Header Ads

YALIYOMKUTA KIDEKU NA UNGO PIA YATAMKUTA
YALIYOMKUTA KIDEKU NA UNGO PIA YATAMKUTA.

Na Happiness Katabazi

YAANI NAMAANISHA YALIYOWAHIKUWAKUTA WANASIASA WENZAKE ,WATENDAJI WAANDAMIZI  WA SERIKALI  PRO.SOSPETER MUHONGO,PRO.ANNA TIBAIJUKA,ANDREW CHENGE, ALIYEKUWA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI ,JAJI FREDRICK WEREMA ,ELICHIM MASWI NA WENGINE WENGI PIA LEO NAE BINGWA WA KUPENDAGA SANA KUSHINIKIZA WANASIASA WENZAKE WATIMULIWE KAZI NA WAJIUZULU NYADHIFA ZAO YAANI ZITTO KABWE NAYE YAMEMKUTA AMETANGAZA RASMI KUJIUZULU UBUNGE NDANI YA BUNGE USIKU HUU.

LICHA ZITTO YEYE KAPATA MAPIGO MFULULIZO NA KUSHINDWA KESI ,KUFUKUZWA UANACHAMA,KUJIUZULU UBUNGE NA KUPOTEZA NAFASI YA UENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE YA PAC.MUHONGO ,TIBAIJUKA YEYE KAPOTEZA UWAZIRI,UJUMBE WA KAMATI KUU (CCM)WA TIBAIJUKA,NA CHENGE NA NGELEJA WAMEPOTEZA NAFASI YA UJUMBE WA NEC.NA ZILE FEDHA ZA ESCROW TIBAIJUKA,CHENGE,NGELEJA WANAZO HAWAJANYANGANYWA NA BADO WANAENDELEA KUWA WABUNGE.

ILA ZITTO VYOTE KAPOTEZA KWA KIPINDI KIFUPI SANA.POLE ZIT TO HIYO NI AJALI YA KISIASA NA PIA MUNGU ANA SABABU YA KURUHUSU MACHUNGU HAYO YAKUFIKE.ALIKUWA NA UWEZO WA KUZUIA YAKUFIKE.

.NAKUSHAURI TULIA ,ACHA KUONGEA ONGEA SANA NA MEDIA UTAFAKARI.MUNGU ALIKUWA NA UWEZO WA KUZUIA HAYO MAPITO HAYO USIYAPOTE LAKINI YEYE KARUHUSU YAKUFIKE.

UENDA ANA SABABU ZAKE AMBAZO HUZIJUI.PIGA GOTI NAMSHUKURU MUNGU KWA YOTE HAYO.NAAMINI HUKUPENDA UACHIE UBUNGE AU UFUKUZWE CHADEMA ILA UNAJIKAZA KIUME.

POLE SANA ILA KAA PEKE YAKO UMUOMBE MUNGU AKUONYESHE ULIKOSEA WAPI?JE HAYO YALIYOKUKUTA NI KISASI CHA MUNGU KWA NIABA YA BAADHI YA WANASIASA WENZAKO NA WATENDAJI WA SERIKALI KUWA WAKATI ULIPOKUEA MWENYEKITI WA PAC,ULIWAUMIZA BILA HATIA?

JE WAKATI ULIPOKUWA UNATENDA KAZI ZAKO KAMA MBUNGE NA MWENYETI WA KAMATI YA PAC ULIKUWA UKITENDA KAZI ZAKO KWA HAKI? JE NA WEWE NI MWANASIASA MWADILIFU SANA KULIKO WANASIASA WENZAKO?

USILIPE KISASI.KUWA MAKINI SANA NA BAADHI YA WANASIASA WENZAKO AMBAO LEO HII WANAJIFANYA WANAKUONEA HURUMA NA KUJIFANYA WANATUMIA UAMUZI WA CHADEMA WA KUKUTIMUA UANACHAMA KAMA GIA  KUJIPATIA UMAARUFU,WANAFKI NI WENGI.

WENGINE WAMEFURAHI SANA MABALAA YALIYOKUPATA KWA MFULULIZO NA KATIKA KIPINDJ KIFUPI TU KWASABABU HIVI SASA MMEFANANA MAANA ZAMANI ETI ULIJIFANYA MALAIKA HUNA DHAMBI WALA TUHUMA.SASA LEO NA WEWE YAMEKUKUTA .

NA WENGINE WAMEFURAHI WAMESEMA KUMBE BAADHI YA WAFUASI WA CHADEMA NAO NI WASALITI KWA VYAMA VYAO NA WATUHUMA ZA KUKANDAMIZA DEMOKRASIA NA KWAMBA KUMBE HATA NA WEWE ZITTO KABWE ULIVUNJA SHERIA NA KANUNI ZA CHADEMA KAMA KWA UAMUZI WAKO WA KWENDA MAHAKAMANI WAKATI WEWE MARA KWA MARA ULIKUWA UKIAMASISHA WATU WAFUATD SHERIA NA WANAOZIVUNJA WACHUKULIWE HATUA,NA WEWE UMEVUNJA SHERIA ZA CHADEMA, CHADEMA WAMEKUCHUKULIA HATUA ZA KISHERIA KWA KUKUTIMUA UANACHAMA NA HUO NDIYO UTAWALA WA SHERIA.

SIJAKUKATAZA USIAMUE ACT ,ILS UKAE UKITAMBUA UKIAMIA ACT KATIKA KIPINDI HIKI KIFUPI KILICHO SALIA TAYARI YALE MADAI YA CHADEMA KUWA ULIKUWA UKIINDA CHAMA CHAKO WAKATI BADO NI MWANACHAMA NA KIONGOZI WA CHADEMA YATAKUWA YAMETHIBITISHWA BILA KUACHA SHAKA.

ZITTO ELEWA KITU KIMOJA, WEWE NA WAFUASI WAKO NA HAKO WAZANDIKI WANAOKULAMBA KISOGO KUWA MENGINE YOTE MSEMAYO NI KAMA MANENO YA MFA MAJI. SABABU KUU INAYOONEKANA NA KUTHIBITIKA KUWA CHADEMA WALIKUFUKUZA UANACHAMA KWA KUTUMIA SHERIA NA SI VINGINEVYO.

SHERIA ILE ILE AMBAYO NAWEWE WAKATI INATUNGWA ULIKUWA KIONGOZI WA CHAMA HICHO NA ULIBARIKI ITUNGWE NDIYO IMEKUSHUGHULIKIA MAANA SHERIA HIYO INASEMA MWANACHAMA YOYOTE ANAYEEBDA KUSHITAKI MAHAKAMANI CHADEMA ATAKUWA AMEJIFUKUZA UANACHAMA NA WEWE NI KWELI ULIISHITAKI MAHAKAMA KUU CHADEMA NA KESI YAKO IKATUPWA.

NA WEWE MWENYEWE JANA ULITUMIA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977, YAANI SHERIA IBARA YA 77(1)(f) INAYOSOMEKA HIVI ; " MBUNGE ATAKOMA KUWA MBUNGE NA ATAACHIA KITI CHAKE KATIKA BUNGE IWAPO MBUNGE ATAACHA KUWA MWANACHAMA WA CHAMA ALICHOKUWEMO WAKATI ALIPOCHAGULIWA AU ALIPOTEULIWA KUWA MBUNGE".

TAMBUA  KIPATO,AJIRA UTAPATA SIKU ZOTE KUPITIA WEWE KUPATA MADARAKA YA KIBUNGE KAMA UNAVYOFIKIRI,AJIRA NI KOKOTE.

