KOMENI KUSAMBAZA TAARIFA ZA UONGO
KOMENI KUSAMBAZA TAARIFA ZA UONGO
Na Happiness Katabazi
MCHANA wa leo hadi hivi sasa nimekuwa nikipokea simu nyingi kutoka kwa wananchi wakinitaka niwathibitishie kuwa ni kweli Mwanamuziki wa Dansi, Nguza Vicking( Babu Seya ) na mwanae Papii Kocha eti wameachiriwa huru na mahakama leo.
Wananchi Hao wakiwemo mashabiki wa muziki wa dansi na wamekuwa na Kucheza na Papii Kocha walifikia Hatua hiyo ya kunipigia ili wapate uthibitisho wa Hilo Kwani wanaamini bado nina Mtandao mrefu wa kupata taarifa za yanayojiri mahakamani kila siku.
Na Uvumi huo ndiyo umesambaa sana Leo Dar es Salaam na vitongoji vyake.
Baada ya kupata taarifa hizo ambazo Hazina hazionyeshi nani amezitoa nilianza kuwasiliana na Vyanzo Vyangu mahususi Vya Habari toka mamlaka husika ili vinipe ukweli wa Habari hizo.
Vyanzo vyote toka Katika mamlaka za dola zilikanusha taarifa na kuziita ni Uvumi wa kijinga na unaosambazwa na watu ambao hawana Kazi za kufanya au wana matatizo ya akili.
Chanzo changu Cha mwisho kilikuwa ni Aliyekuwa Wakili wa Babu Seya,Mabere Marando Alisema Hakuna kitu Kama hicho na wala hakwenda mahakamani Leo na wateja wake Hao na anashangazwa ninani anayesambaza uongo huo.
Itakumbukuwa kuwa Babu Seya na Papii wanakabiliwa na adhabu ya kifungo cha maisha na wanatumikia adhabu hiyo katika Gereza la Ukonga ,Dar es Salaam.
Novemba 20 mwaka 2013 Mahakama ya Rufaa chini ya jopo la majaji watatu lililokuwa Natharia Kimaro, Salum Massati na Mbarouk Mbarouk, walitoa uamuzi wa kulikataa ombi la Nguza Vicking lilokuwa linaomba Mahakama hiyo ya juu nchini ifanyie marejeo hukumu yake iliyoitoa Februali 2010 kwasababu Ina dosari za kisheria
Hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Rufaa nchini Februali 2010 iliwza hukumu kifungo cha maisha warufani hao kwasababu ina dosari za kisheria.
Uvuvi huu wa kijinga unaosambazwa na wapuuzi wachache , sio wa kwanza kusambazwa Kwani hata Ijumaa iliyopita wapuuzi Hao waliingia Kwenye mitandao ya Kijamii na kusambaza taarifa za uongo kuhusu Kesi ya iliyofunguliwa na Mwandishi wa Habari Saed Kubenea dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali inayoombwa Bunge Maalum la Katiba lisimamishwe.
Uvumi wa Kesi hiyo ya Kubenea ulienezwa hivi Kuwa ' Hatimaye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetoa amri ya kusitisha Bunge la Katiba.
Wakati ukweli ni kwamba Septemba 15 Mwaka huu, Mahakama Kuu ndiyo Utatoa uamuzi wa pingamizi la awali lililowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Linaloomba Mahakama hiyo itupilie mbali ombi la Kubenea kwasababu linadosari na pia ukweli ni kwamba hadi sasa Mahakama hiyo bado hata haijaanza kusikiliza Kesi ya Msingi iliyofunguliwa na Kubenea lakini wazushi Hao walidiriki Kusambaza uzushi huo ambao pia umeizushia na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Kuwa imeshasilikiliza Kesi ya Kubenea na kukubali ombi la Kubenea.
Minawauliza hawa wazushi HIvi wanadalili timamu au wana uchizi wa muda? HIvi mtu mwenye akili timamu na anayejua madhara ya uzushi anaweza kueneza taarifa za uongo ambazo kwanza Hana uhakika nayo ila ameamua tu kujifurahisha kwa kuzusha uongo.
Itoshe tu Kusema taarifa kuhusu Babu Seya kuachiwa na Mahakama ni uongo na Mbona wazushi Hao hawataji jina la Mahakama iliyowaachiria Huru?
Wasomi wa Sheria tunaofahamu Kesi ya Babu Seya Ilifika mwisho kimahakama Novemba 20 Mwaka 2013. Hivyo aliyebakia hapa mwenye mamlaka ya kuwaachiria Huru Wafungwa Hao ni Rais wa Tanzania ambaye kwasasa ni Jakaya Kikwete tena baada ya kupelekewa taarifa za Wafungwa Hao na Bodi Ya Parole.
Tukae tukijua tunajenga taifa la Wambea, wazushi na vizabinazabina kwa tabia hii chafu ya miongoni mwa watu wazima kuamua kuzusha taarifa za uongo tena kupitia mitandao.
Hivi mzungu alivyo tuletee hii mitandao sialitutaka tuitumie kwaajili ya KupShana Habari sahihi pia, lakini baadhi ya sisi ngozi nyeusi hasa Watanzania tunakwenda kinyume na kabisa na Malengo ya matumizi wa mitandao.
Niatitimisha kwa Kusema ' Komeni kusambaza taarifa za uzushi' Kwani zina.wta Usumbufu kwa Jamii na watu wa karibu wa wale waliozushiwa uzushi huo.
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blog: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Septemba 8 Mwaka 2014
No comments:
Post a Comment