WANASIASA WAMLIZA MKURUGENZI RORYA
Na Happiness Katabazi,Rorya
HALMASHAURI ya Wilaya ya Rorya mkoani Mara imewalalamikia baadhi ya viongozi wa kisiasa wa Wilaya hiyo kuwa wamekuwa wakikwamisha kwa makusudi jitihada za Halmashauri hiyo za kukusanya Mapato.
Hayo yalisemwa Jana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Ephraem Ole Nguyaine Katika mahojiano Maalum na Gazeti hili ofisini kwake ambapo alisema licha ya Halmashauri hiyo hivi sasa kubuni Vyanzo Vingi Vya Mapato na imefanikiwa Kuongeza idadi ya makusanyo ya mapato ,bado kuna wanasiasa ambao wamekuwa wakiwaamasisha wananchi wasikubali kulipia ushuru na kodi mbalimbali zinazotokana na Vyanzo Vya Mapato.
"Siyo Siri mchezo huu mchana unaofanywa na viongozi wa kisiasa KWA Sababu zao wanazozijua wamekuwa wakiwaamasisha wazi wazi wananchi wasichangie kodi Katika Vyanzo hivyo Hali inayosabaisha Halmashauri kushindwa kufikia Malengo yake iliyokuwa imejiwekea Katika ukusanyaji wa Mapato, unatukera sana na nimeishawachukulia Hatua za kisheria baadhi ya viongozi wa vijijini tumewafikisha Katika kituo ha polisi Utegi na Muda wowote wanaweza kufikishwa mahakamani na pia viongozi wengine wameishakemewa Kwenye vikao husika lakini wanapuuza kwasababu ya Malengo Yao binafsi ambayo hayasaidii nchi"alisema Ole Nguyaine.
Alisema HIvi sasa Halmashauri hiyo imeweza Kuongeza Kasi ya ukusanyaji wa Mapato Kwani Katika Bajeti ya Mwaka 2012/2013 walijiwekea Malengo ya kukusanya sh.1491977000 lakini hata hivyo waliweza kufanikiwa kukusanya sh 76793367020 na Katika Mwaka wa Fedha wa 2013/2014 walijiwekea malengo ya kukusanya sh bilioni 1,931,119,000 hadi kufikia OKTOBA Mwaka Jana waliweza kukusanya jumla ya sh 1945,99433 na Mwaka huo wa Fedha unamaliizika JUNI Mwaka huu, ukilinganisha na Bajeti ya Mwaka 2011/2012 ambao Halmashauri ilikuwa imekadilia ikusanye sh 464,700,000 lakini hawakuweza kufanya vizuri Matokeo yake ikafikia inakusanya makusanyo kidogo ambayo ni sh 282,988,921.
Hata hivyo Alisema Halmashauri Ina Mashaka makubwa kwamba Katika bajeti ya Mwaka 2013/2014 wanaweza wasitimize Malengo Yao ya makusanyo MAKUBWA kwasababu ya viongozi Hao wa kisiasa wamekuwa wakiwaamasisha wananchi wasichangie ushuru wa Pikipiki,ushuru wa masoko ya Utegi,Buganjo na wananchi wanawasikiliza wanasiasa .
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Januari 8 Mwaka 2014
No comments:
Post a Comment