JANA WAKATI UNAAGA BUNGENI ULISEMA MUNGU AKIPENDA UTAWEZA KUWA KATIKA BUNGE JIPYA LA NOVEMBA NA MAPEMA WIKI HII UMENUKULIWA UKISEMA KUWA IPO SIKU UTAKUJA KUWA KIONGOZI MKUBWA KATIKA TAIFA HILI NA UKASEMA PIA WANAOKUTABIRIA KIFO CHA KISIASA WASUBIRI KIDOGO.

HIZO NI NDOTO ZAKO SIKUINGILI.ILA NAKUSHAURI ZITTO NENDA KAFANYEKAZI ZA KITAALUMA KWA MUDA KADHAA ,MIAKA KUMI NI MINGI  KISHA MUNGU AKIKUPA UHAI UREJEE TENA ULINGONI BADO KIJANA MDOGO SANA.

HAKUNA UBISHI DHANA  ZAKO ZA KIPINDI KILE ULIPOPA UMAARUFU SANA ZIMEKWISHA, KUBALI HILO ZITTO.SASA NI WAKATI WA WANASIASA VIJANA KAMA MWIGULU NCHEMBA,JANUARI MAKAMBA, PAUL MAKONDA KUNG'AA KATIKA MEDANI ZA SIASA, HUO NDIO UKWELI MCHUNGU.

ZITTO ELIMU UNAYO YA KUTOSHA TU, SIYO LAZIMA ULITUMIKIE TAIFA KUPITIA UBUNGE MAANA KUPITIA MAHOJIANO YAKO MBALIMBALI LAZIMA UNAONGELEA KUWA UNAPENDA SANA MADARAKA YA KISIASA.

MININGEFARIJIKA SIKU MOJA NIKUSIKIE UNATAMANI KUWA KIONGOZI WA DINI YAKO HATA NGAZI YA TAWI.

NARUDIA TENA KUKUSHAURI KAKA YANGU ZITTO KABWE KUWA KAA CHINI ZUNGUMZA NA MUNGU WAKO MUULIZE NI KWANINI ULIPATA MADARAKA MENGI UKIWA NA UMRI MDOGO GHAFLA MADARAKA YOTE HAYO YAMETOWEKA KWA WAKATI MMOJA? ATAKUPA JIBU.

NA UZINGATIE KWA MAKINI MAANA YA MSEMO HUU ' KILA LIKUEPUKALO LINA KHERI KWAKO'. KIJA ZITTO ACHA KUPIGA MAYOWE KWANI SIKU ZOTE NGOMA YA KITOTO HAIKESHI.

JIFUNZE KUTOKA KWA WAZIRI NA MBUNGE WA MUDA MREFU JOHN MALECELA,JOSEPH MUNGAI WALIOTOKA KWA AIBU YA KUSHINDWA KATIKA UCHAGUZI WA UBUNGE MWAKA 2010 NA MUNGAI AKAISHIA KUFUNGULIWA KESI YA RUSHWA IKAMSUMBUA LAKINI BAADAE MAHAKAMA IKAMFUTIA KESI.

NAAMINI SASA UKIREJEA MAKALA ZANGU TATU ZA MIAKA YA NYUMA ZILIZOKUWA NA KICHWA CHA HABARI, (Zitto Kabwe mbona umsahaulifu), (Zitto Kabwe unajiandalia anguko)  ,(Kashfa ya Escrwo isitugawe), (Zitto Kabwe ndio ujue muosha uwoshwa tena wakati wa kuoshwa ulipuliwa). Na ile makala ya Mwandishi wa habari mwandamizi,Absalom Kibanda iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho (Naliona anguko la Zitto).

 NILIYOKUWA NAKUTABIRIA KATIKA MAKALA HIZO YAMETIMIA.

TAMKO LA ZITTO HILO HAPO CHINI AMELITOA USIKU HUU BUNGENI.By Happiness Katabazi,Machi 20 mwaka 2015
Blogg:www.katabazihappy.blogspot.com
Simu.0716 774494.

No comments:

Powered by Blogger.