UB KUWAFUNDA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU EAC
UB KUWAFUNDA WATETEZI HAKI ZA BINADAMU
Na Happiness Katabazi (UB)
CHUO Kikuu Cha Bagamoyo (UB) , Dar Es Salaam, kimendaa Mafunzo maalumu ya kuwajengea uwezo mpana watetezi wa Haki za Binadamu toka nchi tano za Afrika Mashariki.
Akizungumza na Ofisa Habari wa (UB), Ofisa Mradi huo ambao unaendeshwa na Kitivo Cha Sheria Cha Chuo huko kwa kufadhiliwa na Akiba Uhaki Foundation ya Nairobi Kenya, Teddy Sawaya ofisini kwake Kawe Beach Dar es Salaam,alisema Mafunzo hayo yatashirikisha jumla ya wanafunzi 10.
Sawaya ambaye ni Mhadhiri wa Sheria wa UB, (Pichani) alisema washiriki wa kozi hiyo ni watu wanaotokea Katika Taasisi zinazojihusisha na Kazi ya utetezi wa Haki za binadamu na kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea wigi mpana zaidi Katika eneo Hilo la utetezi wa Haki za binadamu, watetezi Hao wa Haki za binadamu na Jamii kwa ujumla.
Alisema Tayari washiriki wameishathibitisha kushiriki Mafunzo hayo na kwamba Mafunzo hayo hatakuwa yakiendeshwa ndani ya madarasa la Chuo Kikuu Cha Bagamoyo yaliyopo Kawe Beach Dar Es Salaam na Mafunzo yataanza rasmi Septemba 8 mwaka huu ambapo yatafunguliwa ramsi na Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho anayeshughulikia Fedha na Utawala, Dk.Elifuraha Mtaro mafunzo hayo yatamalizika Februali 22 Mwaka 2015.
Hii ni Mara ya pili kwa Chuo Kikuu cha Bagamoyo , kuendesha Mafunzo hayo ya utetezi wa Haki za binadamu kwa kuudhuliwa na washiriki toka nchi tano za Afrika Mashariki .Mara ya kwanza UB iliendesha kozi hiyo Septemba 8- Oktoba 20 Mwaka Jana.
Chanzo: Facebook: University of Bagamoyo
Website: www.uob.ac.tz
Septemba 4 Mwaka 2014
No comments:
Post a Comment