MANISPAA YA KINONDONI 'MTATUUA' KWA TB
MANISPAA YA KINONDONI 'MTATUA' KWA TB
Na Happiness Katabazi
ITAKUMBUKWA kuwa Oktoba 23 Mwaka huu, Kituo cha Dalala Cha Simu 2000 kilichopo Mtaa wa Sinza ' C' Kata ya Sinza Wilaya ya Kinondoni ,Dar es Salaam,kilichopo karibu na Shule ya Sheria kilianza kufanyakazi kwa madaladala kuanza kutoa huduma wanaotumia usafiri wa umma.
Nikiwa Kama Mwananchi na Mwandishi wa Habari mzalendo kwa taifa langu , Kituo hicho kiliapoanza kufanya kazi siku hiyo iliandika Habari ya kupongeza serikali kwa kutujengea Kituo hicho cha kisasa Katika eneo Hilo na picha nilipita na ushahidi wa Hilo, upo Humu ndani ya ukurasa wangu wa Facebook.
Msimamo wangu wa kupongeza serikali kwa kutujengea Kituo hicho uko pale pale haujabadilika ila Leo nakuja na ombi jingine kwa Manispaa ya Kinondoni ambayo Kituo hicho kipo chini yake licha bado hakijazinduliwa rasmi.
Mapema kabisa natanga za maslahi yangu Kuwa Mimi ni miongoni mwa wakazi tunaoishi kandokando ya Kituo hicho Cha mabasi hivyo ninavyoandika makala.
Kituo hicho tangu kilipoanza kufanyakazi , kweli eneo Hilo limekuwa na ongezeko kubwa la Magari na watu na Biashara mbalimbali zimeongezeka Hali inayosabaisha eneo Hilo kugeuka ni eneo la Biashara.
Pia nao matapeli waliojigeuza ni madalali nao wameibuka kwa kuwalaghai watu wanaofika Katika eneo Hilo Kutafuta fremu kwaajili ya kupangisha ili waendeshe Biashara zao.
Matapeli Hao wamekuwa wakiwarubuni watu wenye Shida hiyo Kuwa wao eneo Hilo wanalijua vizuri kumbe ni waongo na Kuwapeleka Katika nyumba za watu wa eneo Hilo ambao wanaendelea na ujenzi wa fremu Kuwa fremu hizo zitapangishwa na kwamba wenye nyumba wanawafahamu watawaunganisha nao ili Wawakodishe hizo fremu.
Matapeli wanawataka watu Hao wawapatie sh.5,000 hadi 10,000 eti kwasasa wamepewapeleka kuwaonyesha fremu hizo Kumbe ni uongo hata Wamiliki wa nyumba hizo hawa wafahamu hata kwa sura. Kuweni makini Mnaotafuta fremu eneo Hilo.
Nirejee kwenye ajenda yangu Leo, ambayo tangu Kituo hicho kianze kufanya kazi ni wazi wakazi wa eneo na watumiaji wa kituo hicho tupo kwenye hatari kubwa ya kupata Maradhi Ukiwemo ugonjwa wa Kifua Kikuu(TB).
Nasema hivyo kwasababu barabara Kuu inayotumiwa madaladala barabara ,Magari madogo watembea kwa miguu Katika eneo Hilo la Kituo , Ina vumbi la kutisha Hali inayosababisha baadhi ya watembea kwa miguu wakiwa wanatembea Katika eneo Hilo kujifunika vitambaa Katika Pua zao.
Na wakazi wa eneo Hilo Ndio tumekuwa Katika wakati mgumu sana Kwani huwezi kukaa nje kwakuogopa vumbi na ukikaa ndani vumbi linaingia ndani na kusababisha nyumba Kuwa Kama kiwanda Cha Kutengenezea cimenti.
Sitanii, ni ukweli mtupu, hatuna raha tena ndani ya nyumba tunazoishi kwasababu ya vumbi kuingia sebuleni hadi vyumbani, ukifagia ukideki ni kazi bure.
Minajiuliza hivi Manispaa ya Kinondoni kupitia maofisa wao hawalioni hili? Hivi Manispaa ya Kinondoni inashindwa kutoa Gari lake Moja likalijaza maji Likaja kumwagia barabara hiyo ili kupunguza vumbi Hilo Kali?
Au Manispaa ya Kinondoni inasubiri wakazi wa eneo hilo siku tuanze kujazana kwa Wingi Katika kitengo Cha ugonjwa wa TB Katika Hospitali ya Sinza Palestina na Mwananyamala tukienda kuchukua vidonge Vya TB kwasababu ya kuathiriwa na vumbi Hilo ndiyo itafurahi?
Au hiyo Manispaa ya Kinondoni ndiyo itasema haina Fedha ya kujaza mafuta Hilo Gari na Fedha ya kununulia maji ya kumwaga Katika barabara hiyo?
Au Manispaa hiyo italileta Gari Hilo Lije limwagie maji barabara hiyo vumbi lipungie siku kiongozi Mkuu wa Kitaifa atakapokuja kuzindua Kituo hicho?
Ebu Manispaa ya Kinondoni acheni ubahiri ,na muwathamini wakazi wanaoishi eneo Hilo Kwani nao ni binadamu na wana Haki ya kuishi na kukingwa na Maradhi yanayokingika.
Kwa vumbi hilo linaloendelea kututesa kutokana na ongezeko la Magari kutumia barabara hiyo, nitakuwa sijakosea nikisema Kituo hicho ama ni kaburi au ugonjwa wa TB kwa wakazi wa eneo Hilo. Tuoneeni huruma wenzenu vumbi litatoa roho zetu.
Uwepo wa Kituo Cha Dalala Cha Simu 2000 Katika eneo Hilo ,isiwe ni Chanzo Cha wakazi wa eneo Hilo kupata TB.
Naamini Manispaa ya Kinondoni ikiamua inaweza kutoa Hilo Gari likaja kuondoa vumbi kwa kuweka utaratibu wa mara kwa mara gari hilo walau mara tatu kwa wiki kuja kumwagia maji hiyo barabara hadi mwisho siku barabara hiyo ikaja Kujengwa Katika ngazi ya lami.
Wakati Kituo hicho kina jengwa,Manispaa ilikuwa ikitoa Gari hilo Kuja kumwagia maji barabara hiyo na vumbi Likawa linapungua.
Lakini pia hata siku Chake Kabla ya Rais wa Marekeni Barack Obama, kuwasili nchini,tulishuhudia usafi wa Hali ya juu na barabara zilikuwa zikimwagiwa maji na Magari hayo.
Na kweli Dar es Salaam, ilikuwa safi sana.Ndiyo maana kila siku natamani Rais Obama awe anakuja hapa Tanzania ili Tanzania tuwe wasafi kweli kweli Kwani sisi ni wachafu wa makusudi na wakujitakia na uenda tuna matatizo Katika akili zetu.
Kwasababu Kama tuna akili timamu tusingekuwa tuna kubali siku zote kulea uchafu na siku tunayosikia Rais Obama ,anakuja basi ndiyo tunafanya usafi.Kumbe tunaweza Kuwa wasafi tukiamua.Mungu atusaidie sana.
Chanzo:Facebook: Happy Katabazi
Oktoba 28 Mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment