VURUGU KWA KISINGIZIO CHA KUTETEA DINI YAKOMESHWE TANZANIA
Na Happiness
Katabazi
OKTOBA 12 mwaka,taifa liliendelea kuandika
historia mbaya ya vurugu za kidini huko Mbagala zilizosabishwa kundi kubwa la
watu wanaodaiwa ni waumini wa dini ya Kiislamu wenye imani kali zilizoambatana na kuchomwa moto na kuharibiwa
kwa makanisa ya Kikristo jijini Dar es
Salaam, katika kile kilichoelezwa kuchukizwa na kitendo cha mtoto wa dini ya
Kikristo ,Emmanuel Josephat (14) aliyedaiwa kukikojolea kukimwagia kitabu
kitakatifu cha Kurani.Kundi hilo liloonekana kufura kwa hasira , lifanya uhabifu huo walichukua hatua ya kufanya uhauribifu huo, baada ya kushindwa kwa jaribio la kukiteka kituo kidogo cha polisi cha Mbagala wilayani Temeke kwa nia ya kumpora mtoto huyo ambaye tayari alikuwa mikononi mwa jeshi la polisi ili waweze kumpiga.
Binafsi nalaani uhuni huu uliofanywa na wahuni wale ambao ni mambumbumbu wa sheria na sheria na maadili ya dini yao ya Kiislamu kwani Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa misingi ya sheria na siyo sheria ya dini ya Kiislamu.
Aiingii akilini watu waliofanya vurugu zile tayari wameishaitia litia taifa letu la mapigano ya kidini ,walielezwa vizuri na jeshi la polisi Temeke watawanyike na kwamba jambo hilo wanalishughulikia kisheria wao wanakaidi amri ya jeshi hilo kisha wakaanza kufanya fujo za kuchoma hadi makanisa.
Tuwailize hivi huo uhuni walioufanya wanayafahamu madhara yake kwa vizazi vya sasa na baadaye?Hivi hayo majengo (Makanisa) ambayo hayana mdomo, ndiyo yalimwagiza Josephat akakojolee kile kitabu cha Korani? Hivi nao waumini wa makanisa yaliyochomwa nao wakikosa subira wakaamua kulipiza kisasi ,nchi hii itakalika?
Ni maovu mangapi yanafanywa na watoto na ndugu wetu tena ya kutisha kama ujambazi,ushoga,usagaji,wizi lakini mbona nyie wazazi mlianzisha vurugu za kidini Mbagala hamuonyeshi kukerwa na madhambi hayo ambayo yamekatazwa kwenye vitabu vya dini za Kiislamu na Kikristo?
Nyie mliotaka kumchukulia hatua Josephat kwasababu ametenda dhambi,mnauhakika kuwa nyie hamna dhambi hata chembe mbele ya binadamu wenzenu na Mungu?Na mkae mkijia mkijua vurugu mlizozifanya ni dhambi mbele ya Mungu na sheria za nchi inayowaongoza.Hivyo mnapaswa pia mtubu na serikali iwachukulie hatua za kisheria kwani serikali kuendela kulea wa aina yenu ni hatari kwa usalama wa taifa letu huko tuendako.
Vongozi wa dini ya Kiislamu watusaidie katika hili kama Korani inawaruhusu wauimini wake wasiheshimu mamlaka ya duniani au wajichukulie sheria mikononi dhidi ya mtu wanayemtuhumu ameidhalilisha dini yao?
Wote mlioenda kufanya fujo Mbagala,tuwaulize hivi ni watu wangapi tena waumini wa dini yenu ambao wengine ni viongozi mnawafahamu wanatuhuma mbaya wanaingia kwenye misikiti na mnakubali wawaongoze ni kwanini hata siku moja hatujawaona mkipandwa na jazba na kuanza kushughulikia watu hao kwa madai kuwa wanadhihaki kitabu hicho cha kurani ambacho wamekuwa wakikitumia kuombea dua mbalimbali wakati ni watu makatili na mafisadi?
Hivi mliofanya vurugu Mbagala mnakabiliwa na umaskini,wengine hamna hata uhakika wa kula chakula bora,umaskini umewakabili kama mimi.Ningewaona wa maana sana siku mngeandama kwa kufuata taratibu mfikishe vilio vyenu kwa serikali kuhusu ugumu wa maisha unaowakabili,miundo mbinu mibovu,lakini hilo limewashinda mkaona mjiingize kwenye ujinga huu ambao chanzo chake ni watoto wadogo kulumbana.
Imeanza kuwa ni mila na desturi sasa katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya nne kwa baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu hivi sasa hasa siku za Ijumaa, kuibuka kusikojulikana na kuanzisha vurugu kama Mbagala, kuandamana bila taarifa hadi Wizara ya Mambo ya Ndani, kutoa matamko ya kushinikiza Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Mitihani ya Taifa, Dk.Joyce Ndelichako hajiudhuru, mara hawamtaki Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Simba,Sheikh Issa Ponda naye anawaongoza baadhi ya waislamu kwenda kuokoa na kudai mali za waislamu huko Chang’ombe,mara wanagomea kuhesabiwa kwenye Sensa na kisha kuwazuia watu wasiende kuhesabiwa kwenye sensa.
Kila siku ya Ijumaa ni siku ya Kuabudu kwa ndugu zetu wa dini ya kiislamu lakini hivi karibuni hususani hapa jijini Dar es Salaam, tumeanza kuona baadhi ya waumini wa dini hiyo wamekuwa wakiitumia siku hiyo kufanya mambo yao hayo ambayo wakati mwingine hayapendezi kusikika kwa watu wanaopenda amani.
Ikumbukwe kuwa Ibara ya 19(1),(2),(3) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambazo zinatoa haki kwa mtu uhuru wa mawazo,imani na uchaguzi wa mambo ya dini,shughuli za uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi.
Lakini Ibara ya 19(3) ya Katiba ya Nchi inasomeka hivi; “Hifadhi ya haki zilizotajwa kwenye ibara hii itakuwa chini ya taratibu zilizowekwa na sheria ambazo ni muhimu katika jamii ya kidemokrasia kwa ajili ya usalama wa jamii,amani katika jamii,maadili ya jamii na umoja wa wa kitaifa”.uhuru kwa mtu kwa mtu kuabudu.
Sasa vurugu hizi zinazoendelewa kufanywa na baadhi ya waislamu wachache kwa kisingizio cha kuipigania dini yao,pia vurugu hizo zinakwenda kinyume na matakwa ya Ibara ya 19(3) ya Katiba ya Nchi.
Naweza kusema jeuri hii waliyonayo baadhi ya waumini wa dini hiyo wanaoshiriki kiufanya vitendo vya uvunjifu wa amani uenda ni kwasababu kipindi kile baadhi yao walivyokamatwa kwa makosa ya kuwazuia watu wengine wasiende kuhesabiwa,wenzao wakaamua kuandamana tena bila kutoa taarifa polisi hadi wizara ya Mambo ya Ndani na hawakuchukuliwa hatua zozote na baada ya muda mfupi tukasikia wale waliokuwa wakishikiliwa na jeshi la polisi wakaachiwa, ndiyo maana uenda inayosababisha hata wafikie hatua sasa ya kujichukulia sheria mkononi kwasababu wameishajiona wao wapo juu ya sheria.
Leo hii taifa letu bado linakabiliwa na changamoto nyingi za kujiletea maendeleo ,tunashindwa kuzitafutia ufumbuzi na kufanyakazi kwa bidii lakini wachache wetu wameanza kuleta vurugu za kidini kwa sababu za kiupuzi kabisa ambazo mwisho wa siku zitakuja kutuletea madhara wote.
Napenda kuwashauri wale wote wanaotamani waione Tanzania leo hii ikiingia kwenye machafuko ya kidini, kisiasa,kikabila waame nchi waende kwenye nchi zenye machafuko ya kisasa,dini na ukabila wakaishi huko kwani huko ndiko hasa kunakowafaa wao ambao wamechoka kuishi kwenye nchi yetu yenye amani.
Mwisho naomba nimshauri Rais Kikwete na viongozi wengine wote walioshirikia nyadhifa za juu za uongozi wa kiserikali wawaeleze hao baadhi ya wauimini wa dini ya kiislamu kuwa sheria ni msumeno na kwamba hakuna aliyejuu ya sheria na kwamba Tanzania haiongozwi na sheria ya dini ya Kiislamu wa Kikrito inaongozwa na sheria za nchi na kwamba kitendo cha serikali ya awamu ya nne kuwa na rais Kikwete,Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman, Makamu wa Rais Kikwete,Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Rashid Othman,Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Jenerali Said Mwema, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Suleman Kova ni waislamu, isihakiwapi uhalali wa wao kufanya vitendo vya uvunjifu wa sheria kwa hisia kwamba waislamu wenzao wameshika madaraka ya juu nchini watawatetea.
Ninachofahamu mimi hao viongozi hao enzi za ujana wao walifanya juhudi wakajiendeleza kielimu wakasoma kwa shida,wakapata ajira na wakaonyesha jutuhudi katika utendaji kazi wao huko kwenye majeshi,na kwenye ulingo wa siasa hadi leo hii wameweza kupata madaraka hayo ya juu ambayo kwa ujinga wenu tu nyie mnaofanya vurugu mnaanzisha vurugu kwa mwamvuli wa kutetea dini ya kiislamu na mkikaa vijiweni baadhi yenu mnajitapa kuwa hakuna wakuwachukulia hatua kwasababu hivi sasa viongozi wa juu wa nchi ni Waislamu wenzenu.
0716 774494
Chanzo:www.katabazihappy.blogspot.com ; Oktoba 17 mwaka 2012
No comments:
Post a Comment