Header Ads

MAKADA SITA CCM HAMMO KWENYE URAIS 2015!

MAKADA SITA CCM HAMMO KWENYE URAIS!
Na Happiness Katabazi
IBARA ya 18(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 , inatoa kwa Mwananchi yoyote kutoa maoni yako.Na Mimi
Leo katika makala hii natumia haki hiyo ya Kikatiba kutoa maoni yangu.

Ibara Ta 21(1) ya Katiba ya nchi inatoa haki ya kuchagua au kuchaguliwa kwa Mtu yoyote anayetaka kufanya hivyo. Nami naheshimu haki hiyo Kwa Watanzania wenzangu hasa makada wale Sita wa CCM wanaendelea kutumikia Adhabu endelevu ya kufanya makosa ya kuanza kampeni za urais mapema na kuvunja Kanuni za Chama hicho.

Makala yangu ya Leo nitajadili    mazingira ya kisiasa na upepo wa kisiasa ulivyo kwa  makada Sita wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  ambao Kamati ya Maadili ya CCM Mwaka 2014  ili wakuta  na hatia ya kuvunja kanuni za Chama hicho na kuanza kampeni mapema za urais Kabla ya muda mwafaka uliopangwa na Chama hicho.

Tujikumbushe  taarifa ya  Kamati ya Maadili ya CCM  iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi ,Nape Nnauye Februali 18 Mwaka 2014  kwa vyombo Vya Habari.

Taarifa hiyo ni hii hapa :  Kati ya tarehe 13/02/2014 na tarehe 18/02/2014 kumekuwa na mfululizo wa vikao kadhaa vya Chama kitaifa vilivyoshughulikia suala la maadili ndani ya Chama. Vikao hivyo ni pamoja na Kamati Ndogo ya Udhibiti tarehe 13-14/02/2014, Tume ya Udhibiti na Nidhamu 18/02/2014 na Kamati Kuu tarehe 18/02/2014.

Waliohojiwa katika mfululizo wa vikao hivi ni wafuatao:- 1. Ndugu  Frederick Sumaye 2. Ndugu Edward Lowasa 3. Ndugu Bernard Membe 4. Ndugu Stephen Wassira 5. Ndugu January Makamba 6. Ndugu William Ngeleja Baada ya kuwahoji ilithibitika kuwa baadhi ya tuhuma dhidi yao ni za kweli na hivyo kupendekeza adhabu. Mapendekezo hayo yalipelekwa kwenye Tume ya Udhibiti na Nidhamu na hatimaye Kamati Kuu ya CCM ambayo ilitoa adhabu kwa wahusika. Kwa ujumla waliohojiwa wamethibitika kuwa na makosa yafuatayo:-

 1. Walithibitika kuanza kampeni za kutafuta kuteuliwa kugombea Urais kabla ya wakati kinyume na Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara 6(7)(i). 2. Wamethibitika kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya Chama na baadhi yao kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya jamii. Kosa hili nalo ni kwa mujibu wa Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara kadhaa za kanuni hizo. 

Kamati Kuu baada ya kuthibitisha makosa hayo imewapa watu wote sita waliohojiwa adhabu ya ONYO KALI na kuwataka wajiepushe na vitendo vinavyokiuka maadili na iwapo wataendelea na vitendo hivyo Chama kitawachukulia hatua kali zaidi. Tafsiri ya adhabu ya ONYO KALI kwa mujibu wa Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara ya 8(ii) (b) ni:- “Mwanachama aliyepewa adhabu ya ONYO KALI atakuwa katika hali ya kuchunguzwa kwa muda usiopungua miezi 12, ili kumsaidia katika jitihada zake za kujirekebisha.” 

Kamati Kuu imeitaka pia Kamati Ndogo ya Udhibiti kuwachunguza na kuchukua hatua kwa wote waliohusika kwa namna moja au nyingine (mawakala na wapambe) kufanyika kwa vitendo hivyo vilivyovunja Kanuni za Chama. Aidha, Kamati Kuu imewaonya vikali Viongozi na Watendaji wa Chama na kuwataka kujiepusha kujihusisha na matendo ya wanawania Urais yanayovunja na kukiuka maadili ya Chama, wametakiwa kuzingatia Kanuni na taratibu.

