BURIANI UKAWA
BURIANI UKAWA
Na Happiness Katabazi
HAPPINESS Katabazi nimepokea kwa furaha kifo Cha Marehemu Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), kilichotokea jana saa nne asubuhi ya Oktoba 2 mwaka huu, jijini Dar es Salaam, kutokana na maradhi ya shinikizo la Damu (BP).
Marehemu Ukawa alikumbwa na umauti Jana wakati akitaka kuingizwa Kwenye Gari akimbizwe hospitalini akatibiwe.
Kwa mujibu wa mashuhuda tukio Hilo, walisema Marehemu Huyo alikuwa ameketi kwenye Televisheni akifuatilia kikao cha Bunge Maalum la Katiba lilokuwa likiitimisha kazi yake mjini Dodoma, na ghafla Ukawa Alipomuona na kumsikia Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Thomas Kashilila akitangaza matokeo ya kura zilizokuwa zimepigwa na wajumbe wa bunge hilo na kumsikia Dk.Kashilila akisema theluthi mbili ya Zanzibar imepatikana na kwamba Katiba iliyopendekezwa na Bunge imepitishwa kwa kupigiwa kura nyingi za ndiyo.
Ndipo marehemu Ukawa hali yake ya kiafya ikabadilika ghafla na alianza Kulalamika kuwa anajisikia vibaya anaomba apepewe ili apate hewa kwani anaona Giza na anapumua kwa Shida sana.
Jamaa waliokuwa wamekaa na Ukawa,walianza kumpepea huku wengine wakimfungua Vifungo Vya shati na Kumvua viatu na kumpepea na wengine wakitafuta Gari ili wamkimbize Hospitali , lakini wakati wakimtoa Ukawa ndani ya nyumba yake wampakize Kwenye Gari ,Ukawa aliwafia mikononi Kabla ya kapakizwa Kwenye Gari Hilo.
Hata hivyo mashuhuda walisema waliukabidhi mwili wa Marehemu Ukawa hospitalini ', ukiwa Tayari wa baridi na Daktari na kwamba hadi marehemu huyo anakumbwa na umauti hakufanikiwa kupata nafasi ya kututubu dhambi zake.
Na walisema kwa mujibu wa ripoti ya daktari ,Daktari amesema Chanzo Cha kifo Cha Ukawa ni ugonjwa wa shinikizo la Damu lilompata baada ya kusikia tangazo kuwa Katiba iliyopendekezwa na Bunge imepitishwa na theluthi mbili ya wajumbe toka Zanzibar imepatikana maana Enzi za Uhai wake Marehemu Ukawa Aliaminisha umma Kuwa theluthi mbili ya wajumbe toka Zanzinar haitapatikana.Marehumu Ukawa amekumbwa na aibu licha ni Marehemu.
Msiba wa Marehemu Ukawa ulifanyika jana ile ile na mwili wake ukazikwa Kinondoni Mtaa wa Ufipa yaani Makao Makuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Na waombolezaji walipata fursa ya Kuweka mashada ya maua Kwenye Jeneza Hilo la Marehemu Ukawa , na Jana jioni ndugu wa Marehemu Ukawa walianza kuweka tanga ndugu ambapo tanga ndugu hiyo ya siku Tatu inamalizika Kesho.
Waombolezaji walikuwa wakitoa sifa za Marehemu Kuwa Marehemu alikuwa ni mkorofi, Ana maneno makali, Mzushi Kwani alikuwa akijitapa ametumwa na Watanzania Kumbe muongo maana hata hajawahi kutoa orodha ya Majina ya Hao Watanzania waliomtuma, mchonganishi,hakutaka Katiba iliyopendekezwa na Bunge ipatikane na alisusia vikao vya bunge akaamua kwenda kusiko julikana maana jimboni alikuwa haonekani,mbinguni haonekani.
Marehemu Ukawa Enzi za Uhai wake alijiapiza na kuaminisha umma Kuwa ni lazima Bunge livunjwe Kwani theluthi mbili ya wajumbe wa Zanzibar haitapatikana.
