Header Ads

DPP:FELESHI AMWEKEA PINGAMIZI SHEIKH PONDA

, Na Happiness Katabazi MKURUGENZI wa Mashitaka (DPP),Dk.Eliezer Feleshi ameiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar e s Salaam,ilikatee ombi la mapitio liliwasilishwa na katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, sheikh Ponda Issa Ponda kwa Madai Kuwa hati ya kiapo inayounga mkono ombi Hilo Kasoro za kisheria. ombi Hilo la DPP-Feleshi ni pingamizi la awali lililowasilishwa Jana na Wakili kiongozi wa serikali Bernad Kongora Mbele JAJI rose Temba Ambapo Wakili Kongora alianza kwa kuikumbusha Mahakama Kuwa Jana shauri Hilo lilikuwa limekuja kwaajili ya usikilizwaji wa ombi la mapitio ya uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro HIvi karibuni alitoa uamuzi wakukataa kumfutia kosa la kwanza la Kutenda kosa la uchochezi wakati yupo ndani ya kifungo Cha Mwaka mmoja nje ambacho kilimtaka asitende makosa na awe raia Mwema lakini Akadaiwa Kutenda makosa ya jinai agosti Mwaka 2013 mkoani morogoro. Wakili Kongora aliomba Mahakama hiyo isitishe kusikiliza ombi Hilo la mapitio kwasababu upande wa jamhuri umebadilisha pingamizi la awali Jana AMBAlo wanaoiomba Mahakama hiyo ilifute ombi Hilo la Ponda na kiapo Chake ambacho upande wa jamhuri umebadilisha kiapo kilichoapwa na Hamidu Mbele ya Wakili Kifunda , kiapo hicho hakionyeshi tarehe ya Kuapwa wala hakionyeshi Kuwa mwapaji anamfamu aliyemwapisha kite do ambacho ni kinyume na kifungo Cha 8 Cha Sheria inayosimamia Viapo ya Mwaka 2002. "kwa Kuwa upande wa jamhuri tumebaini dosari hiyo ambayo Kimsingi kiapo ndiyo kitu muhimu kinachobeba ombi la Mwombaji na KWAKUWA kuna dosari hiyo ni wazi kabisa hata Hilo ombi la mapitio ni Kama halipo mahakamani na kwasababu hiyo tunaiomba Mahakama hii ilitupilie Mbali ombi la mapitio pamoja na kiapo hicho kilichotumika kuwasilisha ombi Hilo Kwani kina makosa hayo" alidai Wakili Kongora. Akijibu hoja hizo Wakili wa Ponda, JUMA Nassor aliomba Mahakama itupilie Mbali pingamizi Hilo la awali la DPP kwasababu halina ukweli wowote Kwani ombi la mapitio waliliwasilisha mahakamani hapo Oktoba 10 na Kiapo hicho kiliapwa Oktoba 8 Mwaka huu na kwamba hata Kama ni kweli kiapo hicho walichonacho upande wa jamhuri kinaonyesha Hakina tarehe ,hakifanyi Mahakama kufikia uamuzi wa kulitupa ombi la mteja Wangu "Ponda" . "Kwa mujibu wa ibara ya 107 ya Katiba ya nchi inaitaka Mahakama kuendelea mashauri wa jicho la Haki na siyo jicho la tekinikalitizi...hivyo dai la upande wa jamhuri Kuwa kiapo kina dosari na kwamba walitenda dosari hizo baada ya kusoma rekodi za Mahakama siyo sahihi Kwani upande wa jamhuri Mbona umeshindwa kutoa ushahidi wa risiti ya Mahakama ijayoonyesha ilifanya upekuzi Katika rekodi ya Mahakama?mbona hawajataka ushahidi wa tarehe walipotoa ya upekuzi huo"Alidai Wakili Nassor. JAJI Rose Temba Alisema amesikiliza hoja za pingamizi Hilo la awali na akaairisha shauri Hilo hadi Desemba 11 Mwaka huu, utakapokuja kwaajili ya kutoa uamuzi wa pingamizi Hilo la awali na akaamuru Ponda arudishwe gerezani kwasababu dhamana yake bado imefungwa na DPP. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Desemba 3 Mwaka 2013.

No comments:

Powered by Blogger.