KESI YA SIMON JENGO YADODA
Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaama,jana ililazimika kuiarisha kesi hiyo ambayo ilikuja kwaajili ya upande wa Jamhuri kumsomea maelezo ya awali aliyekuwa Naibu Mkurugenzi wa Mifumo na Uendeshaji ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Simon Jengo,kwasababu mawakili wa Taasisi ya Kuzia na Kupambana na Rushwa kuwa na udhuru.
Wakili wa Serikali Leonard Chalo mbele ya Hakimu Mkazi Rita Tarimo alieleza kuwa kesi hiyo ilikuja jana kwaajili ya upande wa Jamhuri kumsomea maelezo ya awali lakini hilo haliwezi kufanyika kwasababu mawakili wa Takukuru wanaudhuru hivyo wakaomba kesi hiyo iairishwe.
Januari 30 mwaka huu, Wakili kiongozi wa serikali, Fredrick Manyanda, aliyekuwa akisaidiwa na Ben Lincoln na Shardrack Kimaro, mbele ya Hakimu Mkazi, Ritha Tarimo, alidai kuwa kati ya Juni 2005 na Desemba 2008 akiwa mtumishi wa benki hiyo, alimshauri Gavana vibaya ili benki hiyo inunue mitambo 26 ya kuharibu noti pasipo kujali hali ya BoT.
Hii ni mara ya pili kwa Jengo kushtakiwa. Kesi ya kwanza inamkabili Jengo na wenzake ambayo inaendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala na wanakabiliwa na makosa ya kuisababishia hasara benki hiyo.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Aprili 28 mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment