WAWILI KORTINI KWA UGAIDI DAR
WAWILI KORTINI KWA UGAIDI DAR
WIMBI la Kuwafikisha washukiwa wa makosa ya ugaidi mahakamani limezidi kushika kasi kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi Jana kuwafikisha watu Wengine Wawili kwa makosa mawili ya ugaidi Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar Es Salaam.
Mbele ya Hakimu Mkazi Frank Moshi, Mawakili waandamizi wa serikali Bernad Kongora, George Baraso na Peter Njike walidai Kesi hiyo ugaidi Na.31 ya Mwaka 2014 na kwamba washitakiwa Hao ni Kassim Salum Nassoro na Said Shehe Sharifu.
Wakili Njike alidai kosa la kwanza ni la kula Njama Kutenda kosa la ugaidi kinyume na Kifungu cha 27(c) Cha Sheria ya Kuzia Ugaidi ya Mwaka 2002 na kwamba washitakiwa hao Katika tarehe tofauti Kati ya Januari 2013 na Juni 2014 katika maeneo tofauti Katika eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , walikuwa Njama Kutenda kosa kimyume Cha Sheria hiyo kwa kuwaajili watu ili washiriki kufanya matendo ya ugaidi.
Wakili Njike Alilitaja kosa la pili Kuwa kuwaajili watu ili washiriki kufanya vitendo Vya ugaidi kinyume na Kifungu Cha 21(b) Cha Sheria ya Kuzia Ugaidi ya Mwaka 2002. Kuwa washitakiwa wote Katika tarehe tofauti Kati ya Januari 2013 na Juni 2014 katika maeneo tofauti ya eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , kwa makusudi wakikubali kumwajili Sadick Absaloum na Farah Omary ili washiriki Kutendavitendo ugaidi na kwamba upelelezi wa Kesi hiyo bado haujakamilika.
Kwa upande wake Hakimu Moshi aliwataka washitakiwa wasijibu chochote kwasababu Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza Kesi hiyo na kwamba ni Mahakama Kuu ndiyo yenye Mamlaka ya kusikiliza Kesi hiyo na akaairisha hadi Agosti 6 Mwaka huu itakapokuja kwaajili ya kutajwa ambapo upande wa jamhuri Ulidai siku hiyo utawasilisha ombi Lao.
Julai 17 Mwaka huu, itakumbukwa DPP, aliwafikisha watu 17 mahakamani hapo KWA makosa ya ugaidi..
Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la IJumaa, Agosti Mosi Mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment