ZITTO KABWE NDIO UJE MUOSHA HUOSHWA TENA WAKATI WA KUOSHWA HULIPULIWA
ZITTO KABWE NDIO UJUE MUOSHA UWOSHWA TENA WAKATI WA KUOSHWA ULIPULIWA
Na Happiness Katabazi
MACHI 10 Mwaka huu, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda a Dar es Salaam, Mziray alitoa uamuzi wa kumfukuza mahakamani kwa gharama ombi la Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe lililokuwa Linaomba Mahakama hiyo itoe amri ya Kuzuia CHADEMA isiketi vikao Vyovyote kumjadili wala Kumvua uanachama.
Jaji Richard Mziray Katika uamuzi wake Katika Kesi hiyo ambayo mlalamikaji ni Zitto Kabwe dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya Chadema na Katibu Mkuu wa Chadema ambapo Madai ya Msingi ya Zitto alikuwa anaiomba Mahakama hiyo itoe amri ya Kuzuia Chadema isifanye vikao Vya kumjadili na kutoa maamuzi uamuzi wowote dhidi yake.
Jaji Mziray alisema Kabla ya Kesi hiyo ya Msingi kuanza kusikilizwa wadaiwa hao waliwasilisha jumla ya mapingamizi ya awali matano.
Jaji Huyo alisema mahakama yake imeamua kutolea uamuzi mapingamizi mawili tu Kati ya matano na kwa Sababu hiyo Mahakama yake imekubaliana na mapingamizi mawili ya Mawakili wa wadaiwa na ndiyo itayatolea uamuzi na mapingamizi yaliyosalia haitaitolea uamuzi.
Pingamizi la kwanza lilowasilishwa na Wakili wa wadaiwa Peter Kibatara na John Malia ,waliomba Mahakama hiyo iifute Kesi ya Zitto .
Pingamizi la pili kesi ya Zitto ilifunguliwa Katika Mahakama hiyo kimakosa kwasababu Kesi yake hiyo Zitto Alipaswa aka ifungue Katika masijala ya Wilaya ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kwa maana kwamba Zitto alipaswa kufungua kesi yake msingi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi na siyo Kuifungulia Masijala Kuu ya Mahakama Kuu (main registry)
Jaji huyo alisema (Main Registry) zilianzishwa kwaajili ya kuendesha Kesi Maalum na zaidi zaidi Kesi za Kikatiba , hivyo akatupilia mbali kesi ya Zitto kwa gharama.
Jaji Mziray amesema amekubaliana na pingamizi la Chadema lililotaka mahakama hiyo iifute kesi ya Zitto kwasababu haikupaswa kufunguliwa Mahakama Kuu na kwamba ilipaswa kufunguliwa katika mahakama za ya Hakimu Mkazi(Subordinate Court).
Ikumbukwe kuwa, mwaka jana Zitto Kabwe aliweka pingamizi mahakamani kuzuia kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kumjadili mpaka pale shauri lake litakaposikilizwa na Baraza Kuu la Chama hicho.
Zitto hukujua Hilo.
Binafsi nimefurahishwa na uamuzi huo wa Mahakama Kwani uamuzi wa haki na uliokidhi matakwa ya kisheria na pia uamuzi huo pia umetoa Funzo kwa Mawakili wakurupukaji kama Wakili wa Zitto, Albert Msendo ambao wanatabia ya kukurupuka Kufungua Kesi mahakamani bila kwanza kujipa muda wa kutafari kisheria Je Kesi hiyo hiyo anayotaka kwenda Kuifungua Katika Mahakama anayokusudia Kuifungua, Je Mahakama hiyo Ina mamlaka ya kusikiliza Kesi hiyo ya mteja wake?
Pia uamuzi wa Jaji Mziray pia umetoa Funzo wasomi wa Sheria wa kufahamu madhumuni ya kuanzishwa Masijala Kuu ya Mahakama Kuu na kwamba masijala ile ni Maalum kwaajili ya kushughulika na Kesi Maalum Kama za Kikatiba na nyingine zenye upekee.
Licha Ibara ya 13(5)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, inakupa haki ya kukata rufaa Mahakama ya rufaa kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu.
Mimi binafsi siku shauri ukate rufaa kwasababu ni wazi Chadema tena wakiwemo viongozi wa juu wa Chama hicho na baadhi ya wafuasi wake hawakutaki na hawakuitaji tangu muda mrefu kwa kile wanachokidai Kuwa muda mrefu wamekubaini wewe sisi watoto wa mjini tunakuita wewe ni sawa na ' Chaja ya Kobe' kila simu unaichaji, yaani Simu ya Nokia ,Huwawei na simu nyingine zote Betri zake unaichaji yaani umekuwa ukiisaliti Chadema kwa Chama ambacho wanapingana nacho kimtazamo na kisera.
Kwanini umng'ang'anie Mpenzi asiyekupenda? Chadema hawakutaki, wamekuchoka kwa kile wanachodai wewe unawavurugia Chama chao, achana nao endelea na ule mipango yako ambayo unafikiri ni Siri wa kwenda kujiunga rasmi na Chama chako ulichokiasi kwa siri cha ACT.
Taarifa zilizopo ulikuwa umejipanga umejipanga kuama Chadema kwa mbwembwe na Lundo la wanachama na taarifa hizo zinaenezwa na baadhi ya wanachama wa ACT na watu wako wa karibu na baada ya kuama ufanye Kama anavyofanya Nape Nnauye na Abdulahaman Kinana kuzunguka nchi nzima kuinanga Chadema.
Kwa hiyo Kama taarifa za Mpango huo wa kuama Chadema ni za kweli basi huna budi kuipongeza Mahakama Kuu kwa uamuzi wake wa Jana Katika Kesi yako iliyotupwa.
Kwani uamuzi huo ni Kama umekurahisishia kukufunganisha virago Chadema au uende kukata kupinga Katika Mahakama ya Rufaa, au uende Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, ukafungue Kesi hiyo iliyotupwa Jana na Mahakama Mahakama Kuu maana Jaji Mziray Kasema Kesi yako Ulipaswa ukaifungulie Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na siyo Katika Masijala Kuu ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Kama Huyo Wakili wako Albert Msendo alivyokuingiza 'Chaka' utafikiri sio msomi wa Sheria Akaamua Kufungua Kesi yako iliyotupwa Jana Katika Mahakama iliyokuwa haina mamlaka ya kuisikiliza Kesi yako.Kihoja cha aina yake.
Uamuzi wa Mahakama Kuu wa Kuitupa Kesi ya Zitto na uamuzi wa Chadema wa kumfukuza uanachama Zitto binafsi naufananisha na ' Kumkata Ng'ombe Mapembe na mwisho wa siku Ng'ombe anayekatwa mapembe anabakia kuonekana kama Sungura.
Namuuliza Zitto hivi wale waliokuwa 'wanakubust' kwenye Sakata la Escrow Mbona wameshindwa kukusaidia 'kufanya maghumashi ' ili Kesi yako hii isitupwe na Mahakama? Na Mbona wale waliokuwa wanakubusti wameshindwa kuizuia Chadema isikuvue uanachama?
Tambua sasa Ndio wameishakubwaga sasa wamekaa pembeni wanakutazama unavyo zama Baharini kisiasa wanakucheka wala hawakuokoi,wanaenda Kutafuta mwanasiasa mwingine ambaye bado haja chafuka waanze kumtumia.
Kweli Ndege Mjanja unasa Katika Tundu bovu.Zitto alijifanya mjanja sasa Kanasa Kwenye mtego.Kiko wapi?
Maana Tayari baadhi ya wabunge na wewe Katika majadala wa Escrow mlipayuka sana bungeni na kuushambulia Mhimili wa Mahakama wazi wazi tena bila vielelezo Kuwa Mahakama inanuka na majaji wake ni wachafu.
Tufanye basi ni kweli Mahakama imeoza na Majaji wake ni wachafu ,iweje yeye na wale waliokuwa 'wakimbust Zitto' Kwenye Escrow wameshindwa kumhonga Fedha Jaji Mziray ili atoe uamuzi wa kumpendelea Zitto?
Zitto na Mbunge wa NCCR- Mageuzi , David Kafulila Ubunge wao ulikuwa umeshikiliwa na Mahakama na Kafulila ameshitakiwa na kampuni y IPTL Mahakama Kuu kwa kesi ya madai ya fidia na bado Kesi zao zinaendelea ila Kesi hiyo ya Zitto imemalizika Jana.
Lakini ndiyo walikuwa vinara wakuu paka matope Mhimili wa Mahakama na kuwaundia watu mashitaka kuhusu Escrow kuwa ni wezi ,mafisadi mashitaka ambayo mwisho wa siku Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa iliwafikisha watu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kosa la kupokea rushwa kutoka Katika akaunti ya Tegeta Escrow kinyume na Kifungu cha 15(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya Mwapka 2007.
Zitto,Kafulila ,Deo Filikunjombe kupitia vinywa vyao kila kona walikuwa wakiaminisha umma Kuwa Fedha zile ni za umma na zimeibwa na watu waliwataka Kwenye ripoti ya PAC ambayo Mwenyekiti wa Zitto Kabwe.
Wasomi wa Sheria nikiwemo Mimi niliandika makala za kupinga wazi wazi Katika Escrow Hakuna kosa la wizi kisheria baadhi ya watu wenye akili timamu walinielewa ila kwa wale Bendera Fuata upepo Hawakutaka kunielewa ila kwasasa wamenielewa.
Lakini Desemba Mwaka Jana , Rais Jakaya Kikwete Katika mkutano wake na wazee wa Dar es Salaam Katika hotuba yake alisema Fedha za Escrow Si mali ya umma na Kama siyo mali ya umma hawezi kuwashitaki kwa mashitka ya wizi wa fedha Kama tulivyokuwa tumeaminishwa Ujinga na baadhi ya wabunge na Kamati ya Zitto na Kafulila Kuwa Fedha za Escrow ni mali ya umma na zimeibwa kwa Magunia watu waliotajwa kwenye ripoti ya PCA kwakutumia Benki ya Mkombozi mali ya Kanisa Katoriki.
Watu wenye akili timamu na tunaoona mbali na kufahamu mhimili wa Mahakama ni nini na unafanyaje kazi , tulipowaona hao wabunge wa Mahakama wanapoteza muda mwingi kupayuka majukwaani badala kuongeza nguvu katika kesi zao tuliishia kujisemea moyoni msemo huu: ' Usimtukane Mamba Kabla ujavuka Mto.
Binafsi Nina Imani na Mhimili wa Mahakama hapa nchini Kama kuna watendaji wake wanafanya vitendo Vya utovu wa Maadili ,wanafanya vitendo hivyo wao Binafsi na hawajatumwa na mahakama hivyo haikuwa vyema kwa baadhi ya wabunge wetu wakati wa kujadili ripoti ya PAC kuusisha Mhimili wote wa Mahakama Kuwa unalea na kukumbatia mafisadi wa Escrow na kwamba majajaji Wawili ni mafisadi pale Mahakama Kuu ilipotoa amri ya Kuzuia suala la Escrow lisijadili we bungeni.
Ibara ya 107A(1) ya Katiba ya nchi ambayo inasema Mhimili wa Mahakama ndiyo una jukumu la kutoa maamuzi ya haki Katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa Kuwa Mahakama haifanyi Kazi zake kwa mashinikizo , siasa chafu au kutazama sura au Cheo cha Mtu Bali inafanyakazi kwa kufuata Sheria na Kanuni, tusubiri uamuzi wa Mahakama Kuu katika Kesi ya Madai ya Kashfa ya kampuni ya IPTL dhidi ya Kafulila, Kesi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali mstaafu ambaye Enzi alikuwa Mwanasheria Mkuu alishiriki kikamilifu kuandaa Mabadiliko makubwa ya Sheria za nchi hii na Kada wa CCM, Andrew Chenge ' Mtemi Chenge ambaye anakusudia Kuwasilisha ombi lake la Mahakama Kuu la kuomba Mahakama hiyo iseme Je Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Ina mamlaka ya kusikiliza shauri linalomkabili la kuvunja Maadili ya uongozi wa umma au laa.
Kwani Licha ya Chenge kuwasilisha amri ya zuio iliyotolewa Mahakama Kuu mwaka Jana inayokataza Taasisi zote za umma zisijadili suala la Escrow hadi Kesi za Msingi zilizofunguliwa na Lugemalila mahakamani hapo zitakapotolewa uamuzi.
Sisi wasomi wa Sheria tunasubiri kwa shahuku kubwa uamuzi huo wa Mahakama utakaotolewa Kwenye Kesi hiyo ya Chenge kwasababu utaandika historia mpya ya kisheria (Precedent) wa je taasisi yoyote ikiwemo bunge na taasisi zingine za kiserikali zina mamlaka ya kukataa kutekeeleza amri ya mahakama?
Pia tunasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Katika Kesi iliyofunguliwa na Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kumfungulia mashtaka Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR- Mageuzi), David Kafulila.
Kafulila amefunguliwa kesi ya madai katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na IPTL kwa kushirikiana na Kampuni ya Pan African Power Solutions (T) Limited (mlalamikaji wa pili) na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hizo, Harbinder Sigh Seth (mlalamikaji wa tatu).
Katika kesi hiyo namba 131 ya mwaka 2014, walalamikaji kwa pamoja wanaiomba mahakama imwamuru mbunge huyo awalipe fidia ya jumla ya Sh.bilioni 310 kwa madai ya kutoa kashfa dhidi yao kwa kuwatuhumu kujipatia Fedha kutoka Akaunti ya Escrow, kwa njia zisizo halali.
Siku Mahakama Kuu itakapotoa uamuzi wa Kesi hii , ndipo tunafahamu Alichokuwa akikisema Kafulila kuhusu kampuni ya IPTL Kuwa imepita Fedha Kwa njia haramu hadi kusababisha Baraza la mawaziri kubadilishwa kwasababu waziri mmoja alitimuliwa Kazi ambaye ni Profesa Anna Tibaijuka na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini ,Professa Sospeter Muhongo ,Mwanasheri Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliachim Maswi kusimamishwa kazi kwa kashfa ya Escrow ni kweli au uongo.
Muhongo Katika hotuba yake ya kujiudhuru alisema anajiudhuru kwasababu ya fitna, majungu, Chuki za kisiasa na wafanyabiashara ila anaimani aliifanya Kazi yake kuitumikia taifa kwa uzalendo wa Hali ya juu ni ukweli au uzushi. Ni suala la muda tu, Tuipe Mahakama nafasi ifanyekazi yake.
Niitimishe kwa kukubaliana na Msemo wa msomi wa Sheria Tundu Lissu na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe Kuwa Hakuna aliye maarufu kuliko Chama chao.
Lissu alikuwa akimaamisha Zitto siyo maarufu kuliko Chadema na Msemo huo umethibitika Kuwa ni kweli Zitto siyo maarufu kuliko Chadema Kwani tangu walimpomvua Zitto Cheo cha Naibu Katibu Mkuu, Chama hicho hakijafa na Katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa imeongezeka idadi ya mitaa na vitongoji Kwa kupata ushindi.
Hivyo Zitto ambaye zaidi ya makala zangu Tatu nilishakutaadhalisha Kuwa Umaarufu wako umeporomoka kwa kasi ya ajabu na uamuzi huo wa Mahakama Kuu ambao umeitupa Kesi yako Katika Hatua za awali kwasababu ya makosa ya kiifundi wa Sheria ' Technicalities' , taarifa ya Chadema iliyotolewa kwa waandishi wa Habari kupitia Mwanasheria wa Chadema kuwa.
Uamuzi wa Jaji Mziray umeipata tiketi Chadema ya kutangaza Kumvua rasmi uanachama kwasababu moja ya Ibara ya Katiba ya Chadema, inasema masuala yanayohusu chama ,mwanachama yoyote wa Chadema hataruhusiwa kwenda Mahakamani kushitaki, na endapo mwanachama yoyote atafungua kesi mahakamani basi Mwanachama Huyo Atakuwa amejifukuzisha uanachama.
Na Kama Ibara ya Katiba ya Chadema inasema hivyo basi Zitto Aliyataka Mwenyewe kwa kuamua kuvunja Katiba ya Chama Chake na kukimbilia
Mahakamani.
Pole Zitto uliipenda Chadema lakini Chadema na Katiba Yao hawakutaki hata kukuona kwasababu ulivunja Katiba ya Chadema. Lissu,Freeman Mbowe, Peter Kibara, Dk.Slaa na wana wana Chadema wengine waliapa kuilinda Katiba ya Chadema hivyo Hawakuwa Tayari kuiona Zitto na MTu mwingine akiifunja Katiba ya Chadema halafu wasimchukilie hatua.
Nakutakia kila lakheri Zitto.Hiyo ndiyo Sheria imetumika kuitupa kesi yako na Chadema kukuvua uanachama kwasababu umevunja Katiba kama leo sheria ni mbovu minasema hata kama sheria ni mbovu ndiyo sheria zilizopo tunataka wa tuziheshimu .
Na sisi Wenyeji wa Mkoa wa Kagera tunasemaga ' Sheria Timzano' , yaani sheria siyo mchezo.
Zitto umekuwa mahiri sana na mstari wa Mbele kushupalia wenzio Wafukuzwe uwaziri, madaraka mbalimbali na kweli kupitia Kauli zako na ripoti zako zimeumiza Wengi wakiwemo wakina Profesa Muhongo, Profesa Anna Tibaijuka, William Ngeleja ,Eliachim Maswi ambaye alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati ,Mwanasheria Mkuu wa zamani Andrew Chenge na Mwanasheria Mkuu aliyejidhuru kwa Sakata la Escrow ambalo ulililishia Bango Kuwa kukusanya taarifa ambazo zingine zimetiwa mashakama hadi sasa Jaji Fredrick Werema na wengine Wengi.
Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde Katika mjadala wa Escrow Bungeni alisema anashangazwa na ripoti ya PAC ambaye Mwenyekiti wake Zitto imeshindwa kumtaja Zitto naye alipata mgao wa Escrow na vielelezo akavitoa Bungeni na Mbunge wa Sengerema(CCM), William Ngeleja naye hivi karibuni amenukuliwa akisema Zitto naye alipokea Fedha za Escrow lakini cha ajabu hajajitaja wala kuchukuliwa Hatua Kama wao.
Na baadhi ya walioumizwa na ripoti zako ambazo wengine wanadai baadhi ya ripoti zako zimekuwa na nia ovu dhidi Yao wamekuwa wakikulalimikia sana na Kusema wakati ukifika na wewe utaadhibiwa na Mungu hapa hapa Duniani.
Na kweli kwa tamko la Jana la Chadema lilotolewa na Lissu ni wazi kabisa Mungu amejibu Maombi ya watu wale ambao wanadai uliwahumiza kwa uzushi na wengine sikufichi nikiwemo Mimi uamuzi wa Chadema wa kukuvua uanachama umenifurahisha sana Kwani kupitia makala zangu ikiwemo makala
Yangu ya Aprili 12 mwaka 2012 gazeti la Tanzania Daima lilichapisha makala yangu iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho ‘Zitto Kabwe ,Mbona U msahaulifu?
Maudhui ya makala hiyo nilikuwa namuelezea Zitto kumbe na yeye ni jamiii ile ya baadhi ya wanasiasa wale wale wenye hulka za kinyang’au ambao wanakasumba ya kuzungumza uongo mbele ya umma, ili umma uwapende na uamini kuwa kiongozi huyo ni mtu safi na mtetezi wa wanyonge,ana heshimu sheria na Katiba ya vyama vyao kumbe siyo kweli.
Ieleweke wazi hapo nyuma Zitto alipata bahati ya kupata umaarufu ndani ya jamii kwa kile kilichoelezwa ni mwanasiasa kijana ambaye ana misimamo thabiti na asiyeyumba katika kile anachikiami.
