Header Ads

JAJI WARIOBA ASEMA ANAWASUBIRI WAJUMBE BUNGE LA KATIBA MTAANI




JAJI WARIOBA ASEMA ANAWASUBIRI WAJUMBE BUNGE LA KATIBA MTAANI:
: Azindua Kitabu Cha Maisha Dk.Sengondo Mvungi
: Aipongeza  LHCR kutimiza 19

Na Happiness Katabazi

KITUO Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Leo kinahadhimisha Miaka 19 tangu kuanzishwa kwake tarehe kama ya leo Mwaka 1995.

Pia wakati ikifanya  sherehe ya kumbukizi hiyo Leo ambayo imepangwa kumalizika saa nane mchana  Katika Hoteli ya Mayfair Plaza Dar es Salaam, pia Leo itazindua kitabu Maisha aliyoishi mahasisi wa LHRC, Marehemu Dk.Sengono Mvungi aliyefariki Novemba Mwaka Jana baada ya Kuuwawa kikatili na wahalifu huko nyumbani kwake Kibamba.

Kitabu hicho kimepewa jina la ' Dk.Sengondo Mvungi, Breathing the Constitution'.

Sherehe hiyo ambayo inaendelea HIvi sasa ukumbini hapo ambapo mgeni rasmi wa sherehe hiyo ni Jaji Joseph Warioba ambaye bado ajaanza kutoa hotuba yake.
Mkurugenzi wa LHRC, Dk.Hellen Kijo- Bisimba alisema wanasherehekea kuzaliwa KWA Kituo hicho bila Dk.Mvungi.Akitoa hotuba yake Dk.Bisimba alitoa historia ya Kituo hicho na jinsi Marehemu Dk.Mvungi alivyoapishwa Kituo hicho na alivyokiendeleza.

Dk.Mvungi alisema Leo hii Dk.Mvungi Angekuwa hai anegshangazwa na jinsi Kanuni za Bunge Maalum la Katiba zilivyobadilishwa na kuruhusu wajumbe wa Bunge Hilo Wapiga kura njia ya Mtandao Kama nukushi.

Alisema Leo hii Dk.Mvungi Angekuwa hai anegshangazwa jinsi ya mchakato wa kupata Katiba mpya ulivyo kiukwa.Angeshangazwa pia jinsi Bunge Maalum la Katiba lilivyoshindwa kajivua ubinfasi na upendeleo wa Chama Kimoja.

Kwa upande wake Mke wa Marehemu Dk.Mvungi, Anna Mvungi alisema anaishukuru LHRC kwa kutambua na kuenzi mchango wa Aliyekuwa mumewe, na kwamba Kabla ya Dk.Mvungi akiwa Hai na alipokuwa na wadhifa wa ujumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Marehemu Mvungi alikuwa akimweleza maneno haya:  " Hata  nikifa Leo hii ,Tayari nimeishatimiza Lengo langu la Tanzania Kuwa na Katiba mpya'.

Anna Mvungi na Mama Kagaruki ndiyo walioongoza hadharani hiyo kukata Keki ya kumbukizi ya LHRC na Keki hiyo ilikuwa na muundo wa jengo la ofisi ya LHRC ambapo walipata fursa ya kuwalisha watu mbalimbali akiwemo Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB), Dk.William Kudoja ,  Paramagamba Kabudi, wanahabari Saed Kubenea na Rainfrey Masako, wajumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na wengine.

Kwa upande wake Mhariri wa kitabu Cha Maisha ya Dk.Mvungi, Profesa Chris Peter Mvungi  alisema kitabu hicho kina jumla ya kurasa 465 , picha 157 , nz kina sura 10.

Sura ya kwanza inahusu kushambuliwa kwa Dk.Mvungi, sura yalikuwa jinsi Dk,Mvungi alivyolazwa Katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, na nchini Afrika Kusini baada ya kujeruhiwa vibaya. Sura ya tatu ni Mvungi alivyofariki.

Profesa kimeandikwa kwa lugha mbalimbali  ikiwemo lugha ya Kiingereza , Kiswahili, Kijerumani na lugha ya Kabila la Kipale  Kwani Dk.Mvungi alikuwa ni Mpare.

Kitabu  hicho siyo Cha huzuni ni kitabu Cha sherehe Kwani Dk.Mvungi aliishi Maisha ya mfano na wanasiasa wenzake, wasomi, wanafunzi wake na Jamii yote iliyokuwa ikimzunguka.

Alisema Tume ya Warioba ilikuwa ni Tume bora sana na jinsi tunavyoshuhufia vioja Vya Bunge la Katiba ni ushahidi tosha Kuwa Tume ya Warioba ilikuwa bora na ili fanyakazi nzuri.

Kitabu hiki kiifundishe Jamii kuishi Maisha yaliyo bora Kama Dk.Mvungi.

'Tukiambiwa Kama Bunge la Maaulum la Katiba linapopitisha Katiba ya Bunge iliyopendekezwa kwa sura badala ya Kifungu kwa Kifungu....hii ni Ishara Kuwa Kuwa Tume ya Warioba ilifanyakazi nzuri....historia haiandikwi kwa FFU, ukweli haupendwi kupuuzwa' Profesa Mahina.

Aliwataja waandishi wa kitabu hicho na akawayaja baadhi ya watu waliondika Makala za jinsi walivyomfahamu Dk.Mvungi , miongoni mwao waandishi makala hizo ni Ofisa wa Habari wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB), mtoto wa Marehemu Ambaye ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mkuu wa Shule ya Sheria (UB), Dk.Natujwa Mvungi, Ndimara Tigambwage, Harold Sungusia , Dk.Bisimba, na wengine.

Naye mgeni rasmi  Jaji Joseph Warioba alisema HIvi sasa yeye anaitwa ni ' ni Shida kubwa' lakini kuna Shida ndogo ndogo ambazo ni Kama baadhi ya waliokuwa wajumbe wa Katiba  Kama mjumbe Polepole wataendelea Kusema.

Jaji Warioba alisema Juzi aliipatia nakala ya Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba, nakuona maoni mengi ya wananchi yamepuuzwa na kwamba bado Bunge linatakiwa liwaeleze wananchi kwa mapana ni kwanini imeyapuuza maoni yako.

Alisema Dk.Mvungi alitoa mchango mkubwa na wakipekee Katika Tume aliyokuwa akioongoza  na tume hiyo iliaidi kuakikisha maoni ya wananchi yakiyotolewa kwa tume yake wanayasimamia na kuheshimiwa na kwamba hiyo ndiyo itakuwa ni ndoto yako ya kumuenzi Dk.Mvungi.

Jaji Warioba alisema baada ya kuisoma Katiba hiyo iliyopendekezwa na Bunge  kuna mambo mengi ambayo ni maoni ya wananchi  hawajangizwa Kwenye Katiba hiyo iliyopendekezwa licha kuna baadhi ya maoni ya wananchi yameingizwa.

' Lakini Katika kupitia Katiba iliyopendekezwa na Bunge  nimeona mwelekeo  wa Bunge Hilo la Katiba  maoni Yale yamekataliwanna mambo mengi yamekataliwa' alisema Jaji Warioba .

Jaji Warioba alisema Tume yake ,wananchi wakitaka kuwepo Maadili ya viongozi na umma lakini kwa mujibu wa Katiba iliyopendekezwa na Bunge, imelikataa Pendekezo Hilo.

Aidha alisema wananchi walitaka kuwepo na tunu ya taifa  ambazo tunu hizo ni Utu ,uzalendo ,uwajibikaji,uadilifu,,lugha ya taifa lakini Bunge la Maalum la Katiba limekataa Wazo Hilo la wananchi na Kusema Kusema hizo siyo tunu ya taifa Bali ni Misingi ya Utawala.

' Hivi unaweza Kuwa Mtanzania bila kuwa na hivyo vitu? Misielewi kabisa  Bunge Maalum la Katiba Kusema  uzalendo, ,uadilifu ,tuu  siyo tunu ya taifa? Misielewi kabisa licha hivi sasa Mimi naïtwa ' Shida kubwa  ' lakini  Nawataka watambue kuwa pia kuna shida ndogondogo ambazo ni baadhi ya wajumbe wa Tume ya Katiba, Humphrey PolePole.

Alisema wananchi walitaka wawe na Nguvu ya kumuondoa madaraka mbunge wao  lakini Bunge la Katiba limekataa limesema ni Bunge la Jamhuri ndiyo kitakuwa na mamlaka ya kumuondoa Mbunge.

Kusaka kula Kwa  njia ya Mtandao hakutatuletea maridhiano na sasa naanza kukukata tamaa ya kupatikana kwa Katiba mpya. Tukifika Mwakani ajenda itakuwa ni Katiba mpya, na uenda ikatugawa Watanzania, na uenda mchakato ukaanza upya.Tumeacha mchakato tumegeuza mchakato kwa Itikadi za siasa.
Nataka Amani.

'Nawaambia  wale walioniita 'Mimi ni Shida'muda Si mrefu nao watamaliza kazi yao katika Bunge Maalum la Katiba ,warudi mtaani na watanikuta Mimi na mjumbe mwingine wa Tume ya Katiba, Humphrey Polepole nao waje kutetea Katiba iliyopendekezwa na Bunge na Mimi na Polepole tutaendelea kutetea maoni ya wananchi waliyoyatoa Katika Tume ya Katiba" alisema huku akishangiliwa na wajumbe wakimuita 'ni Shida' na kwamba Katiba Mpya haitapatikana.
 
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
Septemba 26 Mwaka 2014.


No comments:

Powered by Blogger.