Header Ads

KESI YA KUPINGA UCHAGUZI TIMU YA SIMBA YATUPWA





KESI YA KUPINGA UCHAGUZI SIMBA YATUPWA
Na Happiness Katabazi
HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam, imekataa kutoa amri ya Muda ya Kuzuia kufanyika kwa uchaguzi Mkuu wa Simba ulipangwa kufanyika Kesho ,kwasababu Maombi hayo  ya zuio yaliyowalishwa jumahtatu wiki hii na wanachama watatu wa simba, hayapo mAhakamani hapo kisheria.

Uamuzi huo uliokuwa ukisubiriwa kwa shahuku kubwa na wapenzi wa Soko nchini, uliotolewa Jana saa Kumi jioni Na Jaji Augustine Mwarija  ambaye Alisema amesikiliza hoja za pande zote mbili tangu Jana asubuhi na kwamba Mahakama yake imejiridhisha pasiposhaka Kuwa ombi Hilo la zuio halipo mahakamani kisheria hivyo Mahakama yake haiwezi kutolea uamuzi ombi lolote ambalo halipo mahakamani kisheria.

Jaji Mwarija Alisema licha la ombi Hilo la zuio kutokuwepo mahakamani kisheria pia ombi Hilo la zuio Kabla ya wakati  na kwamba kisheria huweZi kuleta ombi la zuio la MUDa wakati Hakuna Kesi ya Msingi ilipofunguliwa mahakamani na kwamba kwa shauri Hilo la wanachama Hao wa simba , bado hawajafungua Kesi ya Msingi ila wamewasilisha ombi la kuomba Mahakama Iwapo Kibali Cha kuwaunganisha wanachama wengine 66 ili nao wawe walalamikaji Katika Kesi ya Msingi ya kumshitaki Mwenyekiti wa simba KWA kuvunja Katika na kwamba hadi Jana asubuhi ombi Hilo la kuomba wanachama Hao kuunganishwa lilikuwa halijasikilizwa.

" Sasa Kwa Kuwa katika Mahakama hii wanachama Hao watatu walikuwa bado hawajafungua Kesi ya Msingi Mahakama hii haiwezi kukubali kutolea maamuzi Maombi Yao ya zuio la MUDa kwasababu kisheria huwezi kutoa amri ya zuio la Muda bila ya kuwepo Kesi ya Msingi mahakamani na hata hivyo ombi hili la zuio la Muda limewasilishwa Kabla ya wakati na kwasababu hiyo Mahakama hii inayatupilia Mbali Maombi ya zuio la MUDa"Alisema Jaji Mwarija.

hata hivyo uamuzi huo ilisababisha wanawake Wawili wanaodaiwa Kuwa ni wanachama wa simba ,walizirai mahakamani hapo na Kisha Kubebwa na kuingizwa Kwenye Gari na kuondolewa Katika eneo Hilo la Mahakama.

Akizungumzia uamuzi huo wa Mahakama, Wakili wa wadaiwa , Juma Nassor Alisema amesikitishwa na uamuzi huo Kwani haulengi kuleta umoja na Amani Katika TIMU ya simba.

Kabla ya Maombi ya zuio la Muda kuanza kusikilizwa Jana ,  Jaji Mwarija alianza kusikiliza ombi  la Mwanachama mmoja wa Simba, Shaban Omar ambaye alikuwa akitetewa na Wakili Jerome Msemwa  lilokuwa liloomba Mwanachama Huyo aunganishwe na awe miongoni mwa wadaiwa katika Kesi hiyo lakini hata hivyo Jaji Mwarija Jana muda mwingi alilazimika Kuwafundisha matakwa ya Sheria yanasemaje na alimwambia Msemwa ombi Hilo la Mteja wake limeletwa wakati siyo mwafaka, ushauri ambao baadae Wakili Msemwa alikubaliana na ushauri wa jaji Huyo na Akaamua kuliko ndoa ombi hilo.

Ombi la Kuzuia uchaguzi kilianzia kusikilizwa Jana saa nne asubuhi,  Wakili wa walalamikaji Revocatus Kuuli alianza kwa kuiambia Mahakama Kuwa wamewasilisha Maombi mawili ,ombi la kwanza la kuomba uchaguzi wa simba usimamishwe na ombi la pili wanaomba wapatiwe Kibali Cha wanachama wengine kuunganishwa Katika Kesi Yao ya Msingi itakayofunguliwa baada ya kupata Kibali hicho.

" Lakini Leo asubuhi, Wakili wa wadaiwa amewasilisha kiapo akiniambia wateja wake ambao ni wadaiwa Kuwa wamekuwa liana na Maombi yetu yote hayo na kwasababu hiyo basi tunaimba Mahakama itoe amri yake" Alidai Wakili Kuuli.

