Header Ads

MAHAKAMA KUU YAMGOMEA DK.SLAA

Na Happiness Katabazi
HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali kwa gharama pingamizi lilowasilishwa mbele yake na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Dk.Willbrod Slaa  lililokuwa likiomba mahakama hiyo ifute kesi ya madai iliyofunguliwa na mkewe Rose Kamili Slaa nee Sakum akiomba mahakama hiyo imzuie  mumewe Dk.Slaa asifunge ndoa na mchumba wake Josephine Mushumbusi.
Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Laurnce Kaduri  ambaye alisema amepitia kwa kina pingamizi lilowasilishwa na Dk.Slaa na majibu yaliyojibiwa na mlalamikaji Rose anayetetewa  na wakili wa kujitegemea Joseph Thadayo na amefikia uamuzi wa kuona hoja zilizowasilishwa mbele yake na Dk.Slaa ziliomba mahakama hii iifute kesi ya msingi iliyofunguliwa na Rose  ni dhahifu na hivyo amezitupilia mbali.
Jaji Kaduli alisema  Dk.Slaa alikosea kudai kuwa  Rose  hakuwa na haki ya kufungua  kesi hiyo ya kumzuia asifunge ndoa na mchumba wake Josephine kwa taratibu za kisheria kwasababu   Slaa na Rose hawakuwai kufunga ndoa  ila kulikuwa na dhana  ya ndoa.
“Mahakama hii inaitupilia mbali tena kwa gharama pingamizi hilo la Dk.Slaa linalosema kuwa Rose hakuwa nahaki ya kupinga ndoa yake kwasababu hakuwa mke wake na wala hawajawai kufunga ndoa kwasababu sheria ya ndoa inasema mtu ambaye umeishawahi kuishi kama mke na mume kwa zaidi ya miaka miwili,sheria inawahesabu kama ni wana ndoa hivyo mahakma hii inasema Rose ana haki ya kufungua kesi ya kuzuia ndoa ya wadaiwa yaani Slaa na Josephine na mahakama inatupilia mbali pingamizi la Slaa na kwamba kesi ya msingi itakuja kutajwa mahakamani hapo Novemba 6 mwaka huu’alisema Jaji Kaduri.
Kesi hiyo ya madai ya ndoa Na.4/2012 ilifunguliwa mahakamani hapo na Rose dhidi ya Dk.Slaa na Josephine kwa mara ya kwanza mapema Julai mwaka huu, akiiomba  mahakama isikubali shauri hilo lipelekwe kwenye Bodi ya Maridhiano ya Masuala ya Ndoa ya kwaajili ya kupatanishwa. Dai la pili, Rose anaiomba mahakama itanganze yeye na Dk.Slaa bado ni wanandoa.Dai la tatu anaiomba mahakama itamke kuwa ndoa baina yake na Dk.Slaa bado halali kisheria na kwamba ndoa nyingine itakayofungwa kinyume na sasa ndoa hiyo itakuwa ni batili.
Katika dai lake nne, mlalamikaji ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum(Chadema) huyo anadai mdaiwa wa pili(Josephine) alimshawishi mumewe(Dk.Slaa) kuivuruga ndoa yake na mumewe ambaye ni mdaiwa wa kwanza.
“Pia nia ya wadaiwa hao wawili ya kutaka kufunga waliyopanga ifungwe Julai 21 mwaka huu katika eneo lolote lile,ndoa hiyo ihesabike kuwa ni batili. Aidha anaiomba mahakama iwaamuru wadaiwa wamlipe fidia ya shilingi 50,000,000 kama gharama za matunzo ya watoto watoto wawili ambao Emiliana Slaa na Linus Slaa aliyezaliwa mwaka 1987 na kwamba walianza kuishi pamoja na Dk.Slaa kama mume na mke, ambao amekuwa akiwahudumia kwa tangu mwaka 2009 baada ya mume wake kumkimbia.
Pia anaiomba mahakama imwamuru mdaiwa wa pili(Josephine) amlipe fidia ya shilingi 500,000,000 kwasababu alimsababishia usumbufu mkubwa na kumharibia ndoa yake na kuongeza kwa kuimba mahakama hiyo impatie nafuu nyingine ambazo itaona inafaa.
Chanzo:Gazeti la Tanznaia Daima la Jumamosi, Oktoba 20 mwaka 2012.

5 comments:

Anonymous said...

I think the admin of this website is really working hard for his website, because here every information is quality based material.my web blog - diet plans that work
my web site - diets that work fast

Anonymous said...

I was pretty pleased to uncover this site. I need to
to thank you for ones time due to this wonderful read!! I definitely
loved every bit of it and i also have you saved to fav to check out new information on your web site.


Also visit my homepage; http://safedietplans.com

Anonymous said...

Good way of describing, and pleasant post to obtain data regarding
my presentation subject matter, which i am going to convey in academy.Stop by my web site; diets that work for women

Anonymous said...

Hello There. I found your blog using msn. This is an extremely well written article.

I will be sure to bookmark it and return to read more
of your useful information. Thanks for the post. I'll definitely comeback.

My homepage - reverse hotmail

Anonymous said...

vapor cigarette, smokeless cigarettes, e cigarette, e cigarettes, e cigarette, smokeless cigarette

Powered by Blogger.