MATUKIO MAKUBWA MAHAKAMANI MWAKA 2013
Na Happiness Katabazi
LEO ndio Jumanne ya mwisho ya mwaka 2013. Kesho panapo majaliwa tunaukaribisha mwaka mpya wa 2014.
Ungana nami mwandishi wa habari za mahakamani wa Gazeti la Tanzania Daima ili uweze kupata mtiririko wa matukio makubwa yaliyotokea mahakamani kuanzia Januari hadi Desemba mwaka huu wa 2013.
DESEMBA 16
HUKUMU YA LIYUMBA JANUARI 15 Mwaka 2014
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,imesema Januari 15 mwaka 201 , itatoa hukumu ya kesi kukutwa na simu gerezani aliyekuwa Mkurugenzi wa utumishi na Utawala wa , Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba .
Hakimu Mkazi Augusta Mbando aliyasema hayo Jana, baada Liyumba kumalizia kutoa utetezi wake. aliomba Mahakama hiyomfutie kesi hiyo na imuachilie huru kwasababu kesi hiyo amebambikiwa.
DESEMBA 11
KORTI KUU YALITUPA OMBI KA SHEIKH PONDA
HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia Mbali ombi la kuomba Mahakama hiyo Ifanyie mapitio lililowasilishwa na katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, sheikh Ponda Issa Ponda kwa Madai Kuwa limekosa thamani katika jicho la sheria.
Uuamuzi huo umetolewa jana asubuhi na Jaji Rose Temba ambapo alianza kwa kuikumbusha mahakama kuwa kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya mahakama hiyo kutoa kutolea uamuzi wa ama ombi hilo likubaliwe au likataliwe kwasababu hatia ya kiapo iliyotumika kuwasilisha maombi hayo ya Ponda yanadosari kwani hayana tarehe inayoonyesha kiapo hicho kiliandaliwa lini.
Jaji Temba Alisema Oktoba Mwaka huu, Mawakili wa Ponda walivyowasilisha ombi Hilo la mapitio tena Kabla jarada Hilo halijapelekwa kwa Msajili wa Mahakama Kuu Wilaya Dar es Salaam kwaajili ya upande wa Ponda na mdaiwa ambaye ni Jamhuri kwaajili ya Msajili kutaka upande wa jamhuri uwasilishe hati kinzani , yeye binafsi alipata fursa ya kuripitia kwa kina jarada la ombi Hilo la alibaini mapungufu hayo Kwenye hati ya kiapo.
"Nilishangaa sana Desemba 2 Mwaka huu, Wakili wa Ponda , Juma Nassoro akipinga Kuwa kiapo hicho lilikuwa Hakina dosari...mimi binafsi nilipitia jarada na kuona rekodi za mahakama katika jarada hilo haziko sahihi na zilirekebishwa kinyemea baadae a kitendo hicho kinahesabika kama ni utovu wa nidhamu na ukiukwaji wa maadili ya uwakili na kwamba Kitendo hicho hakiwezi kuachwa hivi hIvi bali naagiza chombo kinachoshughulika na nidhamu kwa Mawakili nchini kiwachukulie hatua Mawakili wa Ponda na Nassor na Ubaidu Hamidu.
DESEMBA 2
DPP AMWEKEA PINGAMIZU SHEIKH PONDA
Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), Dk.Eliezer Feleshi amemuwekea pingamizi la awali Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda lilokuwa likiomba mahakama hiyo ilifute ombi kuomba mapitio ya uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro ambao ulikataa kumfutia kosa la kwanza la kutenda kosa akiwa chini ya uangalizi wa kifungo cha mwaka mmoja iliyotolewa Mei 9 mwaka huu na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kwasababu hati ya kiapo ina dosari ambazo ni kiapo hakina tarehe.
NOVEMBA 22
10 KIZIMBANI KWA KUMUUA DK.MVUNGI
Watu Kumi wanaodaiwa kumuua Mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya Katiba, Sengondo Mvungi walifikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es salaam, wakikabiliwa na kosa Moja tu la kumuua Dk.Mvungi kwa kukusudia.
Wakili wa serikali Aida Lusumo Mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo aliwataja washitakiwa Hao Kuwa ni chibago Magoze (32),John Kanjunju(29),John Mayunja,Longishu Losingo(29),''Masunga Makunza,Paulo Dondondo(30),mkanda Mlewa(40),zakaria msese(33),msungwa Matonya(30) na Ahmed kilebu(30).
Wakili Lusumo alidai wanashitakiwa kwa kosa la Kua kwa kukusudia kinyume na kifungo Cha 196 Cha Sheria ya kanuni a adhabu ya Mwaka 2002 , Kuwa Novemba 11 Mwaka 2013 huko eneo la msakuzi kino done Dar es salaam, wote kwa pamoja walimuua Dk.Mvungi ambaye alikuwa ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo Dar es salaam na kwamba upelelezi bado haujakamilika.
NOVEMBA 22
BABU SEYA,PAPII KOCHA WANG'ANG'ANIWA TENA
Mahakama ya Rufani nchini iliyoketi Dar es Salaam, imelikataa ombi la kufanya marejeo liliowasilishwa mahakamani hapo na Mwanamuziki wa muziki wa dansi nchini Nguza Vicking ‘Babu Seya’ na mwanae Papi Kocha Mtoto wa Mfalme,ambapo waliomba mahakama hiyo ifanyie marejeo hukumu yake iliyoitoa Februali 2010 ambayo iliyowahukumu kifungo cha maisha warufani hao kwasababu ina dosari za kisheria.
