TUNA 'CHUI WA KARATASI' SIYO WAANDAMANAJI
TUNA 'CHUI WA KARATASI 'SIYO
WAANDAMANAJI
Na Happiness Katabazi
SOTE ni mashahidi kila kukicha tumeshuhudia nchi zenye
machafuko jinsi wanausalama wanavyopambana na raia
wanaovunja Sheria za nchi zao kwa Madai Kuwa wanaendesha
maandamano kushinikiza wapate Haki zao kwa kuvunja Sheria.
Kupitia vyombo mbalimbali vya Habari Vya Kimataifa , tumeona
waandamanaji wa nchi hizo zenye machafuko makubwa kila
kukicha wakipambana bila kuchoka na wanausalama licha
wanausalama wamekuwa wakiwadhibiti lakini raia hao nao
wamekuwa wakijibu mapigo kwa kurusha mabomu , kuchinja
Askari na kuwateka na kufanya uharibifu mkubwa na wala raia
wa nchi hizo hawa ombi vibali Vya kuandamana majeshi
Yao ya Polisi , wao wanaaandamana wanavyotaka na wanapambana
mwanzo mwisho na Askari licha wanauwawa na kuumizwa
sana.Lakini wanapambana.
Binafsi Kama maandishi wa Habari ,nilishiriki kikamilifu
kuripoti maandamano haramu yaliyokuwa yakifanywa na Chama
Cha CUF Miaka ya 2000 - 2002 pale Uwanja wa Kidongo
Chekundu Dar es Salaam, na Mara nyingi yalikuwa yakifanyika
Ijumaa.
Maandamano yaliyopangwa kufanywa na Chadema ,Dar es Salaam,
Januari 5 Mwaka 2008 asubuhi siku hiyo
yalipangwa kuongozwa na Marehemu Chacha Wangwe katika
viwanja vya Bakheresa - Manzese lakini jeshi la polisi
likayasambaratisha.
Lwakatare ambaye hasa ndiye alikuwa
anatoa matamko wakati huo wa kuamasisha
umma Kuwa maandamano hayo siku hiyo ya
Jumamosi ya Januari 5 Mwaka 2008 yangekuwepo licha Polisi
iliyapiga marufuku.
Na hata maandamano yaliyokatazwa na Jeshi la Polisi kwa wiki
mbili Septemba mwaka huu, mfululizo sasa, Lwakatare huyu
Huyo ambaye aliogopa kifanya maandamano Januari 5 mwaka 2008
kwa kuogopa kipondo cha polisi , eti amenukuliwa na Gazeti
la Nipashe la wiki iliyopita Akisema ni lazima
waandamane.Kioja Cha aina yake.
Nakumbuka Usiku huo huo wa Januari 5 Mwaka
2008 , ndiyo watu wasiyojulikana waliovamia Ofisi iliyokuwa
ya Gazeti la Mwanahalisi na kuwajeruhi waandishi wa Gazeti
Hilo, Saed Kubenea na Ndimara Tigambwage.
Gazeti la Mwanahalisi limefungwa na serikali kwa
muda usiojulikana kwasababu lilibaini alifanya
kazi zake kwa kuzingatia Maadili ya Taaluma ya Uandishi wa
Habari.
Siku hiyo ya Januari 5 mwaka 2008 tangu asubuhi hadi
mchana , Askari Polisi walitanda eneo lote la
Kinondoni, Mabibo, Ubungo, Manzese, Tandale, Ofisi za
Makao Makao ya Chadema na Ofisi za Ubalozi wa Kenya
ambapo Chadema walikuwa wamepanga Kupeleka ujumbe wao Katika
Ubalozi huo na Polisi ilikuwa imewazuia na wao
wakasema watatumia njia za mafichoni kuandamana
na kufikisha ujumbe wao Kuwa serikali ya Tanzania
ilishiriki kuchakachua Matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Kenya
ambao ulimpa ushindi Rais Mwai Kibaki ambaye HIvi sasa ni
Rais Mstaafu.
Tangu saa Moja asubuhi waandishi wa Habari tuliokuwa
tumepangwa kwenda kuripoti maandamano hayo na wakuu wetu wa
Kazi tulikuwa tumefika eneo la tukio na ninakumbuka wakati
huo nilikuwa na ujauzito wa mwanangu Queen 'Malkia' na
kwakuanzia tulianzia kuweka kambi Katika Bar Moja iliyopo
eneo la Mabibo karibu na Soko maarufu Kama Mahakama Ya
Ndizi, huku tukishuhudia Magari ya Polisi ya Maji ya
kuwasha' kikojozi' yakiwa yanarandaranda maeneo hayo Tayari
kwaajili ya kukabiliana na waandamanaji wa Chadema
ambao walijigamba wangeandamana hadi Katika Uwanja wa
Bakheresa - Manzese Dar es Salaam.
Ilipofika saa mbili asubuhi Waandishi 'watukutu'
tulianza kumpigia simu Mkuu wa Ulinzi na Usalama wa Chadema,
, Lwakatare kufahamu yeye na msafara wake wanapita njia gani
na kwamba wakafikia Kwenye Viwanja hivyo saa ngapi ili
tuwahi kwenda kuripoti Habari zao?
Natoa mfano huu hai ili wenye akili timamu wajifunze,
hadi Ilipofika saa Saba mchana sisi waandishi wa
Habari Askari wa Jeshi la Polisi mkoa wa
Kinondoni tulikaa na kuanza kupiga soga huku , Polisi
wakitafuta urafiki kwetu waandishi wa Habari tuliokuwa
tikiwasiliana na Wangwe na Lwakatare ili tu
waelewe viongozi Hao wa Chadema muda huo wamefika wapi ili
Polisi sasa wawataarifu Polisi wenzao wawafuate waandamanaji
Hao huko waliko ili wawapatie wanachokiitaji.
Na siku hiyo baadhi ya Makachero wa Polisi walikuwa
wakituambia kwa Siri Kuwa 'Hatua Moja ya atakayeandamana ni
kilungu Kimoja'.Tulicheka sana..
Sisi tuliwaeleza Polisi Kuwa Lwakatare Kasema yupo na
msafara wake wanapita njia za Panya kutokea njia ya Tandale
na wataibukia njia ya Kanisa Katoriki Manzese Kisha waje
Katika Uwanja huo wa Bakhresa.
Na sisi waandishi 'watukutu' tulikuwa tukio nyonya taarifa
za kushushushu kutoka kwa makachero ambao
tunafahamiana nao.
Waandishi na Wapiga picha tulienda Kwenye njia hizo ambazo
Wangwe na Lwakatare walisema ndiyo wanatumia kufika Bakresa-
Manzese na wakatutaka twende tukawapige picha na kweli
tutaondoka eneo la Bakhera tukaenda maeneo hayo ambayo
walitutajia wapo ili tu tu wapigie picha
wanavyotembea Kuja Katika Viwanja Vya Bakhresa na kwamba
Tayari wameamua kutumia njia hiyo kukwepa Polisi.
Tulipita njia zote hizo lakini hawakuwepo na Ilipofika saa
nane Wangwe alinipigia simu akasema yupo Kinondoni nyuma ya
Bar Moja waandishi wa Habari twende , ndiyo waandishi
tulienda tena tulisimama yeye alikuwa amesimama chini
ya Mti huku makachero wa Polisi nao wametuzingira huku
Wangwe akiwa anaongea Kwa wasiwasi baada ya kubaini
makachero nao wamo Kwenye kundi la waandishi wa Habari
wanamsubiri aongee anachotaka kuongea.
Ujasiri wa Wangwe uliyeyuka ghafla
baada ya kubaini Tayari ameishazingirwa na makachero ,
alisema wameamua kuhairisha maandamano hayo na
watayafanya siku nyingine ila ' message sent' na Kisha
akaondoka.
Hali iliyosabisha sisi waandishi wenye akili timamu
kuanza kuwadharau wanasiasa wa aina hii ambao ni
mabingwa wa kutoa vitisho kwa dola kupitia vyombo Vya Habari
lakini pindi dola linapowasogolea ufyata Mkia.
Na huu ni mfano mmoja tu, Mifano ni mingi sana ya hawa
wanasiasa wetu mabingwa wa kupayuka majukwaani na kutoa
maelekezo kwa wanachama wao yanayovunja Sheria.
Waandamaji na wagomaji wa ukweli ni majasiri, Kwanza uwa
wanajua Haki wanayoidai. Kwahiyo hata polisi ikiwazingira na
kutaka kuwashughulikia ,waandamanaji hao upambana hadi tone
la mwisho na Askari Hao ili watetee haki Yao.
Ukijua Haki yako unayoidai, sheria za nchi zinataka nini
huwezi kuandamana Katika maandamano ambayo Jeshi la Polisi
linakuwa limeishayapiga marufuku.
Kwani Ikumbukwe Kuwa Haki ya MTu mmoja inapoishia ndiyo Haki
ya MTu mwingine inapoanzia .Haina maana kuandamana halafu
hajui Haki unayoidai?
Pia aina maana uandamane mitaani halafu uondoke eneo la
tukio bila kupata haki unayoidai.
Sasa naona ajabu sana kwa hawa wafuasi wa Chadema ambao
wametakiwa na viongozi wao wa juu akiwemo Mwenyekiti wa
Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe na Wilson
Kigaira kuandamana nchi nzima bila kikomo halafu wa wakiona
Polisi wamewazingira wana salimu amri mapema ila
wakitoka mikono ni mwa Polisi na Kurejea mitaani
wanaanza kubwatabwata na kuhadaa wanachama wao ambao
hawafahamu Kuwa viongozi wao ni 'Chui wa karatasi,
wanaogopa vifungu, mitama ya Askari polisi' na wala hawana
ubavu wa Kupambana na dola.
Waandamanaji majasiri kwanza Hawaogopi risasi,
virungu,vipepsi, mateke, mitama na Kamwe hawasalimu
amri ya Jeshi la Polisi ijayowataka
watawanyike....waandamanaji Hao majasiri wanakaidi
amri hiyo na wanapambana kufa na kupona na Askari Hao hadi
tone la mwisho.
Ajabu hawa 'waimba mipasho wetu ' yaani wanasiasa
uchwara wa Chadema wanaowatangazia wafuasi wao
waandamane bila Kibali Cha Polisi lakini
Polisi ikiwakaribia wanafyata Mkia mapema kabisa!
Ndiyo mAana Nasema hapa Tanzania Hakuna waandamanaji wa
ukweli ukweli 'majasiri' , Bali kuna waandamanaji
uchwara ambao nawafananisha na 'Chui wa Karatasi'.
Sijui kwanini waandamanaji hao uchwara ambao ni
wanaume wanaogopa Kupambana na wanaume wenzao yaani Polisi
ambao awali Walijitapa hawawaogopi?
Mwanaume anapambana na kusimamia kile alichokisema na
haogopi lolote. Sasa hawa viongozi wenye jinsia ya
kiume wa Chadema waliotoa kauli za kuamasisha wafuasi
wao waandamane halafu wanapoandamana na kudhibitiwa
kilaini na Polisi wanaamua kusalimu amri, HIvi hawa ni
wanaume kweli ambao Tunaelezwa kila siku Kuwa mwanaume
anatakiwa awe ni MTu mwenye msimamo wa kusimamia Yale yote
anayoyasema na kufanya mambo yake kwa vitendo siyo maneno
maneno?
Huu ni ushahidi kwamba hawa waandamanaji uchwara wa Chadema
ni watu wasiyojua Haki zao na hawajui wanaaandamana Kudai
Haki ipi na ni watu wanaoshurutishwa kwenda kufanya
vitendo Vya Uvunjifu wa Sheria na viongozi wao na mwisho wa
siku wanaumbulia vipigo kutoka jeshi la Polisi na
kufikishwa mahakamani wao binafsi.Ni uzuzu wa aina yake.
Hapo zamani watu walikuwa wanapenda Kusema Kuwa ni wanawake
ndiyo wenye tabia ya Kupenda Kusema sema sana. Lakini
sasa naona Hali ni tofauti hapa nchini,wanaume hasa viongozi
wa kisiasa ndiyo wamekuwa na sifa hiyo ya kike ya Kupenda
kuongea ongea ovyo hadharani tena wakati mwingine wanatoa
matamko ambayo yanaamasisha vitendo Vya Uvunjifu wa
Sheria.Aibu sana.
Alhamisi iliyopita Mbowe alikwenda Makao Makuu ya Jeshi la
Polisi kuhojiwa na aliambatana na Mawakili wake , na wafuasi
wa Chama hicho ambao waliitikia wito uliokuwa umetolewa na
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika uliowataka
wajitokeze kwa Wingi siku hiyo kwenda kumsindikiza Mbowe
Polisi ambapo hata hivyo Jeshi la Polisi liliwatawanya
,kukamata na wengine kuwafikisha mahakamani, na
ikadaiwa kuwa baadhi ya waandishi wa Habari walidai
kujeruhiwa na baadhi ya Vya siasa, wanaharakati wakaibuka na
Kusema eti wanalilaani Jeshi la Polisi.
