Header Ads

DOWANS YAIBWAGA TENA TANESCO KORTINI


Na Happiness Katabazi 

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia ombi la Shirika la Umeme (TANESCO) lilolokuwa likiomba mahakama hiyo itoe amri ya kuzuia utekelezwa wa ukazaji wa hukumu ya mahakama hiyo ambayo iliruhusu tuzo ya Dola za Kimarekani 65,812,630.03 iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa migogoro ya Kibiashara (ICC) Novemba 15 mwaka 2010 kwa kampuni ya Dowans Hodlings SA(Costa Rica)Dowans Tanzania LTD isajiliwe hapa nchini. 

Septemba 28 mwaka 2011 jaji wa Mahahakama Kuu Emilian Mushi ambaye alikuwa akisiliza ombi la Tanesco lililokuwa likiomba Tuzo iliyotolewa na amahakama ya ICC kwa Dowans isisajiliwe hapa nchini,jaji Mushi alitupilia mbali ombi hilo la Tanesco na akaruhusu tuzo hiyo isajiliwe hapa nchini kwasababu uamuzi wa mahakama ya ICC ulioipatia tuzo Dowans ulikidhi matakwa ya kisheria. Uamuzi huo wa shauri la madai Na.8/2011 lilofinguliwa la Tanesco dhidi ya kampuni hizo mbili za Dowans ambapo nipigo tena kwa TANESCO ulitolewa jana na Jaji Dk.Fauz Twaib ambapo alisema baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili anakubaliana na hoja za wakili wa wadaiwa(Dowans),Kennedy Fungamtama wakati Tanesco ilikuwa ikiwakilishwa na mawakili wa kujitegemea Richard Rweyongeza, Lugano Mwandambo,Dk.Eve Hawa Sinare,Dk.Ale nguluma na Majura Magafu . Ya kwamba mahakama hiyo haiwezi kusikiliza ombi hilo kwasababu tayari Tanesco walikishwa wasilisha Mahakama ya Rufani taarifa ya kusudio la kupinga hukumu iliyotolewa na jaji Mushi Septemba 28 mwaka 2011 ambayo iliruhusu tuzo hiyo isajiliwe. Jaji Twaib alisema katika kesi hiyo mahakama kabla ya kutoa uamuzi huo ilijiuliza maswali mawili ambayo ni katika mazingira ya kesi hiyo kama mahakama ina mamlaka ya kukubali ombi la Tanesco lilotaka mahakama hiyo izuie utekelezwaji wa ukazaji hukumu wa mahakama hiyo kwasababu tayari Tanesco walishawasilisha hatia ya nia ya kukata rufaa katika Mahakama ya Rufani ya kupitia hukumu ya Jaji Mushi iliyoruhusu Dowans isajiliwe? Pia amejiuliza kama mlalamikaji(Tanesco) ombi lake la kutaka Dowans izuiliwe kutekeleza hukumu ya Jaji Mushi wakati tayari ni Tanesco huyo huyo ambaye akliwasilisha ombi hilo mbele yake pia amewasilisha ombi la kukatia rufaa hukumu ya Jaji Mushi katika Mahakma ya Rufani? Jaji Dk.Twaib katika uamuzi wake ambapo gazeti hili linayo nakala yake alisema mahakama yake kwanza haina mamlaka ya kusikiliza ombi hilo la Tanesco lilotaka mahakama hiyo izuie Dowans wasitekeleze hukumu iliyotolewa na Jaji Mushi ambapo hukumu hiyo ya Jaji Mushi iliruhusu Dowans waanza kukaza hukumu kwa kuanza kuidai Tanesco iilipe tuzo waliyopewa na mahakama ya ICC ambayo ni Dola za Kimarekani 65,812,630. Akichambua hoja zilizowasilishwa na wakili Fungamtama ,Jaji Twaib alisema Fungamtama aliikumbusha mahakama kuwa Tanesco waliwasilisha ombi hilo kwa kutumia kanuni 1192) na 47 ya Kanuni za Mahakama ya Rufani Tanzania ya mwaka 2009. Fungamtama aliendelea kueleza kuwa kanuni ya 47 pia inatumika kwenye ombi hilo ambapo Mahakama ya Rufaa na Mahama Kuu inayomamlaka sawa na kwamba ombi hilo la kuizuia Dowans isitekeleze hukumu ya mahakama Kuu halikuwa limetajwa na tanesco katika maombi yale waliyoyafungua Mahakama ya Rufani. Alidai wakili Fungamtama alidai kuwa ombi hilo la Tanesco la kutaka Dowans izuie kukazia hukumu lingekubaliwa na Mahakama ya Rufani kwa mujibu wa Kanuni ya 11(2)(B) ya Kanuni za Mahakama ya Rufani nchini ya mwaka 2009 na kwamba Fungamtama alidai neno mahakama lilotajwa katika kanuni ya 11(2) ina maanisha Mahakama ya Rufani na siyo Mahakama Kuu na kwasababu hiyo ni Mahakama ya Rufani pekee ndiyo inaweza kukubali ombi mlalamikaji(Tanesco) la kuwazuia wadaiwa (Dowans )wasikaze hukumu ya mahakama kuu. Na kuwa wakili wa tanesco Lugano Mwandambo katika hoja zake mbele ya Jaji dk.Twaib alieleza mahakama kuwa Kanuni ya 11(2)(b) ya Kanuni za mahakama ya Rufani nchini ya mwaka 2009,inaipa mamlaka mahakama na mabaraza kutoka kwenye rufaani zote zinazowasilishwa mahakama ya rufani zitoe amri ya utekelezwaji wa ukazaji hukumu na kwamba kwamujibu wa kanuni hiyo kuna masharti mawili ambayo ni kuwasilisha hatia ya kusudio la kukata rufaa na uwepo wa sababu mathubiti za kushinda hiyo rufaa. Jaji Dk.Twaib alisema mahakama yake hainabwi na maamuzi ambayo yalishawai kutolewa zamani na mahakama hiyo kwa kuwa mahakama hiyo ipo huru katika kufanyazi zake. Jaji Dk.Twaib alisema kwa mujibu wa amri xxxix Kanuni ya 5(1),(2) ya Sheria ya Madai,Sura ya 33 ya mwaka 2002 inayoonyesha majukumu na mahakama kuu na mahakama rufani na kwamba kwa mazingira ya kesi hiyo mahakama yake ilikuwa na mamlaka ya kulikubali ombi hilo la Tanesco kipindi kile kabla ya tanesco haijawasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa katika mahakama rufaa kupinga hukumu ya mahakama kuu iliyoisajli tuzo ya Dowans. “Kwakuwa tayari Tanesco walishawasilisha mahakama ya rufani taarifa ya kusudia la kukata rufaa kupinga hukumu ya mahakama kuu iliyotolewa Septemba 28 mwaka 2011 na Jaji mstaafu Mushi ambayo iliruhusu tuzo ya Dowans isajiliwe ….mahakama kuu hapo mamlaka yake ya kukubali ombi hilo la Tanesco la kutaka Dowans isikaze hukumu hiya ya Jaji Mushi nguvu hizo zinakufa na kwa maana hiyo maamuzi yale jaji Mushi hadi leo hii bado hayajatenguliwa: “Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili ,mahakama hii imekubaliana na hoja za wakili Dowans,Fungamtama kuwa mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza ombi hili liloletwa na Tanesco mbele yake lilotaka mahakama hiyo itoe amri ya kuizuia Dowans isikazie hukumu ya mahakama kuu iliyotolewa na Jaji Mushi ,Septemba 28 mwaka 2011 ambayo ilikubali tuzo ya Dowans isajiliwe hapa nchini na Dowans ianze kudai Tanesco dola za kimarekani 65,812,630.03,hivyo inatupilia mbali ombi hilo la Tanesco na sitatoa amri ya ya kuitaka Tanesco ilipe gharama’alisema Jaji Dk.Twaib. Itakumbukuzwa kuwa Septemba 28 mwaka 2011 mahakama Kuu kanda ya dar es salaam ilitoa hukumu yake katika kesi iliyokuwa imefunguliwa na tanesco dhidi ya Dowans na ikatupilia mbali ombi la Tanesco lilotaka tuzo ya Dowans isisajiliwe. Aidha Novemba 15 mwaka 2010 mahakama ya ICC ilipatia tuzo ya ushindi kampuni ya Dowans ya dola za kimarekani 65,812,630.03 baada ya Tanesco kukutwa na hatia ya kuivunjia mkataba Dowans kinyume na mkataba wao na ikaiamuru tanesco ilimpe dowans kiasi hicho cha fedha. Lakini Dowans haikulidhika na uamuzi huo na kuamua kuja Mahakama kuu ya Tanzania mbele ya Jaji Mushi kuipinga hukumu hiyo ya ICC wakati ikifahamu wazi makubaliano ya Dowans na tanesco katika mkataba wao walioingia walikubaliana endapo wakigombana wataenda kusuluhishwa katika Mahakama ya ICC pekee na siyo mahakama Kuu wala Mahakama ya rufaa. Pia itakumbukwa hukumu hiyo ya ICC ilizusha malumbano hapo nchini na kusababisha baadhi ya watu kutaka Dowans isilipwe kiasi hicho na wengine wakishauri serikali ieheshimu utawala wa sheria na iilipe Dowans fedha zake kwani tanesco ndiyo waliovunja mkataba na Dowans. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Septemba 7 mwaka 2012.

No comments:

Powered by Blogger.