Februali Mosi Mwaka 2015 , Katika Sherehe za Miaka 38 ya kukumbuka kuzaliwa  kwa CCM Mkoani Ruvuma, Mwenyekiti wa Chama hicho taifa, Rais Jakaya Kikwete Katika hotuba yake ya siku hiyo pamoja na mambo mengine alisema kuna wagombea urais wazuri tu 'Presidential Material' ila hawajitambui lakini kuna haja tuwashawishi ili wagombee uongozi.

Lakini Februali 28 Mwaka huu, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa , Nape Nnauye alizungumza na waandishi wa Habari ikiwa ni muda mfupi baad ya kumalizika kwa Kikao cha Kamati Kuu cha siku Moja kilichoketi Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na maadhimio mengine yaliyofikiwa na Kamati Kikuu ni kusimamisha makada wake wa Tatu Professa Anna Tibaijuka nafasi ya ujumbe wa Kamati Kuu, pia William Ngeleja na Andrew Chenge nafasi ya ujumbe wa NEC na kuachia Baraza la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iendelee kuyafanyia Kazi mashauri dhidi ya makada hao watatu.

Na Makada wote watatu wanakabiliwa na mashauri ya Uvunjifu wa Maadili ya umma wakiwa ni watumishi wa umma walinufaika na Fedha za Akaunti ya Escrow  na mashauri Yao yapo Kwenye Baraza la Sekretarieti ya  Maadili ya Viongozi wa Umma.

Aidha Nape alisema pia Kamati Kuu imefikia uamuzi wa makada sita ambao adhabu yao ilikiwa ni miezi 12 ambayo ilikuwa adhabu hiyo imalizike Februali mwaka huu, kuwa bado makada sita wanaendelea kuwa chini ya uangalizi wa kuona Kama Adhabu waliyokuwa wamepewa waliitekeleza Kama waivyoamriwa waitekeleze na mamlaka ya CCM kwa maana makada Hao bado wapo Katika Gereza la CCM.

Kwa uamuzi huo wa Kamati Kuu uliyosomwa na Nape tunaweza Kusema Kuwa uenda Adhabu ile kwa makada wale Sita ambao ni Lowassa, Membe na wanzake ni endelevu maana Miezi 12 imeishapita Kamati Kuu ya CCM ni Chombo cha juu cha Chama hicho Katika kufanya maamuzi Mbali mbalimbali ya Chama hicho.

Binafsi nimekaa chini nimetafari kwa kina Kauli ile ya Rais Kikwete iliyosema tukawashawishi watu wenye sifa za Kugombea urais ili wagombee Kwani kuna watu wanasiasa hizo ila hawajihafamu Kuwa wanasifa hizo ila wanaitaji kushawishiwa na kuwaambiwa Kuwa wanasifa hizo, Pia tamko la Kamati Kuu ya CCM.

Nimefikia uamuzi  wa kuona Kuwa wale makada Sita wa CCM ambao bado wanaendelea kushikiliwa Katika Gereza la CCM Kuwa hawamo Kwenye kinyang'anyiro cha Kugombea urais kupitia CCM Mwaka 2015.

Hivi Nyie makada Sita wa CCM akili Zenu  zinawatuma kabisa eti mtoke  gerezani ambapo mmemfungwa  na Chama chenu baada ya kupatikana na hatia ya kuvunja Kanuni na Maadili ya Chama chenu  halafu mruhusiwe Kugombea na muwe  rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzainia? 

Ni aliyekuwa Rais wa kwanza wa Afrika Kusini marehemu Nelson  Mandela aliyepata  bahati hiyo  ya kutoka gerezani kutumikia Kifungo ambapo Enzi hizo Africa Kusini ilikuwa ikiongozwa na serikali ya Makaburu ndiyo iliyomshitaki .

Mandela  Ambaye alikuwa akimpigia nia Uhuru wa watu weusi kwa ujumla hivyo alikuwa anataka watu  wapate Uhuru na wajitawale na wale Makaburu waondoke wa waachie nchi Yao na hatimaye alitoka gerezani na  Kuwa rais wa nchi hiyo Kwani wananchi wote walimuunga mkono na kukubali awe rais wao kwasababu alikuwa akiwapigania watu weusi wanyonge watoke Kwenye mikono ya koloni Kaburu.

Lakini Nyie makada Sita wa CCM ambao  ni dhahiri sasa Kifungo chenu ni endelevu Kwani hakijulikani kimaisha  lini , mlifungwa gerezani na Kamati ya Maadili ya Chama chenu cha  CCM kwasababu ya mmlivunja Kanuni za chama chenu zilizotajwa kwenye  Kanuni ya Uongozi na Maadili toleo la Mwaka 2010 .

Mlitenda makosa hayo siyo kwaajili ya kutetea maslahi ya wa CCM wote au Wanzania wote la hasha mlitenda makosa hayo kwa makusudi tu kwaajili ubinafsi wenu ,tamaa ya kupata urais ni kwaajili ya kujipanga mapema ili mkilata urais mje mjinufaishe nyie na wafuasi wenu wa chache sana ndani ya CCM.

Watoto wa mjini tunasema  mlitenda makosa hayo ya utovu wa maadili kwa kuvunja kanuni za chama chenu kwa maslahi ya matumbo yenu yaani 'Tumbo Street' siyo maslahi ya Watanzania wote na wana CCM wote.

Makada Sita wa CCM ambapo Adhabu yenu ni dhahiri sasa inaoenekana ni endelevu nawashauri vunjeni kambi Zenu za urais  na zikalisheni chini kambi Zenu mzieleze ukweli Kuwa kwa mazingira mnayo yaona HIvi sasa kupitia Kauli ya Mwenyekiti wa Chama chenu ,Rais Kikwete aliyoitoa Mkoani Songea, uamuzi wa Kamati wa Februali 28 Mwaka huu, ni Dalili za wazi kabisa kwamba Kati ya makada Sita mliopo gerezani ni wazi Hakuna Kada hapo jina lake linapitishwa na CCM Kuwa mgombea urais .

Waambieni ukweli wafuasi  wenu wajue kwamba mission ya nyie kuwa marais wa Tanzania,imevurugika vibaya sana tena wakati 'Pilau ' Ndio  limeiva linataka kupakuliwa watu wale ili waende kuwashawishi  wanachama wengine wanaofaha Kugombea urais Kwani Nyie makada Sita Tayari mmeisha chafuka   na mna rekodi ya Kifungo cha kuvunja Maadili na Kanuni za Chama chenu na hadi sasa Kifungo chenu bado kinaendelea wakati umebaki muda mchache CCM ipitishe jina la mgombea urais apeperushe Bendera ya Chama hicho.

Hivi  inawaingia akili kabisa makada Sita watoke kifungoni halafu CCM ipitishe Moja ya jina makada hao akagombee urais kupitia CCM

Pia Nape ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kaisha tamka  tena adharani Kuwa CCM haitaki   mgombea urais watakayeanza  kwa kumsugua kwa dodoki (yaani anayenuka tuhuma chafu) na Watanzainia wamechoshwa na ufisadi na utovu wa Maadili ya viongozi wa umma na miongoni mwa makada hao wameisha chafuka tuhuma za ufisadi.

Na wengine kuhukumiwa kwa makosa kuvunja Maadili na Kanuni za CCM na Tayari na Kada mwingine Ngeleja licha ya kuendelea kutumia Kifungo hicho pia mashitakiwa tena Katika Sekretatieti na Maadili ya Utumishi wa umma kwa makosa ya kunufaika na mgao wa Fedha za Escrow bila kufuata Taratibu za Sheria ya Maadili ya viongozi wa umma na kusimamishwa ujumbe wa NEC na kwa maana hiyo hata jina lake ikitokea akapitishwa awe mgombea urais ni wazi hawezi kuudhurulia vikao vya NEC na kujipigia kura kwasababu amesimamishwa kuudhuria vikao Vya NEC.

Binfasi baada ya kutafakari matamko hayo na kutazama picha inavyochezwa hivi sasa na uongozi wa juu wa CCM na baadhi ya wananchi  na baadhi ya wafuasi wa kambi za wafuasi hao wa makada Sita ,kwa moyo safi nawashauri Nyie makada Sita ambao Adhabu yenu HIvi sasa haijulikani tena itamalizika lini,msiende lee kupoteza Fedha na muda wenu bure kwaajili yakufanya Maandalizi ya Kugombea urais .

