Header Ads

BABU SEYA,PAPII KOCHA WANG'ANG'ANIWA TENA

Na Happiness Katabazi MAHAKAMA ya Rufani nchini Dar es Salaam, imelikataa ombi la kufanya marejeo liliowasilishwa mahakamani hapo na MWANAMUKIZI wa muziki wa dansi nchini Nguza Vicking ‘Babu Seya’ na mwanae Papi Kocha Mtoto wa Mfalme,ambapo waliomba mahakama hiyo ifanyie marejeo hukumu yake iliyoitoa Februali 2010 ambayo iliyowahukumu kifungo cha maisha warufani hao kwasababu ina dosari za kisheria. Oktoba 30 Mwaka huu, jopo Hilo la majaji watatu walisikikiza ombi Hilo lililowaomba wafanye Marejeo ya hukumu waliyoitoa Februari Mwaka 2010ambapo wanatetewa na Wakili wa kujitegemea Mabere Marando. Uamuzi huo ambao ilisababisha watu kumwaga Machozi Katika Viwanja Vya Mahakama hiyo na wananchi Wengi kukukutana Kwenye Makundi Makundi na Kudai Kuwa Kesi hiyo Inamkono wa Kigogo mmoja serikali ndiyo mAana Mahakama inashindwa kutoa uamuzi wa kuwaachiria HURU ilisomwa na Msajili wa Mahakama ya RUFAA ,Zahara Maruma kwa Niaba ya jopo la majaji watatu Natharia Kimaro,mbarouk mbarouk na Saluma massati. Akisisoma uamuzi huo Maruma Alisema Mahakama ilikuwa na mamlaka ya kusikiliza ombi Hilo la Marejeo na kwamba limebaini Kuwa Hakuna makosa yoyote yaliyofanywa na majaji Hao wakati walipotoa hukumu ya kifungo Cha Maisha kwa Babu SEYA na Papii Kocha Februali 2010 Kama ilivyodaiwa na Wakili Marando Katika ombi lake la Kuomba Mahakama Ifanye Marejeo Katika hukumu Yao. JAJI Kimaro Alisema jopo lake Linafahamu Fika Kuwa Babu SEYA na mwanae kupatia Wakili wao Marando walipokayaga RUFAA, jopo lake liliwatia fursa ya kusikiliza pande zote yaani upande wao na upande wa waombaji RUFAA na warufaniwa ambao ni upand wa jamhuri na kwamba hoja zote zilizowawasilishwa na Wakili Marando Katika usikilizwaji wa OMB Hilo la Marejeo zilikwishwa sikiliza na kuamriwa Katika usikilizwaji wa RUFAA na Nakala ya RUFAA hiyo ni ushahidi tosha unaonyesha hoja zilizowasilishwa na Marando Katika usikilizwaji wa ombi la Marejeo aliziwasilisha Katika usikilizwaji wa RUFAA na jopo Hilo likaziamua. " kwa Kauli Moja Mahakama hiyo inatupilia Mbali ombi la kuomba Ifanyie Marejeo RUFAA yake iliyotoa Februali 2010 liliwasilishwa Mbele yake na Babu SEYA na Papii Kocha kwasababu halina mantiki kisheria"Alisema JAJI Kimaro. Baada ya kumalizia kusomwa kwa uamuzi huo huzuni na vilio vilitawala hukumu babu SEYA na Papii wakionekana kunyongonyea. mwanamuziki Jose Mara aliwaeleza waandishi wa Habari nje ya Mahakama Kuwa wanamnamuachia MUNgu na ameipokea kwa masikitiko ki mkubwa hukumu hiyo ila Ana heshimiwa mwanamuziki hayo ya Mahakama Huku akitokwa na Machozi. Oktoba 30 mwaka huu, Wakili Marando wakati akiwasilisha hoja sake alidai kwa mujibu wa kanuni ya 66 ya Mahakama ya Rufaa ya mwaka 2009 inatoa mamlaka kwa mahakama ya rufaa kufanya mapitio ya hukumu inazozitoa hivyo wateja wake wamewasilisha ombi hilo la mapitio kwasababu wanaamini mahakama yake ilikosea wazi wazi kisheria katika hukumu yake ya Februali 2010 na kwa mujibu wa kanuni hiyo inatoa mamlaka kwa mahakama hiyo kufanya mapitio ya hukumu yake. Wakili Marando alieleza kuwa ombi lake amelileta chini ya kifungu cha 3 aya A ya Kanuni ya Mahakama ya Rufaa ya mwaka 2009 , ikisomwa pamoja na Ibara 13 (3) (6)(a) ya Katiba ya nchi, litaja moja ya utelezi wa wazi wazi wa kisheria uliofanywa na mahakama hiyo, ni kwamba katika