Oktoba 30 Mwaka huu, jopo Hilo la majaji watatu walisikikiza ombi Hilo lililowaomba wafanye Marejeo ya hukumu waliyoitoa Februari Mwaka 2010ambapo wanatetewa na Wakili wa kujitegemea Mabere Marando.
Jaji Natharia Kimaro alisema mahakama yake inalikataa ombi la Babu Seya la kutaka mahakama hiyo ifanye marejeo ya hukumu yake iliyoitoa Februali 2010 ambapo mahakama hiyo ilitupilia mbali rufaa iliyokuwa imekatwa na warufani hao ilioyokuwa ikiomba mahakama hiyo iwafutie adhabu ya kifungo cha maisha jela.Jaji Kimaro alisema Babu Seya ameshindwa kutoa sababu za msingi ambazo zingeweza kuishawishi mahakama hiyo iweze kufanya marejeo ya uamuzi wake ulikwisha utoa Februali Mwaka 2010.
NOVEMBA 11
HASSANOR APANGUA KESI YA KWANZA
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Da es Salaam, ilimwachiria huru Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Soka Mkoa wa Pwani(COREFA), Hassan Othaman Hassan " Hassanoo" na wenzake ambao waliokuwa wakikabiliwa na Kesi ya jinai namba 209/2011 ya wizi wa madini aina ya Kopa yenye Thamani ya sh.milioni 400 kwa maelezo kwa upande wa jamhuri umeshindwa kuthibiisha kesi hiyo.Hata hivyo Hassanoo bado yupo gerezani kwa kesi nyingine ya uhujumu uchumi ambayo tayari ameishawasilisha Mahakama Kuu ombi la dhamana kwasababu kesi ya msingi ipo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama Kuu.
NOVEMBA 8
WACHINA WA KAGASHEKI KIZIMBANI
Raia watatu wa china walifikishwa Katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kosa moja la kukutwa na meno ya tembo vipande 706 yenye thamani ya Sh. Bilioni 5.4
Wakili wa serikali mwandamizi Furaha Nchimbi mbele ya hakimu Mkazi isaya arufani aliwataja Washtakiwa hao ni Huang Gin (50), Xu Fujie (22) na Chen Jinzhan (31) ambao wanatetewa na Wakili wa kujitegemea Edward china. Wakili Nchimbi, alidai kuwa washtakiwa kwa pamoja walikamatwa Novemba 2, mwaka huu katika Mtaa wa Kifaru Mikocheni wakiwa na nyara hizo.
NOVEMBA 7
TISS WALIBARIKI UJENZI JENGO LINALOCHUNGULIA IKULU
ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa majengo nchini (TBA,) Togolai Kimweri anayekabiliwa na mashtaka matano ya matumizi mabaya ya ofisi na mwenzake, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama Taifa (TISS) Rashid Othman, Ikulu waliliridhia kwa maandishi ujenzi wa ghorofa 18 wa jengo linalotazamana na Ikulu.
Kimweri alitoa Maelezo hayo jana mbele ya hakimu Mkazi, Sundi Fimbo wakati alipokukua akiongozwa na Wakili Richard Rweyongeza na Henri Masaba kutoa utetezi wake ambapo alieleza kuwa ni Idara hiyo ya Usalama wa Taifa iliiomba TBA iwapatie ghorofa kwaajili ya ofisi ya TISS.
Kimweri ambaye alidai mashitaka yote Dhidi yake ni ya uongo ,alidai kuwa ujenzi wa jengo hilo ulifuata taratibu zote na kwamba anahisi kushtakiwa kwake kumetokana na kashfa aliyowahi kuipata Waziri John Magufuri iliyowahi kulipotiwa katika vyombo vya habari.Hakimu Fimbo alisema Januari 15 mwaka 2014 atatoa hukumu ya kesi hiyo.
NOVEMBA 7
EKEREGE WA TBS KIZIMBANI
ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Viwango Tanzania (TBS), Charles Ekelege amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu Dar es Salaam, akikabiliwa na makosa miwili likiwemo kosa la matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya dola za Kimarekani 42,543.
OKTOBA 31
KESI YA PAPA MSOFFE BADO MBICHI
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa zaidi ya mara ya tatu sasa imejikuta ikishindwa kutoa uamuzi wake wa ama kumfutia kesi ya mauji au la inayomkabili mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, hapa Abubakar Marijan [50] ‘Papaa Msoffe chuma cha Reli akishiki Kutu, mutu ya Pakee’ na Makongoro Joseph Nyerere, kwa madai kuwa jarada la kesi hiyo limepelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP) kwa hatua zaidi.
OKTOBA 30
MAHAKAMA YAMSIKILIZA BABU SEYA
MWANAMUKIZI wa muziki wa dansi nchini Nguza Vicking ‘Babu Seya’ na mwanae Papi Kocha Mtoto wa Mfalme, wameiomba Mahakama ya Rufaa nchini iifanyie upya hukumu yake iliyoitoa Februali mwaka 2010 ambayo iliwahukumu kifungo cha maisha kwasababu hukumu hiyo ina utelezi wa wazi wa kisheria.
Ombi hilo Na.5/2010 liliwasilishwa kwa niaba yao na wakili wao Mabere Marando jana mbele ya jopo lilelile lilotoa hukumu ya awali ya Februali 2010 ambalo linaongozwa na Jaji Nataria Kimaro, Salum Massati na Mbarouk .S.Mbarouk.
Wakili Marando alidai kwa mujibu wa kanuni ya 66 ya Mahakama ya Rufaa ya mwaka 2009 inatoa mamlaka kwa mahakama ya rufaa kufanya mapitio ya hukumu inazozitoa hivyo wateja wake wamewasilisha ombi hilo la mapitio kwasababu wanaamini mahakama yake ilikosea wazi wazi kisheria katika hukumu yake ya Februali 2010 na kwa mujibu wa kanuni hiyo inatoa mamlaka kwa mahakama hiyo kufanya mapitio ya hukumu yake.
OKTOBA 28
ARCADO NTAGAZWA ASHINDA KESI
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachiria huru waziri wa zamani, Arcado Ntagazwa na wenzake waliokuwa na kesi na kujipatia Mali kwa njia ya udanganyifu zenye thamani ya sh.milioni 74 .9 baada ya kuwaona hawana hatia na hawakutenda kosa Hilo.
OKTOBA 23
UTETEZI KESI YA KIBANDA WAGUNGWA
Mahakama ya hakimu mkazi kisutu Dar es Salaam, imezitaka pande zote mbili katika kesi ya kuandika na kuchapisha Makala a uchochezi inayomkabili aliyekuwa mhariri mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima na wenzake,Absalom Kibanda Ilifungusha utetezi .
OKTOBA 21
WAFUASI WA PONDA WAPUNGUZIWA ADHABU
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetengua adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja jela iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam ,Machi 21 mwaka huu,dhidi ya wafuasi 52 wa Sheikh Ponda Issa Ponda waliotiwa hatiani kwa makosa ya maandamako haramu na kukaidi amri ya Jeshi la Polisi iliyowataka watawanyike kwasababu adhabu hiyo ilitolewa kinyume na sheria husika.
SEPTEMBA 20
SHAHIDI WA MRAMBA AWEKEWA PINGAMIZI
SHAHIDI wa tatu anayemtetea aliyekuwa Waziri wa Fedha,Basil Mramba ambaye ni Naibu Kamishna wa Income Tax , Felisian Busigala (67), alijikuta akishindwa kuendelea kutoa ushahidi wake katika kesi hiyo ya matumuzi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh.bilioni 11.7 inayomkabili Mramba na wenzake kwasababu upande wa jamhuri kumuwekea pingamizi la kwamba hastahili kuwa shahidi katika kesi hiyo kwasababu ushahidi alioanza kuutoa anaonyesha amefika mahakamani hapo kama mtaalamu wa masuala ya kodi na siyo shahidi ambaye anastahili kuzungumzia mashitaka yanayomkabili Mramba.
SEPTEMBA 16
VURUGU ZALINDIMA MAHAKAMA YA KISUTU
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, jana ilikuta ikipata taharuki kufuatia patashika iliyotokea baina ya askari polisi na waliokuwa washitakiwa wanne katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha iliyokuwa ikimkabili Fredy Peter ‘Chege’ na wenzake wanne ambao walikuwa wakipambana na polisi ili waweze kutoka chini ya ulinzi warejee uraini kwasababu mahakama ilikuwa imewaachiria huru.
SEPTEMBA 2
RUFAA YA DPP,MAHALU HAKIELEWEKI
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, jana ilijikuta ikishindwa kaanza kusikilia rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), Dk.Eliezer Feleshi dhidi ya aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia na Grace Martin kwa sababu mwenendo wa kesi hiyo iliyokuwa ikiendeshwa awali katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu haujawekwa kwenye jarada la rufaa ambalo linaanza kutumiwa na Mahakama Kuu kuendeshea rufaa hiyo.
Jaji John Utamwa alisema kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya kaunza kusikilizwa lakini kwa bahati mbaya jarada la rufaa hiyo ndani yake haina rekodi ya kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa ikiwawakabili wajibu rufaa yaani (Mahalu na Grace), ambao
Agosti 9 mwaka jana, walishinda kesi hiyo ya uhujumu uchumi na wizi wa Euro zaidi ya milioni mbili.
AGOSTI 26
NTAGAZWA ALIPONDA JESHI LA POLISI
WAZIRI wa zamani Arcado Ntagazwa ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, analishangaa Jeshi la Polisi na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini kujitwishwa jukumu lisilolao la kuamua kumfungulia kesi ya jinai inayomkabili wakati kisheria kesi hiyo ilipaswa iwe ni ya madai.
Ntagazwa ambaye hivi sasa ni Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na ni msomi wa taaluma ya sheria alieleza hilo jana mbele ya Hakimu Mkazi Gene Dudu wakati akitoa utetezi wake katika kesi ya kujipaia kofia ,fulana zenye jumla ya thamani ya Sh.milioni 74.9 kwa njia ya udanganyifu.
AGOSTI 23
ALEX MASSAWE AFUNGULIWA KESI YA KUGHUSHI
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,imetoa hati ya kukamatwa na kurejeshwa nchini mfanyabiashara maarufu nchini Alex Siliyamala Massawe ili aje kukabiliana na kesi yake mpya ya kughushi nyaraka za umiliki wa ardhi na kutoa taarifa za uongo.
Amri hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Gene Dudu muda mfupi baada ya wakili Mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka kuwasilisha ombi hilo mahakamani na kuiarifu mahakama kuwa upande wa jamhuri umemfungulia kesi Massawe na.150/2013 ya kughushi hati za umiliki wa ardhi na kutoa nyaraka za uongo mahakamani hapo na kumsomea mashashitaka Massawe ambaye anashikiliwa na Askari wa Interpol Dubai bila ya Massawe kuwepo mahakamani hapo .
