Header Ads

HAKIMU GABRIEL MIRUMBE AFARIKI DUNIA

HAKIMU GABRIEL MIRUMBE AFARIKI DUNIA
Na Happiness Katabazi
HAKIMU Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Gabriel Mirumbe amefariki Dunia Jana Agosti 25  Katika Hospitali ya TMJ.

Akizungumza na waandishi wa Habari  za mahakamani Leo ofisini kwake Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Isaya Halfani alisema Mirumbe amefariki Jana na msiba hupo Mbezi Salasala na anatarajiwa kuzikwa Alahmisi wiki hii.

Binafsi Kama Mwandishi wa Habari za mahakamani kwa Miaka 16  sasa , nilimfahamu hakimu Mirumbe tangu alipokuwa Hakimu wa Mahakama ya ila ya ya Kinondoni Mwaka 1999- 2001  na pia akaamishiwa Mahakama mbalimbali ikiwemo Mahakama za mkoa wa Kigoma na Kisha a karejeshwa Katika Mahakama ya Kisutu na Kisha akaamishiwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam na Mwaka Jana akarejeshwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na hadi mauti unafika Jana alikuwa ni Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Nitamkumbuka Hakimu Mirumbe kwa mambo mengi Vituko vyake ambavyo siwezi kuviandika Katika makala hii, ila Nitamkumbuka Mirumbe kwani Mwaka 1999 alipokuwa Hakimu wa Wilaya ya Kinondoni, alipotoa hukumu ya Kumfunga kifungo cha Mwaka mmoja gerezani Mwenyekiti wa Chama Cha Demokracty ( DP), Mchungaji Christopher Mtikila.

Mirumbe alimpatia Adhabu hiyo Mtikila ambaye ni Kinara wa kushinda Kesi baada ya kumkuta na hatia ya Kutenda kosa la kutoa maneno ya uchochezi ambayo haya stahili kutolewa na kiongozi wa dini.

Mtikila alimshitakiwa kwa kosa la kutoa maneno ya uchochezi ambapo Mtikila alivieleza vyombo Vya Habari Kuwa Chama Cha Mapinduzi( CCM), kimembana Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho Marehemu Horace Kolimba.Na Mtikila alitumikia Kifungo hicho Katika Gereza la Keko na alimaliza kutumikia Kifungo hicho hadi Mwaka 2000.

Hata Hivyo Mtikila alikata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam, rufaa yake kupinga hukumu hiyo na rufaa yake ilitupwa lakini pia Mtikila tayari ameishawasilisha ombi la kuomba Mahakama ya Rufaa Ifanyie mapitio hukumu ya Mahakama Kuu.

Pia Nitamkumbuka Hakimu Mirumbe Kwani alikuwa ndiye Aliyekuwa Hakimu wa kwanza kuipangiwa kusikiliza Kesi ya Madai ya kuomba Rushwa iliyokuwa ikimkabili Mtangazaji wa Televisheni ya Taifa (TBC), Jerry Murro na wenzake  ambapo alisikiliza harakahara na siku shahidi wa mwisho wa upande wa jamhuri  aliyekuwa akiongozwa kutoa ushahidi wake na Naibu Mkurugenzi wa Mshitaka marehemu Stanslaus Boniface.

Alipomaliza  kutoa ushahidi wake Hakimu Huyo ambaye alikuwa alisikiliza Kesi hiyo kwa mtindo wa aina yake mAana wakati mwingine mashahidi walipokuwa wakitoa ushahidi wao Hakimu Mirumbe alikuwa amelala na kutuacha waaandishi na watu waliokuwa walisikikiza Kesi wafinyana na kucheka vicheko Vya chini chini , Hakimu Huyo aliinuka na Kutoa uamuzi wa kumuona Murro na wenzake wana Kesi ya Kujibu.

Hata hivyo baadaye uongozi wa Mahakama ulimuondoa Mirumbe Katika Kesi hiyo na Kesi ya Murro ikapangwa kusikilzwa kwa Hakimu Frank Moshi ambaye alisikiliza Kesi hiyo na alitoa hukumu ambapo alimwachiria Huru washitakiwa wote baada ya kuwaona hawana hatia.

Pia Nitamkumbuka Hakimu Mirumbe ambaye hadi anakufa alikuwa ni miongoni mwa Mahakimu wanaosikiliza Kesi ya wizi wa Sh.Bilioni 6 inayomkabili MTu na Mdogo wake ambao ni wafanyabiashara Johnson Lukaza na Mwesigwa Lukaza na kiongozi wa jopo wanaosilikiza Kesi hiyo ni Jaji Edson Mkasimongwa na Pamela.

Baada ya kupata taarifa za kifo Cha Hakimu Mirumbe, nilimpigia simu Mtikila na kumweleza Mirumbe amefariki na amepokeaje msiba huo , Mtikila amenijibu maneno yafutatayo na ninayo nukuu hapa na kaniruhusu niyanukuu:

" Mirumbe amechelewa kufa  alitakiwa afe mapema kwasababu mshahara wa dhambi ni mahuti...wakati aliponifunga Kifungo Cha Mwaka mmoja gerezani siku hiyo anatoa hukumu ambayo hakunipa nafasi ya kujitetea Alisema ananifunga kwasababu amepewa shinikizo na viongozi wa juu wa serikali hivyo alinifunga jela kwa kutonipa nafasi ya kujitetea kwa Kigezo tu anawafurahisha wakubwa wa serikali ya CCM:

" Hivyo Mirumbe amekufa na amekwenda jehanamu Kwani kuna dhambi nyingine hata ukitubu  MUNgu akusamehi na MUNgu hajamsamehe Mirumbe kwasababu alinitendea dhambi Mimi mtumishi wa MUNgu ambaye niliongozwa na Roho mtakatifu Kusema CCM ndiyo iliyomuua Kolimba" Alisema Mtikila.

Nawashauri wasomi wenzangu  wangu kwa wasomi wa sheria na watumishi wa mahakama, mazuri  yaliyoachwa na Hakimu Mirumbe , tuyafuate na Mabaya alitoa acha tusiyafuate.

Mungu aweke mahali panapostahili roho ya Hakimu Gabriel Mirumbe.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Agosti 26 Mwaka 2014

No comments:

Powered by Blogger.