Header Ads

HONGERA MAMA SALMA KIKWETE






Na Happiness Katabazi

WIKI hii Mke wa rais mama salma Kikwete  Alitunukiwa Tuzo ya Dunia  ya Hamasa ya Uongozi (Global Leadership Inspiration  Award),  ambayo imeelezwa Kuwa Msangi wake ni kutambua  uongozi madhubuti na Hamasa  Katika  kutetea  hadhi  ya wa awake Duniani.

Akizunmgumzia Tuzo hiyo, salma Alisema Tuzo hiyo ni heshima kubwa kwa wa awake wa Tanzania, ....Hakuna maendeleo endelevu na  ya ukweli  bila wanawake ,hivyo lazima jitihada zifanyike kushirikisha wanawake Katika  sekta mbalimbali  za maendeleo na akawataka wanawake wanawake nchini kujitokeza kuzungumzia unyanyasaji wa kijinsia unaofanywa na wanaume.

Awali ya yote naupenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa mama salma kushinda Tuzo ambayo pia midi tangaza Tanzania Katika Dunia.

Lakini pia naupenda kuongezea Taasisi hiyo hiliyoamua kutoa Tuzo hiyo kwa mwanamke anayetoka Katika nchi ya Tanzania ambayo nchi yetu imekuwa ikisifika ni miongoni mwa nchi Maskini na pia ndani ya ardhi yake pia kumekuwepo na taarifa za baadhi ya wanawake kufanyiwa ukatiri na wanaume .

Hali iliyosababisha hata Jeshi la Polisi chini ya Utawala wa IGP-Said Mwema na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) chini ya Dk.Eliezer Feleshi kuanzisha Dawati la kushughulikia Kesi za unyanyasaji wa kijinsia na kuzipa kipaumbele .

Hakuna ubishi Kuwa hadi Leo kuna baadhi ya wanaume tena wasomi wananyanyasa wake au wapenzi zao kwa mtindo tofauti.

Kuna baadhi ya wanaume wamebahatika kupata wanawake wamesema lakini wanawakataza wasifanyekazi  na endapo mwanamke wake akimpinga mwanaume Huyo umuanzishia visa Mke Huyo na Mwisho AMA kumterekeza KWA kisingizio Kuwa Mke Huyo ni jeuri.

Leo hii kuna baadhi ya wanaume mabazazi wamekuwa wako fanya unyanyasaji wa kijinsia baadhi ya wanawake kinyume na maumbile KWA kisingizio Kuwa wanaume kuwapatia a hadi nyingi.

Leo hii kuna baadhi ya wanaume wamekuwa wakiwabaka watoto nawasichana mitaani licha wakati mwingine Sisi baadhi ya watoto wa kike ambao hakutakuwa kujiheshimu tumekuwa tukijivunjianheshima Kwa Kuwa nguo za nusu uchi,kujihusisha na ulevi wa kupindukia Hali inayosabaisha wakati mwingine tukose watu wa kutetea sisi wanawake.

Kuna Msemo usemao" Kwenye mafanikio  ya mwanamme mwanamke ameshiriki halikadharika kwenye mafanikio ya mwanamke pia kuna mwanae ameshiriki: 

Hivyo nitakuwa sijakosea Kuwa Kwenye mafanikio hayo mama salma  hadi kupata Tuzo hiyo na kutambulika Duniani hivi  sasa kwasababu tumemshuhuia akiudhulia mikutano mkubwa ya kimataifa akiarikwa na anatoa Hatuba ni wazi kabisa mumewe Rais Kikwete amechangia maendeleo yake.

Nasema Kikwete amechangia mafanikio ya mama salma aliyonayo Hivi sasa kwasababu hajamzuia Mke wake kufanya shughuli zake, licha Kama Kikwete angekuwa na akili mbovu Kama za baadhi ya wanaume  wengine ambao wanaamini mwanamke si Mali kitu na hawezi kufana jambo lolote la ktk kimaendeleo hapa Dunia, angemzuia hata kuanzisha Taasisi ya Wama na kuudhulia mikutano hiyo ya ndani na nje ya nchi.

Hakuna ubishi mama salma Kikwete wa Kipindi kile akiwa mwalimu na mama salma Kikwete ambaye ni Mke wa rais Kikwete na Mwenyekiti wa Taasisi ya wanawake na Maendeleo(Wama) wanautofauti mkubwa kifikra, Katika kuhutubia Mbele ya umma.

KWA wale wanaomfuatilia na kumsikiliza mama salma pindi anapohudumia watakubaliana HIvi sasa mama salma amekubali kupikwa na akapikika hadi Leo hii amekuwa na uthubutu wa kusimama na kuzungumzia mambo yenye mantiki.Pongezi pia KWA wanaomwandalia Hotuba na vazi lake la kitenge AMBAlo HIvi sasa ndiyo imekuwa alama kubwa ya mama Huyo ambaye anawawakilisha wanawake wa Tanzania. 

Naomba Tuzo hiyo iwe chachu pia KWA wanaume ambao bado wataendeleza unyanyasaji wa KWA wanawake.watambue Kuwa kuna baadhi ya wanawake wanauwezo wa kiutendaji ,madarasani, Katika kufanyabiashara ,kupendezesha familia KWA ghalama zao Kwani Hakuna kilichoketi Kuwa HIvi sasa baadhi ya wanaume wamekuwa ni muhiri sana wakubwa na kupendezesha mitaani lakini wanashindwa kutoa Fedha za kuhudumia wake zao na familia zao  Matokeo yake wanawake Hao Hao wanaonyanyasa KWA maneno ya kejeli na vipigo ndiyo wamekuwa wakiendesha familia hizo KWA kuwalaisha watoto,kuwasikia Ada za shule na Fedha za matibabu.

Hongera mama salma Kikwete wa ushindi wa Tuzo hiyo na Tuzo hiyo ni  ishara Kuwa Wama imekuwa mustari wa Mbele kuwasaidia watoto wa kike hapa nchini na Mimi ni miongoni mwa mashahidi Kuwa Wama imekuwa ikiwalipia Ada hada Katika chuo Vicki baadhi ya watoto wa kike.

Nawatakieni kheri ya sikukuu ya Christmas  ambayo siku hiyo mimi nitakuwa nikikumbuka siku yangu ya kuzaliwa.

Mungu  ibariki Tanzania
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili ,Desemba 22 Mwaka 2013.

No comments:

Powered by Blogger.