Sisi waumini wa sheria tunasema tuhuma zitabaki kuwa tuhuma hadi pale zitakapothibitika na mahakama au vikao husika vya chama chake.Lakini kwa kuwa mungu ni mwema kadri siku zinavyozidi kwenda mbele atazidi kutuonyesha kama kweli Zitto ni mwanasiasa msafi ,mhadilifu kuliko wanasiasa wenzake wanaotoka katika vyama mbalimbali vya siasa.
Na kweli utabili wangu huo umetimia hivi karibuni Kamati Kuu ya Chadema, ikatangaza kumvua nyadhifa zote ndani ya chama hicho kwa kile kilichodaiwa kuwa wamebaini kuwa Zitto anakisaliti chama chao.Hali iliyosababisha baadhi ya wanananchi kuanza kumtazama tofauti Zitto.
Itakumbukwa kuwa Zitto alikuwa msatili wa mbele kushinikiza baadhi ya watumishi wa serikali na viongozi wakiwemo mawaziri na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wawajibishwe kwa kile alichokuwa akikidai kuwa wameshindwa kutekeleza majukumu yao na wengine wamekuwa wakikabiliwa na tuhuma mbalimbali na kweli kuna mawaziri waliondolewa kwenye baraza la mawaziri kwasababu ya tuhuma hizo zilizokuwa zikiibuliwa na Zitto na mwisho wa siku zikaungwa mkono na wananchi.
Waswahili wanamsemo wao usemao ‘lililomkuta Boko na Mamba pia litamkuta kwasababu wote wanaishi majini’. Kwa hiyo yaliyowakuta baadhi ya mawaziri kwa kuondolewa kwenye baraza la mawaziri kwa kigezo cha tuhuma tu...ndicho ambacho kimemkuta Zitto mwaka jana kwa Kamati Kuu ya chama chake kumvua nyadhifa zake zote kwa tuhuma kuwa ni msaliti, na Jana Chama Chake kumtimua rasmi uanachama.
Katika makala yangu iliyochapishwa Katika Gazeti la Tanzania Daima Jumapili, Desemba 15 Mwaka 2013) ilikuwa na kichwa ha Habari kisemacho ( ZITTO KABWE UNAJIANDALIA ANGUKO) . Katika makala hiyo nilimuomba sana Zitto aache tabia ya Kuzusha mambo yanayolitikisa taifa wakati akaitwa na mamlaka husika anashindwa kutoa ushahidi.
Niliandika makala hiyo baada ya Zitto kushupalia Kuwa Una ushahidi wa Majina ya baadhi ya viongozi walioficha mabilioni ya Fedha Kwenye Akaunti nchini Uswiss Lakini aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ,Jaji Fredrick Werema alimuita ofisini kwake ale kiapo na Kisha atoe hivyo vielelezo alivyonavyo ili serikali Iweze kuchukua Hatua, Zitto alikuwa akimkwepa Jaji Werema na alishindwa kutoa vielelezo hivyo na kuhesabika ni mtu Mzushi na anayejitafutia Umaarufu wa kisiasa kwa kuchafua wenzie kwa tuhuma za uzushi.
Gazeti la Tanzania Daima Jumapili toleo la Novemba 28 mwaka 2011, ilikuwa na kichwa cha habari kisemacho ;ZITTO AWALIPUA MAWAZIRI :ASEMA HAWAFANYIKAZI ,WANAWAUWAZA URAIS.
Lakini Gazeti la Mwananchi Jumapili la Machi 25 mwaka 2012, lilichapisha habari iliyokuwa na kichwa habari kisemacho ZITTO: NITAGOMBEA URAIS 2015.
Leo kikowapi? Chadema imekupiga Ngumi za uso kwa kukufukuza rasmi uanachama na umeshindwa kuzikwepa.
Mbona wale waliokuwa wakikutumia ovyo ovyo HIvi sasa wamekutelekeza Jangwani Unatakiwa na Jua hawakupi hata Maji ya Kunywa ili usife na kiu?
Maana ulikuwa Hodari sana wakushawishi na Kuzusha na kutaka wanasiasa wenzio na watendaji wa serikali wachukuliwe Hatua ikiwemo kufukuzwa Kazi.
Nimalizie kwa kumwambia Zitto hivi, 'Muosha ,uwoshwa' tena wakati wa kuoshwa ulipuliwa'. Sasa na wewe sasa umeoshwa maana ulizoea kuosha wenzio.
Sasa na wewe Zitto ulikuwa mahiri sana wa kuosha wenzio yaani kuwafukuzisha kazi watu sasa na wewe jana Chadema kupitia wanaume wasomi wa sheria yaani Lissu, Peter Kibatara na Mallia wamekuingiza jando la wanaume la ukubwani siyo jando lile la watoto wadogo wa Kiume.Hongereni Mawakili waliokuwa wakiiwakilisha Chadema mahakamani Katika Kesi hii.
Na hiyo ni rasharasha, Mvua kubwa Kama ile iliyonyesha kule Nzega ikasababisha taifa kutikisika inakujia Katika medani ya siasa maana sikufichi Zitto kaa utambue kuwa una maadui wengi na umeumiza baadhi ya watu bila hatia .
Na ukumbuke wale uliowaumiza nao wana Mungu na walikuwa wakikishe wakisali kumuomba Mungu alipe kisasi kwa watesi wao.
Nafikiri ulisahau kuwa wale watu uliosababisha wakapoteza ajira zao kwa mdogo na makelele yako na uzushi wako kuwa nao wana Mungu na Mungu wao siyo kilema anayetembelea baiskeli ya walemavu yenye miguu mitatu na ni kipofu.
Kwa taarifa yako Mungu wao ni Mungu mwenye Siha nyema siyo kilema wala kipofu anaona na kusikia na anatembea kwa kutumia miguu yake na ni kijana pia anafanyakazi zake kisayansi na anatembea na IPAD iliyounganishwa Internate anajibu maombi haraka ,amesikia kilio chao na sasa Mungu ameanza kuwalibia kisasi kwako kupitia Mahakama na Chadema ambapo kesi yako imetupwa na uanachama wa Chadema umevuliwa kwahiyo hivi sasa siyo Mbunge mwanachama wa Chadema,na umaarufu wako uliokuwa mao kipindi kile ulitokana na wewe kwanza kuwa mwanachama wa Chadema na kisha majukumu mengine ambayo uliwahi kuyafanya.
Na kwa uamuzi wa Chadema wa jana dhidi yako ni wazi hata yale mawazo yako uliyoyatoa bungeni wakati ulipomaliza kuwasilisha ripoti ya PAC kuhusu Escrow ulivyosema eti umeimiss UKAWA, ifute mara moja kwani kwa uamuzi wa Chadema wa kukuvua uanachama ,hawakutaki usiwafuate fuate na UKAWA yako weendelea na ACT yako ambayo siyo Mwanachama wa UKAWA.
Mwisho Niitimishe kwa kumtaka Zitto arejee Msemo usemao(Yaliyomkuta Mamba na Boko pia yatamkuta kwasababu wote wanaishi Kwenye Maji.
Kwa maana kwamba yaliyowakuta wanasiasa wenzake na viongozi wa serikali kwa kuvuliwa madaraka makelele yake na yeye Jana yamemkuta kwa Kesi yake kutupwa na kufukuzwa uanachama kwasababu na yeye pia yupo Kwenye siasa na anaishi Duniani,usikasirike ,furahia Kwani ni wakati wa Mungu sasa kukulipa kutokana na mambo uliyokuwa unawafanyia wenzio wakaumia kwa namna yoyote ile.
Nakushauri nenda kafanye Kazi za taaluma uliyosomea achana na siasa maana hadhi yako na Umaarufu uliokuwa nao wakati upo Chadema haurudi tena.
Zitto siasa uliifanyia papara na daima mwenye pupa hadiriki kula tamu kwasababu kwa umri wako ikasababisha ukawachua wengine wanalazimisha kuaribiwa mustakabali wa Maisha Yao kutokana na siasa zako za kuwalipualipua watu,siasa zilizojaa utashi binafsi,ubabe,Umaarufu wa haraka haraka Pasipo kuzingatia Kuwa siasa ni Uwanja uliojaa kila aina ya Mabadiliko yasiyo tabirika Kama Mabadiliko ya Hali ya hewa.
