KAAYA:NiTALETA MAPINDUZI YA KIUCHUMI CCM ARUSHA
.Apania kupambana makada mamluki
.Ndiye Mkurugenzi Mwendeshaji wa AICC
Na Happiness Katabazi
Swali: Nini kilikusukuma ukajiunga na kwenye ulingo wa siasa?
Jibu: Kama ujuavyo hakuna mtu ambaye siyo mwanasiasa. Hata wewe nakufahamu kwamba ni mawanasiasa!. Hata hivyo mimi ninajifahamu kama mshiriki katika siasa tangu nikiwa mtoto mdogo. Tunzi zangu za mashairi zimejaa siasa. Niliandika sana hasa kupitia magazeti ya Sunday news na daily news makala zilizohusiana na vita vya ukombozi.Nilikuwa mshiriki mkuu katika madadiliano ya midahalo ihusuyo siasa shuleni na vyuoni. Kwa hiyo kujihusisha kwangu katika siasa sikuhusihanishi na uamuzi wangu wa karibuni wa kugombea nafasi ya NEC Mkoa wa Arusha. Matokeo ya uchaguzi huo yalikuwa dhahiri. Nilishinda kwa kiushindo na Mkoa wa Arusha kuweka historia ya kumchagua mgombea wa nafasi ya juu kama hiyo bila yeye mwenyew kuwepo. Nilikuwa safarini nje ya nchi lakini wajumbe walidhihirisha mapenzi yao!
Swali: Hivi karibuni umechaguliwa kuwa Mjumbe wa NEC-Arusha, umejipangaje kwenye ulingo huo wa wadhifa huo mpya ndani ya CCM?.
Jibu: Arusha tumeanza vema, ten sana. Nilichuguliwa kwa kufahamika utendaji wangu ndani na nje ya chama. Nimatarajio yangu kwamba sitaisaliti imani hiyo iliyoonyeshwa kwangu na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Arusha.
Moja, nitatumia uwezo wangu wote wa Kitaaluma na elimu yangu ambayo niliipata kupitia sera sahihi za CCM na misingi iliwekwa na Baba wa Taifa kukishauri chama katika ngazi zote kuendeleza rasilimali zilizozopo na kuwekeza kukiepusha chama na adha ya kuwa ombaomba. Hili litawezekana kwani Mwenyekiti wa Taifa wa CCM na Rais wetu amebainisha nia yake kulishughulikia hili.
Nitashiriki kuhakikisha kwamba adhima hii inakuwa kweli na siyo nadharia. Nimepania kuifanya CCM iepuke fedha ya aibu kutoka kwa wanaoigiza kukipenda chama kumbe wako katika biashara. CCM imara itajengwa na wanachama na Watanzania wenye mapenzi ya kweli na uzalendo na sio watafutaji wanaowania nafasi katika chama ili kuweza kulinda masilahi yao. CCM ni ya wakulima,wafanyakazi, wafanyabiashara lakini wanoongozwa na sifa moja tu nayo ni mapenzi kwa nchi na uzalendo. Mwenye sifa hizi hataweza kamwe kubomo sifa iliyotukuka ambayo CCM imejijengea kwa miaka mingi.
Mbili, kwa kuwa wanachama na wajumbe wamenipa heshima ya kunichagua kwa kutumia kigezo cha uadilifu na mapenzi kwa chama, ninabakia na deni kubwa. Nitalilipa deni hilo kwa kuwaheshimu na kutekeleza watakayonituma kwa unyenyekevu, uadilifu na bila upendeleo kwa yeyote. Nitakuwa kichocheo cha kuisafisha hali ya hewa katika Mkoa wetu ambayo siyo ya kufurahisha sana. Nitajitahidi kuwashawishi wanachama kukienzi tu Chama Cha Mapinduzi na kwamba makundi ndani ya chama ni sumu ya utengamano. Nitafanya kazi ya kushona pale ninapobaini kuna dalili za kuendeleza makundi kwa kuwa mkweli, nisiye na upendeleo, muwazi na muunini wa falsafa ya Mwalimu ambayo ndiyo falsafa ya CCM.
Nitamuunga mkono Mwenyekiti wa Taifa wa CCM na chama changu kwa vitendo katika mradi mkubwa wa Chama wa kupapambana na adui rushwa. Rushwa ikisafishwa ndani ya Chama, serikalini itakuwa ni kutelezea tu.
Tatu, nitaitumia nafasi yangu katika Halmashauri kuu ya Taifa kufafanua kinagaubaga ni kwa namna gani Utaklii wa Mikutano, sekta ambayo niifahamu vilivyo inaweza kuwa injini KUBWA ya kukua kwa uchumi wa Taifa letu. Somo hili likifahamika vema ndani ya Chama, basi serikali itapiga kasi katika kulipa msukumo sahihi. Hata hivyo nilifurahi sana pale Mwenyekiti wa CCM Taifa alipolitaja bayana katika hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM pale Kizota Dodoma.
Swali: Unafikiria idadi ya wanawake waliobahatika kupata a uongozi ndani ya CCM katika uchaguzi mkuu ulifanyika mwaka huu, wanatosha na kama hawatoshi nini kifanyike?
Jibu: Kwanza kabisa hauitafika wakati ambapo tunaweza kusema kwamba idadi ya viongozi wanawake ndani ya CCM na hata serikalini inatosha. Changamoto kubwa ni kuwahamasisha wanawake wote wenye uwezo ambao ni wengi kujitokeza zaidi na zaidi kushiriki katika mchakato. Mimi ninaamini wanawake wana uwezo mkubwa kiuongozi, hata zaidi ya wanaume kwa hiyo uwino kwangu siyo hoja ya msingi. CCM imetoa kipaumbele kwa wanawake na wajitokezo ili Taifa lifaidike na uwezo, umakini na uwelewa wao mkubwa wa masuala ya kijamii, kiuchumi, kisiasa. “The sky is not the limit”. Ikiwezekana wachukue hata nafasi zote kwani bado tutabakia katika mikono salama. Mwanamke wa kulibomoa Taifa letu mimi simfahamu. Wanawake ni waumbaji. Watiwe moyo.
Swali: Ni nini matarajio yako kwenye medani ya siasa, Je unatarajia kuwania madaraka makubwa ndani ya CCM katika uchaguzi ujao?
Jibu: unajua kuna tatizo moja kubwa sana katika uelewa wa wansiasa wetu. Wengi wanatekeleza majukumu yao siyo kwa nia ya kufanya yawapasayo kuitendea jamii na Taifa bali kwa kukukotoa namna ya kuendelea kuwa viongozi. Hata ikiwezekana kwa kufanya mambo yanayoiachia jamii majeraha makubwa, kama vile rushwa. Kipaumbele ni ushindi wao na siyo vyama vyao. Kigezo na uamuzi wa mimi kuendelea kuwania madaraka ndani ya CCM kitakuwa utendaji wangu katika nafasi ambayo wanachama wamenipa tena bure. Uitikio wao kwa utendaji wangu ndicho kitakachokuwa kigezo changu kutamani kuwania nafasi siku za usoni. Kwa sasa hivi siwazi kukosa usingizi kuwawazia uongozi katika uchaguzi ujao. Ukumbuke pia kwamba cheo ni dhamana. Cheo ni deni.Cheo ni changamoto na ni mzigio mkubwa kwa yule anaepania kweli kweli kuwatumikia wananchi kwa moyo wake wote. Kuwania nafasi katika uchaguzi ujao siyo ajenda ya msingi kwa kiongozi mwenye nia ya kweli. Utendaji wake na mafanikio ya chama chake vitakuwa kigezo cha maamuzi kwa wakati muafaka.
Swali: Ni changamoto zipi zinakukabili katika uongozi wako?
Jibu: Kama nilivyosema, ndani ya Chama nitapenda kutumia elimu yangu na hekima nitakayojaliwa na Mwenyenzi Mungu kujenda mshikamano ndani ya chama Mkoani mwetu Arusha. Yanayobakia yatatekelezeka kwa kuisimamia ilani ya Miaka mitano ya Chama Cha Mapinduzi
Swali: Unazungumziaje utawala wako hapo AICC? Unafikiri umeleta mabadiliko ya kimaendeleo?
Jibu: Jibu la swali hili sinalo. Watu sahihi wa kukujibu hili ni wafanyakazi wa AICC, Wakazi wa Arusha na kwa hakika Watanzania wote. Siyo busara kujipia mbiu mwenyewe kwani mbiu utakayojipigia ni ya kujisifu. Nafikiri siyo utaratibu na ustaarabu.
Swali:Tunaomba kufahamu historia ya Ukumbi wa AICC.
Jibu: AICC ilizaliwa baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya awali Afrika Masharika. Serikali ilifanya uamuzi wa makusudi mwaka 1978 kuiunda AICC kama shirika la umma chini ya Wizara ya Mambo ya nje na Ushiukiano wa Kimataifa ili kuridhi mali zote zilizoachwa na Jumuia na pia kuendesha shughuli za mikutano na kupangisha ofisi kwa taasisi mbalimbali za ndani na nje.Haya ndiyo majukumu tunayoendelea nayo. Hata hivyo jukumu la mikutano ndilo jukumu mama na kupitia jukumu hili AICC imeendelea kupeperusha bendara ya taifa ndani na nje ya nchi.
Swali: AICC inakabiliana vipi na changamoto za kibiashara na kumbi zingine za mikutano katika kuakikisha inaendelea kutoa huduma bora zaidi ya kumbi nyingine za kimataifa katika nchi za Afrika Mashariki?
Jibu: Biashara ya mikutano inaendelea kubadilika siku hadi siku. Kwa kuzingatia ukweli kwamba AICC haikujengwa hususan kwa ajili ya Mikutano bali kwa shughuli za ofisi, tutajikita vema katika ushindani kimataifa na kikanda hapo ndoto ya ujenzi wa Kituo sahihi itakapotimia. Hata hivyo tunaendelea kuboresha kilichopo na kushindana vilivyo pamoja na vipingamizi vya mzingi vilivyopo (structural limitations).
Swali: Nataka kujua kuhusu mguu wako,nini kilikusibu hadi mguu wako mmoja ukawa katika hali hiyo?
Jibu; Naam, hili kali. Hata hivyo linadhihirisha uhalisi wako katika kazi ya uandishi wa habari. Wengi huwaza vichwani mwao maswali fulafulani na kuandika watakavyo. Ninakupongeza kwa kuwa muwazi. Mimi niliugua ugojwa wa polio utotoni mwangu. Kwa sababu hiyo mguu wangu wa kushoto uliadhirika. Wazazi wangu, ambao ninaendelea kuwashukuru katika maisha nitakayojaliwa na Mwenyenzi Mungu walilishughulikia tatizo langu kwa uwezo wao wote. Nilifanyiwa upasuaji mara nyingi na katika vipindi mbalimbali vya umri wangu kuniwezesha kuwa katika hali njema zaidi.Ninamshukuru Mungu kwa mafanikio yaliyofikiwa. Lakini hali ndivyo ilivyo kama ulivyoona wewe.
Hata hivyo, sijawahi kujihisi kwamba nina tatizo kwani sivyo nilivyolelewa. Nafikiri unajione mwenyewe. Niko “very sober”. Ninafurahia maisha yangu na kuendelea kutoa mchango wa wangu katika dunia yetu. Zipo dhana mbalimbali zinanzowalenga watu wenye tatizo kama langu. Kwa bahati mbaya wapo hata viongozi, wengine wakubwa tu ambao wamekuwa waumini wa dhana hizo za kipuuzi. Kwa hakika hata kuamini kwamba jamii zao haziwezi kuwapa nafasi za uongozi watu wenye tatizo kama langu. Hawa ni wa kisamehe bure. Ninawashukuru wazazi wangu kwa kunilea vema. Ninalishukuru Taifa langu kwa kubaini uwezo wangu na kunipa dhamana ya kuwa kiongozi. Ninakishukuru Chama Cha Mapinduzi kwa kuhuburi na kutenda kwa vitendo imani yake kwamba binadamu wote ni sawa.
Swali: Naomba kufahamu historia ya maisha yako mapana.
Jibu: Mimi nilizaliwa katika Kijiji cha Mikungani, Tarafa ya Mbuguni Mkoa wa Arusha na Wilaya ya Arusha kwa wakati ule, ambayo kwa sasa hivi inajulikana kamam Wilaya ya Arumeru mnamo tarehe 23 Augusiti 1962. Ni mtoto wa tano wa Mzee Daniel Saitore Kaaya, ambaye kwa wakati huo alikuwa ndiye Jumbe( kumbuka ukolon!) wa eneo lile. Elimu yangu ya Msingi hadi kidato cha nne ilikuwa hapahapo mkoani Arusha na nilimalizia kidato cha sita huko Tosamaganga Iringa Vijijini. Elimu ya juu nilipatie Dar-es salaam, Arusha na baadaye huko Uholanzi ambako nilihitimu shahadi ya uzamili. Nimeudhuria mafunzo mbali mbali ya kitaalamu na kiutawala nje na ndani ya nchi.
Kama ujuavyo fani yangu ni mhasibu nikiwa nimehitimu shahada ya Juu kabisa ya kitaalamu ijulikanayo kama CPA. Nimefanya kazi za kihasibu na ukaguzi AICC. Nimesajiliwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Wahasibu na wakaguzi wa Hesabu NBAA. Nimeongoza idara ya fedha na baadae idara ya Fedha na Utawala AICC kwa muda Mrefu. Nimekaimu mara mbili nafasi ya juu kabisa ya uongozi wa Kituo hadi hapo tarehe 4.4. 2007 Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania aliponiteua rasmi kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa AICC.
Kama sehemu ya Historia yangu sisiti kusema kwamba mimi na mtuzi wa muda mrefu wsa mashairi ya Kingereza. Mwaka 2003 nilitunukiwa medani ya heshima kama mtuzi bora wa Mashairi duniani, nishani ambayo nilikabidhiwa huko Washngton DC, Marekani na International Society of Poets (ISP)
Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa simu 0755312859:katabazihappy@yahoo.com:www.katabazihappy@yahoo.com:

No comments:
Post a Comment