Header Ads

HALIMA MDEE TULIA UZAE
HALIMA MDEE,TULIA UZAE
Na Happiness Katabazi
MAKUNGWI  na wanawake waliotuzidi umri upenda Kuwaasa watoto wa kike hususani wale walitimiza umri halali wa kuingia Kwenye mahusiano hususani  Kwenye ndoa Kuwa :

' Mwanamke yeyote aliyekamilika kuitwa mwanamke na aliyefundwa anapaswa kufanya vurugu, utundu chumbani wakati akiwa na mumewe au Mpenzi wake wakifanya tendo la ndoa '.

Nimelazimika kutumia Msemo huo wa Makungwi  kwasababu , kwa zaidi ya wiki Moja sasa tumeshuhudia Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (Bawacha) Halima Mdee (35) akifanya vurugu na kupingana na amri halali za Jeshi la Polisi Mkoa Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alitangaza kuyapiga marufuku maandamano yaliyokuwa yameandaliwa na Mdee lakini Mdee na wenzake waliipuuza amri hiyo ya Kova na mwisho wa siku Oktoba 4 Mwaka huu, Mdee na wanawake wachache wa Chama hicho walijaribu kuandamana wakaishia  kusambaratishwa na Polisi na Kukamatwa kupelekwa Katika Kituo Cha Polisi Oysterbay 

Oktoba 6 Mwaka huu, Mdee na wenzake wakafunguliwa Kesi ya jinai mbele ya Hakimu Janeth Kaluyenda, Wakili wa Serikali Mkuu, Bernard Kongola alidai Mbali na Mdee washitakiwa wengine ni   Rose Moshi (45), Renina Peter ‘Lufyagila’, Anna Linjewile (48), Mwanne Kassim (32), Sophia Angel (28), Edward Julius (25), Martha Mtiko (27) na Beatu Mmari (35).

Kongola alidai kuwa washtakiwa hao Oktoba 4, 2014, wakiwa Mtaa wa Ufipa, walikiuka amri halali ya kutawanyika iliyotolewa na Mrakibu wa Polisi (SP), Emmanuel Tillf kwa niaba ya Jeshi la Polisi kitendo ambacho ni kinyume na Kifungu cha 124 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Katika shtaka la pili, siku hiyo ya tukio katika eneo hilo, washtakiwa hao wanadaiwa wote kwa pamoja , walifanya mkusanyiko usio halali kwa lengo la kutembea kwenda kwenye Ofisi ya Rais Ikulu .Alidai kuwa kosa hilo ni kinyume na Kifungu cha 74 na 75 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Na washitakiwa Hao walikana Mashitaka ila Masharti ya dhamana walishindwa kutimiza,Mahakama ikaamuru wapelekwe gerezani hadi Jana walipopata dhamana.

Kesi hiyo ikaairishwa  hadi Oktoba 21 Mwaka huu,itakapokuja kwaajili ya washitakiwa hao kusomewa maelezo ya awali kwasababu upelelezi wa Kesi hiyo umekamilika.

Mdee ni msomi wa Sheria na nimiongoni mwa wanasiasa wachache vijana wenye ujasiri wa kujitokeza hadharani kukataa jambo ambalo yeye anafikiri jambo Hilo halina maana.

Mimi Nampongeza kwa kipaji  hicho tu Cha uthubutu wa kujitokeza hadharani Mara kwa Mara kupinga licha Mimi binafsi  wakati mwingine uwa sikubalini Sababu zake nyingine anazotumia kupinga jambo Fulani.

Lakini nitajisikia vibaya   Kama sitampongeza  Mdee ambaye ki umri tupo sawa ,kwa kuweza kuchaguliwa Kuwa Mwenyekiti wa BAWACHA.

 Hakika ameandika historia ya kijana mwenye umri Kama wake kuaminiwa na Chama Chake kupewa nafasi hiyo ambayo anaongoza wanawake ambao ni wanachama wa CHADEMA ambao wengine wamemzidi yeye na mama yake umri.Hongera Mdee kwa ushindi huo.

 Maana matendo mengine anayoyatenda ya kuamasisha vurugu, uzushi ni wazi kabisa anaonekana ni mwali 'msungo'. Yaani ni mwanamke ambaye hajafundwa Mafundo ya kike au kama alifunda basi anayapuuza.

Anachokifahamu yeye ni Mafunzo ya darasani na siasa chafu za ugomvi  ambazo zinazidi  kumshushia heshima yake Kwa Wapiga kura wake wa jimbo la Kawe, Jamii ya wapenda ustaharabu, Amani na Utawala wa Sheria na wasomi.

