Header Ads

VIONGOZI HAWA WA DINI WAMEMGEUZA MUNGU NI STAGE SHOW?


VIONGOZI HAWA WA DINI WAMEMGEUZA MUNGU NI STAGE SHOW?

Na Happiness Katabazi
NIMETAZAMA HAO WALIOJITAMBULISHA VIONGOZI WA DINI KWENYE HII VIDEO NIMECHEKA SANA NA NIMEOGOPA NA NIMEITIMISHA KWA KUONA HAWA NA WALE MASHEIKH  UWENDA WAMEMGEUZA MUNGU NI STAGE SHOW.

JAMANI TUMUOGOPE MUNGU TUSILITUMIE JINA LA MUNGU VIBAYA ATAWAANGAMIZA.MUNGU GANI HUYU KAWATOKEA WATUMISHI WOTE  HAWA KWA PAMOJA AKAWATUMA WAENDE  KUMSHAWISHI MZEE EDWARD LOWASSA AGOMBEE URAIS?NI MUNGU HUYU HUYU TUNAEMUOMBA SOTE?

 TARATIBU JAMANI,MMEKUWA NA HARAKA MNO.IKITOKEA LOWASSA ASIFANIKIWE KUWA RAIS ,WAUMINI WENU TUTAACHA KUWAAMINI.

HALAFU NYIE MMEJITAMBULISHA WAZI WAZI NI VIONGOZI WA  DINI MLIOONA LOWASSA ANAFAA KUWA RAIS ,MNA HAKI YA KUFANYA HIVYO KIKATIBA LAKINI JE HAMUONI SIYO BUSARA KWA NYIE KUJIYOKEZA ADHARANI ADHARANI  KUSEMA MNAMUUNGA MGOMBEA MMOJA  (LOWASSA).

JE IKIJA KUTOKEA CHAMA CHAKE CHA CCM KISIPITISHE JINA LA LAKE KUWA MGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA HICHO, JE NYIE WATUMISHI WA MUNGU MTAKIUNGA MKONO CHAMA HICHO NA KUKIPENDA?

KUMBUKENI CCM, SERIKALI HAIWAPATI VIONGOZI WAKE KWA KIGEZO CHA UDINI. NAWASHAURI NENDENI MKAREJEE IBARA YA  19 YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977, INATOA UHURU KWA MTU BINAFSI KUAMINI DINI AITAKAYO .

JE IKITOKEA MUUUMINI MWINGINE WA DINI MNAYOTOKEA NYIE VIONGOZI WA DINI YA KIKRISTO NA WAISLAMU , MUUMINI MWINGINE MBALI NA LOWASSA NAYE ANATAKA KUGOMBEA  URAIS JE MTAMUUNGA MKONO NA KUMSHAWISHI AGOMBEE URAIS KAMA MLIVYOFUNGA SAFARI KWENDA NYUMBANI KUMSHAWISHI LOWASSA?

KWA MUJIBU WA VIDEO HII KIONGOZI MMOJA ANAONEKANA AKISEMA WANAMTAKA KIONGOZI ANAYETOKANA NA MAOMBI.

USHENZI WOTE TUFANYE JAMANI LAKINI TUSIJARIBU KUMGEUZA MUNGU STAGE SHOW KWANI SIKU MUNGU AKIAMUA KUPANDA  JUKWAANI KUTOA SHOW YAKE YA UKWELI KWA KUTUMIA NENO LA MUNGU KWELI NYIE VIONGOZI WA DINI MTAANGAMIA.

JE IKITOKEA CCM IKAMPITISHA MGOMBEA AMBAYE NI MUUMINI WA DINI YA KIISLAMU AU MKRISTO ASIAMINI KATIKA MAOMBI INA MAANA MTAMKATAA KWA SABABU HATOKANI NA MAOMBI KAMA MLIVYODAI?

SISI WAKRISTO NA WAISLAMU TUNAJUA NI MUNGU PEKE YAKE NDIYO ANAYEOMBWA, NA VIONGOZI WA DINI WANAOJIHESHIMU NA WASIYO MDHIHAKI MUNGU WANAFUNGA NA KUSALI NA KUWATAKA WAUMINI WAO WAMUOMBE MUNGU AWAPATIE RAIS MZURI ATAYEIONGOZA VYEMA NCHI.


ZIARA YENU NYIE MASHEIKH,WATUMISHI WA DINI YA KIKRISTO KWA LOWASSA IMETILIWA MASHAKA NAWASHAURI MUULIZENI MUNGU KWANINI WATU WAMEITILIA MASHAKA SANA?

UKWELI WA AMA MMETENGENEZWA,MMETUMWA KUMFANYIA USANII MZEE LOWASSA AMBAE YEYE NA MAKADA WENZAKE WA CCM KWA KUANZA KAMPENI MAPEMA ZA URAIS  NA HADI SASA WAPO CHINI YA UNGALIZI ,NDIO MZIDI KUTOA FURSA KWA  VYOMBO VYA UCHUNGUZI VYA CCM KUMKUSANYIA USHAHIDI KUWA WAKATI YUPO CHINI YAUANGALIZI BADO ANAENDELEZA MATENDO YANAYOKARIBIA KUFANANA NA YALE YALIYOSABABISHA KUTIWA KIFUNGONI NA CCM WANAUJUA WAO.

KABLA YA LOWASSA KUTIWA KIFUNGONI NA CCM ALIKUWA AKISHIRIKI KWENYE HARAMBEE MBALIMBALI HASA MAKANISA KITENDO AMBACHO KILISABABISHA YEYE AKUTWE NA HATIA YA KUANZA KAMPENI MAPEMA KABLA YA RATIBA YA CCM KUANZA.

NA CCM IKAPIGA MARUFUKU MAKADA WAKE WOTE KUSHIRIKI HARAMBEE BILA KUPATA KIBARI KUTOKA MAKAO MAKUU YA CCM. TUMUULIZE MZEE LOWASSA HAYO MAKUNDI YANAYOKUJA KUMSHAWISHI NYUMBANI KWA KWA KASI YA KUTISHA NA MAPEMA KIASI HIKI,ALIKUMBUKA KUPATA KIBARI KUTOKA CCM MAKAO MAKUU?

SA WATU WANAULIZANA CHINI CHINI UENDA MZEE LOWASSA KAAMUA KUJA KIVINGINE KABISA YAANI KAJA NA MBINU MPYA YA MASHABIKI WAKE KUMFUATA NYUMBANI KWAKE NA SIYO YEYE KUWAFUATA KATIKA MAENEO YAO KAMA MAKANISANI, UWANJANI,UKUMBINI?

 USHAURI WANGU KWA MZEE LOWASSA KUWA MAKINI NA MAKUNDI HAYO HASA YA HAO VIONGOZI WA DINI  KWANI AKUMBUKE MANTIKI YA MSEMO HUU USEMAO KWENYE MSAFARA  MAMBA KENGE  WAMO.

CHANZO: Facebook: Happy Katabazi
Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494.
Machi 24 mwaka 2015.

No comments:

Powered by Blogger.