FREDRICK SUMAYE UPO SAHIHI
Na Happiness Katabazi
JUMAPILI iliyopita waziri mkuu
mstaafu Fredrick Sumaye alifanya mkutano na waandishi wa habari na kueleza
kusikitishwa kwake baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini kuandika habari
kuhusu yeye ambazo alidai hazina ukweli wowote na kwamba hana mpango wa kukiama
chama chake cha CCM.
Sumaye ambaye alishindwa kwenye
kinyang’anyiro cha kugombea ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM,wilayani
Hanang’ mkoani Manyara,bila woga alisema CCM imegubikwa na rushwa
ya kimtandao na kutaadhalisha kama tatizo hilo lisipotatuliwa mapema linawaweza
kuleta madhara makubwa.
Lakini Sumaye alisema licha ya
CCM kukabiliwa na tatizo hilo
hayupo tayari kukiama chama hicho kama gazeti moja
lilivyoandika wiki iliyopita kuwa anataka kuamia Chadema ni wazushi.Na alituasa
sisi wanahabari kuzingatia maadili ya kazi yetu na
siyo kuandika habari za uzushi ambazo mwisho wa siku Tanzania inaweza kujikuta
inaingia kwenye machafuko kama nchi za jirani zilizowai kuingia kwenye vita ya
wenyewe kwa wenyewe kwa sababu ya vyombo vya habari kuandika habari zilizokuwa
zikiibua uhasama.
Bila kuchelewa mimi binafsi naunga
mkono tamko hilo la Sumaye kwani amesema ukweli na ametumia haki yake ya
Kikatiba iliyoanishwa wazi katika Ibara ya 18(a) ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inayosema hivi ‘kila mtu anao uhuru
wa kuwa na maoni na kueleza fikra
zake;”.
Nafahamu fika kuwa kuna watu
watambeza Sumaye kuwa rushwa ndani ya CCM kaiona leo baada ya kushindwa nafasi
ya ujumbe wa NEC ?, lakini minasema ni afadhali leo hii Sumaye
ameweza kuwa jasiri na kutueleza
tatizo hilo kwani hata Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa,
Dk.Edward Hosea analifahamu fika tatizo hilo na ndiyo maana wakati wa uchaguzi
Dk.Hosea amekuwa wakiwamwaga mashushushu wake kwenye chaguzi hizo.
Hii ni mara ya pili kwa Sumaye
kuwahasa wanahabari, mara ya kwanza aliviasa vyombo vya habari aliposhinda kesi
yake aliyoifungua Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam mwaka 2006 dhidi ya Gazeti
la Tanzania Leo ambalo limekufa hivi sasa ambalo lilichapisha habari ya uongo
ambayo ilisababisha Sumaye achukiwe na wananchi tena na kumbuka wakati habari
hiyo inachapishwa taifa lilikuwa likikabiliwa tatizo la uhaba wa vyakula
iliyosema Sumaye anamiliki Shilingi Trilioni tatu kwenye akaunti yake na Sumaye
alishinda kesi,uongozi wa gazeti hilo ulishindwa kuleta ushahidi na haukuwa na
huwezo kuwamlipa fidia Sumaye kama walivyoamriwa na mahakama na matokeo yake
mmiliki wa gazeti hilo alienda kwenye mkutano ulioitishwa na Sumaye kwa
waandishi wa habari na mmiliki huyo alienda kuomba msahama na kukiri habari ile
ilikuwa ya uongo.
Na si Sumaye wala Dk.Hosea tu, hata
Rais Jakaya Kikwete naye alishaitaka TAKUKURU kuwashughulikia wana CCM wanaoa
rushwa na si hivyo tu Kikwete alishawai kusema ndani ya CCM watu hawaaminiani na
kwamba mtu hawezi kumwachia glasi ya maji mwenzie kwa kuhofia kuthuliwa.Pia
Kikwete alishawahi kusema ndani ya serikali unakuta Waziri asemeshani na Naibu
wake au Katibu Mkuu wa wizara yake. Sasa misioni Sumaye amekosea wapi,nasisitiza
yupo sahihi kama alivyokuwa Kikwete ambaye alitueleza siri hizo tena za hatari
zinazowahusu wanachama wake na wateule wake ambazo tulikuwa
hatuzijui.Nawapongeza viongozi wote hao kwa kuwa wawazi kwetu na tuwaunge mkono
kwa uwazi huo siyo kuwalaumu.
Hakuna ubishi kwa sisi tunafuatilia
kwa undani na ukaribu siasa zinazofanywa na vyama vingi vya siasa kama
CCM,Chadema,TLP. CUF tuhuma za rushwa zimekuwa kiibuliwa na wanachama wa vyama
hivyo licha kwa upande wa vyama vingine vimekuwa vikikabiliwa na tuhuma za
kupeana vyeo kwa mtindo wa undugu,fedha,kiukanda na rushwa ya
ngono.
Sumaye ametusaidia kupaza sauti
kuhusu rushwa nyakati za uchaguzi ndani ya chama hicho lakini pia binafsi
namuuliza Sumaye yeye au wapambe wake nao hawakushiriki kwa namna yoyote hata
kutoa rushwa ya senti moja kwa wapiga kura wale wa uchaguzi ule?Au naye Sumaye
alitoa rushwa wapiga kura wakatafuta fedha zake na wakamchinjia
baharini ndiyo maana kaamua kulalamika adharani?
Sikuwepo kwenye uchaguzi wa CCM
wilaya ya Hanang’ hivyo inaniwia vigumu kumuhukumu Waziri Mary Nagu kuwa alitoa
rushwa ndiyo akashinda U-NEC au Sumaye alitoa rushwa fedha zake zikaliwa
bure.
Nigeukie hoja ya Sumaye alivyoviasa
vyombo vya habari kuwa vizingatie maadili ,ni kweli namuunga mkono Sumaye kwani
hata mimi nimeishawahi kuandika makala zaidi ya nne ya kuwaasa wanahabari
wenzangu kuwa baadhi yetu tumekuwa tukiandika habari ambazo ni za
uongo,uzushi,kuchafua watu wasiyo na hatia kwa makusudi jambo kwanza
linadhalilisha taaluma ya habari na pia kuwaletea madhara makubwa watu wasiyo na
hatia.
Ifike mahala sasa wale waandishi wahabari
wenzetu wanaokubali kutumika vibaya kuandika habari zisizozingatia vigezo ambazo
zinawazulia uongo na kuwachafua baadhi ya wananchi
wenzetu wakiwemo viongozi,taasisi,vyama na serikali ambao wengine wana umri kama
wazazi wetu kuwa na hofu ya Mungu na kuanza kujiuliza hivi habari hiyo ya uongo
na uzushi unayoiandika dhidi ya watu hao ndiyo habari ya uongo na uzushi
ingeandikwa dhidi yako au mzazi,mkeo,mume wako wako au ndugu yako
ungejisikiaje?
Mnaowatendea ubaya kwa
makusudi kupitia karamu zenu ni binadamu hawajatolewa Nyongo,wanaumia na
wanapata madhara na kuwashushia heshima na wengine wanaweza kuvumilia na wengine
hawana moyo wa kuvumilia na siku nao watakapoamua kutumia njia haramu kuwadhuru
wanahabari wanaowachafua,tusijekulalamika wala kuandamana.
Kwani hata rais Kikwete
mwaka 2008 alipokwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kumtazama
Mkurugenzi Mtendaji wa Gazeti la Mwanahalisi,Saed Kubenea aliyekuwa amelazwa
hapo kwaajili ya kumwagia kimiminika kinachodhaniwa kuwa ni Tindikali usoni
alitutaka waandishi wa habari tujilinde na kujiadhari kwani habari na makala
tunazoandika siyo kila mtu anazifurahi ,kuna wengine zinawaumi wanashindwa
kuvumilia wataamua kutushughulikia.
0716 774494
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Oktoba 12 mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment