Header Ads

UB ILIVYOPANIA KUINUA ELIMU YA BIASHARA,UWEKEZAJI KIMATAIFA


UB ILIVYOPANIA KUINUA ELIMU YA BIASHARA,UWEKEZAJI KIMATAIFA

Na Happiness Katabazi

AGOSTI 11- 22  mwaka 2014, Chuo Kikuu cha Bagamoyo ( UB) kilichopo Mikocheni kwa Warioba Dar es Salaam, kiliandika historia mpya kwaniaba ya serikali Tanzania, kwa kuendesha  Mafunzo ya siku 14 ya jinsi ya kujadili mikataba ya Biashara na Uwekezaji  Kimataifa .

Mafunzo hayo ambayo yameshirikisha maofisa Biashara waandamizi toka serikali za nchi nane ikiwemo Tanzania na yalifadhiliwana na Taasisi ya Nordic Afrika ya Chuo Kikuu Cha Uppsalla , Sweeden  ambayo Taasisi hiyo ili wakilishwa na Profesa Francis Matambalya na mtandao wa vyuo vikuu vitano ambapo UB ni mwanachama wa mtandao wa (TANUP/PUTAna serikali   iliwakirishwa na  Biashara toka Wizara ya Viwanda na Biashara na Ofisa Biashara wa Wizara hiyo  Elia Mtweve.

Akizungumza Katika siku ya Kufunga Mafunzo hayo Ijumaa iliyopita Katika Hoteli ya Habour View Da Es Salaam,  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB), Profesa Costa Rick Mahalu aliishukuru Taasisi ya Nordic Afrika ya Chuo Kikuu Cha Uppsalla, Sweedn kilichowasilishwa na Mtanzania ambaye ni mwadhiri wa Uchumi wa Chuo hiyo nchini Sweeden, Profesa Matambalya  kukubali ombi la Chuo Kikuu Cha Bagamoyo la kufadhiliwa Mafunzo ya jinsi kuandaa majadaliano ya Biashara na uwekezaji  kwa maofisa wa fani ya Biashara toka nchi  nane ambapo Tanzania kupitia Chuo Kikuu Cha Bagamoyo.

Profesa Mahalu pia alisema  anaishukuru  serikali ya Tanzania kukubali Mafunzo hayo ambayo ya naenda kusababisha Chuo Kikuu Cha Bagamoyo Oktoba Mwaka huu kuanzisha  shahada mpya ya jinsi ya kuanda mjadala ya Kibiashara na uwekezaji ambayo itakuwa ni shahada ya kwanza kuanza kutolewa Katika vyuo vikuu hapa nchini na nchi zilizoshiriki Katika Mafunzo hayo, yaendeshwe hapa nchini.

Profesa Mahalu alisema  washiriki wa Mafunzo hayo walitokea nchi Tanzania ambayo ni Mwenyeji,   Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Lesotho, Kongo, Malawi, Ethiopia, Zambia na Madagascar.Na Baadhi wa washiriki ni maofisa wa juu wa serikali wa nchi wanazotoka na mmoja ni Mkurugenzi  wa Taasisi za Sekta Binafsi nchini Lesotho, Thabo Quesi na wengine wanatoka Vyuo Vikuu Vya vya mataifa Yao.

' Kwa Kuwa Mafunzo haya yameletwa UB, Kwaniaba ya Chuo Kikuu Cha Bagamoyo, tunaahidi kufanya mradi wa Mafunzo haya ni endelevu na unakuwa  kwa kasi Kwani Tayari tumeishaanzisha Taasisi mpya itakayokuwa chini ya Shule ya Biashara na Utawala ya UB inayoongozwa na Dk.Lenny Kasoga  ambapo Taasisi hiyo itakuwa inatoa  Mafunzo ya jinsi ya kuandaa majadiliano ya Kibiashara na uwekezaji :

" Nanaiomba serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara iruhusu maofisa wake wa Biashara waje kusoma shahada hiyo Kwani shahada hiyo itakuwa ni mpya na itawasaida maofisa Biashara wetu kukabiliana na tatizo la kushindwa kufanya vizuri Katika eneo la majadiliano na Biashara ya Kimataifa na wananchi wengine Waje kusoma kozi hiyo" anasema Profesa Mahalu.

Profesa Mahalu Alisema Seneti ya UB Imefikia uamuzi wa kuwatunuku  uprofesa kuwa maprofesa  wa UB, wasomi wanne waliobobea Katika fani Biashara na kutokana na Seneti imejiridhisha Kuwa wasomi Hao wamefanya mambo Makubwa kupitia taaluma ya Biashara .

Aliwataja wasomi Hao Kuwa ni Dk.Dickson Yeboah ambaye ni Mfanyakazi wa Shirika la Biashara la Dunia (WTO) yenye makao yake makuu  Geneva Uswiss, Dk.Francis Matambalya,Dk. Baoudoiun Michael na Mkurugenzi wa Mtangamano  wa Biashara toka Wizara ya Viwanda na Biashara nchini, Lucas Saranga Kuwa maprofesa.Na kwamba kuanzia siku hiyo ya Agosti 22 Mwaka huu ,wasomi Hao wametunukiwa Kuwa ni maprofesa.

Aidha Balozi Mahalu anasema sherehe za ufungwaji wa Mafunzo Yale uliambatana na kuwatunuku uprofesa na pia kuzindua Mtandao wa vyuo vikuu vitano  (TANUP/PUTA)  ambavyo vyuo vikuu hivyo vi nafanyakazi Kwa kushirikiana ambapo ulizinduliwa Mtandao huo.

Mkuu wa Shule ya Biashara na Utawala ya Chuo Kikuu Cha Bagamoyo, Dk.Lenny Kasoga , Profesa Lucas  Saranga, Profesa Yeboah ,Profesa Matambalya , Profesa Baoudoiun na Profesa Vale Karugaba ambao wote walikuwa ni wakufunzi katika mafunzo hayo kwa nyakati tofauti walisema waliweza kuwafundisha washiriki wa mafunzo hayo mambo makuu matano:

Moja, kiwango cha biashara na uwekezaji kilichofikiwa.Pili, misingi ya uwekezaji  na mazingira ya biashara katika ngazi ya kimataifa, Tatu; Uchambuzi wa uwiano wa ushindani  wa kibiashara na uwekezaji ngazi ya kimataifa. Nne; Nadharia  ya majadiliano ya Biashara na uwekezaji kwa   vitendo.Tano; kushiriki kwa majadiliano ya Biashara  na uwekezaji.

Aidha Matambalya ambaye Taasisi yake ndiyo Imebadili Mafunzo hay ya kwanza kutolewa nchini anasema yeye ni Mtanzania na anafanyakazi Katika Taasisi hiyo ya kigeni ya Nordic ,Uppsalla,Uswiss ataakikisha huo mradi wa Mafunzo ambao wameupeleka UB, unakuwa endelevu na Taasisi yake itaendelea kufadhili ili Watanzania wengi waweza kusoma kozi hiyo ili mwisho wa siku taifa liweze kuondokana na tatizo la Kuwa na wataalamu wasiyobobea Katika eneo la majadiliano ya Biashara na uwekezaji na kuingia mikataba na wawekezaji .

Kwa upande wake  Aliyekuwa mgeni rasmi katika kufunga mafunzo hayo ,Mkurugenzi Msaidizi  wa Idara ya Elimu ya Juu serikali imewataka   washiriki wa mafunzo ya jinsi ya kujadili  mikataba ya Biashara na uwekezaji   kutumia taaluma hiyo waliyoipata kwaajili ya kuleta manufaa kwa mataifa Yao.

Dk. Mbwambo kwaniaba ya Waziri wa wizara hiyo, Dk.Shukuru Kawambwa anasema  serikali  inakipongeza Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB), kwa kuandaa Mafunzo hayo ambayo yameshirikisha maofisa wajuu wa serikali mbalimbali Kwani kupitia Mafunzo Hao maofisa Hao wameweza kubadilishana uzoefu wa masuala ya nchi zao kuhusu Sekta ya masoko na uwekezaji.

Dk.Mwambo anasema  kila kukicha baadhi ya nchi za Africa zimekiwa zikigundulika kuwa na utajiri mkubwa aridhini na mfano mzuri ni nchi ya Tanzainia ambayo imegundulika kuwa ina nishati ya gesi , madini hivyo kupitia mafunzo hayo  kwa upande wa Tanzania  Wizara ya Viwanda na Biashara iliwakirishwa na maofisa wake Wawili wameweza kupata ujuzi ambao utaki saidia serikali ya kuweza kufanya vizuri Katika uandaaji wa masoko na uwekezaji wafanyabiashara wa Kimataifa watakaokuwa wanakuja kuwekeza nchini.

' Nchi nyingi za Afrika ikiwemo Tanzania zimegundulika Kuwa na  utajiri mfano Tanzania hivi sasa imegundulika Kuwa na  nishati ya gesi hivyo Mafunzo hayo yataisidia nchi kuondokana na tatizo kuingia mikataba na wawekezaji wa kigeni ambayo italeta tija kwa mataifa ya nchi zinazoendelea.

Nao washiriki wa Mafunzo hayo Bifou Lufuma toka Serikali ya Kongo na Thabo Quesi  (Lesotho) na Elia Mtweve kutoka Tanzania wanasema Mafunzo hayo yamewajengea uwezo na kwamba watakuwa mabalozi wazuri Katika maeneo Yao ya Kazi na kwamba wanaiopongeza UB kuendesha Mafunzo ambayo ni ya kwanza kutolewa hapa nchini.

Mwandishi wa makala hii ni:
Ofisa Habari wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB)
0716 774494
Blog:www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook: Happy Katabazi
Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Agosti 30 Mwaka 2014







No comments:

Powered by Blogger.