Header Ads

MAHAKAMA YATUPA OMBI LA SHEIKH PONDA

Na Happiness Katabazi
HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali ombi la kuomba Mahakama hiyo ifanyie mapitio lililowasilishwa  na Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda kwa madai kuwa limekosa thamani katika jicho la sheria.

Uuamuzi huo umetolewa jana asubuhi na Jaji Rose Temba ambapo alianza kwa kuikumbusha mahakama kuwa kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya mahakama hiyo kutoa kutolea uamuzi wa ama ombi hilo likubaliwe au likataliwe kwasababu hatia ya kiapo iliyotumika kuwasilisha maombi hayo ya Ponda yanadosari kwani hayana tarehe inayoonyesha kiapo hicho kiliandaliwa lini.

Jaji  Temba alisema alisema Oktoba Mwaka huu, Mawakili wa Ponda walivyowasilisha ombi Hilo la mapitio tena Kabla jarada Hilo halijapelekwa kwa Msajili wa Mahakama Kuu Wilaya Dar es Salaam kwaajili ya upande wa Ponda na mdaiwa ambaye ni Jamhuri  kwaajili ya Msajili kutaka upande wa jamhuri uwasilishe hati kinzani , yeye  binafsi alipata  fursa ya kuripitia kwa kina jarada la ombi Hilo la alibaini mapung hayo Kwenye hati ya kiapo.

"Nilishangaa sana Desemba 2 Mwaka huu, Wakili wa Ponda , Juma Nassoro akipinga Kuwa kiapo hicho lilikuwa Hakina dosari...mimi binafsi nilipitia jarada na kuona rekodi za mahakama katika jarada hilo haziko sahihi  na zilirekebishwa  kinyemea baadae a kitendo hicho kinahesabika kama n utovu wa nidhamu na ukiukwaji wa maadili ya Uwakili na kwamba Kitendo  hicho hakiwezi kuachwa hivi hivi na ninaagiza vyombo vinavyoshughulika na nidhamu kwa Mawakili nchini kiwachukulie hatua Mawakili wa Ponda na Nassor na Ubaidu Hamidu.

Akizungumzia hoja kiapo Kuwa kinadosari , JAJI Temba Alisema anakubaliana na pingamizi la awali la upande wa jamhuri lililowasilishwa mahakamani hapo Desemba 2 Mwaka huu na Wakili kiongozi wa serikali Bernad Kongora  AMBAPO ni kweli Mahakama yake  imebaini  Kuwa kiapo kile Hakina tarehe na baadae kilifanyiwa marekebisho kinyumela.

"Kwa kuwa hati ya kiapo na dosari hiyo ya kutokuwa na tarehe ,Mahakama hii pia inakubaliana na Wakili wa Jamhuri Kongola kuwa ombi la mapitio nalo limekosa thamani katika jicho la sheria  na  kwa maana hiyo Mahakama yake inakubaliana na pingamizi la awali la upande wa jamhuri kuwa kiapo kinamapungufu na kwasababu hiyo pia inatupilia mbali ombi la Ponda lilikuwa linaomba Mahakama ifanyie mapitio uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.

Desemba 2 mwaka huu, Kongora aliwasilisha pingamizi la awali aliomba Mahakama hiyo itupilie Mbali ombi ilo la Ponda kwasababu hati ya kiapo ina dosari.

Oktoba Mwaka huu, Ponda aliwasilisha  ombi la mapitio ya uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro HIvi karibuni alitoa uamuzi wakukataa kumfutia kosa la kwanza la Kutenda kosa la uchochezi wakati yupo ndani ya kifungo Cha Mwaka mmoja  nje ambacho kilimtaka asitende makosa na awe raia Mwema lakini  Akadaiwa Kutenda makosa ya jinai  agosti Mwaka 2013 mkoani morogoro.

Wakili Kongora aliomba Mahakama hiyo isitishe kusikiliza ombi Hilo la mapitio kwasababu upande wa jamhuri umebadilisha pingamizi la awali Jana AMBAlo wanaoiomba Mahakama hiyo ilifute ombi Hilo la Ponda na kiapo Chake ambacho upande wa jamhuri umebadilisha kiapo kilichoapwa na Hamidu Mbele ya Wakili Kifunda , kiapo hicho hakionyeshi tarehe ya Kuapwa wala hakionyeshi Kuwa mwapaji anamfamu aliyemwapisha kite do ambacho ni kinyume na kifungo Cha 8 Cha Sheria inayosimamia Viapo ya Mwaka 2002.

Akijibu hoja hizo Wakili wa Ponda, JUMA Nassor aliomba Mahakama itupilie Mbali pingamizi Hilo la awali la DPP kwasababu halina ukweli wowote Kwani ombi la mapitio waliliwasilisha mahakamani hapo Oktoba 10 na Kiapo hicho kiliapwa Oktoba 8 Mwaka huu na kwamba hata Kama ni kweli kiapo hicho walichonacho upande wa jamhuri kinaonyesha Hakina tarehe ,hakifanyi Mahakama kufikia uamuzi wa kulitupa ombi la mteja Wangu "Ponda" .


Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Desemba 12 mwaka 2013.

No comments:

Powered by Blogger.