Kwani kwa ushahidi huo wa mazingira kupitia matamko hayo minaona   Hamtoshi Kuwa wagombea urais kupitia CCM ,mjidiskolifai wenyewe sasa ili muweze kuinusuru CCM  na nchi  ili CCM Iweze kufanya maamuzi  mazuri ya kupata mgombea urais anayefaa.

Wakati umefika sasa wa Nyie makada Sita binafsi mjiulize Kifungo gani hicho kisichokuwa na mwisho?. Wafuasi wa kambi za makada Hao Sita nawashauri Ameni  kambi mapema .

Mfano mzuri ni wa msomi wa sheria William Ngeleja ambaye naye ni miongoni mwa makada Hao Sita wanaondelea kutumikia Adhabu na Februali 28 mwaka huu,Kamati Kuu imemsimamisha ujumbe wa NEC na wakati huo ni mshitakiwa  Katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kujibu makosa ya uvunjwaji wa Maadili ya uongozi wa umma na Machi 3 Mwaka huu, Ngeleja alipanda Katika kizimba cha Sekretarieti hiyo kutoa utetezi wake.

Hakuna ubishi Kuwa Tayari Ngeleja ana rekodi  Kutiwa hatiani kwa makosa ya uvunjaji wa Maadili na Kanuni za CCM na bado yeye na wenzake wakina Membe ,Lowassa, Sumaye na wengine wanaendelea na Adhabu hiyo ambayo ni wazi sasa haijulikani tena itaisha lini na tena ameshitakiwa Kwenye Sekretarieti ya Maadili ya Umma na wakati huo huo Kamati Kuu imemsimamisha kuudhuria vikao Vya NEC.

Kwa watu wenye akili timamu tumebaini Kuwa Ngeleja ' Kwishineiiii ' ,Kwani hali hiyo CCM haiwezi kupitisha jina lake Kuwa mgombea urais kwasababu amepatikana  na hatia  na bado mashitakiwa kwa Kesi mpya ya utovu wa Maadili Katika Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa umma ya utovu Maadili ya umma ambayo bado haijatolewa uamuzi.

Na kwa Hali  ilivyo sasa na CCM ilivyo na sifa  Mbaya Machoni kwa baadhi a wanachi ,CCM itafanya kila linalowezekana limsimamishe mgombea urais wake ambaye aandamwi na rekodi chafu za Kifungo cha utovu wa Maadili au tuhuma za Rushwa ,Makundi yanayofanya siasa chafu dhidi ya wenzake na anayetaka kukigawa Chama.

Na Nyie wafuasi wa makada Sita nawasii muheshimu Kanuni   za CCM ,ili mtoe fursa kwa CCM ipitishe mgombea urais   safi asiye na kashfa wala Kutiwa hatiani,mfungwa,mtuhumiwa na mumuunge  mkono ili muonyeshe  ukomavu wa siasa kwa chama chenu na mumuenzi Baba wa Taifa, Marehemu Julias Nyerere ambaye alisema kiongozi anaweza kutoka chama chochote kile ila kiongozi bora ni lazima atoke CCM.

Niitimishe kwa Kusema Kuwa CCM bado inawagombea wazuri tu wenye sifa za Kuwa wagombea urais na wala hawajaanza kujipitisha pitisha mitaani Kama wanawake Malaya wanatafuta mabwana.

Wawafuate  wawashawishi  wagombee urais Kwani  Katika hawa makada Sita ambao Tayari wameishanasa Kwenye mtego wa Nyavu za Kanuni za Maadili ya CCM toleo la Mwaka 2010 na kuendelea na kuandamwa na tuhuma mbalimbali ufisadi,utovu wa maadili na hira za kila aina hawafahi Majina Yao kupitishwa na CCM Kuwa wagombea urais wa CCM . Na huo ndiyo ukweli mchungu ambao hampendi kuusikia masikioni mwenu.

