Header Ads

DPP AZIDI KUMBANA SHEIKH PONDA


DPP AZIDI KUMBANA PONDA
Na Happiness Katabazi
UPANDE wa Jamhuri Katika ombi la kuiomba Mahamaka Kuu Kanda ya Dar Es Salaam, itoe amri ya kusimamisha usikilizwaji wa Kesi ya Msingi inayomkabili Mwenyekiti wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu , Sheikh Ponda Issa Ponda Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro, umeiomba Mahakama hiyo ilitupe  ombi Hilo kwasababu linadosari.

Maombi hayo yaliwasilishwa Jana na Wakili  Mwandamizi wa Serikali, Bernad Kongora Mbele ya Jaji Lawrence ambapo ombi Hilo la Ponda lilikuja Jana kwaajili ya kuanza kusikilizwa lakini hata hivyo ombi Hilo la Msingi lilishindwa kuanza kusikilizwa kwasababu upande wa jamhuri ulikuwa umewasilisha pingamizi la awali la kutaka ombi Hilo la Ponda litupwe ambapo Jana Mahakama hiyo  ilianza kusikiliza pingamizi Hilo.

Ombi Hilo la Ponda dhidi ya jamhuri  Linaomba Mahakama hiyo itoe amri ya usimamishe  usikilizwaji wa Kesi ya Uchochezi inayomkabili Ponda Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro  hadi rufaa iliyokatwa na Ponda Katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam, itakapomalizika.

Wakili Kongora alidai  pingamizi Lao Lina hoja mbili, hoja ya kwanza ni kwamba  ombi Hilo ambalo liliwasilishwa mahakamani hapo kwa Kufungwa mkono na hati ya kiapo na chemba Samansi , chemba Samansi na hati ya kiapo zinadai za kisheria na dosari hizo hazirekebishiki na paragrafu hiyo ndiyo Msingi wa ombi la Ponda Kwani Ponda Mwaka 2012-2013 alimshitakiwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na akafungwa Mwaka mmoja nje , na kwamba Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam hakuwepo Katika Mahakama ya Kisutu  na Sheria Na.3 ya Sheria zilizoandika ya mwaka 2011, inaelekeza wazi jinsi utaratibu wa kuandika hati za Viapo.

ALidai Kuwa Kuwa paragrafu  ya tano na Sita ya ombi Hilo la Ponda anayetetewa na Wakili Nassor Juma, zinamaombi ambayo hawatakiwi kuweka Kwenye hati ya kiapo.

" KWA mtazamo wa upande wa jamhuri Tunaona hili ombi la Ponda ni ombi ambalo Linaomba Mahakama hii Ifanyie mapitio Kesi inayomkabili Ponda mkoani Morogoro....sasa sisi tunasema Mahakama hii imefungwa mkono yaani haina mamlaka ya kufanyia mapitio kwasababu kwa mujibu wa Kifungu ha 44(1)a Cha Sheria Mahakimu na Mahakama(MCA), Kwani Kifungu hicho kinatoa mamlaka ya wa Mahakama kuitisha jarada na kilikatazwa kutoka Mahakama za Hakimu Mkazi na siyo Kama Alivyofanya Ponda kulileta ombi Hilo mwenye mahakamani' alidai Wakili Kongora.

hata hivyo Kongora alidai Kuwa Mahakama hiyo unafungwa mkono kusikiliza ombi Hilo kwasababu Tayari ombi Hilo lilishasilishwa mahakamani hapo na Majaji Wawili Tofauti ( Jaji Itemba na Augustine Mwarija ambao Maombi hayo mawili yananoga nana na ombi la sasa yalikuwa na namba 12 na 13 Mwaka 2014 na Majaji Hao wote walitupilia Mbali Maombi hayo ya Ponda.

' Mtukufu Jaji Maombi hayo sasa Tunaona Ponda ameamua kurudisha ombi hili Hilo mwa mtindo tofauti ...Tunaomba ombi litupwe" alidai Wakili Kongora.

kuhusu hoja ya pili, Wakili Huyo wa serikali alidai Mahakama hiyo imefungwa mkono kutoa amri ya Kusimamisha usikilizwaji wa Kesi Morogoro  kwasababu Kifungu hicho Cha 44(1) a Cha Sheria ya Mahakimu na Mahakama, hakitoi Haki Kwa Mahakama kutoa amri hiyo inayoombwa na Ponda.Kifing hicho kinatoa Haki Kwa Mahakama kuitisha jarada la Kesi husika iliyofunguliwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi na kilifanya uchunguzi na siyo mlalamikaji apeleke ombi mahakamani la kuomba Mahakama Ifanyie uchunguzi Kesi iliyopo Katika Mahakama ya chini Kama Alivyofanya Ponda.

' Ni rai ya upande wa jamhuri Kuwa Mahakama itupilie Mbali ombi Hilo la Ponda kwasababu linadosari za kisheria na Mahakama haina mamlaka ya kutoa amri ya Kuzuia usikilizwaji wa Kesi inayomkabili Ponda, mkoani Morogoro kwasababu ni Mahakama Kuu ndiyo ilikuwa na mamlaka ya kuitisha jalada la kesi inayomkabili Ponda mkoani Morogoro na kwa si kama alivyofanya Ponda kuleta mwenye ombi hilo mahakamani hapo linaloomba mahakama ifanyie uchunguzi kesi ya Morogoro na itoe Amri ya kuzuia usikilizwaji wa kesi ya Morogoro hadi pale rufaa aliyoikata Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, itakapomalizika.alidai Kongora.

Kwa upande wake Wakili wa Ponda, Nassor Juma alidai baada ya kusikiliza hoja za upande wa jamhuri Kuhusu pingamizi Hilo la awali dhidi ya mteja wake, ananiomba Mahakama Iarishe shauri Hilo ili aweze kupata  muda wa kujiandaa  kujibu hizo hoja mAana hoja zilizoibuliwa Leo na Kongora zimemchanga na hivyo Hakuwa a jiandaa na Jaji Kaduri akaairisha Kesi hiyo hadi Septemba Mosi Mwaka huu, Kesi hiyo itakapokuja kwaajili ya Wakili wa Ponda Kuja Kujibu hoja za upande wa jamhuri.

Awali Jana Kabla ya kuanza kusikilizwa KWA pingamizi Hilo, Wakili Kongora alidai rufaa iliyokatwa na Ponda dhidi ya jamhuri ambapo Jaji Kaduli alikuwa Amepangwa kusikilizwa Kesi zote mbili yaani rufaa ya Ponda kipinga hukumu ya Kisutu na ombi Hilo la kuomba Kesi ya morogoro isimame, Kongora alidai baada ya uchunguzi wa upande wa jamhuri umebaini Hakuna rufaa yoyote iliyokatwa na Ponda Katika Mahakama hiyo kwasababu Ponda hakuwasilisha kwanza hati ya nia ya kukata rufaa mahakamani hapo hivyo kisheria unachukuliwa Hakuna rufaa iliyokatwa na Ponda.

Hata  hivyo Jaji Kaduli Alisema ameisikiliza pia hoja hiyo kuhusu rufaa ya Ponda ila hataweza kuitolea uamuzi kwasababu hawezi kusikiliza Kesi zote mbi zilizofunguliwa na MTu mmoja(Ponda) na kwamba alilerejesha jarada la rufaa ya Ponda kwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo ili aweze kumpamga Jaji  mwingine wa kusikiliza rufaa hiyo na kwamba yeye atabaki alisikiliza ombi Hilo la P onda Linaloomba Mahakama hiyo itoe amri ya kusitisha usikilizwaji wa Kesi ya Morogoro na akaamuru Ponda are erejeshwe gerezani.

Ponda aliwasilisha mahakamani hapo ombi la Kuomba Mahakama hiyo itoe amri ya Kuzuia Kesi ya ya uchochezi inayomkabili Morogoro ,isiendelee kusikilizwa hadi pale rufaa yake aliyoikata mapema Mwaka Jana ya Kapinga hukumu iliyotolewa Na Mahakama ya Kisutu Mei 9 Mwaka Jana, ambayo ilimtia hatiani Kwa kosa la kuingia Kwa jinai Katika Kiwanja Cha Markas Chang' ombe, ambapo Mahakama hiyo ilimfunga Kifungo Cha nje Cha Mwaka mmoja, lakini Agosti Mwaka Jana, alifikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro akikabiliwa na Kesi mpya ya uchochezi na kutenda kosa wakati yupo chini ya uangalizi wa Kifungo Cha Mwaka mmoja nje.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima  la Jumanne, Agosti 5 Mwaka 2014.

No comments:

Powered by Blogger.