RAIS HAFANYI MAAMUZI BILA KUUNDA TUME
Na Happiness Katabazi
NI miaka miwili tangu Rais Jakaya Kikwete aingie Ikulu, na katika kipindi hicho, hajawahi kufanya maamuzi yoyote kuhusu kero zinazowagusa wananchi bila kuunda tume.
Ni stahili nzuri ya uongozi unaojali misingi ya utawala bora na kuheshimu haki za binadamu, lakini si mara zote stahili hiyo inaweza kutumika. Kuna wakati Rais Kikwete alipofanya ziara kwenye wizara mbalimbali, alipofika Wizara ya Fedha, alisema ushahidi wa mazingira unatosha kumchukulia hatua mtumishi
bila kuthibitishwa na mahakama.
Lakini leo, hafanyi maamuzi mazito bila kwanza kuunda tume au kamati, hata kwa mambo yaliyo wazi kabisa, inawezekana stahili hiyo inatokana na kuwaonea aibu baadhi ya watendaji walio na uhusiano naye wa karibu.
Nikirejea kwenye hoja yangu ya uundwaji wa tume, wakati Watanzania walipokuwa wanakerwa na mwenendo wa Jeshi la Polisi ambalo lilikuwa limepoteza mwelekeo na kuwa sehemu ya ujambazi, rais aliunda tume iliyoongozwa na Jaji Mussa Kipenka, kuchunguza mauaji ya watu wanne wakazi wa Mahenge, mkoani Morogoro.
Tume hiyo ilifanya kazi nzuri na ilimtia matatani pamoja na watu wengine ACP-Abdallah Zombe ambaye hadi sasa anakabiliwa na kesi ya mauaji.
Tunakumbuka pia rais aliunda tume ya kuchunguza mikataba na sheria ya madini baada ya vilio vya Watanzania, akiwemo Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), kuwasilisha hoja binafsi bungeni, lakini Bunge likakengeuka na kutoa adhabu kwa kile walichokiita kulidanganya Bunge na kusema uongo dhidi ya aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi.
Alipofukuzwa Zitto, wananchi walihamaki, wakamuunga mkono rais naye akawageuka wabunge wa CCM kama kinyonga na kuunda tume kupitia upya mikataba ya madini na sheria zake. Tume hiyo ambayo pia yumo Zitto, bado inaendelea na kazi yake.
Hii ina maana kwamba rais hajui nini kinatokea kwenye sekta ya madini, wala kuna tatizo gani licha ya ukweli kwamba aliwahi kuongoza Wizara ya Nishati na Madini, hivyo anangojea tume aliyoiunda imletee mapendekezo.
Hivi majuzi tu, Bunge liliunda tume ya kuchunguza mkataba wa Richmond, uamuzi wa kuunda tume hiyo ulifanyika baada ya hoja hiyo iliyoasisiwa na upinzani, kuletwa na mbunge wa CCM.
Hoja hiyo ingeletwa na mbunge wa upinzani lazima ingepingwa kama ilivyopingwa hoja ya Buzwagi iliyowasilishwa na Zitto. Kwa hiyo Bunge letu lisijisifu sana eti limebadilika na kuanza kutetea maslahi ya wananchi.
Ukweli ni kwamba halijabadilika, ni Bunge lilelile la CCM, isipokuwa safari hii, lilikuwa na mpango maalum wa kujinusuru kutokana na tuhuma na kashfa nyingi zilizokuwa zikiikabili serikali.
Lakini tukirudi kwenye hoja, baada ya Dk. Harrison Mwakyembe kuwasilisha ripoti yake na aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa kulazimishwa kujiudhulu, kumekuwa na usemi kwamba rais alivunja Baraza la Mawaziri. Kwa hakika hilo halikutokea.
Kilichotokea ni kwamba Waziri Mkuu akijiudhulu, Baraza la Mawaziri linavunjika. Kwa hiyo hilo ni tukio la kawaida la kikatiba na wala Kikwete hastahili kupongezwa eti amevunja Baraza la Mawaziri.
Tatizo kubwa ni kwamba, rais aliyajua haya yote ya Richmond na Dowans, lakini hakuchukua hatua kwa kuwa wahusika walikuwa ni watu wake wa karibu, na ndiyo maana amekaririwa akisema yaliyompata Lowassa ni ajali ya kisiasa.
Maneno dhidi ya Richmond yalikuwa mengi kiasi cha kutohitaji hata kuunda tume kuchunguza tuhuma hizo. Je, ina maana kwamba rais hakuwa na uamuzi wowote hadi kuunda tume na itoe mapendekezo?
Kwenye fedha za EPA, kelele zilipigwa nyingi, lakini rais alinyamaza hadi taarifa ya Enrest &Young iliposema kuwa zaidi ya sh bilioni 133 zimeporwa, ndipo alipochukua hatua ya kubadilisha uteuzi wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Daud Ballali ambaye hadi sasa hajulikani alipo.
Tukumbuke kuwa uchunguzi huo ulifanywa kutokana na shinikizo la wafadhili, kwani wizi huo pia ulibainishwa na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali, lakini serikali ilifumbia macho, hadi ilipopewa amri na wafadhili.
Zipo kashfa nyingi ambazo kwa stahili ya Rais Kikwete, kila moja inasubiri iundiwe tume na kutoa mapendekezo yake, jambo ambalo binafsi naliona si jema kwani kuna tuhuma ambazo hazihitaji kumaliza hela za walipa kodi kuundia tume.
Je, Rais Kikwete anangojea ashinikizwe ndipo uchunguzi ufanyike kuhusu kashfa zilizosalia? Kwa mfano lini tutaambiwa ukweli kuhusu gharama za ujenzi wa minara pacha ya BoT?
Je, ni kweli kwamba gharama hizo zilipandishwa kitapeli kutoka sh bilioni 83 hadi kufikia sh bilioni 523? .
Kama hoja hii inabeba ukweli wowote, basi Watanzania tujiandae kusikia habari kuhusu kashfa hii kubwa kuliko zote zilizowahi kuikabili Benki Kuu yoyote duniani.
Naamini hasira za Watanzania zitakuwa maradufu ya zile walizokuwa nazo kuhusu kashfa ya Richmond. Tatizo ni kwamba hakuna tume ilishaundwa na rais kuchunguza kashfa hii. Je, Rais Kikwete anangoja nini?
Kuhusu ufisadi utokanao na kashfa ya EPA, tayari tumeelezwa na serikali kwamba mafisadi hao wameanza kurejesha fedha. Tatizo lililopo ni njia ambayo serikali inataka kutumia kuwashughulikia mafisadi hao.
Nchi ina sheria ya jinai ambayo ikivunjwa, mtuhumiwa hufunguliwa mashitaka na kuamriwa na mahakama ya wazi kurejesha mali aliyoiba na pia kutumikia adhabu. Katika sheria zetu hatuna utaratibu wa mahakama za siri zinazoendeshwa na makachero wa Usalama wa Taifa.
Tukiruhusu mafisadi wakahukumiwa na mahakama za siri za aina hii, tutakuwa tumevunja msingi mkuu wa utawala wa katiba na sheria za nchi.
Lazima kila raia achukuliwe kuwa ni raia mwema na mtiifu wa sheria mpaka mahakama itakapothibitisha pasipo shaka kwamba ana hatia.
Hivyo, hatuko tayari kusikia kwamba mafisadi wanarejesha fedha kwa siri na kuachwa wakiendelea kutamba mitaani. Lazima sheria ichuke mkondo wake.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
0755 312859
katabazihappy@yahoo.com
www.katabazihappy.blogspot.com
Chanzo:Gazei la Tanzania Daima la Alhamisi Machi 6,2008

1 comment:
Maovu yote yanayotokea ya ufisadiMh.Rais -nasikitika kusema ni mshiriki namba moja.Hawezi kutuoa uaamuzi wowote.Hizi tume zinazoundwa ni geresha au mazingaombwe.Tume hizo zinatumia mamilioni ya pesa kutafiti kitu ambacho kiko wazi.Tume ya Richmund imetoa taarifa zake mafisadi wanafahamiki mbali na kujiuzulu hakuna hatua zozote za kisheria zilizochukuliwa,BOT badala ya mafisadi kufikishwa katika vyombo vya sheria hakuna hatua zozote mbali ya kutangaziwa ya kua mafisadi wamerudisha fedha walizo ziiba huu ni ushahidi tosha kufikishwa mahakamani .Mh.Rais tumechoshwa na hizo tume zako kama kweli zinalengo la kupambana na Ufisadi basi ziznzpogunduz mzpungufu katika wizara husika wanaohusika wachukuliwe hatua.Vinginevyo haya ni mazingaombwe yaliyopitwa na wakati.MUNGU IBARIKI TANZANIA
Post a Comment