Hakimu Dudu alisema anakubaliana na ombi hilo la wakili Kweka na kwamba mahakama yake imetoa amri ya kukamatwa kwa Masawe kokote alipo na arejeshwe nchini ili aje akabiliane na kesi yake hiyo mpya iliyofunguliwa mahakamani hapo.
AGOSTI 23
ALIYEGUSHI SAINI YA PINDA KORTINI
MFANYABIASHARA Amadi Ally Popi(35), jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, akikakabiliwa na makosa mawili likiwemo la kughushi barua inayoonyesha imeandikwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Inspekta Said alidai kuwa tarehe na siku isiyofahamika ndani ya jiji la Dar es Salaam, kwa nia ya kudanganya Popi alighushi barua yenye kumbukumbu Na,DA21/3078/01A/142 ya Desemba 3 mwaka 2012 akijaribu kuonyesha kuwa barua hiyo ni halali na ilikuwa imeandikwa na kusainiwa na Waziri Mkuu Pinda.
AGOSTI 22
TRAFIKI 'FEKI' ATINGA KORTINI
TRAFIKI ‘feki’ James Hassan (45) Mkazi wa Kimara alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam, akikabiliwa na makosa mawili likiweko kosa la kujifanya askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani.
Wakili wa Serikali Nassor Katuga mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi,Joyce Minde,alidai kuwa Agosti 14, mwaka huu, eneo la Kinyerezi katika eneo la mnara wa Voda, mshitakiwa kwa njia ya udanganyifu alijitambulisha kwa Inspekta wa Polisi, Gabriel Chiguma, kuwa ni askari wa kikosi cha usalama barabarani.
AGOSTI 19
PONDA AFUTIWA KESI DAR
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, saa moja asubuhi imemfutia kesi mpya ya uchochezi katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Sheikh Ponda Issa Ponda.
Hakimu Mkazi Hellen Liwa alisema amefikia uamuzi huo wa kumfitia kesi Ponda kwasababu wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka kuwasilisha mahakamani hapo hati ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk.Eliezer Feleshi chini ya kifungu cha 91 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 , kwasababu DPP hana haja ya kuendelea kumshitaki Ponda katika kesi hiyo ya jinai na. 144/2013 na hivyo namwachiria huru.
AGOSTI 19
PONDA AFUNGULIWA KESI YA UCHOCHEZI MOROGORO
SHEIKH Ponda Issa Ponda afunguliwa kesi mpya ya makosa ya uchochezi na kutenda kosa wakati yupo chini ya ungalizi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro mbele ya Hakimu Mkazi Richard Kabati.
Alifikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa wanausalama akitokea Dar es Salaam, saa chache asubuhi baada ya kufutiwa kesi na DPP katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kisafirishwa na kuingizwa moja kwa moja katika mahakama hiyo na kusomewa mashitaka hayo na mahakama ikaamuru mshitakiwa huyo awe anaishi katika gereza la Segerea Dar es Salaam na ikakataa kumpatia dhamana kwasababu DPP amefunga dhamana ya Ponda hivyo mahakama yake haina mamlaka tena ya kumpa dhamana.
AGOSTI 19
VIGOGO DECI WAKUTWA NA HATIA
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imewahukumu kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya jumla ya Sh.milioni 21 vigogo wanne wa iliyokuwa kampuni ya Development Entrepreneurship for Community Initiative (DECI) baada ya kuwakuta na hatia ya kutenda makosa kuendesha shughuli za kupokea amana za umma bila leseni.
AGOSTI 15
JELA KWA KUPATIKANA NA URANIUM
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemhukumu kwenda jela Duncan Mwananemela(41) na Silvia Mwemis (42) wahukumu watu wawili kwenda jela miaka mitatu kwa kosa la kukutwa wakilimi madini aina ya Uranium Kg. 6.5 kinyume na sheria.
AGOSTI 14
KIBANDA ANA KESI YA KUJIBU
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemuona aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima,Absalom Kibanda na wenzake wanaokabiliwa na kesi ya kuandika na kuchapisha makala ya uchochezi wana kesi ya kujibu.
AGOSTI 6
ALIYEMTEKA DK.ULIMBOJA AFUTIWA KESI AFUNGULIWA KESI MPYA
MKURUGENZI wa Mashitaka nchini(DPP), Dk.Eliezer Feleshi jana alimfutia kesi ya kujaribu kumuua na kuteka Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini Steven Ulimboka, raia wa Kenya Joshua Mulundi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, baada ya kuona hana haja kuendelea kumshitaki kwa makosa hayo ambayo yalikuwa hayana dhamana.
Hati hiyo ya DPP iliyowasilishwa chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 kwaniaba yake na Wakili Mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka jana mbele ya Hakimu Mkazi Waliarwande Lema ambapo wakili Kweka aliambia mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja kwaajili ya kutajwa lakini upande wa jamhuri hauna nia tena ya kuendelea kumshitaki Mulundi kwa kesi hiyo.
Kwa upande wake Hakimu Waliarwande alikubaliana na hoja hiyo ya wakili Kweka na akamfutia kesi hiyo Mulundi ambaye yupo gerezani tangu Julai 13 mwaka jana hadi sasa kwasababu makosa ya kujaribu kuua na kumteka nyara Dk.Ulimboka hayana dhamana na ni Mahakama Kuu ndiyo ilikuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo ambayo imefutwa jana
Hata hivyo muda mfupi baada ya Hakimu Lema kumfutia kesi hiyo Mulundi, askari kanzu walimkamata tena Mulundi na kisha kumfikisha kwa hakimu mkazi mwingine mahakamani hapo Alocye Katemana na kisha wakili Kweka akaiambia mahakama kuwa upande wa jamhuri umemfungulia kesi mpya mshitakiwa huyo ambayo itakuwa na shitaka moja tu.
Wakili Kweka mbele ya Hakimu Katema alimsomea shitaka hilo mshitakiwa ambapo Julai 3 mwaka jana, katika Kituo cha Polisi Oystebay mshitakiwa huyo alitoa taarifa za uongo kwa ofisa wa polisi ambapo alimweleza ofisa huyo wa polisi yeye na wenzake ambao waliokodiwa kwenda kumteka na kumjeruhi Dk.Ulimboka jana ambalo si kweli kosa ambali ni kinyume na kifungu cha 122 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 na kuongeza kuwa upelelezi wa kesi hiyo mpya umekamilika.
AGOSTI MOSI
PINDA ABURUZWA MAHAKAMANI
KITUO cha Sheria na Utetezi wa Haki za Binadamu(LHRC) na Chama Cha Wanasheria Tanganyika(TLS), jana vilifungua kesi ya Kikatiba katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, vikiomba mahakama hiyo itoe tafsiri za kisheria katika baadhi ya Ibara.
Kesi hiyo ya Kikatiba ambayo imepewa namba 24 ya mwaka huu,na ambayo bado haijapangiwa jaji ambapo wadaiwa ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Taasisi hizo ambazo zinatetewa na mawakili wa kujitegemea Haroud Sungusia , Francis Stolla na wengine 17, na kwa mujibu wa hati yao ya madai ambayo gazeti hili inayo nakala yake , walalamikaji hao wamewasilisha jumla ya maombi mawili ambao wanaomba mahakama itoe tafsiri ya kisheria katika Ibara hizo na kwamba wamewasilisha kesi hiyo ya Kikatiba chini ya sehemu ya Tatu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo inaainisha Haki na Wajibu Muhimu.
JULAI 29
HAKIMU PAMELA KALALA ASHINDA KESI
HAKIMU Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam,imemwachia huru Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala ,Pamela Kalala, aliyekuwa akikabiliwa na makosa mawili ya kuomba na kupokea rushwa ya Sh. 900,000 baada ya kuomba hana kesi ya kujibu.
JULAI 24
WANNE WAONGEZWA KESI YA CHEMUNDUGWAO
HATIMAYE Wahudumu wa wawili wa Idara ya Uhamiaji jana walifikishwa kalifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, nakuunganishwa katika kesi ya wizi wa Paspoti 26 inayomkabili Mwanamuziki wa muziki wa Asili nchini, Chingwele Che Mundugwao na wenzake ambapo hadi kufikia jana kesi hiyo imefanya kuwa na jumla ya washitakiwa tisa akiwemo raia mmoja wa Uingereza.
JULAI 21
OFISA JKT KIZIMBANI KWA PEMBE ZA NDOVU
OFISA uvuvi wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Suleiman Isanzu Chesana na anayekabiliwa na kesi ya kukutwa na meno ya Tembo yenye thamani ya Sh.bilioni nne, jana tena kwa mara nyingine amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam akikabiliwa na kesi nyingine ya kukutwa na meno ya teambo Kg.781 yenye thamani ya Sh.bilioni 9.3.
JUNI 19
IDD SIMBA AFUTIWA KESI YA UHUJUMU UCHUMI
HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemwachiria huru Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la UDA,Idd Simba, na wenzake watatu waliokuwa wakikabiliwa na makosa mbalimbali likiwemo kosa la uhujumu uchumi kwa maelezo kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk.Eliezer Feleshi amewasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea kuwashitaki.
JUNI 20
ALIYEJIFANYA MWANDISHI WA HABARI JELA MIAKA MITATU
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam, imemhukumu kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya Sh.500,000 Msambazaji wa Gazeti la Mtandao,Salum Hassan Goko baada ya kumkuta na hatia ya kujifanya Mwandishi wa habari wa gazeti hilo na kuomba na kupokea rushwa ya Sh.200,000 kutoka kwa Meneja wa Kampuni ya Vinywaji Baridi aina ya Pepsi, Rashid Chenja.
JUNI 11
LWAKATARE NJE KWA DHAMANA
HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imempatia dhamana Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare na mwenzake Joseph Ludovick wanaokabiliwa na kosa moja la kula njama utaka kumdhuru kwa sumu Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Denis Msacky.
Hakimu Mkazi wa Mahakama Alocye Katemana alitoa uamuzi wa kumpatia dhamana Lwakatare na wenzake jana saa mbili asubuhi ambapo alisema jana kesi hiyo ilikuja kwaajili ya yeye kutolea uamuzi maombi ya dhamana na mapingamizi ya dhamana yaliyowasilishwa mahakamani hapo Mei 13 mwaka huu, na wakili wa washitakiwa hao Peter Kibatara na wakili wa jamhuri Prudence Rweyongeza na Ponsia Lukosi ambapo mawakili wa jamhuri waliomba mahakama isimpatie dhamana.
JUNI 3
CHEMUNDUGWAO KORTINI JWA WIZI WA PASPOTI 26
MSANII wa muziki nchini, Chigwele Che Mundugwao 46, ofisa Manunuzi wa Idara ya Uhamiaji, Shemweta Kilwasha (31), Mhandisi wa Idara ya Zimamoto na Ukoaji, Keneth Pius 37 na mfanyabiashara, Ally Jabir ( 34) jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, wakikabiliwa na jumla ya mashitaka manne likiwemo kosa la wizi wa jumla ya Pasipoti 26.Na hadi leo wapo gerezani kwasababu DPP amewafungia dhamana.