hukumu hiyo kuna baadhi ya aya inasomeka kuwa majaji hao walikubaliana na hoja yake iliyodai kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, wakati inasikiliza kesi hiyo, ilikosoea kufuata utaratibu wa kurekodi ushahidi wa watoto waliokuja kutoa ushahidi katika kesi hiyo na kwamba mahakama ya rufaa ikasema licha ya taratibu za kurekodi ushahidi wa watoto kukiukwa, mahakama yake iliona kuna ushahidi unaounga mkono na kwamba mahakama ya rufaa ilitumia ushahidi wa kuunga mkono ndiyo walioutumia kuwatia hatiani waomba rufaa kwa adhabu ya kifungo cha maisha “waheshimiwa majaji kwasababu jopo lenu katika hukumu yake lilikiri wazi wazi kuwa mahakama ya kisutu ilikosoea kurekodi ushahidi wa watoto wa dogo ambao walidai walitendewa vibaya na waomba rufaa(Nguza na Papii), na sheria za nchi zipo wazi kabisa zina sema endapo mahakama itabaini kuwa mahakama ya chini ilikiuka taratibu za kurekodi ushahidi wa watoto wa dogo, basi ushahidi ule wa watoto wa dogo uliotumika katika mahakama ya chini kuwatia hatiani washitakiwa, ushahidi huo wa watoto unafutwa na waomba rufaa au washitakiwa wanaachiriwa na pia maamuzi ya kesi mbalimbali yaliyokwisha kutolewa na mahakama hii; “Nafahamu ni kazi ngumu sana kuwashawishi nyie majaji kubadili uamuzi wenu mlioutoa katika hukumu ya Februali 2010 ambapo mliwatia hatiani wateja wangu, ila kwa uterezi huo wa kisheria niliouanisha unaonyesha katika hukumu yenu mlikubaliana na hoja yangu kuwa Mahakama ya Kisutu ilikosea kurekodi ushahidi watoto wadogo ,naamini mtatumia busara zenu na kufuata sheria inayosema wazi wazi kuwa endapo utaratibu wa kurekodi ushahidi wa mtoto utakiukwa basi ushahidi huo utafutwa na wateja wangu wataachiliwa huru, basi leo naiomba mahakama hii iwaachirie huru wateja wangu’ alidai Marando. Kwa upande wao mawakili wa upande wa mjibu maombi (DPP),Angaza Mwipopo,Jackson Mlati, Imaculata Banzi na Joseph Pande waliomba mahakama hiyo itupilie mbali ombi hilo kwasababu sababu zote alizozitoa jana ni sababu ambazo alizitoa wakati wa usikilizwaji wa rufaa na ziliamliwa katika hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo Februali mwaka 2010. Jackson alidai kama Marando anaona hukumu ya mwaka 2010 ilikuwa na dosari , basi angeomba mahakama hiyo impangie jopo la majaji watano wa kusikiliza ombi na siyo ombi lake kuja kusikilizwa na jopo la maji watatu wale wale waliotoa hukumu ile ambayo Marando anadai ina dosari. “Hoja za Marando ni za kirufaa, na hoja zake zote anazotaka kuonyesha hukumu ya mahakama hii ina dosari zilishaamriwa na mahakama hii wakati ikisiliza rufaa ya wateja wake mwaka 2010 na tunamtaka Marando aelewe kuwa hakuna maamuzi yasiyonamwisho hivyo sisi tunaomba ombi la Marando linalotaka mahakama hii ifanyiwe mapitio hukumu yake halina msingi”alidai wakili Jackson. Aliyekuwa Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Addy Lyamuya, mwaka 2004 aliyekuwa jaji wa Mahakama Kuu Thomas Mihayo liliwatia hatiani waombaji na kuwafunga kifungo Cha Maisha lakini jopo hilo la majaji wa tatu linaloundwa na Jaji Kimaro ,Massati na Mbarouk liliwatia hatiani Nguza Vicking na Papii kocha na kuwaachiria huru wanae wawili kwa makosa ya kuwabaka watoto wadogo na likawahukumu kifungo cha maisha gerezani. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Novemba 22 Mwaka 2013

No comments:

Powered by Blogger.