MAREKANI KUIPIGA 'TAFU' UB
MAREKANI KUIPIGA 'TAFU' UB
Na Happiness Katabazi
CHUO cha Southern University kilichopo jimbo la Louisiana nchini Marekani kimetoa tamko la pamoja na Chuo Kikuu cha Bagamoyo(UB) cha Tanzania juu ya makubaliano kushirikiana .
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizo, Dk.Elifuraha Mtaro ambaye ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB), anayeshughulikia Fedha na Utawala, ofisini kwake Mikocheni kwa Warioba, jijini Dar es Salaam Leo alisema UB imepokea kwa Furaha tamko Hilo ambalo amelishika Katika picha inayombatana na habari hii.
Dk.Mtaro alisema tamko Hilo ambalo limesainiwa na Seneta wa Jimbo la Louisiana, Rick Gallot Jr, lilitolewa hivi karibuni Katika mkutano wa viongozi wa nchi za Afrika ambapo kwa Tanzania iliwakirishwa na Rais Jakaya na mkutano huo uliitishwa na Rais wa Marekani, Barack Obama.
Dk.Mtaro alisema kwa mujibu wa tamko Hilo Southern University ambalo lilipata Baraka ya Seneti hiyo ambapo Seneti hiyo ya Louisiana ilitoa tamko la kiserikali ambalo lilisisitiza kwamba serikali ya jimbo Hilo itaungana na serikali ya Tanzania Katika kuendeleza taaluma, utafiti na huduma za Jamii Katika vyuo vikuu hivyo viwili.
Imetolewa: Ofisa Habari wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB)
Oktoba 21 Mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment