Header Ads

HEKO CLOUDS MEDIA GROUP KUANDAA MPAMBANO WA BENDI YA FM ACADEMIA .V.TWANGA PEPETA LEO






HEKO CLOUDS MEDIA GROUP KUANDA MPAMBANO WA BENDI YA FM ACADEMIA .v TWANGA PEPETA LEO

Na Happiness Katabazi
KWANZA kabisa napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa kampuni ya Clouds Media Group chini ya wakurugenzi wake Joseph Kusaga na Ruge Mtahaba kwa kuandaa pambano hilo la aina yake.

Pambano hilo litausisha bendi mbili maarufu nchini, Fm Academia ' Wazee wa Pamba'   dhidi ya African Stars ' Twanga Pepeta' litakalofanyika katika ukumbi Escape One ,Dar es Salaam kuanzia saa mbili usiku.

Nimelazimika kuipongeza Clouds Media Group leo kwasababu hatimaye kampuni hiyo sasa imekumbuka ilikotoka na uenda imeona nayo ni miongoni mwa watuhumiwa wa kuuzika muziki wa dansi nchini.

Kwa wapenzi wa muziki wa dansi nchini ambao tulipata bahati ya kuona na kushiriki maonyesho ya bendi hizo mbili tangu bendi hizo zinaanzishwa ,mtakubaliana na mimi kuwa redio Clouds Fm inayomilikiwa na kampuni hiyo ilishiriki kikamilifu kutoa fursa ya kukuza muziki wa bendi ya Dansi hasa wa bendi ya Twanga Pepeta chini ya Mkurugenzi Asha Baraka na Fm Academia.

Lakini kwa zaidi ya kama miaka sasa siyo siri redio maarufu nchini na redio nyingine ni kama ziliupa kisogo mziki huo na kuamua kuubeba muziki wa kizazi kipya na huo ndiyo ukweli.

Wanamuziki wa bendi za muziki wa dansi walilalamika sana na pia sisi wapenzi wa muziki wa dansi na hatimaye leo kilio chetu kimesika na kampuni ya Clouds Media Group na kuamua kuaandaa mpambano huo mkali wa aina yake ambao utakutanisha wapenzi wa muziki wa dansi wa miaka ya nyuma na wale wapenzk wapya wa bendi hiyo.

Huu ni mwanzo mzuri naomba Ruge na Timu yake isiishie hapo na Redio Clouds ikumbuke ilikotoka kwani muziki wa dansi wa waliokuwa wakiupiga katika redio yao miaka ya nyuma kwa asilimia kubwa ulichangia kuipatia umaarufu redio hiyo na kusababisha redio kuwa na wasikilizaji wengi.

 Hongera sana Clouds Media Group kwakuandaa pambano hili la leo ambalo hakika litaleta burudani ya aina yake na kuwaondoa malalamiko kwa wanamuziki wa dansi ambao wamekuwa wakilalamikia redio na Televisheni zimeporomosha muziki wa dansi kwasababu kutwa nzima vituo hivyo vyautangazaji vinapiga muziki wa kizazi kipya na muziki wa dansi haupigwi kama zamani haki iliyosababisha baadhi ya wapenzi wa muziki wa dansi kusema kuwa miziki hiyo ya bongo flavour kupigwa redioni mara kwa mara nj sawa na kupiga kelele tu redioni.

Nawatakia kila la kheri bendi ya Fm Academia, Twanga Pepeta,pambano limalizike salama na lifane.

Clouds Fm pambano hili liwe mwanzo wa kampuni yenu kuzinduka usingizini na kuanza tena kuuinua muziki wa dansi nchini kama ilivyokuwa ikifanya katika kipindi cha mwaka 2003 kuendelea na ikumbukwe wapenzi wengi wa muziki wa dansi ni watu wenye heshima zao na vipato vya kueleweka.

Binafsi ni mpenzi wa muziki wa dansi naomba Clouds Media Group ione haja sasa ya kuanza kuinua mziki huo pia.

Chanzo: Facebook:  Happy Katabazi
Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Machi 28 mwaka 2015.

No comments:

Powered by Blogger.