Sasa wewe hukutaka kukuubali ukweli Kuwa siasa zile ulizokuwa unafanyia wenzio Je ulitarajia na wewe yangekukuta kama yaliyowakuta wahanga wa siasa zako Kama Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye Kutwa ulikuwa unashinikiza Atukuzwe Kazi Kwani ameshindwa Kazi na unakusanya saini ya kumng'oa bila mafanikio, Lowassa, Ngeleja, Muhongo, Tibaijuka na wengine.
Vilio ,masikitiko na maombolezo Yao binafsi na watu wao wa karibu dhidi yako hukuvisikiliza Je Leo nani atakufariji kwa yaliyokukuta ?
Ama kweli Leo yametimia Muosha Uwoshwa tena wakati wa kuoshwa ulipuliwa.
Yaani yule Muosha maiti kule Mochwari ipo siku nayeye ufariki Dunia na maiti yake inaoshwa wana watu wengine.
Uliwazungumza wenzio kwa Mabaya huku ukiwa umeketi Katika Kiti cha Enzi ambacho wewe ulifikiri Enzi hiyo haina mipaka wala mwisho kuwajenga hisia za Utawala wako Kwenye hisia zako
Ukajenga nchi ya kusadika yaani wewe ndiyo mtawala, na wala Ukawa siyo msikivu ,hisia zako ndizo zikawa zinakutawala na kufanya maamuzi ya Moja kwa Moja ya kuwathiri wale wote kwa Bahati Mbaya Katika fani zao za Maisha wakawa ni wenye kukutana na wewe Mithili ya kimbunga sasa na wewe Leo Imefika siku yako.
Pengine hili litakuwa nifundisho kwa wanasiasa vijana wenye hamu ya kupata Umaarufu na utashi binafsi katika medani ya kisiasa chini ya kisingizio cha uzalendo wa nchi hii Kumbe ni wanafki na wao ni wachafu wanatuhumiwa kwa ufisadi.
Hukuwafaa Chadema, Chadema ndiyo Chama Kikuu cha upinzani,Kama Zitto angelikuwa ni Msafi na kwa hayo aliyokuwa anawaaminisha Watanzania Kuwa yeye ni Mtetezi wa wanyonge na Mpenda haki kikweli kweli basi Chadema wangemkumbatia na wasinge mfukuza uanachama.
Zitto akufaa Chadema ,ACT mnatarajia atawafaa kwa lipi ?
Watanzania Tujiulize sasa Zitto alikuwa mbunge, Mwenyekiti wa kamati ya PAC, Naibu Katibu Mkuu Chadema Kwani sasa vyeo vyote vimponyoke Mara Moja wakati alikuwa akijitapa yeye ni Mpinga ufisadi na anayeshimu Katiba ya Chadema?
Mfano mzuri leo hii nani atasikiliza nyimbo zako na midundo yako ni sawa na miziki ya z ilipendwa ambapo miziki ya zilipendwa mtu usikilizwa wakati anataka kujikumbuka enzi za muziki ule ulivyotamba lakini siyo kama muziki mpya.
Historia itakukumbuka kwa mazuri na mabaya yako, itakuwa ni vizuri zaidi ukapumzika siasa wewe ni kijana msomi unafani yako ya uchumi ni ushauri wa bure rudi nyumbani kwenu kazungumze na wazee wakupe ushauri na wakuombee dua uende ukaanze Maisha katika Kazi mpya isiyo ya kisiasa kwani siasa imeishakupa mkono wa buriani. Buriani Zitto siasa kwa kheri.
Aidha Bendi ya Wananjenje ina wimbo wao maarufu wa mduara unamaneno yafuatayo ( Boko wala wa wenziooo ,Tiii ....Boko nawe utaliwa weee) Sasa Zitto ulizoea kula vya wenzio yaani kufukuzisha wenzio kazi na kuwapatia kadhia kwenye majukumu yao sasa na wewe jana umeliwa yaani namaanisha (Chadema) imekufuta uanachama na Mahakama Kuu imetupa kesi yako.Naomba kutoa hoja.
Mungu ibariki Tanzania
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
Machi 11 Mwaka 2015
0716 774494.
No comments:
Post a Comment