Lakini Jana theluthi mbili ya wajumbe toka Zanzibar ilipatikana na Katiba iliyopendekezwa na Bunge ikapitishwa na Oktoba 8 Mwaka huu, Bunge Hilo litamkabidhi Rais Jakaya Kikwete. Ukawa ndiyo akajikuta amepatwa na ugonjwa wa BP na kufariki Dunia ghafla bin vuu.Poleni sana Wafiwa.
Marehemu Ukawa amefariki Kipindi Kizuri wakati Watanzania Wengi hatukuwa tukimuamini tena na Kumuunga mkono mAana tulishambaini Ukawa ni kiongozi asiyeitakia Mema Tanzania ,alikuwa anaamasisha wananchi wavunje Sheria za nchi na waandamane na wagome bila kikomo na Matokeo yake baadhi ya wafuasi wake walijaribu kuandamana lakini jeshi la polisi mikoa yote iliweza kuyasambaratisha maandamano Kabla hata hawajaandamana.
Unapoizuzungumzia Ukawa ,hasa Unaizungumzia Chadema na CUF. Lakini Katika Ukawa , Chadema ndiyo ilikuwa na Nguvu na sauti Kwani hapa Tanzania Bara ndiyo Chama Kikuu Cha upinzani na ndicho chenye wabunge wengi kuliko CUF, NCCR- Mageuzi na ilikuwa Ikiungwa mkono na baadhi ya viongozi wa Taasisi za kidini.
Wakati Bunge Maalum lililokuwa linafanyakazi yake kuliibuka vitendo Vya baadhi ya wajumbe toka kundi la Ukawa, CCMkutolea maneno yaliyofaa na niliwahi kukemea tabia hii kupitia Moja ya makala zangu.
Lakini Marehemu UKAWA ambaye naye alikuwa ni miongoni mwa wajumbe wa Bunge hilo yeye alidai ameshindwa kuimarisha vijembe hivyo na kwamba Akiamua kwenda kushitaki kwa wananchi Kuwa wajumbe wa Bunge Hilo toka CCM wamekuwa wakiwadhalilisha sana.
Watanzania waliwasilikiliza na kuwapima na Mimi Nikiwa mmoja wao nilimsikiliza Ukawa na kumuona Hana hoja ya Msingi maana Kama kutolewa lugha ya kejeli hata wao nao walikuwa wakiwatolea wenzao lugha za kejeli Cha Msingi wasisusie vikao Vya Bunge.
Ushahidi wa kuthibitisha Kuwa nilimshauri Marehemu UKAWA kupitia makala yangu ya Agosti 3 Mwaka huu,iliyokuwa na kichwa Cha Habari kisemacho " Ukawa Rudini Bungeni", huo hapo ndani ya makala hiyo nilimshauri Marehemu Ukawa arudi ndani ya Bunge akatetee Katiba ya wananchi akiwa ndani ya Bunge,na kwamba kususia bunge siyo suluhisho na mwisho wa siku sisi tutamfananisha Ukawa ni sawa na 'kamanda aliyeama kambi vitani',Marehemu alinipuuza Hadi Jana umauti wa ghafla ulimkuta na ameacha historia Mbaya na rekodi yake hapa nchini imeifadhiwa Kuwa Ukawa alikuwa Hana mapenzi Mema na nchi yake.
Kifo hicho kilichomkuta Marehemu Ukawa Jana, ni Ishara Mbaya kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 hasa kwa Chadema na CUF.
Hatua ya Jana Bunge kupitisha Katiba iliyopendekeza ni wazi 'kisaani' kimepinduliwa pinduu.
Hakuna Cha Ukawa tena kusikilizwa na wananchi, wananchi wanachotaka sasa nikuiona na kuisoma Katiba iliyopendekezwa na Bunge walisomea wenyewe na wataalamu wawaelimishe kuhusu kilichopo ndani ya Katiba hiyo ya Bunge la Katiba na sisi wasomi wa Sheria nao HIvi sasa tuna shahuku kubwa ya kuipata nakala hiyo ili tuweze kuisoma na wahadhidhiri wa Sheria waweze kuwafundishia wanafunzi wao wa fani ya Sheria vyuoni.
Hivyo ule Wimbo wa ' Rasimu ya Tume Warioba'. HIvi sasa umechuja. Wimbo unaotamba sasa ni Wimbo wa ' Katiba iliyopendekezwa na Bunge au Katiba ya Mzee Sugu ,Samuel Sitta'.
Sasa kwakuwa Marehemu Ukawa alisusia Bunge Hilo na yeye Ukawa alikuwa Mtetezi wa rasimu ya Tume ya Jaji Warioba ambayo Tayari ilishakufa tangu Jana na kuzaliwa Katiba iliyopendekezwa na Bunge, sijui sasa Marehemu Ukawa atafufuka aanze kuipinga Katiba iliyopendekezwa na Bunge?
Jibu hawezi kufufuka tena kwasababu Ukawa yupo jehanamu kwa baba yake shetani na shetani Hana huwezo wa kumfufua Marehemu.
Labda Ukawa Angekuwa ameenda mbinguni , Mungu angeweza kumfufua kwasababu Mungu Ana mamlaka ya kuumba, kuruhusu mtu afe na kufufua Katika wafu. Pole sana Marehemu Ukawa maana hivi sasa upo Katika ziwa la Moto jehanamu na umekuwa Kuni huko jehanamu.
Na ndiyo basi tena ulilolitaka halikuwa tulia huko huko jehanamu uungue na Moto maana hayo ndiyo malipo ya sala za watu tulizokuwa tu liloombea taifa, Bunge Hilo limalize salama Kazi yake na wale wote wenye jicho la husuda ,wanaotaka kuleta machafuko ,Mungu awashughulikie ,sasa hiyo ndiyo Adhabu yako.
Marehemu Ukawa Enzi za Uhai wake aliposusia vikao Vya Bunge Hilo, akajigeuza yeye ni mbunge wa Tanzania Kumbe siyo.
Wakati Marehemu Ukawa analazimisha wananchi waamini Bunge lilikuwa linafanya ubakaji wa Demokrasia ya kuichakachua kinyume Cha Sheria Rais ya Warioba wakati akijua Kifungu Cha 25(2) Cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2014.
Chama Cha Mapinduzi kupitia Katibu Mkuu wake,Abdullaman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, walizidi kuchanja Mbuga kuimarisha Chama ' kustimleti' wanachama wake.Na wakati huo CCM kupitia wanachama wake wakawa wanakiwalisha vyema Chama chao ndani ya Bunge Maalum la Katiba kwa njia ya Amani.
Na kwa mtazamo wangu ,mbinu hiyo inayotumiwa na CCM kupitia kwa Kinana, Nape na waliokuwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba,ni Moja ya kujisafishia njia ya kupata ushindi mzito wa CCM Katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.
Wakati CCM imejiimarisha na kujijenga hivyo kimkakati, Siyo Chadema, CUF , NCCR Mageuzi Navyo kila Chama kwa wakati wake havifanyi harakati za kustimuleti wanachama, zaidi Tunaona Chadema viongozi wake wanaowaamasisha wanachama wao waandae maandamano haramu ambayo Jeshi la Polisi lime yapiga marufuku.
Tunachokishuhudia ni kwa baadhi ya viongozi wa vyama hivyo Vya upinzani kila mtu akijitafutia Umaarufu binafsi kwa Malengo yake binafsi ya kupata Ubunge au kutetea Kiti Cha Ubunge na wengine wabunge wa Ukawa nao wamenukuliwa wakisema wa kiombwa Kugombea urais, watagombea.
Mbatia ambaye ni Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi yeye anadaiwa kuwa anataka Kugombea Ubunge jimbo la Vunjo.
Viongozi wengine wa Ukawa nao Wanadaiwa Kuwa wanataka Kugombea urais hivyo akili zao na Nguvu za wanazielekeza kwa jinsi ya kuwashika wajumbe watakaopitisha Majina Yao ndani ya vikao husika Vya vyama vyao na siyo kuvijenga kwanza vyama vyao na kuviandaa kupata ushindi Katika uchaguzi wa serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu Mwaka 2015.
Na hapa ndipo vyama Vya upinzani hapa nchini vinapokosea na mwisho wa siku uchaguzi ulifanyika wakishindwa wanaanza kujitetea CCM imewaibia kura, Tume ya Uchaguzi wa Taifa, haipo Huru.
Tafadhali sana Vyama Vya upinzani hatutataka tena kusikia utetezi huo Mara baada ya Uchaguzi wa serikali za mtaa, uchaguzi Mkuu kumalizika.Maana mmejimaliza wenyewe ,badala ya Kujenga vyama vyenu na kujiandaa kikamilifu na uchaguzi wa serikali za mitaa karibu Mwaka mzima sasa mmeupoteza kwa kuzungumzia Habari za Ukawa,Ukawa na mwisho wa siku hamjafanikiwa.
Wakati wenzenu wa CCM walikuwa wakifanya mambo yote kwa wakati mmoja.Yaani CCM ilijigawa Makundi . Moja ya kundi Lao linaloongozwa na Kinana, Nape linazunguka mikoani kuimarisha Chama chao na kustimuleiti wachama wao na wengine kuingia ndani ya Bunge Maalum la Katiba kutunga Katika iliyopendekezwa.
Ipo siku Chadema watakuja kukubaliana na Mimi Kuwa Huyo Mshauri anayewashauri viongozi wa juu watoe matamko ya kuamasisha wanachama wao washiriki maandamano yasiyo na Kibali ni Mshauri Mbaya sana ambaye ala Lengo Moja baya sana la kuisambaratisha Chadema na Watanzania wameishaanza kuona Chadema ni Chama Cha Vurugu na Watanzania ni wapenda Amani.
Mapema kabisa niliisa Chadema Kuwa kijitambue Kuwa ni Chama Kikuu Cha upinzani na kina wabunge Wengi, na siyo vyama Vya upinzani vinapenda mafanikio hayo ya Chadema,Chadema haikunielewa ila ikalazimisha urafiki na baadhi ya vyama Vya upinzani ambavyo vyama hivyo havina mvuto tena wa kisiasa hapa nchini ila vimeanza kusikika kupitia Marehemu Ukawa.
Tangu Jana Katiba ilivyopitishwa na Bunge , wafuatiliaji wa mambo ya siasa wanaamini hiyo ni Ishara Mbaya kwa Chadema na siyo Ukawa tena ambao ilikuwa Ikiundwa na CUF, NCCR Mageuzi.
Wafuatiliaji Hao wameibuka na mtazamo huo Kwasababu ni wazi Chadema Ndio ilikuwa na sauti na wajumbe Wengi Kwenye Ukawa kuliko Vyama vingine.
Hivyo ni Ishara Mbaya Kwa Chadema Kuwa jaribio la kutaka kuandamana bila kukoma na kuvunja Sheria za nchi na limeshindikana, Njama Yao ya upotoshaji umma Kuhusu Kuwa Bunge Maalum la Katiba halipo Kuhalili na linafuja Fedha za wananchi, Theluthi mbili ya wajumbe wa Zanzibar haitatimia zimeshindwa vibaya sana na wameumbuka wao Chadema na Marehemu Ukawa.
Nalipongeza Bunge Hilo lilokuwa likiongozwa na 'Mzee Sugu au Mutu ya Danjeee'- Samuel Tengeneza Sitta na Makamu wake Samia Suluhu.
Pia nimpongeze Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa Katiba iliyopendekezwa na Bunge, Mtemi Andrew Chenge na Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni , Profesa Costa Ricky Mahalu. Sitta, Chenge.Mahalu wote hawa ni wasomi wa Sheria tena siyo wa kubabaisha.
Hongereni na timu yenu mmefanyakazi ambayo mmeandika historia na mmeacha alama Kwenu na vizazi vyenu.
Na kwa wale Ukawa nao wameacha historia Mbaya ambayo siyo ya kupigiwa mfano ya kususia Bunge hilo na Mara kwa Mara wakawa wananukuliwa na vyombo Vya Habari wakiliombea dua mbaya Bunge Hilo Kuwa akidi haijatimia Mara Bunge litarejeshwa, Matokeo yake Bunge alikuhiishwa wala kuvunjwa na akidi ikatimia na Katiba iliyopendekezwa na Bunge imepatikana. Kweli dua la Kuku halimpati Mwewe.
Na kwa wale wasomaji wa makala zangu watakumbuka Kuwa tangu mchakato wa Bunge Maalum la Katiba lianze kuandika Katiba hiyo, nilijiokeza kuandika makala zaidi ya Tatu na makala hii ya Leo ni ya nne.
Makala ya kwanza niiliitoa Agosti 3 Mwaka huu, ilikuwa na kichwa Cha habai kisemacho: " Ukawa Rudini Bungeni'. Makala pili il ilichapishwa Kwenye Gazeti la Rai la Septemba 18 Mwaka huu, ambayo ilikuwa na kichwa Cha Habari " Freeman Mbowe, Dozedozee".
Makala ya tatu niliandika Septemba 22 mwaka huu,ilikuwa na kichw acha habari kisemacho 'Wanaolazimisha maandamano ni maajenti wa shetani". Makala ya nne ilichapishwa Katika Gazeti la Rai la Septemba 25 Mwaka huu, ilikuwa na Kichwa Cha Habari : " Tuna Chui wa Karatasi,siyo waandamanaji. Na Leo naandika makala hii yenye kichwa Cha Habari kisemacho ' Buriani Ukawa'.
UKAWA ambao wengine ni wabunge wakati wa Kipindi kile Cha Bunge linaandaa Katiba iliyopendekezwa wakasusia Bunge. Hawakuweza kujulikana wapo Duniani au mbinguni! Maana majimboni Kwao walikuwa hawaonekani wala bungeni hawaonekani.
Kwa kitendo historia hii iliyoandikwa Jana na Bunge akidi ya wajumbe kupatikana, Je Ukawa hawaoni hii ni aibu Na fedhea kwao?
Kwa Sababu ni Ukawa ndiyo alikuwa akipayuka mitaani Kutaka Bunge Hilo livunjwe Kwani ni matumizi Mabaya ya madaraka na ufujwaji wa Fedha za walipa kodi kwa kitendo Cha Sitta kulazimisha Bunge liendelee wakati akijua wazi theluthi mbili ya Wajumbe toka Zanzibar haitapatikana.
Marehemu UKAWA ambaye alikuwa akiitetea na hakutaka kabisa rasimu ya Tume ya Jaji Joseph Warioba isiguswe wala kukosolewa wala kupunguzwa kitu chochote kile ili wakifahamu kifungu cha 25 (2) cha Sheria ya Mabadiliko Sura ya 8 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2014 ,yanalipa madaraka Bunge Maalum la Katiba kuboresha rasmi ya Warioba au kuweka vitu vipya.
Hadi Jana umauti unamkumta Marehemu Ukawa,alikuwa hajatubu dhambi zake Mbele ya Watanzania ikiwemo dhambi ya kuchochea wananchi waandamane bila vibali vya Polisi, uongo na upotoshaji mkubwa kuhusu majukumu ya Bunge hilo, Marehemu alikuwa akiwadanganya Watanzania Kuwa kura za kupitisha Katiba iliyopendekezwa na Bunge hazitatosha Kwani theluthi mbili toka Zanzibar haitapatikana, hakuungama.
Na kwakuwa hakuungama, aliendelea kushupaza shingo hadi umauti umemkuta , ni wazi Marehemu Ukawa amekwenda jehanamu ya Moto kwenda kuonana na baba yake Shetani Kwani Biblia in atuambia Shetani ni Baba wa Uongo, na Ukawa hapa Duniani alikuwa ni muongo,mchonganishi, mkorofi, aambiliki na hizo ni miongoni mwa sifa walizonazo wafuasi wa shetani.
Hivyo Ukawa alikuwa ni Ajenti wa shetani ambaye alikuwa anaenda kuona Katiba iliyopendekezwa na Bunge Hilo hazipatikani na Tanzania I naingia Kwenye machafuko ya wenyewe kwa wenyewe kwa kisingizio Cha mchakato wa Kuipata Katiba.
Lakini Kwa Kuwa bado Mungu anaipenda Tanzania na watu wake wanaipenda Kwasababu kuna baadhi ya viongozi wa dini akiwemo kiongozi wa Kanisa la Elishadai la Boko Basiaya,Dar es Salaam, Kanali Mstaafu ,Bruno Kinunda na waumini wake kila Ibada ya Jumapili tulikuwa tunaanza ibada kwa kujitakasa dhambi zetu na kuliombea taifa na mchakato na Bunge Maalum la Katiba lifanyekazi zake kwa Amani na utulivu na kweli Hilo limefanikiwa na Bunge Hilo kumaliza Kazi yake Jana kwa Amani .
Hongera Lilokuwa Bunge Maalum la Katiba kwa kumaliza Kazi yake salama licha Bunge lilipitia Katika wakati mgumu wa kurushiwa vijembe na kuonekana linawasaliti Wananchi jambo ambalo Si la kweli .Binafsi nimefurahishwa na Hatua hiyo ya Bunge Hilo kutuletea Katiba iliyopendekezwa na Bunge.
Wasomo wa Sheria tunasema Hatua inayofuata ni Katiba hiyo kupelekwa Kwa wananchi ili wapigie kura ya ndiyo au Hapana.
Hivyo wananchi msipotoshwe ,kisheria bado Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haijapatikana.
Tutulie, Tusikubali kushawishiwa na maajenti wachache wa shetani kuingia mitaani kuanza kuipinga Katiba hiyo iliyopendekezwa na Bunge wakati bado hata haijatangazwa Katika Gazeti la Serikali ,na hatujaisoma na kuielewa na mambo gani mazuri na mabaya yapo ndani ya Katiba hiyo.
Na ieleweke Kuwa kila Mtanzania mwenye umri wa kupiga kura Ndiyo ataruhusiwa kupiga kura ya ndiyo au Hapana kuhusu Katiba hiyo Katiba hiyo.
Tayari kuna watu wameanza kutoa maneno ya kejeli kuhusu upitishwaji wa Katiba hiyo,lakini wapingaji Hao hawana hoja zenye mashiko na Hakuna hata mmoja aliyeipata nakala na kuisoma na kuilewa. Wapingaji Hao ni sawa na Mfa Maji haishi kutapatapa.
Ni wajinga na wapuuzi wachache ambao wao kila kitu kinachofanywa na serikali, Bunge wanapinga eti tu kwasababu Taasisi zao zinaendeshwa na wanapata ufadhili kutoka kwa 'mwabana' zao huko nje ya nchi kwa Kigezo Kuwa wao ni wakosoaji wa kubwa kila kitu kinachofanywa na serikali na ni Watetezi wa Haki za binadamu huku wakisahau Haki inaendana na wajibu.
Wakati Bunge Maalum la Katiba lilipokuwa likifayakazi yake tulishuhudia Jaji Joseph Warioba baadhi ya Wanasheria , wanaharakati ambao wamesoma somo la Katiba wanafahamu hatua za kutengenezwa kwa Katiba, wakitoa matamko ya kupotosha umma kuhusu mamlaka ya Bunge Hilo.
Nao baadhi ya waandishi wa Habari ambao hata somo la Sheria la Katiba Hawajawahi kulisoma na hata hawafahamu Hatua zinazotakiwa zipitiwe wakati taifa husika linatengeneza Katiba yake.
Waandishi hao baadhi ambao wamepachikwa jina la 'Mavuvuzela ya Ukawa' , Katika Kipindi chote hicho hawakutaka kujifunza Hatua hizo na Matokeo yake wakajikuta wao wanaingia Kwenye Mkumbo wa kupelekeshwa na kuaminishwa uongo na marehemu Ukawa na kisha wakauchapisha Kwenye vyombo Vya Habari. Nao wameumbuka Kama alivyoumbuka Marehemu Ukawa Jana.
Historia ya maandishi Yao nayo itawahukumu kwasababu baadhi ya waandishi nao walikuwa wakiandika Bunge litavunjwa, Bunge limechakachua rasimu ya Warioba na kupuuza maoni ya wananchi bila Kuwa na ushahidi wa hayo.
Na Mbaya zaidi baadhi ya Wanasheria na waandishi wa Habari walidiriki kupotosha umma kuhusu amri mbili tofauti zilizotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Katika Kesi ya Kuomba Bunge Maalum la Katiba lisimame ambayo imefunguliwa na Mwandishi wa Habari Saed Kubenea.
Ambapo Mahakama hiyo ilitoa amri ya kutupilia Mbali ombi la Kubenea na kuruhusu Bunge Hilo liendelee na Kazi yake.Kuna baadhi ya waandishi na Wanasheria baada ya Mimi kuandika Habari kupitia Mtandao wakinipa ya Kuwa Mahakama hiyo haijatoa amri hiyo ilihali ukweli ni kwamba Mahakama ilikuwa imetoa amri ya kulitupa ombi la Kubenea lilokuwa linataka Bunge lisimame. Kioja Cha aina yake.
Aidha kwa makusudi Marehemu Ukawa na wafuasi na baadhi ya waandishi wa Habari waliamua kupotosha ukweli kupitia mitandao amri ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ya Septemba 25 Mwaka huu, Katika ombi dogo Na. 28/2014 lilofunguliwa na Kubenea dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambapo Mahakama hiyo pamoja na mambo mengine ilisema Bunge Maalum la Katiba Lina madaraka ya kufanyia maboresho na kuongeza vitu Katika rasimu ya Tume ya Warioba kwa mujibu wa Kifungu ha 25(2) Cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2014.
Sijui walikuwa na Lengo gani yarabi. Na wengine nao akiwemo Warioba alisema hafahamu hiyo theluthi mbili ya Wajumbe toka Zanzibar itapatikana wapi maana eti haipo na kwamba Sitta ,ni jeuri sana.
Niitimishe Kwa Kusema Tanzania ni yetu sote ,hivyo sote Tushikamane kuilinda na kuijenga.Mchakato wa kuipata Katiba mpya isiwe Kigezo Cha kuisambaratisha Amani yetu.
Tutumie majukwaa sahihi na wakati sahihi kuisoma Katiba iliyopendekezwa na Bunge.Na Kwa Kuwa Ukawa Tayari ameishafariki na kuzikwa na ile rasimu Tume ya Jaji Warioba, ni imaini Yale malumbano na uchonganishi wa kipuuzi hautakuwepo kabisa au utapungua sana.
Labda Mzimu wa Ukawa uibuke na kuanza Kuzusha sokomoko, lakini kwakuwa Tayari Watanzania walishambaini Marehemu Ukawa ndiyo alikuwa Mzushi ,Kisarata Mtaa, kizabinazabina na aliwasaliti ,watajiuliza maswali haya;
Je Mzimu Ukawa ulikuwa ni miongoni mwa wajumbe waliyoshiriki kuitunga Katiba iliyopendekezwa na Bunge?
Watajijibu Kuwa hakushiriki kwani alisusia bunge.Na Kama alisusia Bunge atawezaje kufahamu kwa kina ni njema ya Bunge la Katiba kutengeneza Katiba iliyopendekezwa?
Watajijibu kuwa Mzimu wa Ukawa una nia ovu ya kutaka kuikwamisha kwa makusudi Katiba iliyopendekezwa na Bunge .
Watanzania hawausikiliza Mzimu huo wa Marehemu Ukawa, wataupuuza na watamtimua Kwani anawezakuwaletea matatizo ya kufunguliwa Kesi mahakamani na kupigwa virungu na Polisi na kulala selo Kama Marehemu Ukawa alivyowasabishia wa kapigwa virungu na Polisi na kufunguliwa Kesi za jinai mahakamani za makosa Kama kuingia kwa jinai, kufanya mkusanyiko haramu.
Buriani Marehemu Ukawa ,hatutakuona tena.
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blog: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Oktoba 3 Mwaka 2014.

No comments:
Post a Comment