Jumamosi iliyopita Chadema mkoa wa Arusha walidai
wataandamana lakini Kamanda wa Polisi Mkoani hapo Liberatus
Sabas na Mkuu wa Upelelezi wa mkoa huo Duan Nyanda walikuwa
wamejipanga kisawasawa na waliakikisha hakuna
mwandamanaji atakayepata fursa ya kuingia mtaani
kuandamana ambapo Polisi wa Arusha walizingira nyumba
ya Mbunge wa Arusha, Godbless Lema na Joshua Nansari
Pia Ijumaa iliyopita Polisi Mkoani Morogoro iliwasambaraisha
wafuasi wa Chadema ambao walikuwa wakitaka kuandamana na
kuwakamata baadhi na kuwafikisha mahakamani.Pia Jumapili ya
Wiki iliyopita Mkoani Mtwara ,Polisi walifanikiwa kuzima
jaribio Lao la kuandamana.
Lakini Jumapili iliyopita tulimsikia Kigaira akitangaza kuwa
chama hicho kitafanya maandamano ya wiki nzima ambayo
yataanzia Septemba 22 mwaka huu.Na hadi leo hii makala hii
imechapishwa sijasikia wala kuona wakiandamana. Tusubiri
Tuone Kama maandamano hayo yatafanyika na Lengo Lao
litatimia.
Mimi napenda Mageuzi naninapenda vyama vyote Vya siasa Kwani
vinaleta Changamoto na Kamwe siwezi kubeza mchango
uliotolewa na baadhi ya vyama upinzani hapa nchini .
Chadema ni miongoni mwa Chama Cha upinzani ambacho
kilitokewa Kupendwa na baadhi ya watu na kweli
kimefanyakazi kadri ya uwezo wake.
Wenye macho tuliona na Chadema kiliapoanza kujikwaa Kwa
kuanza kujihusisha chini chini kuamasisha watu washiriki
kwenye vitendo vya kufunja sheria kama kulazimisha kufanyika
kwa maandamano, migomo nilitaadharisha kupitia kalamu
yangu ila baadhi ya wanahabari wanafki wanaojikomba
kwa viongozi wa juu wa Chama hicho walinipinga na kuniona
adui na wengine walipendekeza nifukuzwe na Kazi Katika vikao
vyao Vya Siri.
Lakini ona Leo hii Kauli ya Mbowe Yakutaka wanachadema
wagome na waandamane bila kikomo ilivyoporomosha heshima na
uaminifu wa Chama hicho kwa Jamii ya wapenda Amani? Leo hii
Chadema imebatizwa ni Chama Cha vurugu na sumu hiyo inazidi
kusambaa na inaendelea kusambaa.
Sumu ya aina hiyo ya ya Chama Cha vurugu,udini , ndiyo
iliyokikaghalimu hadi Leo Chama Cha Wananchi CUF.
Chadema Huyo Mshauri anayetoa ushauri Chama hicho kifanye
maandamano yaliyoharamishwa na jeshi la Polisi,
mhepukeni maana hafai amewapa ushauri ambao
umeishaporomosha heshima ya Chadema na
viongozi wake.
Jumapili iliyopita Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim
Lipumba aliongea na waandishi wa Habari pamoja na mambo
mengi alisema CUF inalaani Polisi kupiga waandishi wa Habari
na inaunga mkono maandamano yaliyotangazwa na Chadema licha
Polisi Mara Kadhaa imetoa tamko la kutapiga marufuku
kwasababu maandamano hayo ni haramu.
Binafsi ni Mwandishi niyependa kutunza Kumbukumbu
mbalimbali. Mwaka 2005 wakati Mkuu wa Jeshi la Polisi
alikuwa ni Omar Mahita alizungumza na vyombo Vya Habari na
Kusema Kuwa Polisi imekamata Shehena ya silaha Kama mapanga,
Visu na kwamba Kontena Hilo lilikuwa limeingizwa nchini na
CUF kwaajili ya Kuja kufanya vurugu Katika uchaguzi
Mkuu Oktoba 2005.
Wakati huo Mimi nilikuwa Mwandishi wa Gazeti la Mtanzania,
kweli kashfa hiyo ya kuingiza Shehena hizo za silaha
za Jadi nchini ziliigharimu CUF , Kwani Jamii
ilicharuka na vyombo Vya Habari viliwageuzia kibao na kila
siku vyombo Vya Habari vikawa vinachapisha Habari ya kulaani
CUF kwanini imefanya kitendo hicho Hali iliyosababisha
baadhi ya wafuasi wa CUF kuona waandishi wa Habari
wanatumiwa na CCM kuchafua CUF Kuwa ni Chama Cha Magaidi
Hali iliyosababisha CUF kuingia Kwenye uchaguzi Mkuu huku
ikiwa Imeandamwa na kashfa hiyo ya ugaidi na kupiga
waandishi wa Habari.
Wakati CUF ilipokuwa ikiandamwa na kashfa hiyo, Jeshi la
Magereza nalo lilituhumiwa Kuwapiga waandishi wa Habari
ambao ni Wapiga picha Mpoki Bukuku sasa yupo gazeti la
(Mwananchi) na Kidanka Christopher ambao nao walidaiwa
kudharau amri ya Jeshi la Magereza ambayo
iliwataka waondoke Katika eneo la Askari Magereza walilokuwa
wa nafanyakazi lakini waandishi hao walidaiwa kukaidi
amri hiyo na Askari Magereza waliwashughulkia kikamilifu
sambamba na kuwachania mashati, Kuwapiga na kuwaacha vifua
wazi.
Hali iliyosabisha Kituo Cha Haki za Binadamu, waandishi wa
Habari kulaani na kushinikiza Aliyekuwa waziri wa
Mambo ya Ndani wakati huo Mwaka 2005 , Omar Mapuri
ambaye pia Alikuwa na wadhifa wa Katibu Mwenezi wa CCF Taifa
ajihudhuru.
Waandishi wa Habari walipitisha azimio la
kususia kuandika Habari za Mapuri Hali iliyokuwa imeiweka
Katika mtego Mbaya Kwani Mapuri ni kiongozi wa CCM lakini
ghafla ilikuja na mbinu nyingine ya
kujinasua katika mtego ili waweze kuingia Kwenye kampeni za
,wala 2005 bila vikwazo.
CCM ikatangaza Kuwa imemzuia Mapuri asiongelee jambo lolote
linalohusu CCM licha nyadhifa zake aliendelea kuzushia.
Na kweli Mbinu hiyo iliisadia CCM na hatimaye ikaibuka
na ushindi mzito ambao ulimuweka Rais Jakaya Kikwete
Madaraka kwa Mara ya kwanza Desemba 21 Mwaka 2005, Kwani
tarehe hiyo Kikwete ndiyo aliapishwa na Aliyekuwa Jaji Mkuu
wa Tanzania ,Agustino Ramadhani Kuwa Rais wanne wa nchi
hii.
Jeshi la Magereza lilifikia uamuzi wa kuwatoa kafara
Askari wake waliodaiwa Kuwapiga waandishi hao ,
wakashtakiwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na
mwisho wa siku Kesi ikaisha na Askari Magereza wale
wakarudishwa Kazini na hivi sasa wapo Kazini nawafahamu.
Naye Mpoki Bukuku alifungua Kesi ya Madai ya zaidi ya
sh.Milioni Mia Moja dhidi ya Waziri wa Mambo ya Ndani,
kwasababu alisababishiwa madhara na Kesi hiyo ya Bukuku
ilifunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Binafsi nilipokuwa Mwandishi wa habari za
mahakamani,nilikuwa nikiiripoti kesi ya Bukuku lakini muda
mchache baadae Bukuku alikubali kwenda
kumaliza Kesi hiyo na mdaiwa ambaye ni Wizara ya Mambo ya
Ndani nje ya Mahakama, na wakati alipoenda kuimaliza
nje ya Mahakama ,Bukuku hakutuleza waandishi wa Habari
za Mahakamani kuwa ameamua kufuta hiyo kesi na anaenda
kuimaliza nje ya mahakama. Ila wakati alipofungua hiyo
Kesi alitusaka na kutuomba tuiandike.
Wakati kashfa hiyo Ikiendelea
kuiandama CUF Kuwa ni Chama Cha Magaidi , kuna siku
Moja Kabla ya kampeni rasmi za uchaguzi Mkuu kuanza ,CUF
iliitisha mkutano na waandishi wa Habari ofisini kwake
Buguruni, na miongoni mwa waandishi tuliofika siku hiyo
mchana Mwaka 2005 ni Mimi na Aliyekuwa Mpiga picha wa
Mlimani TV, wakati huo akiwa Mpiga picha wa Star TV,
Maximilian John ambaye alifariki Mei 24 Mwaka
huu, tulifika hapo Ofisi za CUF na ghafla tuliona
baadhi ya watu wanaodaiwa Kuwa ni wafuasi wa CUF wakianza
kutushambulia ,minilipata upenyo nikakimbia, Marehemu
Maximilian alidakwa na kupigwa na kupasuliwa eneo la
kichwani na Kisha alikimbizwa Hospitalini na kushonwa
nyuzi kazaa.
Profesa Lipumba wala hakujitokeza kulaani kitendo hicho
kilichodaiwa kufanywa wafuasi wake kwa waandishi wa Habari.
Na baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 , CUF
Ilijikuta ikipoteza majimbo yote Tanzania Bara.
Ni huyu huyu Lipumba mapema Oktoba Mwaka 2012 wakati
zilipoibuka vurugu zilizohusisa waumini Wengi wa dini ya
Kiislamu, Katika mkutano wake na waandishi wa Habari alisema
Kuwa Kesi ya jinai 245/ 2012 Jamhuri dhidi ya Shekh
Ponda Issa Ponda na wenzake ilikuwa imefunguliwa Oktoba 18
Mwaka 2012 Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Mbele ya
Aliyekuwa Hakimu wa Mahakama hiyo Victoria Nongwa Kuwa ni
Kesi ya Madai na Si jinai.
Baada ya kumshuhudia Lipumba akitoa tamko Hilo la
upotoshaji wawazi na Mbaya zaidi unafanywa na mtu
mzima Kama Lipumba, msomi, niliandika haraka makala
iliyokuwa na kichwa Cha Habari kisemacho " Profesa Lipumba
ni mbumbumbu wa Sheria, acha Sheria ichukue mkondo wake'.
Makala hiyo ilikuwa inalengo la kumsuta Lipumba aache
tabia yake ya kupotosha umma kwa Kusema Kesi iliyokuwa
ikimkabili Sheikh Ponda Katika Mahakama ya Kisutu ni ya
Madai wakati Si kweli, Kesi ile tuliyoiripoti mwanzo hadi
Ilipofika Tamati Mei 9 Mwaka 2013 , ilikuwa ni Kesi ya
Jinai,na Mahakama ilitamka Kuwa ni Kesi jinai na ilijikuta
na hatia Ponda Kwa kosa Moja la kuingia Kwa jinai Katika
Kiwanja Cha Markas Chang'ombe.
Kwa Kumbukumbu hizo hapo juu, Wafuasi wa Chadema
msikubali pia kuona Lipumba ni MTu mwema sana
mkaendeleza kufanya maandamano, mtakuwa mnakosea huyu
anazungumza ofisini akimaliza anarudi nyumbani kwake kulala.
Alipotosha Kesi ya Ponda Matokeo yake Mahakama ikamuumbua na
Kusema Kesi hiyo ni ya jinai na Ponda anafungwa Kifungo Cha
Mwaka mmoja nje.
Na Lipumba huyu huyu aliyejifanya Anamuonea huruma Ponda
Kuwa anaonewa, hata siku Moja sikuwahi kumuona akifika
pale Mahakama ya Kisuti Kuja hata na chupa ya Maji ya Kunywa
au magazeti Kuja kumuona Ponda. Ni Mke mwenzangu yaani Mke
halali wa Ponda na wanawe ndiyo wanamuangaikia Ponda.
Narudia tena ,Chadema kaeni chini jitazameni upya na
Mmtazameni Kwa makini Huyo Mshauri wenu anayewashauri
mlazimishe kufanya maandamano ambayo kwa zaidi ya Mara Tatu
Jeshi la Polisi imeyapiga marufu lakini nyie mnayalazimisha
tena adharani Kwani Tayari ameishawaingiza mtaroni .
Nakifahamu Vyema Chama Cha NCCR- Mageuzi ,siyo Chama
Chenye historia ya Kudai Haki zake Kwa njia ya Uvunjifu wa
Sheria.Hivyo Narudia tena Chadema itazame CUF ,NCCR- Mageuzi
kweli inawaunga mkono kuandaa maandamano hayo haramu?
Mbona hatuwaoni wafuasi wa NCCR- Mageuzi, CUF Katika
maandamano hayo ambayo yanasambaratishwa tangu wiki
iliyopita na Polisi? Tunasikia ni wafuasi wa Chadema pekee
tu?