Kinachonikera kwa Mdee hii tabia yake ya kufanya 'Usela Mavi' wakati amelelewa Katika familia ya wasomi Kwani baba yake ni msomi na Mdee  Mwenyewe amepata fursa ya kusoma shule lakini tunamshangaa anatenda matendo ambayo hawapaswi kutendewa na mtu Kama yeye.

Mdee ni msomi wa Sheria na msomi yoyote wa Sheria, Mwaka wa kwanza wa shahada ya kwanza ni lazima ufundishwe  somo la Criminal Law ambalo somo Hilo mwalimu pamoja na mambo mengine anatumia Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 ya Mwaka 2002 ( Penal Code).

Na hiyo Sheria inaweka wazi makosa mbalimbali kwa Kifungu kwa Kifungu Mdee amelisoma na kufaulu somo Hilo na anafahamu Kuwa ndani ya Sheria Hilo Kuwa kuna kosa la kukaidi amri ya Jeshi la Polisi, kufanya mkusanyiko haramu Adhabu zake ni zipi.

Lakini Mdee ambaye amekuwa akijitapa eti yeye ni Mwanasheria mzuri ndiyo amekuwa miongoni mwa wasomi wa Sheria ambao ameshitakiwa Kutenda  matendo ya kuvunja Sheria wazi wazi kwa kukaidi amri ya Jeshi la Polisi iliyokuwa ikimtaka asiandamane kwa Kigezo eti Rais Jakaya Kikwete amealika  Ikulu.

Nimuulize Halima hivi Rais Kikwete ni Hawara yako,ndigu yako hadi mkutane sehemu huyo Kikwete akupe mualiko uende Ikulu ,wewe na hao wafuasi wako bila Katibu wa Rais kujua mualiko huo?

Rais ni Taasisi kwa wale tunaofahamu, hivyo huwezi kujikurupukia tu ukaamka Leo ukachukua  kundi la wahuni wenzio na mabango juu ukasema unaenda Kumuona Rais Ikulu eti Rais Kikwete amekupa Mwaliko?

Kama siyo kumsingizia Rais na kumchonganisha Rais Kikwete na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ni kitu gani? 

Maana Kama Rais Kikwete alikualika kweli.Si haraka sana Rais angetengua amri ya Kamanda Kova ya kuwazuia msiende kumuona Ikulu?

Unafikiri ni kwanini amri ya Kova iliendelea kubaki Kama ilivyo? 

Jibu ni Jepesi tu ,Halima ni muongo, Mzushi na aliyekuwa anataka kujipatia umaarufu wa kijinga Kuwa eti Mwaliko wa Rais Kikwete amemwalika Ikulu. 

Alichokuwa akikitafuta Mdee ni kutaka kujionyesha yeye ndiyo Mwenyekiti Mpya wa BAWACHA na kwamba ni ngangari kweli kweli kuliko Mwenyekiti aliyepita Suzan Lyimo na hivyo anaushawishi mkubwa wa kuweza kuwashawishi wanachama wanawake wa Chama hicho waweze kuandamana mwisho wa siku sifa anapata Mdee Kuwa ni mwanamke Shujaa na aliogopi jeshi la polisi, Kumbe ni Ujinga mtupu.

Kama Mdee kweli wewe uliogopi Jeshi la Polisi kwanini ile Oktoba 4 Mwaka huu, mlivyo andamana ,Polisi ilivyo watawanya ,kwanini wewe uliogopa KISAGO ukakimbia Kwenda kujificha ili kukwepa kipondo Cha Polisi?

Kama wewe ni Shujaa kweli kwanini Oktoba 7 Mwaka huu, ulipofikishwa Katika Mahakama ya Kisutu  kwanini uliyakana hayo Mashitaka?

Maana Kabla hujafikishwa mahakamani ulikuwa ukijigamba kupitia vyombo Vya Habari Kuwa kuandamana ni Haki yako na hutakiwi kuomba Kibali?

Kama wewe ni Shujaa kwanini ulikubali kupewa dhamana?

Shujaa au kamanda gani anaogopa kukaa gerezani kweli licha ni kweli dhamana ni Haki yako ?

Ningekuona Wewe ni Shujaa  kweli usingeomba dhamana ungesema upo Tayari kwenda kukaa gerezani ili ukiwa kule gerezani pia huweze  kutoa hoja zako kwa mahabusu wa kike zinazohusu  msimamo wako na Chama Chako Cha kuipinga Katiba iliyopendekezwa Bunge na kujua matatizo yanayowakabili.

