MRAMBA AYASUTA MASHITAKA YAKE
Na Happiness
Katabazi
WAZIRI wa
fedha wa zamani, Basil Mramba ameendelea kuyasuta mashitaka yanayomkabili
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, na kudai kuwa siyo yeye
aliyeiarika nchini kampuni ya Alex Stewart,wala kuiongezea mkataba wa nyongeza
kampuni hiyo na wala kuiarifu kuwa ilikuwa imeteuliwa na serikali ya Tanzania
kuwa imeshinda tenda na kwamba inahitajika kuja kufanyakazi hapa nchini wala
kuingia mkataba na kampuni hiyo.
Mramba
aliyasema hayo mbele ya jopo linaongozwa na Jaji John Utamwa, Sam Rumanyika na
Hakimu Mkazi Saul Kinemela wakati alipokuwa akihojiwa na wakili wa Waziri wa
Nishati na Madini wa zamani, Daniel Yona na Katibu Mkuu Mstaafu wa Wizara ya
Fedha, Gray Mgonja, (Elisa Msuya na Profesa Leonard Shaidi), baada ya juzi
wakili wa Mramba (Peter Swai) kumaliza kumuongoza mshitakiwa huyo kutoa utetezi
wake.
Mramba
ambaye alikuwa akijibu maswali ya wakili Msuya kwa kutumia nyaraka mbalimbali
ambazo zinaonyesha ziliandikwa na Benki Kuu na kusainiwa na marehemu Gavana
Daudi Balali zikionyesha kuwa ni BoT, ndiyo iliarika kampuni hiyo kuja
kufanyakazi ya kukagua dhahabu nchini na siyo yeye kama inavyodaiwa katika kosa
la pili katika hati ya mashitaka na upande wa jamhuri na kwamba ni Benki kuu
ndiyo iliiandikia barua kampuni hiyo kuifahamisha kuwa imeshinda tenda na kwa
hiyo BoT inaoipatia mkataba wa nyongeza wa kuendelea kufanyakazi ya ukaguzi wa
madini.
“Kwanza
nayashanga hayo mashitaka kuwa eti mimi na Yona na Mgonja ndiyo tuliiarika hapa
nchini kampuni hiyo, ukweli umeanishwa kwenye nayaraka hizi ambazo zimetolewa
mahakamani kama utambulisho ambazo zionyesha wazi ziliandikwa na BoT kwa
kampuni hiyo sasa nashangazwa leo hii nashitakiwa mimi kwa kosa hilo ambalo
halina ukweli wowote”alida Mramba.
Alindelea
kudai kuwa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge katika barua
yake ya Mei 2 mwaka 2003 aliyomuandikia Yona
nakala kwa waziri wa Fedha ,BoT katia maoni yake Chenge alisema
anakubaliana na ushauri wa serikali wa kuileta nchini kampuni hiyo ije ifanyekazi na kwamba hakukuwepo ulazima wa kulipeleka
jambo hilo kwenye bodi ya ukaguzi wa dhahabu
na alitoa ushauri wa kisheria kuhusu mkataba huo ambao uliingiwa na BoT
na kampuni hiyo kuwa taratibu zote zilifuatwa na akashauri kuhusu mkataba huo
kuwa hauitaji leseni na akaelekeza kuwa
gharama za kodi, gharama za uendeshaji wa mradi huo zitabebwa na serikali.
Jana
mawakili hao walimaliza kumhoji Mramba na ilikuwa ikitakiwa wakili Kiongozi wa
upande wa Jamhuri Fredrick Manyanda aanze kumhoji Mramba lakini hata hivyo
wakili Manyanda alidai hakuwa tayari jana kufanya hivyo anaomba akajiandae lakini hata hivyo Jaji Utamwa aliamua
kuiiarisha kesi hiyo hadi Novemba 28-30 mwaka huu, ambapo itakuja kwaajili ya
mawakili wa serikali kuanza kumhoji Mramba na jaji huyo akatoa hati za wito wa
kuitwa mahakamani mashahidi wa mshitakiwa huyo ambapo shahidi mmoja wapo ni
Chenge.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Oktoba 12 mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment