MAKUWADI WA WAGOMBEA URAIS CCM WADHIBITIWE
Na Happiness Katabazi
TANZANIA ni nchi ambayo wananchi wake kwa ridhaa yao waliamua taifa Lao liongozwe kwa utawala wa Sheria na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.
Sisi wasomi wa fani ya Sheria tunasema Katiba ndiyo Sheria mama na inapotekea Kifungu chochote Cha Sheria nyingine kina kwenda kinyume na Ibara yoyote ya Katiba , basi Kifungu hicho kitahesabika na Mahakama Kuwa ni Kifungu batiri Kwani kina kwenda kinyume na Ibara Fulani ya Katiba ya nchi yetu.
Mapema wiki iliyopita Jaji Joseph Warioba aliibuka na kutaja sifa za mgombea urais ambaye anafaa kuiongoza Tanzania baada ya uchaguzi Mkuu kumalizika Mwaka 2015. Miongoni mwa sifa alizozitaja Jaji Warioba alisema rais ajae awe kijana, wazo ambalo zimezua mjadala wengine wakimuunga mkono wengine wakimpinga.
Na Kwa upande mwingine naweza Kusema Kuwa mtazamo huo wa Warioba ndiyo Kama umewazindua usingizini makuwadi wa kambi za wagombea urais wa mwaka 2015 ambapo ni kweli makuwadi hao wamezinduka nakuanza kutumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuwafagilia wagombea wao watarajiwa wa kiti ha urais na kuwasiliba makada wa CCM ambao wanatajwatajwa kugombea urais.
Na sisi waandishi wa Habari tusipokuwa makini na hawa baadhi ya wanasiasa uchwara wetu wa hapa nchi na makuwadi wao, tutajikuta kuanzia wiki iliyopita hadi Oktoba mwakani, tutajikuta vyombo vyetu vya habari tunashindwa kuchapisha Habari za kuchochea maendeleo ya nchi na Matokeo yake tunaanza kununuliwa na kukubali kuchezewa akili zetu na makuwadi wa wagombea watarajiwa wa Kiti Cha urais Kuwa tunazipa kipaumbele Habari za Kuwafagilia wagombea wao.
Tuwe macho na mchezo huu machafu, Kwani binafsi Nina uzoefu na hili Kwani Kipindi kile Cha kuelekea mchakato wa kumpata rais wa Mwaka 2005, Nilikuwa ni mwandishi wa gazeti la Mtanzania enzi Waliokuwa makuwadi wa wagombea urais Mwaka 2005 ,walianza mapema kuwaweka mifukoni baadhi ya wahariri na waandishi na hatimayeKukazuka misuguano ndani ya vyumba Vya Habari wa baina ya baadhi wahariri na wahariri kwa kushinikiza baadhi ya wahariri wachapishe Habari na makala za kuwapamba wagombea urais wao.
Ibara ya 39(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 , inaanisha wazi sifa za mtu kuchaguliwa Kuwa Rais wa Tanzania.
Ibara 39(1) (a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Sheria ya Uraia;
(b) Ametimiza umri wa Miaka arobaini:
(c) ni Mwanachama , na mgombea aliyependekezwa na Chama Cha siasa;
(d) ambazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi;
(e) Katika Kipindi cha Miaka Mitano Kabla ya Uchaguzi Mkuu hajawahi Kutiwa hatiani Katika Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.
Ibara 39(2) Bila ya kuingilia haki na Uhuru wa mtu Kuwa na yake , kuamini dini atakayo, kushirikiana na wengine na kushiriki shughuli za umma kwa mujibu wa Sheria za nchi , mtu yeyote hatakuwa na sifa za kuchaguliwa kushika Kiti Cha Rais wa Jamhuri ya Muungano Kama Si Mwanachama na mgombea aliyependekezwa na Chama Cha siasa":
Ni kweli Ibara ya 18 (a) ya Katiba ya nchi inasema ' kila mtu anao Uhuru wa Kuwa na maoni na kueleza fikra zake'.
Lakini je huu ni wakati mwafaka wa wazee wetu hawa kujitokeza adharani Kusema mgombea urais wa Mwaka 2015 awe kijana? Hivi Ibara ya 39 ya Katiba inasema mgombea urais ajae awe ni kijana?.
Huyo mgombea urais kijana Mbona basi hatuambiwi ujana wake ni wa umri gani? au Tayari Katiba mpya imeishapatikana na Ibara ya kuruhusu mgombea urais kijana imeisha wekwe na imeanza kufanyakazi? Maana Ibara ya 39(1) (b) inasema mgombea urais awe Ametimiza Miaka 40.
Binafsi mtu yoyote atakayeapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania baada ya uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 kumalizika Kuwa ndiye rais wa Tanzania , minitamuunga mkono na nitamkubali Kuwa ndiye rais wa nchi yangu.
Lakini tujitazame sasa nchi yetu HIvi sasa inaelekea Kwenye Uchaguzi wa serikali za mitaa, badala ya kuamasisha wanachama wa vyama vyao na wananchi kwa ujumla kushiriki uchaguzi huo wa serikali za mitaa badala yake wazee wetu Hao wanatoa matamshi ambayo ni wazi yameibua misuguano Katika kambi za wagombea urais watarajiwa.
Minafikiri ni jambo Jema kwa sasa Kwa vyombo Vya Habari kutoa kipaumbele kwa kuchapisha Habari za kuamasisha maendeleo zaidi na kuibua maovu na kutoa dira Katika mambo mbalimbali na kupaza sauti za wanyonge kupitia kalamu Zenu, hawa " wanasiasa uchawara' wanaotumia makuwadi wao ambao hivi sasa wamekuwa wakiwasaka waandishi wa wawaingize kwenye kambi zao kwa njia mbalimbali .
Makuwadi hao wengi wao wakiwa ni wanaume moja ya mbinu chafu wanayotumia kuwateka waandishi wajiunge na kambi zao ni fedha na kujaribu kuanzisha ghafla mahusiano ya kimapenzi na waandishi wa kike ambao wanachama waandishi Hao watawasaidia Katika kambi zao.
Makuwadi hao ambao HIvi sasa wa kujiunga kwa Wingi Kwenye Facebook kwa majina yao halisi na ya kufikirika na kuomba Kwakasi urafiki kwa waandishi wa habari ambao nao wamejiunga na facebook ili kila siku wawe wanafanya mawasiliano na baadhi ya waandishi ili wajenge ukaribu kupitia facebook na kupata taarifa mbalimbali za kila siku za mwandishi husika na waandishi wengine, kutufuatilia nyendo zetu wanahabari eti tutakutanaga na watu gani, tu napenda nini, Mara wajisemesha wanataka kuanzisha magazeti hivyo wanataka waandishi wanaowataka wao wawapate mbinu za kitaaluma za jinsi ya kuanzisha magazeti na kutuahidi mishahara minono.
Kwa Bahati Mbaya au nzuri kuna baadhi ya waandishi wa Habari , Njama hizi za makuwadi hawa bado hawajazibaini ila kikubwa Cha makuwadi hawa wanachokitaka hasa ni Kuwa karibu na Waandishi wa Habari ili waweze Kuwa wanapata taarifa zinazohusu kambi za mahasimu zao Kwani wanaamini nao Hao mahasimu wao nao wanatumia waandishi wa Habari na waandishi wa Habari tunasifika kwa sifa ya kutojua kutunza Siri na sifa hiyo imekuwa Ikitimiza kikamilifu na makuwadi wa kambi za wagombea urais kushikishana adabu.
Ukimtazama Huyo mtu anayemfuata Mwandishi Kuwa eti anataka kuanzisha Gazeti, hafanani kabisa na hayo anayosema.Ni vichekesho vitupu. Ni hatari sana na Ujinga wa aina yake mgombea urais mtarajiwa kwa sasa kuwatumia makuwadi wake wa msafishe jina na wampambe na kuumuuza kupitia vyombo Vya Habari na Mitandao ya kijamii.
Mbinu hii jamani ilishapitwa na wakati Kwani sio kila mbinu aliyoitmia Mtu Fulani kufanikisha jambo Fulani kwa wakati Fulani akafanikiwa kupitia mbinu hiyo, halafu na wewe Leo hii Katika mazingira yaliyokwisha badilika na wewe unaamua kutumia mbinu ile ile aliyotumia mwenzio Miaka 10 iliyopita utafikiri unaweza kufanikiwa. Unaweza usifanikiwe Kwani kila zama na kitabu Chake jamani.
Tena kaunzia sasa serikali kupitia Idara ya Habari Maelezo iwe macho na Katika kutoa vibali Vya kusajiliwa magazeti mapya Kwani hawa makuwadi wa wanasiasa haw ashindwi kuanzisha magazeti kwaajili ya Kazi Moja ya kuchapisha Habari za kuchafua wagombea wenzao kwa kuzuliana Habari za uzushi na kampeni zikiisha magazeti Yao wanafunga.
Kambi yoyote ya mgombea urais HIvi sasa inaona silaha yake kubwa ya kupata ushindi ndani ya CCM ili apitishwe Kugombea urais, ni kambi iliyofirisika kimkamati mapema.
HIvi Karibuni Kamati ya Maadili ya CCM, ilitoa Adhabu kwa wanachama wake Kadhaa ambao iliwakuta na hatia ya kufanya kampeni za ugombea urais Kabla ya wakati na ikawaweka chini ya uangalizi....lakini sasa Mbona HIvi Karibuni tumemsikia Naibu Waziri wa Mawasiliano , Sayansi na Teknolojia , January Makamba Akisema Kuwa atagombea .
Hakuna Sheria ya nchi inayombana MTu kutangaza Mapema nia yake ya Kugombea urais Kabla ya wakati lakini Kamati ya Maadili ya CCM, iiliwatia hatiani akiwemo Edward Lowassa, Bernad Membe na wengine kwa maelezo Kuwa wamekiuka Maadili ya CCM kwa kufanya matendo yanayoonyesha wameanza kampeni mapema, sasa tuiulize CCM, Makamba haijamsikia ?Au Kunya anye Kuku akinya Bata Kaarisha ?
Maana Membe,Lowassa na wagombea wengine hadi sasa Hawajawahi kujitokeza adharani kutamka Kuwa watagombea urais na walichukuliwa ikiwemo kupewa onyo Kali.
Ila kilichopo mitaani na ndani ya vyumba Vya Habari ni kushuhudia baadhi ya watu wanaojitambulisha Kuwa wapo karibu na Lowassa na Membe kuwa makada hao maarufu ndani ya CCM na wapo 'msituni' wanajifua kimya kimya na kwamba watagombea urais Mwaka 2015.Tusubiri Tuone.
Minasema yote Kheli na MUNgu hawatangulie ila kinachonikera ni hawa makuwadi wa baadhi ya watu wanaotajwa Kugombea urais kuanza mapema kuwapigia chapuo wagombea wao na kuanza kutumia mbinu chafu za kuwachafua wagombea wenzao kupitia vyombo ya Habari na Mitandao ya kijamii wakati bado muda rasmi wa kuanza kampeni haujatangazwa.
Hata hivyo kuna taarifa zisizo rasmi huku mitaani zinadai Kuwa hawa vijana wanatajwatajwa Kugombea urais ni danganya toto na kwamba Hao vijana ( siyo Makamba) wanatumika Kama Chambo na baadhi ya makada maarufu wa CCM ambao Tayari kila kukicha wanatajwa Kuwa watagombea urais, ili wapoteze Lengo na hatimaye wananchi waanze kuwajadili vijana Hao Kumbe vijana Hao wanakazi Maalum ya kuwakinga wagombea husika wasizongwe kwa wakati huu na wananchi. Ipo siku Mungu ataanika ukweli.
Ikumbukwe kuwa miongoni mwa hawa walio jitokeza adharani HIvi sasa kupendekeza eti rais ajae awe ni kijana, alipo ingia ramsi madarakani Rais Jakaya Kikwete, Desemba 21 Mwaka 2005 , baadhi yao ndiyo waliokuwa wa kwanza kuinanga serikali inayoongozwa na rais (Kikwete), ambaye tuliaminishwa kuwa ni rais kijana.
Kwa Kuwa Rais Kikwete ni " Mkubwa wa Akili' , aliwapatia madaraka mbalimbali karibu wote Waliokuwa wakosoaji wa serikali yake na walivyokosa haya wakosoaji hao walikubali madaraka hayo kwa mikono miwili , wakachekelea waliyopewa na rais Kikwete ambae alivyoingia madarakani walikuwa wanamuita ni rais ' mhuni, msanii, cheki bobu na hana akili na hataweza kuingoza Tanzania na ni rais anayependa kuchekacheka ovyo ovyo hata Katika mambo yasiyostahili kucheka".
Waliokuwa wakimdhihaki Kikwete Wengi walikuwa wakiwaunga mkono waliokuwa wagombea wao wa urais Katika kampeni za uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2005" wagombea wao walishindwa.
Wakaanza kulipa kisasi kwa kuikosoa serikali ya awamu ya Nne inayoongozwa na Rais Kikwete, lakini Kumbe serikali ya Kikwete nayo ilikuwa na vijana wake Kama Amos Makalla ambaye kwasasa ni Naibu Waziri wa Maji, walianza kujibu mapigo kwa wakosoaji wa serikali ya Kikwete na mwishowe Kikwete alikuja kuwatea wakosoaji Katika Nafasi mbalimbali ikiwemo Bunge la Katiba, Tume ya Marekebisho ya Katiba iliyokuwa Ikiongozwa na Jaji Warioba.
Hivyo serikali, CCM, Watanzania wote tuwe macho na watu wa haina hii Kwani Tusikubali kuruhusu msuguano huu uanze sasa kushika kasi tena kupitia vyombo Vya Habari ni wazi hata Habari za kimaendeleo kwa ujumla wake , habari kuhusu jinsi vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinavyofanya kazi ya kuwadhibiti wahalifu na kuakisha nchi yetu naendelea kuwa na amani na usalama, uchumi wetu, Kilimo, elimu sitakuwa hazisikiki kwa mapana yake Matokeo Habari za wagombea urais Mwaka 2015 ndiyo zitakuwa zinabeba uzito Kwenye vyombo Vya Habari. Tusikubali wendawazimu huu na Hao makuwadi wadhibitiwe mapema mAana siku zote wapambe wana Nguvu kuliko wenye Mali.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika
Chanzo: www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook: Happy Katabazi
Julai 8 Mwaka 2014.
Simu: 0716 774494
No comments:
Post a Comment