Kamanda  gani akiona kilungu Cha Polisi na Gari za Maji ya kuwasha'Kikojozi' Ana kimbia?

Unatakiwa ukae upambane na Polisi Kwani ulijigamba licha Polisi imekataza maandamano yenu ,wewe na wanachama wako mtaandamana na nauogopi Polisi.

Mdee Tanzania hii unayoiona hivi sasa watu wanaishi kwa amani tofauti na nchi za wenzetu , Elewa Kuwa  watu walipoteza Uhai wao,Jasho Lao wakaijenga nchi hadi Leo hii wewe umeikuta,ukasoma, umepata madaraka ambayo ya nakulevya hadi unaanza jeuri ya kukaidi amri ya Jeshi la Polisi.

 Mamlaka husika hazitakuacha ufanye huo uhuni wako ambao mwanamke yeyote mwenye haiba  ya kike hawezi kufanya .

Na Mbaya zaidi ulichokuwa ukikipigania Cha kutaka Rais Kikwete asipokee Katiba iliyopendekezwa na Bunge hujafanikiwa Kwani Jana jioni Kikwete na Rais wa Zanzibar Dk.Mohamed Shein wameipokea Katiba kutoka kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta na tumemshuhudia Rais alishindwa kuficha hisia zake na akajikuta akitamka zaidi ya Mara mbili kwamba anayofuraha sana sana kuona tendo Hilo la Kihistoria ilifanyika chini ya uongozi wa serikali yake na akasema kabisa Katiba  ile ni nzuri sana na awashawishi Watanzania waipigie kura ya ndiyo.

Ila Kwa mwanamke ambaye Hana haiba ya kike  na Mwanamke ambaye hajithamini na hatambui mambo yapi  mwanamke afanye na mengine asifanye ,atayafanya Kama wewe Mdee ambaye tunakuhesabu ni msomi,kiongozi lakini unashiriki hadharani Kutenda matendo ya kuvunja Sheria. 

Kiongozi yoyote mzuri anatakiwa awe ni mfano wa kuwaongoza wafuasi wake wafikie malengo waliyoyakusudia.

 Sasa  Mdee  ambaye ni kiongozi lakini unawaongoza wafuasi wako waende njia isiyo sahihi kwa kushiriki vitendo vya uvunjifu wa sheria na matokeo yake mmeishia kushitakiwa na kulala Gerezani na kujitia nuski.

Halima  tambua kuwa hata kama mwanamke awe na fedha ,mali ,madaraka kiasi gani bado mwanamke anatakiwa hajiheshimu na afanye matendo ambayo mwanamke anatakiwa atende .

Siyo mwanamke asimame hadharani atende matendo ya kihuni huni  ambayo tumezoea kuona yanatendwa wanaume wahuni wahuni au wanawake wahuni wahuni tu ,Kama wewe ulivyotenda.

Labda ni mwambie Mdee  vitendo hivyo vya ukahidi na Kauli ambazo hazipaswi  kutolewa kwenye kinywa Cha mwanamke mwenye haiba ya kike,Hupaswi kujifanya.

Wanaopaswa kufanya matendo Kama hayo ni baadhi ya wanawake kama Asha Ngedere,  na wanawake wengine ambao kufanya vitendo vya kihuni, kusutana na wengine hadi wameunda vikundi vinavyokodisha kwaajili ya kuchamba watu, ambao wanawake hao wanaofanya vitendo hivyo vya kihuni wanapatikana sana huko uswahili mitaa ya Mburahati Madoto, Kigogo Luhanga, Mburahati kwa Binti Kahenga ,vurugu ndiyo sifa zao tena wanaona fahari kuona watoto wao wanafuata nyayo za mama zao za kufanya vitendo Vya kihuni na kishenzi.

 Mdee Hupaswi kufanya vitendo vya uvunjifu wa sheria na vya kihuni huni, waachie wakina Asha Ngedere  , wewe unapaswa hivi sasa ukae katika ofisi mpya ya Bawacha ,  ubuni mipango yako yakuwaletea wanachama wako na taifa maendeleo kwa njia amani.

Una mambo mengi ya kufanya siyo kuanzisha maandamano haramu .

Hivi kweli unashindwa kuketi kitako ukaanzisha hata taasisi yako binafsi ,Ukaanda harambee za kuchangia kutokomeza mimba za utotoni, au kufanya utafiti wa ni kwanini wanawake wengi wanashambuliwa na ugonjwa wa UTI na mambo mengine,ukaalika watu wenye Fedha zao wakashiriki harambee wakachangia Fedha utapata za kuendesha Programu hizo?

