ya 20 Kuwa unakwenda  kinyume na Ibara ya 13 (6)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.

Kwa mujibu wa nakala ya hukumu hiyo inaonyesha imesainiwa na Msajili wa Mahakama ya Rufani ,John Kahyoza ,Januari 31 Mwaka huu, inasema jopo la Majaji wa Tano walioketi Dar Es Salaam.

Jaji Bernad  Luanda,Kipenka Mussa,Bethuel  Mmilla, Stellah Mugasha  na Jacob Mwambegele kwa Kauli Moja walitoa hukumu hiyo ya  ya kutupilia   rufaa hiyo Na.65/2016 iliyokuwa imekatwa mahakamani hapo na Mwomba Rufani ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Mjibu Rufani ( Mtobesya ) .

Jaji Kipenka  alisema jopo Hilo baada ya kupitia Sababu nne za Mwomba rufaa kukata rufaa ambazo miongoni mwa Sababu hizo Kuwa Mahakama Kuu ilikosea Kusema Kifungu hicho kinamnyima fursa  mshitakiwa kupinga hati hiyo ya DPP ya Kuzuia dhamana na kwamba Mahakama Hiyo ilikosea kisheria kukubali kutolea uamuzi shauri ambalo Mwombaji alikosea kunukuu Ibara ya Katiba    hoja ambazo  Jaji Mussa  azina mashiko.

" Mahakama ya rufaa imetupilia  Mbali kwa gharama rufaa iliyokatwa Mbele yetu na Mwanasheria Mkuu wa serikali iliyokuwa ikiomba  Mahakama hii itengue uamuzi  ya Mahakama Kuu uliokuwa umetamka  kuwa  Kifungu 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kwasababu kwasababu ni kweli Kifungo kicho kinakwenda kinyume na Ibara ya 13 (6)(a)  ya Katiba ya nchi;

"Na Mahakama hii ya Rufani nayo inakubaliana na hukumu ya Mahakama Kuu Kuwa Kifungu hicho cha 148(4) Sheria hiyo ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinafunja matakwa ya  Ibara hiyo ya Katiba hivyo uamuzi wa Mahakama Kuu ulikuwa sahihi na Mahakama hii imekataa   kutengua uamuzi ule hivyo utabaki kama ulivyo na Mwanasheria Mkuu wa serikali alipe gharama za Kesi kwa Mjibu  Rufani( Mutobesya) aliyekuwa anatetewa na Wakili wa kujitegemea ,Mpare Mpoki.

Ibara ya 13(6) (a) ya Katiba ya nchi inasomeka hivi ;   " Wakati Haki na wajibu kwa mtu yeyote inapoitajika kufanyiwa maamuzi na Mahakama au Chombo kingine chochote kinachohusika, basi mtu Huyo Atakuwa na Haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia Haki ya kukata Rufani au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na maamuzi ya Mahakama au Chombo hicho kingine kinachohusika" .

Disemba  22 Mwaka 2015 , Jopo la Majaji watatu wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam Katika Kesi ya Kikatiba Na 29 /2015 ,Shabani Lila ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani kwa sasa,Kihiyo  na Ruhangisa  ambaye alistaafu Ujaji wa kwa Hiari mwaka 2017 ,ambapo jopo hilo lilikubaliana na hoja za malalamikaji Mtobesya Kuwa Kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ,kina kwenda kinyume na Ibara ya hiyo ya Katiba ya nchi.

Mwaka 2016 ,Mwanasheria Mkuu wa serikali alikataka rufaa Mahakama ya Rufani nchini, kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu akiomba utenguliwe uamuzi huo kwasababu nne ambazo miongoni mwa Sababu hizo ni kwamba Mahakama ilikosea Kusema hati ya Kufunga dhamana ya mshitakiwa inayowasilishwa mahakamani na DPP inammnyima mshitakiwa Haki ya kuipinga hati hiyo ya DPP Katika Chombo kingine.

Desemba 22 Mwaka 2015 , Jopo la Majaji watatu wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam Katika Kesi ya Kikatiba Na 29 /2015 ,iliyofunguliwa na Mtobesya dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni Shabani Lila ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani kwa sasa,Kijiyo na Ruhangisa  ambaye alistaafu Ujaji wa kwa Hiari ambapo jopo lilikubaliana na hoja za malalamikaji Mtobesya Kuwa Kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ,kina kwenda kinyume na Ibara ya 13 (6)(b) ya Katiba ya nchi.

Kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, ni Kifungu ambacho kinampa mamlaka Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) , Kuwasilisha mahakamani kwa maandishi hati ya Kufunga dhamana kwa mshitakiwa yoyote wa makosa ya jinai ambayo makosa hayo kwa mujibu wa Sheria yana dhamana ila DPP Ana mamlaka ya kutumia Kifungu hicho Kufunga dhamana ya mshitakiwa kwa Sababu ya Usalama wa mshitakiwa na pindi DPP akiwasilisha hati hiyo ya Kufunga dhamana Mahakama Inakuwa haina uwezo wa kupingana na hati hiyo kama imebidhi matakwa yote ya kisheria.

Kwa Mujibu wa hati yake ya Madai ilioambatanishwa na kiapo Chake   Chake Juni 30 mwaka 2015 ,Mutobesya alidai  Kuwa Ibara 26 ( 2) ya Katiba ya nchi inasomeka kama ifuatavyo;  " Kila mtu Ana Haki , kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria , kuchukua Hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba na Sheria za nchi".

Na Kuwa Kifungu cha 4 na 5 Cha Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Binadamu(BRADEA)

Hivyo alitumia  Kifungu na Ibara hizo za Katiba kwenda Kufungua Kesi Mahakama Kuu ili kuiomba Mahakama Kuu itamke Kuwa Kifungu cha 148(4) cha Sheria hiyo  kinakwenda kinyume na Ibara 13(b)(a) ya Katiba ya nchi na kwamba Ibara ya 26 (2) ya Katiba ya nchi inampa Haki ya kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi  ya Katiba na sheria  za nchi.

Itakumbukwa Kuwa   Kifungu hicho cha 148(4) cha Sheria hicho ,ndicho kilichotumika  Kumfungia dhamana Kiongozi wa Taasisi na Jumuiya za Waislamu ,Sheikh Issa Ponda aliyekuwa anatetewa na wakili wa kujitegemea na wakili Nasoro Juma wakati upande wa Jamhuri ulikuwa ukiwakilishwa na wakili mwandamizi wa serikali ,Tumaini Kweka mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Victoria Nongwa ambapo DPP wa enzi hizo, Dk.Eliezer Feleshi aliwasilisha hati ya kufunga dhamana ya Sheikh Ponda ambaye yeye na wenzake 49 walikuwa wakikabiliwa na makosa ya wizi,uchochezi ,kuingia kwa jinai na  makosa aliyokuwa akishitakiwa nayo katika kesi hiyo namba 245/2012 yalikuwa na dhamana ambapo na  Sheikh Ponda alikaa gerezani tangu Oktoba 18 mwaka 2012   hadi Mei 9 mwaka 2013  mwanzo wa kesi hadi kesi ilipomalizika ambapo alipatikana na hatia ya kutenda kosa la kuingia kwa jirani akaacbiwa huru ila mahakama ikamtaka awe mtu mwenye tabia njema.

Kifungu hicho pia kulitumika Kumfungia dhamana kwa Mara ya pili Katika kesi ya kutoa maneno ya uchochezi Na.128/2013  iliyokuwa imefunguliwa na Jamhuri dhidi yake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro mwaka 2013  ambapo Hakimu Mkazi Mary Moyo alimwachiria huru Sheikh Ponda .

Katika kesi hii Ponda muda wote alikuwa amekaa gerezani kwasababu DPP alitumia kifungu hiyo kumfunga dhamana.

Hata hivyo Sheikh Ponda kupitia wakili wake Juma Nassor alikata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,kupinga hukumu ya mahakama ya Kisutu ilimfunga kifungo cha mwaka mmoja na alishinda rufaa yake .

Na upande wa Jamhuri akurudhishwa na hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro iliyomwachiria huru Sheikh Ponda ambapo Jaji Edson Mkasimongwa  alisema hakuna mahali popote  ambapo imethibitishwa kuwa mtu fulani alichochewa kufanya mkusanyiko usio halali wala mtu aliyeumizwa imani yake.
Pia Kifungu hicho ambacho Tayari Mahakama Kuu ,Mahakama ya Rufani nchini imeisha kitangaza Kifungu hicho kinakwenda kinyume  na Katiba ,Ndio kimetumika na DPP Kuzuia  dhamana Mbunge wa Mbeya Mjini , Joseph Mbilinyi ( SUGU)  ambaye anasota gerezani wakati kosa a alishitakiwa nalo
Lina dhamana .

CHANZO: www.katabazihappy.blogspot.com
5/2/2018.

No comments:

Powered by Blogger.