Header Ads

SERIKALI YAKIPONGEZA CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO (UB)
SERIKALI YAKIPONGEZA CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO
Na Happiness Katabazi
SERIKALI imewataka   washiriki wa mafunzo ya jinsi ya kujadili  mikataba ya Biashara na uwekezaji   kutumia taaluma hiyo waliyoipata kwaajili ya kuleta manufaa kwa mataifa Yao.

Rai hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi  Msaidizi Idara ya Elimu ya Juu ya Wizara ya Elimu ya Juu,  Dk.Jonathan Mbwambo kwaniaba ya Waziri wa wizara hiyo, Dk.Shukuru Kawambwa  wakati akifunga  Mafunzo hayo ya siku 14 yaliyoshirikisha maofisa wa juu wa fani ya biashara wa serikali za nchi nane ambayo yaliratibiwanna Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB) ambayo yalifadhiliwa na Chuo Kikuu Cha  Nordric Africa Institute, Uppsalla cha nchini Sweeden chini ya Profesa Francis Matambalya na kuwezeshwa na Mtandao wa Vyuo Vikuu Vitano TANAUP/PATU  ambapo UB, ni mjumbe wa Mtandao huo.

Dk.Mwambo Alisema kwanza serikali  inakipongeza Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB), kwa kuandaa Mafunzo hayo ambayo yameshirikisha maofisa wajuu wa serikali mbalimbali Kwani kupitia Mafunzo Hao maofisa Hao wameweza kubadilishana uzoefu wa masuala ya nchi zao kuhusu Sekta ya masoko na uwekezaji.

Dk.Mwambo alisema kila kukicha baadhi ya nchi za Africa zimekiwa zikigundulika kuwa na utajiri mkubwa aridhini na mfano mzuri ni nchi ya Tanzainia ambayo imegundulika kuwa ina nishati ya gesi , madini hivyo kupitia mafunzo hayo  kwa upande wa Tanzania  Wizara ya Viwanda na Biashara iliwakirishwa na maofisa wake Wawili wameweza kupata ujuzi ambao utaki saidia serikali ya kuweza kufanya vizuri Katika uandaaji wa masoko na uwekezaji wafanyabiashara wa Kimataifa watakaokuwa wanakuja kuwekeza nchini.

 Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB), Profesa Costa Mahalu  Alisema UB,  nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania zimekuwa  zikikabiliwa na matatizo  ya jinsi ya kuandaa masoko na kuandaa mikataba yenye tija na wawekezaji hivyo kupitia Mafunzo hayo yamesaidia kuwajengea uwezo washiriki kwenda kukabiliana na Changamoto hiyo.

Profesa Mahalu  Alizitaja nchi zilizoshiriki Katika Mafunzo hayo ya Kimataifa Kuwa ni wenyeji Tanzania, Kenya,Uganda, Burundi, Rwanda, Lesoto, Kongo, Malawi ,Ethiopia , Zambia na Madagascar.

Alisema UB Katika Mwaka mpya wa masomo     inaanza kutoa Shahada ya jinsi ya kujadili mikataba ya biashara na uwekezaji   ili iweze kuwajenga wanafunzi wengi wa Watanzania waweze kuwa bora katika eneo hilo la masoko na kuandaa mikataba ya kuiingia na wawekezaji katika sekta mbalimbali.

Aidha Balozi Mahalu Alisema Seneti ya UB, imemuidhinisha Dk.Dickson Yeboah kutoka Geneva Uswiss, Dk.Francis Matambayla, Dk. Baoudoiun Michael na Mkurugenzi wa Mtangamano wa Biashara toka Wizara ya Viwanda na Biashara nchini, Lucas Saronga Kuwa Maprofesa wa UB.

Kwa upande wake Profesa Francis Matambalya toka  Taasisi ya Nordic Africa  ya Chuo Kikuu Cha Uppsala, cha nchini Sweden ambao ndiyo waliofadhili Mafunzo hayo Alisema Kuwa yeye ni Mtanzania na anampenda nchi yake na ataakikisha kila Mara Taasisi hiyo ya Sweden inaleta Fedha kwaajili ya kuendesha Mafunzo hayo ili nchi za Tanzania na Africa kwa ujumla ziondokane na tatizo la kutokuwa na wasomi waliobobea Katika eneo Hilo la kuandaa masoko na jinsi ya kuandika mikataba na wawekezaji wa kigeni Katika sekta mbalimbali.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi,Agosti 23 Mwaka 2014


No comments:

Powered by Blogger.