Kwasababu baadhi ya makada hao Sita miongoni mwao wamekuwa ni mahiri na mabingwa wa kusukia wenzao mizengwe, majungu, fitna na kuwazushia  fitna ili wachafuke na wao wao wanekane ni watu safi Kumbe nao ni washenzi tu wa tabia  ambao Kutwa wanatumia wapambe wao kulandalanda Kwenye vyombo Vya Habari na Kwenye mitandao ya kijamii kuchafua wenzao ili Hali nao ni wachache na wanatumikia Kifungo Katika 'Gereza la CCM'.

Naunga mkono hoja ya Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Dk.Hans  Kitine Katika mahojiano aliyofanya na Gazeti la Mtanzania Jumapili mapema Mwaka huu, pamoja na mambo mengine alisema kwa mtazamo wake yeye anaona makada wote wote wanaotajwa tajwa Kugombea urais na ambao wanaotumikia Adhabu ya Miezi 12 hawana sifa za Kuwa Marais wa  nchi hii kwasababu ni wahuni wahuni tu.

Kweli ni wahuni na hawafahi kwasababu Kama wameshindwa kuheshimu Kanuni za Maadili za Chama Chao na wakazivunja na wanaendelea kuzivunja,Majina Yao ya kupitishwa mmoja wao Akawa mgombea urais Si ndiyo watakuwa vinara wa kuvunja Sheria za nchi kwa makusudi kwaajili ya kutimiza 'mission zao  'chafu au kuumiza watu kwa wakati huo?

Nafahamu makala hii haitawapendeza makada hao Sita na wapambe wao ambao baadhi ya wapambe wa kambi hizo wamewageuza migodi Makada hao sita ya kujipatia fedha kwa kuwapa taarifa za uongo kuwa watapitishwa kuwa wagombea urais kumbe uongo mkubwa wanawalia fedha zao na wafuasi Wengine ni wanafki mchana wao wanajifanya wapo Kwenye kundi la Kada (X)  usiku anapeleka taarifa za kambi ya kada huyo kwa kambi ya kada (x).

Na yaona haya na wahusika wakuu wa tabia hii chafu ni makada wengi wenye jinsia ya kiume tena ni watu wazima wenye wake na watoto majumbani mwao ambao pia wamekuwa wakijinasibu  mitaani na Kwenye vilabu Vya Pombe kwamba mgombea urais fulani anayemuunga mkono   ametumwa na Rais Jakaya Kikwete kuchukua fomu.

Upuuzi mtupu Kwani hawaonyeshi ushahidi unaonyesha lini,wapi na saa ngapi Rais Kikwete alikaa na wagombea Hao akiwaambia wagombea urais na atakubali kuwaunga mkono.

Na baadhi ya wafuasi wa kambi hizo hao wamekuwa Binafsi nawafanisha makada hao wa kiume sasa na wamawake malaya wanaouza mihili yao ili wapate fedha.

Mwisho Nimalizie kwa Kusema Kuwa kwa mazingira ya kisiasa tuliyonayo hivi sasa na jinsi ya Kamati ya CCM inavyoendelea kuwashughulikia bila huruma makada wake.

Nasema hivi  makada Sita wa CCM mliopo kifungoni Katika Gereza la CCM hammo Kwenye Urais , mjiondoe mapema na msitishe kumwaga Fedha kwa wapambe wenu mnaofikiri wanawafanyia kampeni Kumbe wanawalia Fedha Zenu na Wengi wanawaandikieni ripoti na kuzidi kuwakusanyia ushahidi Kuwa licha bado mpo Kwenye Kifungo na uchunguzi lakini bado mnaendelea kuvunja Kanuni za Chama kutoa Rushwa na kufanya kampeni za urais Kabla ya wakati.

Ni Ngumu sana  majina yenu  kupitishwa  Mkawe wagombea    urais Kwani mmejimaliza wenyewe kwa matendo yenu ambayo yamedhibitisha hamkutana kutii Sheria na Kanuni za Chama chenu cha CCM bila shuruti.Watanzania na wana CCM kwa ujumla bado hawajafikia hatua ya kuitaji rais mwenye 'conviction' yaani aliyefungwa baadaya kupatika na hatia ya makosa ya kuvunja maadili. Makada Sita CCM hammo Kwenye urais!.

Mungu Ibariki Tanzania
0716 774494
Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
Machi 5 Mwaka 2015.No comments:

Powered by Blogger.