Header Ads

FM ACADEMIA 'NGWASUMA' BAND LEO NI USHINDI TU
FM ACADEMIA 'NGWASUMA' BAND LEO NI USHINDI TU

NA HAPPINESS KATABAZI

MI HAPPINESS KATABAZI WALA SIFICHI  NINA MAPENZI YA DHATI NA BENDI YA FM ACADEMIA 'NGWASUMA'TANGU INAANZISHWA HADI SASA.NIMEKUWA KARIBU SANA NA WANAMUZIKI HAWA TANGU BENDI INAANZISHWA NA KIPINDI KILE BAADHI YAO WAKAWA WANAFUNGULIWA KESI ZA KUISHI NA KUFANYAKAZI HAPA NCHINI BILA KIBARI.

LEO BENDI YANGU YA FM ACADEMIA INAPANDA JUKWAANI KATIKA UKUMBI WA ESCAPE ONE,DAR ES SALAAM KUCHUANA NA BENDI YA TWANGA PEPETA.NAZITAKIA BENDI ZOTE AMANI NA UTULIVU,ZIENDE ZIKATOE BURUDANI AMBAYO TUMEIKOSA KWA MUDA MREFU SISI WAPENZI WA MUZIKI WA DANSI.NAISHUKURU SANA MUANDAAJI WA MCHUANO HUO AMBAYE NI KAMPUNI YA CLOUDS MEDIA GROUP.

SINA SHAKA KABISA KUWA BENDI YANGU YA FM ACADEMIA NDIYO ITAIBUKA MSHINDI KWASABABU INA SAFU NZURI YA WAIMBAJI ,WATUNZI,NA WACHEZA SHOW WAZURI NA WAPIGA VYOMBO WAZURI.

KILA MWANAMUZIKI WA BENDI HII ANANIKOSHA KATIKA ENEO LAKE NAWAPENDA SANA.
ILA MWENZENU SAUTI YA MWANAMUZIKI KAKA YANGU KINGOMBE BLAISE 'KING BLAISE' NAIPENDA SANA.

UKISIKILIZA ALBAMU MPYA HA CHUKI YA NINI , WIMBO YA FAKATI ,MAPENZI YA KISASA NA DAI CHAKO ULAUMIWE UTAONA NA KUISIKIA SAUTI MWANANA YA KING BLAISE,KWAKWELI INANIPA KIWEWE.

PIA NAPENDA JINSI PABLO MASAI ALIVYONA PUMZI YA KUCHEZA NA KUIMBA SAUTI YA JUU. MULEMULE NAE PIA ANASAUTI NZITO NA ANAYEONEKANA NI MWANAMUZIKI WA KURUSHA VIJEMBE VYENYE KUFUNDISHA KATIKA JAMII.MULE MULE FBI NI MTUNZI WA WIMBO WA MAPENZI YA KISASA.

PATCHO MWAMBA NAE NI MWANAMUZIKI MWENYE SAUTI YA AINA YAKE NI KAVU NA AMBAYE AKIONEKANA KWENYE VIDEO UNAWEZA KUMUONA NI MWANAUME MWENYE  MALI NA FEDHA NYINGI SANA.

WAKATI KATUMBI JESUS NAYE SAUTI YAKE NI NZITO NA YENYE KUPEMBELEZA. PRESIDENT NYOSHI ELSADAT YEYE ANA SAUTI NYEMBAMBA SANA AMBAYE NAYE ANA PUMZI YA KUIMBA NA KUCHEZA.

NAITIMISHA KWA KUSEMA WANAMUZIKI WA BENDI YANGU YA FM ACADEMIA NA WAPENDA WOTE, WANAFANYAKAZI NZURI YA KUBURUDISHA NA KUELIMISHA JAMII,NI WANAMUZIKI AMBAO LICHA NI RAIA WA NCHI YA DRC CONGO,TUMEKUWA TUKIISHI NAO VIZURI NA WATANZANIA AMBAO TUNAPENDA MUZUKI WA DANSI HASA WA KUTOKA CONGO,TUMEIGA BAADHI YA TABIA ZAO IKIWEMO KUPENDA KUVAA VIZURI,KUPAKA MIKOROGO,MITINDO YA NYWELE, KUWA WASAFI MUDA WOTE KUZUNGUMZA LUGHA YA KISWAHILI ILIYOCHANGANYIKA NA MANENO YA LUGHA YA KIKONGO MAN, ILA BAADHI YA WANAUME WA TANZANIA WAMEIGA TABIA YA KUPENDA KULELEWA NA WANAWAKE WENYE FEDHA 'MALIO', TABIA INADAIWA IMESHAMILI HUKO CONGO DRC  AMBAKO WANAUME WA KIKONGO UPENDA KULELEWA NA WANAWAKE WENYE FEDHA.

NIMETOKA MBALI NA BENDI HII NIMEANDIKA HABARI NYINGI ZA BENDI HII HADI IKAFIKA MAHALI ALIYEWAHI KUWA MWANAMUZIKI WA BENDI HII ROGER MUZUNGU KUNITUNGIA WIMBO WA HESHIMA KWA WANAWAKE .NA MWANAMUZIKI WA BENDI HII AITWAYE MULE MULE FBI KATIKA WIMBO WAKE WA MAPENZI YA KISASA KUNIRUSHA KATIKA WIMBO HUO.

NAITAKIA USHINDI MNONO LEO BENDI YA FM ACADEMIA DHIDI YA TWANGA PEPETA KATIKA UKUMBI WA ESCAPE ONE,KIINGILIO SH.20,000 KWA SH,15,000.

CHANZO: FACEBOOK: Happy Katabazi
BLOGG: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Machi 28 mwaka 2015..

No comments:

Powered by Blogger.