Wakili wa walalamikaji, Revocatus Kuuli alidai Kuwa anaomba 
 asubuhi wakili anaye mtetea Mwenyekiti wa Timu a Simba, Ismail Aden Rage na Bodi ya wadhamini wa timu hiyo, Juma Nassor , aliliieleza mahakama kuwa baada ya wakili wa walalamikaji Revocatus Kuuli, kuwapatia nakala ya madai yao, upande wa wadaiwa wamekubaliana na madai ya walalamikaji kuwa madai yao mawili yaliyoomba mahakama hiyo itoe amri ya muda ya kuzuia uchaguzi mkuu wa timu hiyo uliopamgwa kufanyika kesho na ombi la pili liloomba mahakama hiyo iwapatie Kibali Cha kuruhusu wanachama wengine waunganishwe Kama walalamikaji Katika Kesi ya Msingi itakayofunguliwa mahakamani halo mara baada ya kupata kibali ha mahakama.

Wakili Nassor alieleza Kuwa Sababu hiyo mmoja wa wadaiwa Katika Kesi hiyo Hamis Kilomoni kwaniaba ya wadaiwa wote amewasilisha Maombi hayo chini ya kiapo ambayo wadaiwa na wapingani na Maombi ya walalamikaji anaomba Kuzuiwa KWA uchaguzi Mkuu, Kwani ni wazi Kesi hiyo ilipofunguliwa na wanachama watatu Wa simba imenyesha picha Msingi wake ni mtafaruku uliotokana baada ya baadhi ya wagombea wanafasi Mbalimbali Katika uchaguzi huo, waliondolewa Kuwa wagombea na Kamati ya Uchaguzi ya Simba.

"Mtukufu Jaji Lengo letu sisi wadaiwa ni kwamba Tunataka kuona Amani, umoja, mshikamano uimalike ndani ya Simba, uchaguzi huu usiwe Chanzo Cha kuleta VURUGU, mpasuko ndani ya Simba...hivyo sisi wadaiwa tunaomba wale wagombea ambao waliondolewa katika uchaguzi Kwa Sababu mbalimbali , nak waruhusiwe Kugombea  ili Amani na utulivu na umoja uwepo Kwenye klabu ya simba na kwamba tumekubaliama Kesi hii twende tukamalize nje ya Mahakama" Alidai Wakili Nassor.

Wakili Nassor aliomba Mahakama Kifungu Cha 9 Cha Sheria ya Mashauri ya Madai ya Mwaka 2002, kuondoa Kesi hiyo jambo ambalo Jaji Mwarija alisema Wakili Nassor.

Ilipofika saa tano, Jaji Mwarija aliarisha Kesi hiyo hadi saa 7:30 mchana ili aje atoe maamuzi ya ama Kuzuia uchaguzi wa simba au laa.

Ilipofika Muda huo, Mawakili Hao wa pande mbili waliambia Mahakama Kuwa Kesi ilipoarishwa walikuwa na wakakubaliana maridhiano wa Lengo la kuamasisha umoja ndani ya simba hivyo Wakili Kuuli akaomba Mahakama itoe amri ya kuliandoa shauri Hilo mahakamani ili waende kujimaliza nje ya Mahakama.

kitendo ambacho Mara kwa  Mara kilifanya Jaji Mwarija Kuwauliza Mawakili wa pande zote mbili Kuwa hayo maridhiano Yao wameyawasilisha chini ya Kifungu gani Cha Sheria Kwani kilichopo mahakamani hakionyeshi Kama pande hizo mbili zimelidhiana na kwamba kuna Sita za wagombea na kwamba tarehe ya uchaguzi isogezwe Mbele wala wagombea Waliondolewa Kwenye uchaguzi waruhusiwe Kugombea.

" Hii ni mahakama na Mahakama inatakiwa itoe amri kutokana na Maombi yaliyowasilishwa Mbele yake KWA mujibu wa Sheria husika, sasa Maharishi tena shauri hili hadi saa 10 jioni  ili niwape MUDa Nyie Mawakili wa pande zote mbili Muende kuweka hayo maelezo yenu mapya Katika hati yenu ya maridhiano Kisha tukirejea saa Kumi jioni nitakuja kutoa uamuzi ambao ni wa kisheria " Alisema JAJI Mwarija.

Juni 23 mwaka huu, wananchama Hao watatu kupitia Wakili wao Kuuli walifungua   mahakamani hapo Maombi hayo madogo, Na.291/2014  Josephat Waryoba, Said Lly Monero na Hassan Hassan, ambao wanamshitaki Rais wa Timu ya Simba, Ismail Aden Rage na Bodi ya Udhamini ya Timu  hiyo.

Kwa mujibu wa hati hiyo inayonyesha walalamikaji wana jumla ya Madai matatu ambayo dai la kwanza wakiomba Mahakama hiyo itoe amri ya kuwazuia wadaiwa kuitisha uchaguzi Mkuu uliofangwa kufanyika Kesho.

CHANZO: Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Juni 28 Mwaka 2014.



No comments:

Powered by Blogger.