JAJI BWANA NDIYE MWENYEKITI MPYA BARAZA LA CHUO KIKUU HA BAGAMOYO(UB)
JAJI BWANA NDIYE MWENYEKITI MPYA WA BARAZA LA CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO(UB)
Na Happiness Katabazi
BODI ya Wadhamini ya Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB), imemteua Jaji wa Mahakama ya Rufaa nchini, Dk.Stephen Bwana Kuwa Mwenyekiti mpya wa Baraza la chuo hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Jana Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB), Mikocheni Dar Es Salaam, Dk.William Kudoja alisema Bodi ya Wadhamini ya chuo hicho ambayo Inaongozwa na Professa Paramaganda Kabudi Ndiyo ilimteua Jaji Bwana kushika wadhifa huo mpya baada ya kuona Ana sifa za vigezo Vya kushika wadhifa huo.
Dk.Kudoja ambaye ni Naibu Makamu Mkuu wa UB anayeshughulikia Taaluma, alisema jaji Bwana ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) ya nchini Cambodia.
Jaji Bwana aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali Kama Jaji wa Mahakama Kuu Seychelles 1994-1999, Jaji wa Mahakama Rufaa ya Seychelles 2004-2009 , Kaimu wa Rais wa Mahakama hiyo ya Rufaa ya Seychelles kuanzia Mwaka 2006-2008.
Mbali na kushika nyadhifa hizo Jaji Dk.Bwana pia aliwai Kuwa Mshauri wa Benki ya Dunia kuhusu Uboreshaji wa Shughuli za Mahakama Afrika Kati ya Mwaka 2003-2008, Msajili wa Mahakama ya rufaa nchini Mwaka 1989-1994 na Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mwaka 1989 na Hakimu na Hakimu Mkazi Mwaka 1974.
Dk.Kudoja alisema Mwenyekiti huyo wa Baraza la UB, Jaji Bwana atawaongoza wajumbe wajumbe 19 wa Baraza Hilo kutekeleza majukumu hayo ambao nao wanapitishwa na Bodi ya Wadhamini wa chuo hicho na watatekeleza majukumu waliyopewa.
Mbali na Jaji Bwana Alisema wajumbe wa Baraza Hilo ni Profesa Esther Mwaikambo kutoka Taasisi ya Vyuo Vikuu Binafsi(IES), Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya juu nchini, Dk.Sylvia Temu, Mkurugenzi Mtendaji Mstaafu wa Kituo Cha Uwekezaji nchini(TIC), Emmanuel Ole Naiko, Vicent Jonas, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi, George Simbeye, Wakili Mwandamizi wa Serikali Malata Gabriel , Mhadhiri wa Sheria wa chuo hicho, Baraka Mkami, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Halima Kihemba, Makamu Mkuu wa chuo hicho ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge la Katiba, Profesa Costa Mahalu, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mercy Sila, Dk.William Kudoja
Aidha Alisema wajumbe wengine ni Naibu Makamu Mkuu wa UB anayeshughulikia Fedha, Dk. Elifuraha Mtalo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Kilimo Sokoine anayeshughulikia Taaluma Profesa Peter Gillah, Mwenyekiti wa Kampuni ya Proin Promotions Limited Johnson Lukaza, Mathias Massawe, Mkurugenzi wa Sayansi na Teknolojia Katika Wizara ya ya Mawasiliano ,Sayansi na Teknolojia Profesa Evelyn Mbede, Balozi na Wakili mwandamizi nchini Mwainaidi Sinare Maajar, Wakili wa kujitegemea Vulfrieda Mahalu na Mkuu wa Shule ya Elimu ya UB, Profesa Elias Bayona.
Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Agosti 17 Mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment