Header Ads
LEO NINAYO FURAHA SANA

MIMI HAPPINESS KATABAZI Leo ninayo Furaha kwasababu makala yangu iliyokuwa ikimzungumzia jinsi nilivyomfahamu aliyekuwa Marehemu ' mume wangu' Dk.Sengondo Mvungi  'aka' Rais Mdhulumiwa' ,yenye kichwa cha habari kisemacho : " KIFO CHA DK.SENGONDO MVUNGI KIMENIUMA", kuingizwa kwenye kitabu cha maisha ya Dk Mvungi kilichoandikwa na Legal Human Right Center(LHCR) na kuzinduliwa na Jaji Joseph Warioba leo katika Hoteli ya Mayfair Dar es Salaam.Kitabu hicho ambacho kimezinduliwa Leo kinaitwa ' Sengondo Mvungi Breathing the Constitution'. 

Naishukuru LHCR kuona Umuhimu wa kuingiza makala yangu ambayo ipo Katika Ukurasa wa 78 Kwenye kitabu hicho ambacho kina sura 10 na kurasa 465 ,Kwani ni Wengi waliandika makala za kifo Cha Mvungi lakini siyo wote waliopata bahati ya LHCR kuingiza makala zao Katika kitabu hicho ambacho. Ninafuraha kwasababu nikiwa Mwandishi wa Habari kitaaluma makala yangu imeingizwa Kwenye kitabu hicho ambacho kimeandikwa na watu wenye nyadhifa kubwa serikali na Kwenye Jamii na watu maarufu na watu wenye umri mkubwa kuliko Mimi. 

Natoa ushauri  kwa wazazi msiwe wa kwanza kuwazuia watoto wenu kusomea fani ambazo wanapenda kuzisomea.
Binafsi mama yangu Mzazi hakutaka nisomee Kazi ya uandishi wa Habari lakini Leo hii yeye ndiyo anakuwa mtu wa kwanza Kusema uwa Amini Kama tumbo lake liliweza kumzaa mtoto mwenye taaluma ya uandishi wa Habari ambaye ni Mimi. Nitakukumbuka Daima Dk.Mvungi ukiyefariki Novemba 12 mwaka 2013, Kwani nafahamu mchango wako Kwangu. 

By Happiness Katabazi
Ofisa Habari Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB)
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
0716 774494

No comments:

Powered by Blogger.