Chadema jitazameni upya maana hii sumu ya Chadema ni
Chama Cha Vurugu imawatafuna Kwani Kuna baadhi ya watu
waliokuwa wanaipenda Chadema baada ya Kusikia agizo la Mbowe
la kuwataka waandamane bila kikomo,wamesema wameishapoteza
Imani na Chama hicho Kwani Bila Amani , Chadema haiwezi
haiwezi kufanya siasa kwa Amani.
Hao baadhi ya waandishi wa Habari na hiyo CUF wanaowahaada
Kuwa wanaujua mkono maandamano yenu haramu,
ipo siku ndiyo watakuwa wa kwanza kuwachekea na
Kusema Chadema imepoteza mvuto.
Na huo ubishi wenu wakulazimisha mfanye maandamano Kwa
lazima mkae mkijua , ubishi huo unaweza kusababisha
kumletea madhara makubwa Mwenyekiti wenu Mbowe,
Kwani Tayari Mbowe ameishahojiwa na Polisi, na hamjui
Polisi na ofisi ya DPP itamshitaki Kwa Mashitaka gani au ha
itamshitaki, lakini Nyie ndiyo kwanza mnazidisha kulazimisha
kutekeleza agizo Hilo la Mbowe.
Kama mnaakili timamu hasa wewe Kigaila ulipaswa ujiulize ni
kwanini tangu Mbowe atoke kuhojiwa na polisi amekuwa kimya?
Kumbukeni mtu yoyote anayetamka maneno yanayoamasisha watu
Wengi watende makosa na kuvunja sheria za amani
atashikitakiwa kwa kosa Hilo Kifungu Cha 55 na Mbowe alitoa
tamko lile la kutaka wana chadema waandamane, wagome tena
bila kibari cha polisi kosa ambalo linaangukia katika
kifungu hicho ambacho mshitakiwa akipatikana na hatia
atahukumiwa Kifungo Cha Jela Mwaka mmoja.
Baada ya agizo Hilo la Mbowe ,baadhi ya wafuasi wake wa
mikoa ya Morogoro, Dar es Salaam,waliitikia wito licha
walidhibitiwa kwa haraka na Polisi iliwakamata na Mkurugenzi
wa Mashitaka kuwafungulia Kesi za jinai mahakamani ambapo
Moja ya kosa ni la kuingia kwa jinai Katika eneo la
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kinyume na Kifungu cha 85.
Na Kifungu Cha 124 kinasema mtu yoyote anayekaidi amri
iliyotolewa na mamlaka za dola Kama Mahakama, Polisi Atakuwa
ametenda kosa la kukaidi amri ya mamlaka na Mara nyingi kosa
Hilo uwa wanashitakiwaga nalo waandamanaji haramu
ambao pindi wanapoandamana ,Jeshi la Polisi utoa tangazo
Mara Tatu la kuwataka watawanyike,wakikaidi ndipo
Polisi uanza Kupambana nao na kuwakamata na DPP kuwafungulia
Kesi za Jinai ikiwemo kosa Hilo la kukaidi amri halali ya
Jeshi la Polisi.
Na kosa hili walishitakiwa nalo wafuasi 52 wa Sheikh
Ponda, ambao walikuwa wakikabiliwa na makosa ya
kukagua mkusanyiko haramu, kukaidi amri ya Jeshi la Polisi
iliyowataka watawanyike na wasiandamane kuelekea ofisi
za DPP ambapo Machi 21 Mwaka 2013, Aliyekuwa Hakimu Mkazi wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Sundi Fimbo aliwatia
hatiani kwa makosa hayo na akawa hukumu Kifungo Cha Mwaka
mmoja gerezani.
Na wafuasi kupitia Wakili wao Mohammed Tibanyendela walikata
rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kupinga Adhabu
hiyo ambapo Oktoba 21 Mwaka 2013. Na aitakumbukwa Kesi hiyo
ilifunguliwa na kusikilzwa na kuamriwa Katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi kwa siku 33 tu.
Oktoba 21 Mwaka 2013 Jaji Salvatory Bongole wa Mahakama Kuu
Nfiye alikuwa alisikiliza rufaa hiyo ya wafuasi wa Ponda,
ambapo alisema Mahakama ya Kisutu ilikuwa sahihi kuwatia
hatiani na makosa hayo mawili ila Mahakama ile ikikosea
kuwapa Adhabu ya Kifungo Cha Mwaka mmoja Jela Kwani Sheria
ya Jeshi la Polisi inatamka wazi Kuwa mshitakiwa yeyote
anayepatikana na hatia ya Kutenda makosa ya mkusanyiko
haramu na kukaidi amri ya Jeshi la Polisi iliyowataka
watawanyike ,atahukumiwa Kifungo Cha Miezi Mitatu Jela na
faini ya sh.50,000.
Na Hao wafuasi wa Ponda licha Mahakama Kuu , Oktoba 21 Mwaka
2013 Kusema Mahakama ya Kisutu ilikosea kuwapatia Adhabu ya
Kifungo Cha Mwaka mmoja Jela ,na ikawachiria huru siku hiyo
kwasababu walikuwa wameishakaa Jela muda mrefu, lakini
Tayari wafuasi wale walishasota Jela toka Machi 21 Mwaka
2013 , na tena walitawanywa Katika Magereza Mbalimbali
na walitumikia Adhabu hiyo gerezani zaidi ya Miezi Sita
wakati Mahakama Kuu ikaja Kusema walipaswa kisheria
kutumikia Kifungo Cha Miezi mitatu na kulipa faini ya
sh.50,000.
Kifungu Cha 74 kinatoa tafsiri ya kosa la mkusanyiko
haramu.Kifungu Cha 75 kinatoa Adhabu kwa mshitakiwa
anayepatikana na kosa la kufanya mkusanyiko haramu.
Kifungu Cha 55 kinakataza Mtu kushawishi
watu watende makosa ya jinai ambayo yanavunja Sheria na
kuhatarisha Amani.
Natoa raia kwa baadhi ya waandishi wa Habari wenzangu
waache tabia ya kuandika makala za kuunga mkono
matamko ya baadhi ya wanasiasa yanayo wataka wafuasi wao
wafanye vitendo Vya Uvunjifu wa Sheria Kama tamko
lililotolewa na Mbowe, Septemba 14 Mwaka huu, lilowataka
wafuasi wa Chama Chake waandamane bila Ruhusu ya
Polisi.
Vifungu hivyo hapo ya Sheria kuwa wale watakaoenda kuvisoma
Kwani vifungu hivyo vyote vipo ndani ya Sheria ya Kanuni ya
Adhabu ya Mwaka 2002 , na nakala ya hukumu ya wafuasi wa
Ponda ' Precedent' , zinaonyesha wazi kukaidi amri ya Jeshi
la Polisi iliyokutaka usiandamane,utawanyike ni kosa
kisheria.