MEI 31
MAHAKAMA YA RUFAA YATENGUA HUKUMU YAKE
HATIMAYE jopo la majaji watano wa Mahakama ya Rufaa nchini limetungua hukumu iliyotolewa na jopo la majaji watatu wa mahakama mwaka 2011 ambayo ilikuwa ikimtaka mtu yoyote anayepinga ubunge wa mbunge aliyepo madarakani kuwasilisha kwanza mahakamani ombi la kuomba mahakama impangie kiwango cha kulipa dhamana ya kufungua kesi za uchaguzi ngazi ya ubunge.
Uamuzi huo wa ambao imeandika historia mpya katika tasnia ya sheria ya nchini, ulitolewa jana mchana na jopo la majaji watano wa Mahakama ya Rufaa Dar es Salaam, Januaria Msofe, William Mandia, Salum Massati, Angela Kileo, Nataria Kimaro ambao walisema wamekubaliana na hoja za wakili wa kujitegemea Herbet Nyange ambaye aliomba mahakama itoe tafsiri ya kifungu cha 111 cha Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2010, kinachomtaka anayefungua kesi ya uchaguzi ya kupinga matokeo ya ubunge, kwanza alazimike kuwasilisha ombi mahakamani la kuomba mahakama impangie kiasi cha kulipa dhamana kabla ya kesi ya msingi kuanza kusikilizwa.
Jaji Msofe alisema jopo lake lilisikiliza hoja za wakili Nyange kuhusu kuomba tafsiri ya kifungu hicho na kuipitia hukumu iliyotolewa mwaka 2011 na jopo la majaji watatu wa mahakama hii, alisema wamekubaliana na hoja wakili Nyange ya kwamba ni kweli uamuzi wa rufaa ile ya jopo la majaji wa tatu ulikuwa na makosa.
“Kwa sababu hiyo jopo hili la majaji watano leo linatangaza kuwa limetengua uamuzi wa majaji wenzetu wa tatu ambayo ulikuwa unamtaka mtu yoyote anayewasilisha ombi la kupinga ubunge wa mbunge kuwasilisha kwanza ombi la kuomba pangiwe kiwango cha kulipa dhamana ya kuendesha kesi yake ya kupinga ubunge;
“Hivyo jopo letu linatamka kuwa kuanzia sasa mtu yoyote anayeta kufungua kesi ya kupinga ubunge hatalazimika tena kuanza kuwasilisha ombi mahakamani la kuomba apangiwe kiasi cha kulipa hivyo badala yake jopo hili linatoa ruhusa kwa mtu mwenye uwezo wa kifedha wa kulipa dhamana ya kufungua kesi ya kupinga kesi afungue kesi ya kupinga ushindi wa ubunge moja kwa moja na kwa yule mtu ambaye hana huwezo wa kifedha wa kuweka dhamana ya fedha mahakamani kama anavyoakiwa na sheria ya uchaguzi kulipa kwanza Sh.milioni tano, basi mtu huyo awasilishe ombi mahakamani la kuomba apunguziwe kiasi hicho cha fedha kwaajili ya dhamana ya kesi”alisema Jaji Msofe.
Aidha jaji huyo alisema baada ya mahakama yake kutoa uamuzi huo jana , mahakama yake imesema itaanza kusikiliza rufaa iliyokatwa na Chiriko dhidi ya Lugora katika tarehe ambayo itakuwa imepangwa na uongozi wa mahakama ya rufaa.
Wakili Nyange ambaye anamtetea mwomba rufaa katika rufaa ya ubunge wa jimbo la Mwibara, Chiriko Haruni Davidi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) dhidi ya Mbunge wa Mwibara Bunda, Mkoani Mara, Kangi Lugora, wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo Chiriko anapinga ubunge wa Lugora anatetewa na wakili Melkizedeck Lutema na Mwanasheria Mkuu wa Serikali anayetetewa na wakili wa serikali Wakili wa Serikali Mkuu, Obadia Kameya akimwakilisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali alioupata mwaka 2010 kuwa ushindi wake ulikuwa umekiuka sheria ya uchaguzi.
MEI 29
MWAKALEBELA AIBWAGA TENA TAKUKURU
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Iringa imetupilia mbali rufaa iliyokuwa imekatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa dhidi ya aliyekuwa mgombea ubunge wa Iringa Mjini(CCM), Fredrick Mwakalebe na mkewe Celina iliyokuwa ikipinga uamuzi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa ambayo ilifuta kesi hiyo hiyo ya madai ya kushawishi na kutoa ruhwa kwa sababu hati ya mashitaka ilikuwa na mapungufu.
Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Mkuya ambaye alisema rufaa hiyo iliwasilishwa mahakamani hapo na PCCB na wakili wa Mwakalebela, Alex Mgongolwa aliwasilisha pingamizi la awali ambalo liliomba mahakama hiyo iifute rufaa hiyo kwasababu hati hiyo ya rufaa ilikuwa haijaambatishwa na nakala ya uamuzi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa ambayo iliwafutia kesi hiyo wajibu rufaa kwa sababu hati ya mashitaka ilikuwa na dosari
MEI 23
JOSEPHINE MUSHUMBUSI SI MKE WA MAIMBO
HATIMAYE Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, imetupilia mbali rufaa iliyokuwa imekatwa na aliyekuwa mume wa Josephine Mushumbusi, Maimbo baada ya kuiona rufaa hiyo haina msingi wowote kisheria.
