MABOSS IMTU KIZIMBANI. DPP AWAFUTIA KESI,WAKAMATWA TENA
MABOSS IMTU KIZIMBANI,DPP AWAFUTIWA KESI,WAKAMATWA TENA
Na Happiness Katabazi
WAHADHIRI wanne wa Chuo Kikuu Cha Tiba Cha
IMTU ,Mbezi Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni wakikabiliwa na makosa mawili likiwemo kosa la la kushindwa
Kufukia viroba 83 vya viungo Vya binadamu.
Mwendesha Mashitaka Mwandamizi wa Polisi Magoma Mtani Mbele ya Hakimu Kwey Rusemwa aliwataja washitakiwa Hao Kuwa ni aliwataja washitakiwa Hao Kuwa ni Venkat
Subbaiah(57), Appm Shankar Rao (64), Prabhakar Rai(69), Dinesh
Kumar(27).
Magoma alidai kuwa washtakiwa hao Julai 2014 katika eneo la Mpigi
Majohe walishindwa kufukia viroba 83 vya viungo vya binadamu
waliyoitumia kufundishia wanafunzi wa udaktari kinyume na kifungu cha
128 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Mwaka 2002.
Alidai kuwa washtakiwa hao kwa pamoja pia walishindwa kuandaa hati
kwa kampuni ya Corona ya kuthibitisha kufukiwa kwa mabaki hayo na washitakiwa walikana Mashitaka hayo na upande wa jamhuri ukadai upelelezi bado haujakamilika.
Hakimu Rusema Alisema ili washitakiwa wapate dhamana ni kila mshitakiwa awe wadhamini wawili ambao ni watanzania na
wanaofanya kazi kutoka kwenye taasisi zinazotambulika kisheria.
Kutokana na masharti hayo ya dhamana washtakiwa watatu waliyakamilisha
lakini mmoja wao alishindwa kuyakamilisha baada ya kuwa na mdhamini
ambaye si raia wa Tanzania.
Wakati Taratibu hizo zikiendelee , Wakili wa Serikali Salum Ahmed aliingia
mahakamani hapo na kuiomba mahakama kuifuta kesi hiyo chini ya kifungu
cha 91 (1) cha Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (CPA) ya Mwaka 2002 kwa kuwa
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya Kuendelea na Kesi hiyo ambayo il ifunguliwa Jana Alasiri mahakamani hapo.
Baada ya kuwasilishwa kwa ombi hilo, Hakimu Kwey Rusemwa aliwaachia
huru washtakiwa hao, lakini muda mfupi baadaye walikamatwa na askari
wa jeshi la polisi na kuwekwa chini yaulinzi mkali.
Baada ya Polisi kuwakamata washitakiwa Hao waliwekwa chini ya Ulinzi baada ya muda mfupi baadae walipandishwa Kwenye gari aina
ya Toyota Land Cruser lenye namba za usajili KXO 6 EFY na Toyota RV4
lenye namba za usajili T366 AVG na kuondoshwa Katika eneo Hilo la Mahakama na kupelekwa POLISI ambapo hadi waandishi wa Habari unaoendoka hatukuweza kufahamu wameenda kuifadhiwa Katika Kituo gani Cha POLISI.
Wakati washtakiwa hao wanaotetewa na Wakili Gaudiosus Ishengoma
wakiwa chini ya ulinzi, wakili wao huyo alionyesha hali ya
kusikitishwa kwa kitendo hicho na kudai kuwa DPP aliwafutia mashtaka
wateja wake na kuwaachia huru ili awafungulie mashtaka mengine ambayo
hayana hata dhamana.
Chanzo: Facebook. WwwHappy Katabazi. Julai 29 Mwaka 2014
No comments:
Post a Comment