Lakini umeama kujigeuza Kituko Mbele ya Jamii ya wanawake wastaarabu ya kushiriki kushinikiza kufanya maandamano haramu. 

Kama Fedha, madaraka unayo.Tatizo Lako nini  Mdee  hadi unaamua kushiriki vitendo hivyo Vya kihayawani ambayo vinakushushia heshima?

Umri ndiyo huo una unazidi kukutupa mkono na ukae ukijua  hivyo vitendo vya 'Usela Mavi' unavyofanya vina mwisho  wake.

Mwanamuziki Banza Stone aliwahi kuimba ' upatapo fahamu ujue Umepotea'.

Ebu Mdee  achana na usela Mavi , anza kuweka fikra na matamanio ya siku Moja na wewe uitwe mama wa Fulani.

Mshirikishe Mungu Katika matamanio hayo ,Mungu atakupa mtoto na ukishampata mtoto ni wazi utakuwa busy sana na kuangaika na mambo ya mtoto na familia yako kwa ujumla na utajikuta unaoendokana na vitendo hivyo Vya kihuni  ambavyo mwanamke mkorofi akisha bahatika kupata mtoto wake anaachana navyo  Kwani anaona akiendelea  anavyo anakuwa kama anamdhalilisha mtoto wake.

Achana na wazimu huu unaoufanya wa kujifanya wewe ni jike dume, umesababisha watu kuanza kuhoji Kuwa Mdee ni mwanamke kweli?Anaujua uchungu wa Mwana?Na je Halima amebahatika kupata mtoto?

Na Wengi wanahoji hivyo kwasababu wanasema wanashangaa na kujiuliza kuwa hivi Mdee alishawahi kubeba mimba na akalea mtoto na kuitwa mama hawezi kufanya hayo anayoyafanya? 

Wanajiuliza   Mdee  ni mwanamke wa aina gani ambaye hana uchungu hadi anaamasisha wanawake wa Chadema  waandamane Katika maandamano  haramu ambayo wanaenda kupigwa ma Polisi na kufunguliwa Kesi mahakamani na hadi wakalala gerezani siku Moja?

Na wengine wanadiriki Kusema Mdee pamoja na usomi wake na madaraka aliyonayo ,anaitaji kutafutiwa Makungwi kama Bibi Hindu, Bibi Chau wamfunde ili ajue mwanamke anatakiwa aweje ,avae mavazi gani, na vitendo gani afanye Mbele za watu na yapi asifanye.

Maana licha ya madaraka na usomi aliyonayo,wakati mwingine tunamshuhudia akitenda na kuongea mambo ambayo mwanamke aliyefundwa kuwa mwamke na kuwa kiongozi , hapaswi kuyatenda Kama ya kupayuka payuka ovyo ovyo tena wakati mwingine kwa hoja zisizo na mashiko utafikiri hayawani.

Kuna wanawake wako Tanzania  mashughuli dini Kama Dk.Asha Rose Migiro, Profesa Anna Tibaijuka na wengine Wengi, huwezi kuwasikia wakifanya vitendo Vya kihuni huni na vya kuamasisha watu Wavunje Sheria.Wao ubishina Kwa hoja, ustaarabu.

Bado namkumbuka   aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake ya  Chama cha Tanzania Labour(TLP), Getrude Pwila  Enzi zile Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP- Omar Mahita.

Kwa mama huyu alikuwa ni rafiki yangu nalilikuwa naandika Habari za Chama Cha TLP kinachoongozwa na 'mume wangu wa zamani', Agustine Mrema.

Pwila alikuwa ni mwanamke machachari sana kila uchao alikuwa akiwaamasisha wanawake wa TLP waandamane Katika maandamano haramu hadi Wizara ya Mambo ya Ndani huku wakiwa wamevua  Fulana wamebaki na Sidiria tu na walikuwa wakiaa nje ya ya Wizara ya mambo ya ndani tangu asubuhi hadi jioni wakitoa maneno ya kulikashfu Jeshi la Polisi, Rais aliyekuwa madarakani, Benjamin Mkapa na aliyekuwa Msajili wa Vyama Vya Siasa, Mahundi.Na zoezi Lao la kubaki NA Sidiria walijifanya zaidi ya Mara tano Kipindi kile Cha Miaka 2002- 2004.

Mimi ,Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi, Jocye Mmasi tulikuwa ni miongoni mwa waandishi tuliokuwa tukishiriki maandamano hayo na kuandika Habari.