MEI 9
PONDA AFUNGWA MWAKA MMOJA NJE
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemhukumu kifungo cha nje cha mwaka mmoja Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Sheikh Ponda Issa Ponda aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya uchochezi na wizi wa malighafi zenye thamani ya Sh.milioni 59 baada ya kumkuta na hatia katika kosa moja la kuingia kwa jinai katika kiwanja cha Chang’ombe Markazi.
Sambamba na hilo, mahakama hiyo imewaachiria huru washitakiwa wengine 49 baada ya kuwaona hawana hatia katika makosa matano yote waliyokuwa wakishitakiwa nao kwasababu upande wa jamhuri umeshindwa kuleta ushahidi wa kuishawishi mahakama iwaone wanahatia na kwamba akasema upelelezi uliofanywa na jeshi la polisi katika kesi hiyo ni dhahifu na kwamba mahakama haiwezi kumfunga mtu kwa ushahidi wa hisia tu.
MEI 8
RUFAA YA DPP,ZOMBE YAFUTWA
MAHAKAMA ya Rufaa nchini, jana iliifuta rufaa iliyokuwa imekatwa na Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), Dk.Eliezer Feleshi ya kupinga hukumu ya kesi ya mauji ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliyomwachiria huru aliyekuwa Mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Dar es Salaam(ACP)-Abdallah Zombe na wenzake baada ya kubaini kuwepo kwa dosari katika hati ya kukatia rufaa hiyo.
MEI 8
LWAKATARE AFUTIWA MAKOSA YA UGAIDI
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemfutia jumla ya makosa matatu ya tuhuma ugaidi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Wilfred Lwakatare ambaye alikuwa akikabiliwa na jumla ya makosa manne ya tuhuma za ugaidi.
MEI 17
DPP ASHINDA RUFAA YA KESI YA RICHMOND
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeufuta uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Saalam, uliomuona Mkurugenzi wa kampuni ya Richmond Ltd, Naeem Adam Gire aliyekuwa akikabiliwa na makosa ya kughushi,kuwasilisha nyaraka za uongo na kutoa taarifa za uongo kwa maofisa wa umma kuwa wana kesi ya kujibu.
MEI 24
RAMA 'MLA WATU'AFUTIWA KESI YA MAUAJI
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemwachiria huru mtoto Ramadhamani Selemani Mussa, maarufu kama ‘Rama mla kichwa’,na mama yake mzazi Hadija Ally waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya mauji.
Rama na mama yake walikuwa wakikabiliwa na kosa la kuua kwa kukusudia mtoto Salome Yohana (3), kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) ya mwaka 2002.
APRILI 22
GODBLESS LEMA AIBWAGA CCM
Dar es Salaam. Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ameibuka kidedea baada ya Mahakama ya Rufani iliyoketi jijini Dar es Salaam, kutupilia mbali maombi ya marejeo ya rufaa iliyomrejesha bungeni.
APRILI 22
DOSARI ZA KWAMISHA RUFAA YA DPP,ZOMBE
MAHAKAMA ya Rufaa nchini, jana ilijikuta ikishindwa kuanza kusikiliza rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP)-Dk.Eliezer Feleshi dhidi ya Aliyekuwa Mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Dar es Salaam(ACP)-Abdallah Zombe na wenzake baada ya mahakama hiyo kubaini dosari katika hati ya kukata rufaa.
Rufaa hiyo Na.254/2009 inayosikilizwa na jopo la majaji watatu Edward Rutakangwa,Mbarouk Mbarouk na Bethek aMila, ambayo jana ilikuja kwaajili ya kuanza kusikilizwa kwa siku mbili mfululizo , jaji Mbarouk kabla ya kuanza kusikiliza hoja za rufaa hiyo aliutaka upande wa mwomba rufaa(DPP), wameiweke sawa mahakama kuwa katika hati ya kukata rufaa ya ya kupinga hukumu ya mahakama kuu ya kesi ya mauji Na.26/2006 ya Zombe na wenzake inasomeka kuwa hukumu ya mahakama kuu iliyotolewa na Jaji wa mahakama ya rufaa Salum Massati.
APRILI 9
WALIOFANYA VURUGU KITUO CHA POLISI KAWE KIZIMBANI
WATU 12 walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kwa makosa nane yakiwemo makosa ya kuaribu vioo vya magari ambavyo ni vielelezo na kuwajeruhi kwa mawe askari polisi wa Kituo cha Polisi Kawe. walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kwa makosa nane yakiwemo makosa ya kuaribu vioo vya magari ambavyo ni vielelezo na kuwajeruhi kwa mawe askari polisi wa Kituo cha Polisi Kawe.
APRILIAPRILI 3
SHEIKH PONDA ANA HATIA-JAMHURI
UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya uchochezi na wizi wa malighafi ya Sh.milioni 59 inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Sheikh Ponda Issa Ponda wenzake 49 umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, iwaone wanatia kwa mujibu wa kesi inayowakabili na iwahukumu kwa mujibu wa sheria.
APRILIAPRILI 15
LWAKATARE ASIKILIZWA MAFICHONI
OMBI la Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare, la kuiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kuifuta kesi inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jana lilisikilizwa mafichoni, hivyo kuibua malalamiko makubwa kwa wafuatiliaji.
Kesi hiyo ambayo inafualitiliwa na wananchi wengi, iliendeshwa katika chemba ya Jaji Lawrence Kaduri, hatua iliyowafanya hata waandishi wa habari za mahakamani kuzuiwa na askari wa Jeshi la Magereza kuingia ndani ya chumba hicho kidogo.
Badala yake waandishi hao walilazimika kufanya juhudi za ziada kuwashawishi askari hao ili angalau wamruhusu mmoja wao, Faustine Kapama, aingie ndani asikilize halafu baadaye awasimulie, ombi ambalo hatimaye lilikubaliwa, hivyo wengine zaidi ya 15 kubaki nje.
APRILI 3
11 KIZIMBANI KWA KUUA BILA KUKUSUDIA
HATIMAYE Mfanyabiashara Razah Hussein Razah na wenzake 10 jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, wakikabiliwa na jumla ya makosa 24 ya kuua bila kukusudia.
Itakumbukwa kuwa Machi 29 mwaka huu, ghorofa mmoja lililokuwa linajengwa katika mtaa wa Indragand lilianguka na kusababisha watu idadi hiyo ya watu 24 kupoteza maisha.
MACHI 25
ANAYEDAIWA KUMUUA TRAFIKI KORTINI
ANAYEDAIWA kumuua askari wa kikosi cha Usalama Barabarani wiki iliyopita, Elikiza Nnko, Jakson Stephen Fimbo jana alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na makosa ya matatu likiwemo kosa la kuingilia msafara wa kiongozi.
Mbele ya Hakimu Mkazi Kwey Lusema wakili mwandamizi wa serikali Lasdilaus Komanya alilitaja kosa la kwanza ni la kusababisha kifo cha trafiki huyo kupitia kwendesha gari kwa hatari na kwamba Machi 18 mwaka huu, katika barabara ya Bagamoyo katika mataa ya Bamaga jijini Dar es Salaam, mshitakiwa akiwa ni dereva kiongozi wa gari lenye namba za usajili T328 BML aina ya Land Lover Discovery.
MACHI 21
WAFUASI 53 WA SHEIKH PONDA JELA MWAKA MMOJA
HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imewahukumu kwenda jela mwaka mmoja wafuasi 53 wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Sheikh Issa Ponda waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya kula njama na kufanya maandamano haramu.
MACHI 21
LWAKATARE AFUTIWA KESI YA UGAIDI,AFUNGULIWA TENA KESI YA UGAIDI
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,ilimfutia kesi ya makosa ya ugaidi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare na Ludovick Joseph kwa sababu ya Mkurugenzi wa Mashitaka( DPP), Dk.Eliezer Feleshi kuwasilisha hati ya kuwafitia kesi hiyo washitakiwa kwa sababu hana haja ya kuendelea nayo.
Sambamba na hilo, DPP ilimfungulia kesi ya makosa ya ugaidi upya Lwakatare na mwenzake ambapo kesi hiyo mpya namba Na.6/2013 ambapo imepangiwa kwa hakimu mpya Aloyce Katemana.
MACHI 25
KAJALA ATIWA HATIANI,WEMA SEPETU AMLIPIA FIDIA YA SH.ML.13
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imewahukumu kwenda jela miaka nane au kulipa faini ya Sh.milioni 13 msainii wa Filamu nchini, baada ya kumtia hatiani katika makosa ya kula njama kuamisha umiliki wa nyumba, na kuamisha umiliki wa nyumba iliyokuwa iliyokuwa imezuiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali isiuzwe.
MACHI 18
LWAKATARE WA CHADEMA KORTINI KWA UGAIDI
Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, Dk.Eliezer Feleshi amemfikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema),Wilfred Lwakatare na mwenzake kwa makosa ya ugaidi.wakatare wa Chadema kortini kwa Ugaidi.
MACHI 13
ASKARI POLISI KORINI KWA WIZI WA SH.ML.150
HATIMAYE waliokuwa askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam,watano jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kosa la wizi wa Sh. Milioni 150 mali ya Mire Artan Ismail.ari Polisi kortini.
MACHI 4
MAHAKAMA YAMNG'ANG'ANIA SHEIKH PONDA
HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemuona Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49 wana kesi ya kujibu.
FEBRUALI 12
ALIYEMWIBIA RAIS MWINYI JELA MIAKA MITATU
HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemuhukumu adhabu ya kifungo cha jumla ya miaka jela , Abdallah Mzombe (39) baada ya kumkuta na hatia ya makosa ya wizi sh. Milioni 37.4 mali ya rais Mstaafu Alli Hassan Mwinyi Sh 37.4 milioni.
JANUARI 29
LULU NJE KWA DHAMANA
HATIMAYE msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amepata dhamana baaada ya kutimiza masharti matano aliyopewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, juzi wakati mahakama hiyo ilipokuja kusikiliza ombi lake la kuomba apatiwe dhamana katika kesi inayomkabili ya kuua bila kukusudia aliyekuwa msainii mwenzie Steven Kanumba.
JANUARI 16
WEREMA APIGANIA UBUNGE WA AESHI
HATIMAYE Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG)nchini,Jaji Fredrick Werema amewasilisha sababu 10 katika Mahakama ya Rufani nchini akiomba mahakama hiyo itengue hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga ambayo Aprili mwaka jana ilimvua ubunge, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini(CCM), Aeshi Hillary kwasababu hukumu ile ilikuwa na dosari za kisheria.
www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Chanzo:Gazeti la Tanzanja Daima la Jumanne,Desemba 31 Mwaka 2013
No comments:
Post a Comment