Header Ads

DPP AKWAMISHA KESI YA VIGOGO SUMA JKT

DPP, Eliezer Feleshi
Na Happiness Katabazi 

KESI ya matumizi mabaya ya madaraka inayomkabili Mkurugenzi wa Shirika la Kujenga Taifa (SUMA JKT), Kanali Ayoub Mwakang’ata na maofisa wengine wa jeshi hilo jana ilishindwa kuendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kwasababu jarada la kesi hiyo bado lipo kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP),Dk.Eliezer Feleshi Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Tabu Mzee mbele ya Hakimu Mkazi Aloyce Katemana alieleza kuwa kesi hiyo jana isingeweza kuendelea kwasababu bado DPP haijarudisha jarada la kesi hiyo mahakamani hapo tangu ilipoliitisha jarada hilo ofisini kwake hivi karibuni. 

Hata hivyo Wakili Tabu aliomba kesi hiyo iarishwe na ipangiwe tarehe ya kuja kuwasomea maelezo ya awali washitakiwa hao, ombi ambalo lilikubaliwa na Hakimu Katemana ambaye aliarisha kesi hiyo hadi Oktoba 26 mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya upande wa Jamhuri kuwasomea maelezo ya awali washitakiwa hao. 

 Mbali na Kanali Mwakang’ata washitakiwa wengine ambao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza na TAKUKURU, Julai 2 mwaka huu, ni Luteni Kanali Mkohi Kichogo,Luteni Kanali Paul Mayavi,Meja Peter Lushika,Sajenti John lazier,Meja Yohana Nyichi na Mkurugenzi wa Miradi ya Matrekta wa SUMA JKT-Luteni Kanali Felex Samillan wanaotetewa na wakili wa kujitegemea Majura Magafu.

Wanakabiliwa na makosa ya kula njama na matumuzi mabaya ya madaraka kuwa washitakiwa wakiwa ni wajumbe Ilidai kuwa Machi 5 mwaka 2009 katika chumba cha mikutano cha ofisi ya SUMA JKT Dar es salaam,wakiwa ni wajumbe wa bodi na Bodi ya Tenda ya SUMA JKT kwa makusudi walitumia madaraka yao vibaya kwa kutoa maamuzi ya bodi hiyo ambayo yaliyoonyesha yametolewa na TAKOPA kwa madhumuni ya kununua magari na vifaa vya ujenzi bila kupata idhini ya kutoka Bodi ya ya Wakurugenzi ya TAKOPA. 

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Septemba 29 mwaka 2012.

No comments:

Powered by Blogger.