Leo hii Pwila amepotea Katika ulingoni wa siasa, hasikiki tena na ukizungumza naye anajutia kitendo kile alichokuwa akijifanya cha kuongoza wanawake wa TLP kuvua nguo na kubaki  na Sidiria pale nje ya Makao makuu ya Jeshi la Polisi na Wizara ya Mambo ya Ndani.

Sasa na wewe Mdee ukae ukijua wewe ni Kama una beep tu, hata hujamfikia Pwila Kwani Pwila alikuwa anaushawishi mkubwa kwa wafuasi wake walishapigwagwa sana Polisi lakini mwisho wa siku walipokuja kutambua uhuni ule waliokuwa wakiufanya kwanza ulikuwa ukiwadhalilisha  wao wenyewe binafsi.

Walipokuja  kubaini wao kama wanawake wa TLP walichokuwa wakikipigania kwa njia  ya maandamano haramu eti jeshi la Polisi lina mnyanyasa Mrema ni batiri .

Waliachana na vitendo hivyo na ndiyo ikawa Chanzo Cha umoja wa wanawake TLP kusambaratika na wanawake Wengi kaumua kuiama  TLP  kwasababu ya kubaini Pwila alikuwa alikuwa alikuwa akiwaongoza Kutenda vitendo Vya Uvunjifu wa Sheria ambavyo mwisho wa siku walikuwa wakaishia kupigwa virungu na Polisi ,kufunguliwa Kesi mahakamani na kupelekwa gerezani.

Sasa wanawake wenye akili timamu ambao mnaoamini Katika Utii wa Sheria bila shuruti  wa  Bawacha  ,mfano huo hapo  juu wa Pwila msiuupuze Kwani sote ni mashahidi Enzi za mtangulizi wake Mdee, Suzan Lyimo akiwa Mwenyekiti wa Bawacha, hatukuwa hi kumshuhudia Lyimo akiwaamasisha  wanawake washiriki vitendo Kama hivyo Vya kuvunja  Sheria Kama afanyavyo Mwenyekiti Mpya wa Bawacha ,Mdee  ambaye hata Ofisi mpya ya Bawacha ajaikaa vizuri, ajaeleza kwa vitendo vipaumbele vyake ni nini.

Pwila hakuwa na elimu kama Mdee  ila alikuwa na ushawishi na Tayari alikuwa ni Mzima , Mdee  ni kijana na bado    ana Muda mrefu Mungu akimjalia  wa kulitumikia taifa hili  na kujiandalia rekodi safi.

Sasa kwa mtindo huu wa Mdee  tena mtoto wa kike kutaka Kupambana na Polisi kwa jeuri ya kijinga na Mbaya zaidi unawaamasisha wanawake wachama Chake washiriki vitendo hivyo ,vitamsababishia kumporomosha au kumfuta  Kwenye Medani za siasa nchini Kwani Watanzania ni watu wasiyopenda ni wapenda Amani na utulivu.

Tambua Mdee  wewe ni kiongozi kijana ,unapofanya mambo mazuri au Mabaya sifa hizo unazipata wewe na vijana wenzako kwa ujumla.

Hujachelewa  unaweza kubadilika licha Tayari umeishaingia Kwenye rekodi Mbaya ya Watanzania Kuwa Mdee  ni kiongozi ambaye analazimisha maandamano ambayo yamekatazwa na Polisi hivyo wewe ni Mpenda Vurugu.

Na Kwa taarifa yako Mdee  ,siasa hizo unazotaka kuzileta hapa  Tanzania, haziwezekani,ndiyo maana wewe na Chama Chako kila mlipokuwa mkijaribu  kufulukuta kuhusu kutaka kufanya maandamano  yenu mliyosema mtaandamana nchi nchi nzima bila kikomo, hamjafanikiwa kwasababu Watanzania na vyombo Vya dola havitaki aina ya siasa mnavyotaka kulileta hapa nchini .

Kwasababu mbinu yenu ya kufanya siasa ilikuwa haina  kheri zaidi ya kutuletea vurugu na mbinu yenu ya kufanya maandamano imeshadoda sijui mnabuni mbinu gani nyingine ili iwarejeshee umaarufu kwasababu Tayari Chama chenu kinashuka Kwa kasi Umaarufu kwasababu mmoja tu ya kulazimisha matendo yanayovunja Sheria Kama maandamano haramu.

Mdee tambua hapa Tanzania  kuna wanawake wameshika   nyadhifa kubwa na nyeti nchini,lakini wanaojiheshimu na niwatiifu wa Sheria za nchi Yao, watiifu na Kamwe hutawaona wafanya vioja Kama unavyofanya wewe Vya kushiriki vitendo Vya Uvunjifu wa Amani kwa makusudi.

Wanawake Hao wengine wapo Kwenye majeshi yetu ,serikalini na taasisi mbalimbali za kiraia wametulia tulia.

Na wana uwezo wa kusaliti nchi,au kuanzia vurugu na wanaushawishi  na mvuto mkubwa sana kuliko wewe lakini wametulia wanaipenda nchi Yao na wanatii Sheria za nchi bila shuruti.

Iweje wewe Mdee ambaye umedhiirisha wazi Huna Nguvu wala karama  ya kushawishi wanawake wote wa Chadema wakatii agizo  Lako la kuwataka wanawake wa Chadema waandamane kupinga Katiba iliyopendekezwa na Bunge Kwani  tulishuhudia siku ulipo ulipoandamana ukashughulikiwa.

Ni idadi   ndogo sana ya wanawake  wa Chadema waliitikia agizo Lako  na wanawake wengine wa Chadema ambao tuna wafahamu ambao tupo nao mitaani, wasomi na wamama watu wazima wenye akili timamu na wenye utashi walikataa kushiriki   Walisema hawawezi kukubali kuingizwa kwenye  matatizo na Mdee, kwasababu wanamfahamu Mdee ni mtu wa aina gani na mwisho wa siku watakuja kuonekana wao ni mahayawani Kwani wasingekuwa mahayawani wasingeitikia wito haramu wa Mdee  wa kwenda kushiriki maandamano haramu na kweli hawakwenda. 

Ona sasa ukahidi wako kwa Jeshi la Polisi umekufanya wewe na wafuasi nane muingie Kwenye orodha ya washitakiwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kwasabu hiyo Tayari mmeishakuwa  ni Kama watumwa wa Mahakama hiyo ambao mtatakiwa   mfike tarehe itakayopangwa wakati ulikuwa na uwezo  kabisa wa kujizua  usitende makosa unayoshitakiwa nayo.

Sasa  utajikuta badala ya kwenda kutimiza majukumu mengine ,unakwenda kushinda Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia hatima  ya Kesi yako.

Muulize Mzee Mabere Marando,Agustine Mrema ,Samson Mwigamba na wengine wanafahamu  vizuri madhara ya kushitakiwa kesi za aina hiyo uliyoshitakiwa nayo hadi leo wamekoma kushiriki vitendo kama hivyo ulivyoshitakiwa nayo.

Mimi napenda sana kukaa nyuma ya wanasiasa wa vyama vyote na kufualitia matamko wanayoyatoa na uchapaji Kazi wao.Ila nachukizwa mwanasiasa yoyote ambaye anaamasisha wafuasi wake watende matendo ya kuvunja Sheria za nchi na kuhatarisha Amani ya nchi kwa makusudi.

Hii tabia sipendi Kwani mwisho wa siku wanatumia ni wafuasi siyo viongozi Hao wakuu na hata wanapopelekwaga gerezani wanasiasa wenye vyeo Vya juu  huifadhiwa  Kwenye vyumba vyenye hadhi wale wafuasi wa kiongozi Huyo uwekwa Kwenye selo ya 'Kajambanani'.

Mdee Jana Oktoba 8 Mwaka huu,  wakati unaondoka Katika Mahakama ya Kisutu ulitamka baadhi ya maneno Kuwa ulivyolala gerezani Juzi wala hawajakukomoa.

Hivi kwani kuna mamlaka ilikuwa imepanga kukukomoa ulalae gerezani kwa makusudi?Kwani ulivyokuwa gerezani ' ulikula Bata'.

Huo uongo wadanganye watu ambao Hawajawahi kutembelea magezera na kupata Habari za Magereza wanayolala mahabusu na hawajawahi kuona picha za magereza yetu.Kama kule gerezani ulikolala  Juzi ulikuwa 'unakula Bata', kitu gani sasa kimekufanya urudi uraiani?

Hayo ni maneno ambayo umejitutumua  tu Mbele za watu ila naimani ukipata wasaa na kukaa peke yako,HIvi sasa utakuwa unajua ni kwanini ulitenda makosa   yaliyosababishwa ufunguliwe Kesi mahakamani maana hata Askari Magereza wenyewe wanaowalinda  Wafungwa,mahabusu lakini  kila siku wanasema  gerezani siyo sehemu nzuri ya Mtu kupelekwa na ndiyo Mtu yoyote akitoka gerezani Kama ni muumini wa dini ya Kiislamu anaenda kufanya Kisomo na Kama ni Mkristo anaenda kufanya Misa Maalum ya kumshukuru kumalizana na Mkosi wa kulala gerezani na kushitakiwa mahakamani lakini ajabu wewe mwanamke wenzetu unashangilia jambo hilo. Ni ajabu sana.

Sasa namshangaa Mdee ,anavyotuambia 'amekula bata' gerezani.Kwa hiyo Ana Ana maanisha Kuwa HIvi sasa  Magereza yetu ni mazuri sana hadi watu tuanze kuvunja Sheria kwa makusudi huku uraiani ili tupelekwe gerezani nasisi 'Tukale Bata? 

Nijuavyo Mimi Hakuna bingwa wa Shida na Mara kwa Mara mahabusu wamekuwa wakinilalamikia Kuwa gerezani siyo kuzuri na taarifa nilizo nazo ni kwamba baadhi ya mahabusu wa gereza la Keko wanaokabiliwa na Kesi za Madawa,Mauaji wamegoma.

Ule umati uliofika Jana mahakamani kukulaki ukitokea gerezani, Kwani miongoni mwao ni wanaume, kwanini usingewauliza ni kwanini wanaume wale walishindwa kuwaruhusu wake ,wapenzi zao washiriki  kwenye yale maandamano haramu  ambayo yamesababisha ufunguliwe kesi na ulale gerezani?

Baadhi ya wanachama waliofika mahakamani Kisutu Jana nawafahamu na wengine wana vyeo Vya udiwani nilivyowauliza kwanini ni wanafki wakamshangilia Mdee Kinafki uwa eti ni Shujaa lakini Oktoba 4 Mwaka huu,walizuia wake na wapenzi wao wa kike wasishiriki maandamano haramu yaliyokuwa yameandaliwa na Mdee walinijibu wake zao wana watoto na watoto wao bado wanaitaji kulelewa NA mama zao  ,ila Mdee kwakuwa bado hajajaliwa na Mwenyezi Mungu kupata mtoto ,maandamano Yale yanamfaaa Kwani hata akiumizwa na kupoteza Maisha Hana Hasara.

Jibu hili liliniuma sana na Kusema kweli mla nawe hafi nawe.Misina ushahidi Kama Mdee Hana mtoto na Kamwe siwezi kumsimanga mwanamke mwenzangu ambaye haja bahatika kupata mtoto. 

Na ni lilitimisha kwa kuwaona wanaume wale na baadhi ya wanawake wa Chama hicho ni wanafki ,wakamshangilia Mdee kinafki na Kumbe hawampendi Mdee kwa dhati.

Hadharani wanajifanya wanamshangilia Mdee ,ila wakikaa vipembeni wanamkebehi Mdee.Ni unafki na dhambi ya Haki ya juu.

Mdee unapaswa utambue ndani ya vyama Vyama Vya siasa vina Siri nzito zilizofichwa kwa baadhi ya viongozi wa vyama hivyo ambao hata wewe uwenda hufahamu Kama wana siri hizo.Siku ukija kufahamu ,utatayari.

Kama una akili timamu unapaswa ujiulize ni kwanini wewe na baadhi ya wanachama mmetuhumiwa kutenda   makosa hayo Jumamosi iliyopita chap chap mmefikishwa mahakamani  lakini Mwenyekiti wa Chama Taifa Freeman Mbowe alitoa maneno mazito ya kutaka viongozi wake wanaandaa maandamano yasiyo na kikomo na wasiombe Kibali Polisi ,  Septemba   14 Mwaka huu.

Siku chache baadae aliitwa Polisi akahojiwa na Polisi wakamsindikiza hadi Uwanja wa Ndege akasafiri kwenda Nchini Afrika Kusini na hadi Leo kimya bado hajafikishwa mahakamani  Licha anaweza kufikishwa muda wowote DPP akiona Ana Haja ya kumshitaki.

Rais Kikwete kila siku anasema ' akili za kuambiwa changanya na za kwako'. Hivi vyama vya upinzani vijana wenzangu msiviingilie kwa pupa sana ,vina siri nzito ndani yake na hivi vyama tutake tusitake vinawenyewe na hao wenyewe walivyovianzisha walivianzisha kwa malengo maalum ambayo siyo yale yaliyowekwa kwenye Katiba za vyama.

