Header Ads

KESI YA KIBANDA YASHIKA KASI

Na Happiness Katabazi

HATIMAYE upande wa Jamhuri katika kesi ya kuandika na kuchapisha makala ya uchochezi inayomkabili Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda na wenzake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, uliupatia upande wa utetezi nakala ya mlalamikaji katika kesi hiyo kama ulivyokuwa umeamriwa na mahakama hiyo kufanya hivyo.


Sambamba na hilo Mbele ya Hakimu Mkazi Frank Moshi , Wakili Mwandamizi wa Serikali Prosper Mwangamila aliikumbusha mahakama kuwa kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya mashahidi wa upande wa jamhuri kuanza kutoa ushahidi na kwamba wamekuja na mashahidi wa wawili ambao ni Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza(ACP), George Mwampashi na Rafael Hokororo na wapo tayari kwaajili ya kuanza kutoa ushahidi.

Lakini hata hivyo Hakimu Moshi alisema hakimu anayesikiliza kesi hiyo Waliarwande Lema amepata hudhuru hivyo yeye amepewa kesi hiyo jana kwaajili ya kuiarisha na hivyo anaiarisha hadi Oktoba 22 mwaka huu, nakuwataka mashahidi wote wafike bila kukosa.

Kwa mujibu wa nakala ya maelezo ya mlalamikaji wa kesi hiyo ambaye ni Mrakibu Mwandamizi wa Polisi(SSP), David Hizza ambaye anafanya kazi katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai katika Jeshi la Polisi nchini, alidai kuwa moja ya majukumu yake ni kufuatilia matishio ya uhalifu pamoja na matukio ya uhalifu a kwamba anakumbuka Novemba 30 mwaka 2011 alipata nakala ya gazeti la Tanzania Daima toleo la Namba 2553.

Hizza alidai katika kulisoma nilikuta makala iliyokua katika ukurusa wa 14 ambayo ilisomeka ‘Kalamu ya Mwigamba’ na ikaonyesha kuwa imeandikwa na mtu aitwaye Samson Mwigamba ambaye ni mdaiwa wa kwanza na makala hiyo ilisomeka ‘Waraka maalumu kwa askari wote’ na katika kuisoma makala hiyo alibaini kuwa mwandishi alionyesha kuwaandikia askari wanaofanya kazi katika majeshi ya Jeshi la Polisi,Jeshi la Kujenga Taifa,Kikosi maalum cha Kuzuia Magendo,Jeshi la Magereza na Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

“Katika kuusoma waraka huo yapo maeneo ambayo niliyaona kuwa ni uchochezi kwa askari hao kuwafanya wasiwatii viongozi wao jambo ambalo linaweza kuleta uasi jeshini.Maneno niliyoyaona kuwa ni uchochezi ni haya; “Napenda tena kurudia kwamba si lazima askari mfanye kila ambacho wakubwa wenu wanataka na kuwaamuru kufanya’

“Na pia kulikuwa na maneno yanayochochea chuki kwa askari dhidi ya serikali yao ambayo ameitaja kuwa inawategemea wao lakini huku ikiminya haki zao na wazazi wao ‘Lakini wale wa Tanzania wako tayari kung’oa uhai wa raia wengi ili mradi kuzuia nguvu ya umma inayodai haki na wanafanya hivyo kwa sababu ya hofu ya kung’oka madarakani jambo ambalo hawataki kabisa kulisikia.Na ndugu zangu askari napenda kuwaambia kwamba yote yanafanywa na watawala wetu kwa kuwategemea ninyi.Wanaminya haki zenu ninyi wenyewe,haki za wazazi wenu,marafiki zenu,jamaa zenu na majirani zenu”alidai SSP-Hizza.

Hizza alidai maneno kwamba askari wako tayari kung’oa uhai ili kuzuia nguvu ya umma yanaashiria uchonganishi kati ya raia kung’oa uhai ili kuzuia nguvu ya umma yanaashiria uchonganishi kati ya raia wa kawaida na askari kuonyesha jinsi askari wasivyojari utu wa raia jambo ambalo linachochea chuki dhidi ya majeshi yetu kwa raia na kwamba kitendo cha kuwaambia askari wasiwatii viongozi wao wanaowaamuru katika shughuli zao ni kuwashawishi wasitii kiapo cha utii walichofanya wakati wanaajiriwa kama askari ‘kinachomtaka kila askari kuwa mwaminifu na mtii kwa jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa uaminifu kuitumikia na kuilinda jamhuri wakati wote wa utumishi wao na kutii amri zote za rais na viongozi walio juu yao’.

“Ushawishi huo alioufanya mwandishi wa makala hiyo ni uvunjaji wa sheria za nchi na baada ya kuusoma waraka huo niliwasiliana na viongozi wangu katika idara na wote baada ya kuupitia walikuwa na maoni kuwa una taarifa za kiuchochezi hivyo ni vema waliohusika wahojiwe na hatua stahiki zichukuliwe na nilimtafuta naye mahojiano na hatua stahiki zichukuliwe na nilimtafuta mwandishi wa makala hiyo(Mwigamba) na kufanya naye mahojiano na akakiri kuwa ndiye aliyeandika waraka huo lakini akadai alifanya hivyo kwa lengo la kuelimisha”alidai Hizza.

Aliendelea kueleza kuwa maelezo ya Mwigamba yaliandikwa kisha akapelekwa mahakamani hapo pia alimwita Mhariri Mtendaji wa gazeti hili Absalom Kibanda ambaye naye alimhoji juu ya uhalali wa gazeti lake kutoa waraka huo ambao ni wa kichochezi lakini naye akadai waraka huo ni wa kawaida na siyo wa uchochezi kwa askari hivyo naye alipelekwa mahakamani na kwamba alimwita na kumhoji Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwananchi Communication ambaye ni mshitakiwa wa tatu, Theophil Makunga ambaye kampuni yake ndiyo ilichapa gazeti hilo na kumhoji.

Aidha alidai kuwa kwa upande wa Makunga alidai anao mkatana na kampuni ya Freemedia ambyo nio watoaji wa gazeti hilo unaonyesha kuwa jukumu la kisheria la yaliyomo katika katika gazeti hilo anayewajibika ni Free Media na sio wao.Ili kulithibitisha hilo kisheria nilifanya mahojiano na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Raphael Hokororo ambaye alidai jukumu la uchapaji haliondolewi na mkataba huo bali linabaki kwa kampuni hiyo ya uchapaji na alikusanya ushahidi na kisha kulipelekea jalada kwa maoni ya kisheria.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Septemba 11 mwaka 2012.





No comments:

Powered by Blogger.