Hivyo wanahabari tutumie kalamu zetu kuelimisha umma
vizuri kwa maslahi ya taifa letu. Na Kama Mwandishi wa
Habari ,Mhariri hufahamu Kuwa kuandamana bila
Kibali Cha Polisi ni kosa ,uliza kwasababu Kifungu Cha
8 Cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Mwaka 2002, kinasema
kutojua Sheria siyo kinga ya kutokuadhibiwa.
Kwahiyo na sisi waandishi wa Habari ambao tunaandika makala
ambazo badala ya kufuata miiko ya taaluma, Sheria za nchi
zinataka nini badala yake tunaingia mapenzi na ukereketwa wa
baadhi ya vyama tunavyoviunga mkono au wanasiasa tunaowaunga
mkono kuelekea Uchaguzi Mkuu Mwaka 2015.
Tukae tukijua tunaweza kujikuta tunaingia matatani kwa
kushawishi pia wananchi mAana kupitia mitandao kuna baadhi
ya waandishi wanasema maandamano ya Chadema ni halali wakati
Si kweli ,Jeshi la Polisi iliyapiga marufuku.
NI aibu sana kwa Mwandishi wa Habari mwenye hadhi ya Mhariri
Kusema kupitia mitandao Kuwa maandamano ni Haki na
muandamanaji haitaji kupata Kibali Cha Polisi.
Ni Mbowe huyu huyu aliwataka wanachama waandamane bila
kuomba Kibali Cha Polisi lakini rekodi za wazi za Jeshi la
Polisi zinaonyesha maofisa wa Chadema ngazi za Wilaya na
Mikoa kuanzia wiki iliyopita na wiki hii walipeleka
Maombi Katika ofisi mbalimbali za Jeshi la Polisi kuomba
Kibali Cha kufanya maandamano ya kutaka Bunge Maalum la
Katiba lisiendelee.
Kama siyo Ujinga na uchochezi ,ushetani ni kitu
gani?Tuwaulize Hao waandishi wanasema ni sahihi watu
kuandamana bila Kibali Cha Polisi Kuwa wao walishawai
kuandamana Mara ngapi bila Kibali?
Na hapa ndipo kila siku ninapo shauri wana Habari wenzangu
Twendeni tukajiendeleze zaidi kielimu ikibidi Katika fani
nyingine tofauti ili ukiamua kuandika makala kuhusu jambo
Fulani unakuwa unalielewa kwa mapana yake.
Waandishi wenzangu tujifunze kwa waandishi wenzetu waliopo
Kwenye nchi ambazo zilishawahi kuingia Kwenye
machafuko.Tumeshuhudia kule Kenya, Rwanda baadhi ya
waandishi wa Habari wameshitakiwa Katika Mahakama za
Kimataifa kwa makosa ya jinai kutokana na kuandika
,kutangaza Habari ambazo zilichochea machafuko nchini mwao.
Pia waandishi mnaojitiwa mnaunga mkono maandamano hayo
ambayo yamekatazwa na Jeshi la Polisi, muige mfano kwa
Aliyekuwa Mwenyekiti Mkoa wa Arusha, Na Mhasibu wa Chadema
Makao Makuu na Aliyekuwa mwandishi wa safu ya ' Kalamu ya
Mwigamba', Samson Mwigamba, yaliyomkuta baada ya yeye na
Aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima,
Absalom Kibanda ,Theophil Makunga kwa makosa ya kuandika na
kuchapisha makala ambayo upande wa jamhuri Ulidai ni ya
kichochezi lakini hatimaye Hakimu Mkazi Wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, Waliarwande Lema kuwaachiria Huru wote
baada ya kuona upande wa jamhuri ilishindwa kuleta ushahidi
mzuri.
Kwa wale waliokuwa wakiisoma safu ya Mwigamba wakakubaliana
na Mimi Mwigamba alikuwa akiandika na kuelimisha lakini
wakati mwingine alikuwa akikitetea wazi wazi sera na Yale
yote yaliyokuwa yakifanywa na Chama Chake licha wakati
mwingine nilikuwa natofautiana nae na ninamweleza na tu
naendelea urafiki wetu.
Mwigamba siku aliposhitakiwa pale Mahakamani Kisutu na
Hakimu Lema akaamuru apelekwe gerezani na alikaa kwa siku
kadhaa katika gereza la Keko kwa kukosa dhamana kwa siku
Kadhaa alipotoka gerezani na kuanza Kuwa anataka
nyumbani kwake Arusha Kuja Dar es Salaam, Kuja kuudhuria
Kesi yake Dar es Salaam, wakati huo huo Chadema Makao Makuu
walimuondoa nafasi yake ya uhasibu na wakati huo huo kibarua
Chake kule Ofisi za Umoja wa Mataifa Arusha kimeota Nyasi na
wakati huo huo anakabiliwa na Kesi yeye na waliokuwa wafuasi
wenzio wa Chadema waliofanya maandamano na kusababisha watu
Kadhaa kupoteza Maisha.
Mwigamba ni rafiki yangu na Mtani wangu, baada ya kusongwa
na matatizo hayo alikuwa akinifuata na kuniambia sasa
anakubaliana na taadhari niliyokuwa nikimpa awali iliyokuwa
ikimtaka achunge kalamu yake na asitumie Karamu yake kutetea
Chama Chake hata sehemu isiyo Sahihi.
Nilimhoji ni kwanini ananieleza maneno hayo, alisema Chadema
ilimhakikishia itamwekea Wakili wa kumtetea na kumlipa
lakini imeshindwa kufanya hivyo Matokeo yake yeye ndiyo a
namlipa Wakili.
Mwigamba alisema yeye ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa
Arusha anashitakiwa lakini Cha kushangaza siku ya Kesi,Makao
Makuu ya Chama hicho haimpi hata Ofisa mmoja wa Chama
amsindikize mahakamani na wala Makao makuu haiulizii wala
kufuatilia Mwenendo wa Kesi yake.
Mwigamba Kabla ajaondolewa Kwenye Chama hicho alisema
amejitunza mengi Kuwa wanasiasa sio watu wa
kuwategemea Kwani wanakutuma ufanye jambo tena la hatari na
ukipata matatizo wanakuacha solemba. Ni kweli nilimuuliza
wakili aliyekuwa akimtetea Mwigamba, ni mwalimu wangu wa
sheria alinijibu ni kweli hayo aliyonieleza Mwigamba.
Hilo Liwe funzo kwa waandishi wenzangu tujifunze,
tusikubali kutumiwa na watu au wamiliki vyombo kuandika
habari, makala ambazo zinavunja sheria za nchi kwani mwisho
wa siku kama ni kesi za jinai za kuandika makala za
uchochezi ,mshitakiwa wa kwanza ni mhariri, mwandishi, na
mchapishaji na wanashitakiwa binafsi.Ni wamiliki wachache
sana wanakubali kuwawekea mawakili wa kuwatetea waandishi na
wahariri wao pindi wanaposhitakiwa mahakamani.
Pia napenda kumuasa Mbowe ajiepushe kutoa matamko kufanya
vitendo vya kuvunja sheria ambayo mwisho wa siku
vinasababisha idadi ya Kesi za jinai zinazomkabili
kuongezeka.
Mbowe ajitambue Kuwa licha ya Kuwa ni mwanasiasa pia ni
mfanyabiashara.Atambue vyeo Vya siasa hapa Tanzania
havitabiriki Leo unacho Kesho Hauna.Wanaojifanya Leo hii
wapo karibu yake na wamtukuza Wengi wao wa wamtukuza na
kumnyenyekea kwasababu ya madaraka ya kisiasa aliyonayo.Siku
madaraka hayo ya kisiasa yakiondoka hawatakuwa na Habari
naye wala kumsujudia.
Na Mifano siyo ya Kutafuta, Mbowe Jifunze kwa Mkurugenzi wa
Usalama wa Chadema, Lwakatare Enzi zile Lwakatare akiwa na
madaraka ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mbunge wa
Bukoba mjini kupitia Chama Cha CUF.
Nakumbuka alikuwa ni Lwakatare kweli siyo Lwakatare wa sasa
alikuwa alivaa suti zinataka, akiongea jambo linatekelezwa
lakini baada ya kukosa Ubunge,wapambe waliokuwa wakizunguka
kinafki wakiwemo baadhi ya waandishi wa habari 'maslahi'
walimu acha solemba hadi Leo hii nafikiri unamuona.
Kumbuka Mrema akiwa Mwenyekiti TLP, Katibu wa Chama hicho
Miaka ya 2000 alikuwa Harlod Jaffu, Hamad Tao na
waligeukana.
Mbowe pia Jifunze madhara ya kufunguliwa Kesi za jinai
yaliyompata Mwenyekiti wa Chama Cha (TLP), Augustine Mrema
ambaye upenda kunitania Mimi ni First Lady wake,
wakili Mabere Marando ambaye Marando akiwa Chama Cha
NCCR na Mrema aliwahi kufunguliwa Kesi ya Uchochezi Katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro na wengine.
Mrema alikuwa akikabiliwa na Kesi za jinai zaidi ya tano
Hali iliyokuwa ilisababisha anatoka chumba Cha Hakimu huyu,
anaingia chumba Cha Hakimu mwingine kusikiliza Kesi nyingine
pale Mahakama ya Kisutu akitoka Kisutu tunakwenda nae
Mahakama Kuu kukabiliana na Kesi nyingine zilizokuwa
zikikabili licha alijifanya jeuri siku Moja mume wangu '
Mrema alikiri Mbele yangu Kuwa Kesi za jinai zimemletea
madhara makubwa kiuchumi, kufanya na hataki tena mchezo
huo.
Kuna watu walikuwa walijifanya hawatishiki na kwamba
wapo juu ya Sheria lakini Leo wapo gerezani wametulia tuli
tu na mfano mmoja wapo ni yule Kiongozi wa Jumuiya za Uamsho
na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI),Sheikh
farid Kama Kiongozi wa Sheikh Farid Ahmed
(43) na wenzake ambao wanakabiliwa na Kesi ya ugaidi Katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Septemba 3 Mwaka huu,
mshitakiwa mmoja Katika Kesi hiyo Salum Ally Salum ,
alifunja ukimya na Kuonyesha suruali yake ilivyoloa
Kwenye makalio akasema ni madhara ya kulawitiwa na
kuingizwa miti na Askari Polisi.
Mara Kadhaa niliwahi kuandika makala za kumuonya Mbunge wa Arusha Mjini Godbles Lema (Chadema),aache tabia ya kuamasisha watu kufanya vurugu ikiwemo tukio la Lema kwenda Chuo Kikuu Cha Dodoma kwenda kuamasisha wanachuo waandamane hadi bungeni Kipindi kile mjadala wa kuanza mchakato wa kuandaa Katiba mpya unaanza, akasabisha wanachuo Hao kupigwa virungu.
Nilikuwa nikimuona Lema ache tabia hizo za Kupenda kuchochea vurugu na kumtaka ajitambue Kuwa yeye ni kiongozi na Watanzania ipo siku watamchoka na tabia yake hiyo ya kihuni na Umaarufu wake utapita.Hakunielewa.
Leo hii yametimia na sote ni mashahidi, Lema wa Mwaka 2010 -2013 siyo Lema wa sasa Kwani amechuja kisiasa , wafuasi wake waliokuwa wakimpungia mkono kwa kila jambo aliyokuwa akili sema wamemkimbia.Lema umaarufu wake uporomoka kwa kasi na chanzo hasa Cha kuporomoka ni baada ya wale wafuasi wake aliyokuwa wakiwajaza Ujinga Kule Arusha wanaaandamana na kusababisha vurugu, wameshtukia hawamuungi tena mkono.
Na taarifa za duru za kisiasa na kipelelezi zina sema Lema hapo awali alikuwa hawezi kufanya maandamano yake bila kwanza baadhi ya wafuasi wake ambao ni madereva Pikipiki, wachuuzi wa Bidhaa Kwenye masoko yaliyo rasmi na siyo rasmi kumruhusu afanye maandamano na Makundi hayo yalikuwa tayari kuacha kazi zake kuingia mtaani mjini Arusha kufanya maandamano.
Na kwa wale madereva Bodaboda ambao walikuwa wakimuunga mkono Lema na wakawa waandamana na wengine Bodaboda zile zilikuwa Si Mali yao zilikuwa ni za matajiri wao.
Wakati walipokuwa wakianda kushiriki maandamano hayo na hiyo BodaBoda ,Polisi ilikuwa iliwatawanya na ilipokuwa ikiwatanywa madereva Bodaboda wananiambia wanaacha BodaBoda , Polisi Mkoani Arusha ikazichukua zile pikipiki inaendelea kuzishikiria hadi sasa na wale madereva wa Bodaboda wanaogopa kwenda Polisi Kudai Polisi iwarejeshee pikipiki kwasababu endapo watafika Polisi kuomba warejeshewe pikipiki hizo , ni wazi Polisi itawakamata na kuwafungulia Kesi.
Sasa madereva Hao wa Pikipiki kwa kutumiwa na Lema kuvunja Sheria wamejikuta pia wakipoteza kitendea kazi ambazo ni pikipiki na kupoteza ajira kwasababu ya wao walikubali kutumiwa vibaya na Lema kufanya vurugu wakajikuta wanaacha Kazi zao zinazowaingizia kipato ambayo ni kuendesha Pikipiki , Matokeo yake walivyo kimbila na Polisi , pikipiki wakaziacha eneo la tukio kwa kuhofia kukamatwa na Matokeo yake baadhi ya matajiri wanawadai madereva Hao pikipiki zao kwasababu wao waliwakabidhi pikipiki zao wakazifanyie Biashara na siyo kwaajili ya kushiriki maandamano haramu yakumuunga mkono Lema.
Leo hii Lema watu wanaomuona Kama 'Kibuzi Malika' , umaarufu wake Umetoweka kwasababu kubwa Moja ya kuwa kiongozi anayesifika kuanzisha vurugu Katika Jiji la Arusha tangu alipachaguliwa Kuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha mkono Mwaka 2010.
Na Makundi hayo yaliyokuwa yake tiki hivi sasa yamejitambua Kuwa Lema alikuwa akiwatumia vibaya ndiyo maana hivi sasa Arusha ipo shwari, Yale maandamano ya Chadema yaliyokuwa yanaongozwa na Kuratibiwa na Lema hayapo tena Kwani Makundi hayo yanasema hawataki tena kutumiwa vibaya na Lema Kwani mwisho wa siku madhara wanayapata wao watu wa Hali ya chini, yeye Anazidi kunufaika kisiasa kupitia ushiriki wa Makundi hayo Katika maandamano.
Ni sifa Mbaya sana kwa kiongozi wa siasa hasa hapa Tanzania Kwani Watanzania wanapenda Amani na wamefunzwa hivyo na kuwabadilisha Si Kazi rahisi.
Niitimishe Kwa Kusema hakuna Waandamanaji majasiri Tanzania,
bali kuna Chui wa karatasi. Hakuna wapinzani wa kweli nchini
ila kuna wapingaji .
Hakuna waandamanaji,wagomaji majasiri . Wagomaji
majasiri tunaowaona Kwenye nchi za wenzetu zenye
machafuko na Sheria zipo kwaajili ya kukomesha vitendo
hivyo.Tunaitaji Amani na wanasiasa wetu washindane kwa
hoja bila vurugu..
Amani tuliyoikuta na tuliyonayo HIvi sasa ambayo naona
miongoni mwetu imewakinai na wanataka kuona machafuko
yakianza nchini, tukae tukijua kuna watu wakipoteza Uhai
wao, akili zao, Nguvu zao kuakikisha Tanzania inakuwa nchi
Huru na Amani na ndiyo mAana hata Leo hii tunapata jeuri ya
kuandika, kulala na kuamka salama kwasababu kuna Askari wetu
wa majeshi mbalimbali Wanakesha macho wanatulinda.
Kwahiyo wachache wetu tusijitie wazimu Leo hii kutaka
kuhatarisha Amani yetu kwa mambo ya kipuuzi na ya siyo na
tija.
Anayeona amechoka kuishi Tanzania kwasababu eti serikali hii
ni ya kibabaishaji basi minashauri ahame nchi aende
kuishi Kwenye nchi ambazo anafikiri zinaongozwa na malaika
na ni serikali bora kuliko Ya Tanzania.
Au Kama vipi kikundi au mtu huyo ajipindue aiingie
msituni Kama anaweza.Wanaume wa ukweli Kama Joseph Kony wao
ni watekelezaji siyo waropokaji, wameona serikali ya Uganda
ni ya ovyo wameamua kuingia msituni wanaendeshana na Rais
Yoweli Mseveni na umoja wa Mataifa , kuliko Nyie
wapingaji uchwara wa Tanzania ambao baadhi yenu
mmejigeuza kama waimbaji wa muziki wa mipasho ' Taarabu'
kutwa kutoa matamko yasiyo na tija kwa taifa na vyama vyenu
na jamii kwa ujumla ambapo ikitokea mkubwa wa
mbavu mbavu na dola ,mnafyata Mkia.
Baadhi ya Viongozi wa Chadema acheni tabia ya kuamasisha
vitendo Vya Uvunjifu wa Sheria. Nalipongeza Jeshi la
Polisi chini ya IGP- Ernest Mangu Kwa kuweza
kusambaratisha maandamano hayo haramu na kuwafikisha
mahakamani wahusika,
Jeshi la polisi lipuuze kebei zinazotolewa na wananchi
wachache ambao zinadai jeshi hilo lifumuliwe kwasababu
halina wasomi, linavunja Sheria bila wanchi Hao Kusema Jeshi
Hilo limevunja Sheria zipi.
Nasema jeshi lipuuze kebehi hizo kwasababu midomo ni mali
yao na wanaongea mambo wasiyoyafahamu kwani sisi tuliozaliwa
na kulelewa katika familia za askari na tumekuwa
tukifuatilia historia za majeshi yetu, tunakiri kwamba
majeshi yetu hivi sasa yanawasomi wengi ukilinganisha na
miaka ya nyuma, na majeshi yetu kadri siku zinavyozidi
kwenda yanazidi kupiga Hatua za kimaendeleo na kwa
Bahati Mbaya Hao wanaotaka Jeshi la Polisi lifumuliwe
liundwe upya hata kozi ya Mafunzo ya awali yanayotolewa na
Jeshi la Polisi Kule CCP- Moshi Hawajawahi kuhudhuria Kama
Mimi.
Na Mbaya zaidi Wanaishia kupendekeza Jeshi la Polisi
lifumuliwe lakini hawasemi likishafumuliwa ,wanataka Jeshi
Hilo lisukwe vipi. Waswahili wanamsemo wao usemao " Mdomo
nyumba ya maneno".
Chapeni Kazi ,raia hasa sisi waandishi wa habari tunaheshimu Sheria za nchi na kuunga
mkono Kauli mbiu ya Jeshi la Polisi ya " Utii wa Sheria bila
shuruti', tunaowaunga mkono kwa Kazi yenu na Katu musichoke
kuwapatia kile wanachokiitaji kutoka kwenu wale wote
wanaovunja Sheria za nchi kwa makusudi.
Tanzania siyo nchi ya wahuni, ni nchi yenye heshima yake
ambayo wananchi wameamua dola Lao linaongoze kwa kufuata
Sheria.
Mungu Ibariki Afrika
Facebook: Happy Katabazi
Chanzo: Gazeti la Raia , Alhamisi, Septemba 25 Mwaka 2014
Sent from my iPad
No comments:
Post a Comment