Sisi wenye bahati  ya kuteta siku moja moja na baadhi ya viongozi wa vyama hivyo wanatuelezaga mengi na tumeishaona mengi sana.Minakutazama  tu .Shauri yako. .Nenda Taratibu, Wazaire wanasema ' Malembe Malembe'

Mdee hayo madaraka uliyopewa yasikutie wazimu, wakiamua walioviunda vyama hivyo ambayo hata siku Moja huwaoni Kwenye vikao Vya vyama hivyo Vya upinzani, wao wanakaa Mbali ,wanaviendesha vyama hivyo wakiwa Gizani, wakiamua siku kukung'oa madarakani , watakusukia ajenda Moja iliyosimama na watakunyang'anya hayo madaraka na utakuwa Huna la kufanya .

Na hao wanaokuvimbisha  kichwa Leo maana  Tayari wameisha kufahamu  Kuwa wewe ni kiongozi unayependa sifa ,kusifiwa hata ukifanya Ujinga  ndiyo watakuwa wa kwanza kukugandamiza Kuwa ulikuwa ukikiua Chama. Nayasema haya nimeyaona na siku ya kikufika ndiyo akili itakuwa sawa.

Mdee bado hujafikia kipaji Cha ushawishi wanawake wakuunge mkono Kama kipaji alichokuwaga nacho wanasiasa wanawake wa Enzi  zile TANU, BIbi Titi Mohamed, Lucy  Lameck. Bado sana.

Nimalize  kwa kumwambia Halima  Mdee Tulia uzae .Mdee nakushauri zingatia  maneno ya Makungwi Kuwa 'mwanamke anapaswa kufanya vurugu chumbani' siyo barabarani Kama ufanyavyo . 

Achana na tabia ya kufanya vitendo vya kihuni ambavyo unafikiri vitakupa umaarufu wa sifa mbaya. 

Na hao Leo  wanaojifanya kukushangilia wengine kupitia mitandao ya kijamii mwisho wa siku ndiyo watakwa wa kwanza kukuangamiza. 

Hata waliokuwa wafuasi 52 wa Kesi ya Sheikh Ponda Issa Ponda ,walipofikishwa mahakamani mwaka jana kwa makosa kama yako,wao na wapambe wao walikuwa na vibweka sana tena zaidi ya wewe na hadi walikuwa wakitaka kutupiga waandishi wa Habari ndani ya mahakama lakini kesi Yao ilipoanza kushika kasi akili iliwakaa sawa,walikuwa wapole na Wakaanza kujikomba kwa waandishi wa Habari ,mapolisi, askari magereza na watumishi wa Mahakama.

Sasa na wewe Mdee Jana ilikuwa ni Haki yako kupayuka Yale maneno uliyopayuka pale Mahakamani, lakini Kesi ikianza kushika kasi lazima utatulia tu , wale wafuasi wako walikuja kwa Wingi mahakamani Jana hutauona, idadi ya umati ule utapungua. Tumeyaona haya.Tusubiri wakati.

Haya Bunge Maalum la Katiba limemaliza muda wake Marais wetu Wawili wa pande zote wamekabidhiwa  Katiba iliyopendekezwa na Bunge ,NA wameisifu Kuwa ni Katiba bora  na wamesema wa awashawishi wananchi waipigie kura za Ndio nyingi.

Sijiu sasa kijana mwenzangu Mdee unajipanga 'atoke vipi' ,maana  ndiyo basi tena Katiba ya Samuel Sitta imeishapatikana , na Biashara yenu ya kufanya maandamano haramu ndiyo haina Soko tena maana Polisi wameacha tena kuwadekeza.

Na Joto hili sijui kombati mtazivalia wapi,sizitawavuka?

Mdee nakushauri ongoza wanawake wenzako wa Bawacha ambao Wengi nawafahamu ni wanawake na wasichana wanaojiheshimu Kama wakina Ester Wasira kufikia Malengo mliyojiwekea .Usiwaongoze wanawake wenzako kwenda kufanya matendo ambayo yamekatazwa na Sheria.

Naendelea kutoa rai kwa  Jeshi la Polisi chini ya IGP- Ernest Mangu, liendelee kufanya Kazi zake kwa mujibu wa Sheria na lisimuonee haya wala huruma Mtu yoyote hata akiwa ni mwanamke.

Kama mwanamke anashiriki maandamano haramu basi mwanamke Huyo ni wazi amejizatiti Kupambana na Polisi, Polisi na Nyie pambaneni naye  Kwani Sheria ni Msumeno.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blog: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Oktoba 9 Mwaka 2014


No comments:

Powered by Blogger.