Header Ads

WAKANDARASI WAZALENDO SASA MSHINDWE WENYEWE

Na Happpiness Katabazi IJUMAA ya wiki hii, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi John Ndunguru kwaniaba ya serikali alitia saini mkataba wa ujenzi wa daraja la Mto Mbutu lilopo wilani Igunga mkoani Tabora na makampuni 13 ya wakandarasi wazalendo watakao jenga daraja hilo ambapo ujenzi wa daraja hilo utagharimu jumla ya Sh bilioni 12. 34 ambao unatarajiwa ukamilike Septemba mwakani. Mkataba huo ulisainiwa katika sherehe za utiwai saini zilizofanyika siku hiyo katika ofisi za wakara wa Barabara Tanroads,Morocco Jijini Dar es Salaam, na kuudhuliwa na watendaji wa wizara hiyo na waandishi wa habari ambapo mimi ni miongoni mwa waandishi wa habari tulioalikwa kushiriki kushuhudia tukio hilo ambalo limeandika historia mpya mpya hapa nchini. Kwani wakandarasi wazalendo kwa muda mrefu wamekuwa wakilailalamikia serikali kwa kushindwa kuwajengea uwezo kwa kuwapatia zabuni za ukandarasi na matokeo yake serikali imekuwa ikitoa kwa wingi tenda za ukandarasi kwa makampuni ya nje hususani kampuni toka nchini China wakati kuna watanzania wazalendo wanaweza kufanya shughuli hizo za kikandarasi. Akizungumza katika sherehe za utiaji saini wa mkabata baina ya serikali na makampuni hayo 13 Ndunguru alisema hatua hiyo ni ya kihistoria na pia ni utekelezwaji wa ahadi iliyowahi kutolewa na serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa itawajengea uwezo makandarasi wazalendo kwa kuwapatia tenda za ukandarasi. Na kwamba serikali imeamua kuwapatia kazi hiyo na kuwa kazi hiyo waliyopewa ni changamoto kwao kwani kuna makampuni mengi ya kigeni yamekosa fursa hiyo badala yake serikali imetoa fursa hiyo kwa makampuni hayo Akizungumza kabla ya kutiliana sanii kwa mkataba huo, Mkurugenzi wa Wakala wa Barabara Tanzania, (TANROADS), Patrick Mfugale alisema makampuni hayo ya wakandarasi 13 wameungana katika mradi huo wa ujenzi wa daraja katika bonde la mto mbutu lenye upana wa kilomita 3. “Daraja hilo litajengwa kwa zege na saruji, litakuwa na urefu wa mita 40 na upana wa mita 10.7, litakuwa na uwezo wa kubeba gari lenye uzito wa juu unaokubalika kisheria hapa nchini ambao ni tani 56,”alisema. Mfugale alisema daraja la mbutu pia litahusisha ujenzi wa makaravati saba ya zege yenye upana wa mita 8 hadi 14 ambayo yatajumuisha ujenzi wa tuta la barabara lenye urefu wa kilomita tatu kwa kiwango cha changarawe. “Jumla ya kampuni 13 yakiwemo Skol Building Contractors Ltd, Del Montel (T) Ltd, Mayanga contractors Company Ltd,CASCO Construction Ltd, Electrics International Company Ltd, KIKA construction Company Ltd, GEMEN engineering Company Ltd, Milembe Construction Company Ltd, Lukolo Company ltd ,MAC Contractors Co.Ltd,Nyakirang’anyi Construction Ltd, Nyegezi J.J construction Ltd na Concrete Maters company (T) Ltd ,”alisema Mfugale. Vile vile imeelezwa mawasiliano yataimarishwa kati ya wananchi wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga na Meatu iliyopo Shimiwi na wilaya ya Igunga wakati wote. Kwani ujenzi wa daraja hilo umetokana na mvua kubwa iliyonyesha kipindi cha nyuma ambayo ilisababisha uhalifu mkubwa wa daraja hilo hali iliyosabisha wananchi. Naye mwakilishi wa makampuni hayo 13 akizungumza kwaniaba ya makandarasi hao Injinia Stephen Makigo alisema wanaishukuru Serikali kuwakumbuka na hatua hiyo itasaidia kukuza uchumi kwani fedha hizo zitazunguka ndani. Kwa kiai Aidha aliakikishia serikali kuwa watafanyakazi kwa ushirikiano na umahiri wa hali ya juu kwani wakijenga daraja hilo chini ya kiwango siku nyingine serikali itashindwa kuwaamini na kuwapatia kazi nyinge za kikandarasi. Alisema inatarajiwa wakandarasi wazalendo watakapokamilisha ujenzi wa mradi huu watakuwa na uwezo wa kujenga miradi mingine inayofanana na huu na hivyo kupunguza serikali kuwa tegemezi kwa wakandarasi wa nje kwa kazi za ujenzi wa barabara. Aidha alisema fedha zinazolipwa kwa miradi inayotekelezwa na wakandarasi wazalendo kwa kiasi kikubwa itabaki na kuzungushwa nchini hivyo kukuza uchumi wa wa Tanzania na pia miradi itakayotekelezwa na wananchi itaongeza ajira kwa wananchi na kusaidia kuinua vipato vyao. Binafsi napongeza hatua hiyo ya serikali ya kuwakumbuka wakandarasi wetu wa ndani na kuwapatia mradi mkubwa kama huu ili waweze kuanza ujenzi.Lakini pia nayapongeza makampuni hayo 13 kwa uamuzi wao mzuri wa kujiunga pamoja na kukubaliana kufanyakazi kwa pamoja kwaajili ya kulijenga daraja hilo ili wananchi wenzetu wa Igunga nao waweze kuwa mawasiliano ya uhakika ya barabara kutoka eneo moja hadi nyingine katika vipindi vyote vya mwaka kati ya vijiji vilivyopo katika tarafa ya Igurubi yenye wakazi zaidi ya 94,449 na mji wa Igunga. Hakuna ubishi kwa hatua hiyo ya serikali kuwapatia kazi hiyo makandarasi wa ndani kwa kiasi fulani utasaidia fedha za serikali zitakazowalipa makampuni hiyo,zitalipwa kwa kiwango cha fedha za Tanzania na siyo kegeni hivyo ni dhahiri serikali itajikuta inatumia angalau kiasi kidogo cha gharama ukilinganisha na kama zabuni hiyo ingekuwa imepewa makampuni ya nje,serikali ingelazimika kuwalipa wakandarasi hao wan je kwa kutumia fedha za kigeni wakati kila kukicha fedha yetu inazidi kumezwa na dola ya kimarekani. Napenda kuyaasa makampuni hayoi 13 yalibahatika kupewa kazi hiyo na serikali, yaende kufanya kazi waliyoomba na kwa makubaliano waliyokubaliana na serikali katika mkataba waliouingia baina yao, kwani endapo makampuni hayo yataenda kufanyakazi chini ya viwango,ni wazi kabisa watakuwa wamesababisha yale makampuni mengine ya ukandarasi wazalendo ambayo hayakuoata fursa ya kuchaguliwa kujenga daraja hilo ,nao hawataaminiwa tena serikali yetu kupewa tenda za ujenzi kwani kuna msemo mmoja usemao ‘samaki mmoja akioza wote wameoza’. Na tunamuomba Waziri wa Ujenzi, John Magufuli na timu yake ukali ule ule anaowanyesha makandarasi wageni ambao ni wazembe, tunataka auonyeshe kwa makandarasi wazalendo hasa katika mradi wa ujenzi wa daraja la Mbutu,pindi atakapobaini wakandarasi hao wanazembea bila ya kuwaonea haya. Ninaimani hapa nchini kuna wakandarasi wengi wamesoma vizuri na ndiyo maana hata hayo makampuni ya kigeni yanayopewa tenda na serikali yetu kujenga mabarabara mwisho wa siku makampuni hayo ya kigeni yanaamua kuwatumia wakandarasi wa Kitanzania kuwasadia kujenga ujenzi. Lakini nimalizie kwa kuiasa serikali yetu nayo itoe fedha kwa wakati kwa wakandarasi ambao wameishaingia nao mkataba wa kufanya shughuli za kikandarasi kwani kuna manung’uniko ya chini chini ya muda mrefu ambayo baadhi ya wakandari hata wa miradi midogo ya ujenzi wamekuwa wakiilamikia serikali kwa kushindwa kuwapatia kwa wakati fedha wakandarasi ili wawendelee na ujenzi na matokeo yake wakandarasi hao wamekuwa wakijikuta ama wakijenga chini ya kiwango idi mradi akamilishe ujenzi ndani ya muda wa mkataba waliokubaliana. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika. 0716 774494 www.katabazihappy.blogspot.com Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Aprili 30 mwaka 2012

No comments:

Powered by Blogger.