Header Ads

SAFI SANA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA




SAFI  SANA  VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA 

Na Happiness Katabazi 
BAADHI ya vyombo vya habari leo vimemnukuu  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP- Ernest Mangu akisema jeshi lake limefanikiwa Kumtia nguvuni mtu mmoja  ambaye wanamhutumu alihusika moja kwa moja na tukio la uvamizi  Kituo cha Polisi kilichopo  Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, Septemba 5 Mwaka huu ,usiku na kuua polisi wawili na kuiba silaha mbalimbali Mali za Jeshi Hilo.

Kwa mujibu wa IGP- Mangu, mtu huyo ambaye hakumtaja jina alikamatwa Septemba 6 Mwaka huu, usiku huko Mkoani Geita   akiwa na silaha mbalimbali yakiwamo mabomu ya machozi.

Mangu alisema baada ya kumkamata mtu Huyo ambaye hakutaka Kumtaja jina kwasababu bado wanaendelea na upelelezi, mtu Huyo aliwaonyesha mahali  zilipo bunduki sita aina ya SMG, pump action tatu na mabomu 11 ya machozi, kitendo ambacho kinaonyesha moja kwa moja  alihusika kwenye tukio la uvamizi wa Kituo hicho Polisi Bukombe na kuua Askari wale Polisi ambao hatakuwa na hatia.

“Jitihada za kumkamata mtu huyo zilifanywa na polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama,” alisema IGP-  Mangu

Jana Katika ukurasa wangu huu wa Facebook niliandika makala iliyokuwa na kichwa Cha Habari kisemacho ' POLISI MALIZANENI NA MAJAMBAZI WA AINA HII'. 

Maudhuhi  ya makala hiyo  yalibeba ujumbe wa kulaani tukio la Mauji ya Polisi ndani ya Kituo Cha Polisi Bukombe baada ya watu wasiyojulikana kuvamia Kituo hicho wakiwa na silaha za kivita na kuua Askari Hao na Kisha kutokomeza na silaha mbalimbali.

Nikiwa muumini wa Amani  Narudia tena Kusema wazi Kuwa  nachukizwa na Uhalifu wa aina  yoyote. 

Ndani ya makala ya Septemba 7 mwaka 2014 nilieleza wazi  kuwa binafsi  ninaliamini Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama pindi vinapoamua kuacha mzaa na kufanyia Kazi kikamilifu jambo Fulani.Vikiamua kulivalia njuga  jambo Fulani ulifanya kwa haraka na mwisho wa siku ufanikiwa kutimiza adhima Yao. 

Na mfano mzuri ni tamko la  IGP- Mangu kwa vyombo vya habari Leo ambapo Amedai  Katika Hatua za awali za wapelelezi toka vyombo mbalimbali Vya Ulinzi na Usalama wa kishirikina na Jeshi lake, juzi usiku walifanikiwa kumtia nguvuni mtu mmoja ambaye wanamshuku moja kwa moja alihusika kutenda unyama ule ambao siyo tu umekatisha uhai wa askari polisi wawili wa siyo na hatia lakini tu  naweza Kusema tukio Hilo limelidhalilisha pia jeshi la Polisi.

Kwa sasa  ' watoto wa mjini' tunasema  haiwezekani kupigwa au kufanyiwa uhuni ' Viwanja Vya nyumbani'.  

Sasa wahuni / majambazi ambao watoto wa mjini tumewapachika jina Kuwa ' hawana dini',  kwa jeuri wameweza kuwafanyia uhuni   Polisi Katika 'Viwanja vyao Vya nyumbani' yaani ndani ya Kituo Cha Polisi Bukombe. Inatisha sana.

Narudia tena tukio Hilo na matukio mengi ya Uhalifu yananikera, naamini huo ni mwanzo mzuri tena Katika muda mchache  tu tangu wahuni Hao wafanye mauaji hayo na vyombo Vya Ulinzi na Usalama vikafanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja ambaye aliwapa ushirikiano polisi akaenda kuwaonyesha silaha alikokuwa ameziifadhi.

Naamini mtuhumiwa Huyo  hakuwa  peke yake Katika tukio lile la kinyama kwasababu kwa mujibu wa   maelezo ya Jeshi la Polisi kuhusu tukio lile, yanadhiirisha wazi waliotenda tukio ile ni zaidi ya mtu mmoja.

Hivyo  navitia moyo vyombo vyote Vya Ulinzi na Usalama kuakikisha wanakamata bila kuonea mtu, mhalifu yoyote aliyeshiriki Kutenda tukio lile  kwasababu Uhalifu huu wa kuvamia Vituo Vya Polisi sasa umeanza kuonekana ni Fashion mpya ya majambazi kujipatia silaha.

Kwani tungali tukikumbuka tukio Kama Hilo lilitokea Juni 11 Mwaka huu, Katika Kituo Cha Polisi Mkamba Wilaya Ya Mkuranga  Mkoani Pwani, ambapo majambazi Hao walimua Askari Polisi mmoja Joseph Mbilinyi na kuondoka na silaha lakini hata HIvyo siku Chache baadae wahalifu Hao walikamatwa na kufikishwa mahakamani. 

Na ninawasikitikia sana Nyie wahalifu mtakao kamatwa na kuhusishwa na tukio Hilo Kwani ni lazima mtashitakiwa na  Kesi zaidi ya Moja.Kesi ya kwanza itakuwa  ni Kuua kwa kukusudia Askari Hao kinyume na Kifungu ha 196 Cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Mwaka 2002, Kesi ya Polisi kukutwa na silaha Mali ya Jeshi la Polisi na makosa mengine ambayo Mwanasheria wa Kanda atawandalia Kesi nzuri sana 'iliyosimama' na kuwafikisha mahakamani.

Mkae mkijua  kosa la kuua bila kukusudia  halina  dhamana na wapelelezi wa Kesi hizo Zenu ni  Jeshi la Polisi  ambao mlienda kuwavamia na kuwaua Polisi wenzao kinyama na kuiba  silaha  kituo chao cha polisi Bukombe na kuwaua askari wenzao na kuiba silaha zao. 

Nawaonea huruma sana Nyie wahalifu wote mtakao kamatwa na kushitakiwa kwa tukio la kuvamia, kuiba silaha na kuua askari Kituo  cha Polisi Bukombe, kwasababu uenda hamkufahamu madhara mtakayopata baadae baada ya Kutenda tukio Hilo.Kwa taarifa yenu Polisi ni ' wahuni' sana kushinda Nyie.Nawasikitikia sana.

Hongera  sana vyombo vyote Vya Ulinzi na Usalama vilivyoshirikiana na Jeshi la Polisi  kumkamata Mtu huyo Septemba 6 mwaka huu na silaha hizo ikiwa  ni siku Moja tu tangu tukio Hilo la Uhalifu litokee Septemba 5 mwaka huu, na ninaomba mzidishe kasi Katika upelelezi wa kuwasaka wahalifu wengine bila ya kumuonea ili mwisho wa siku wakakutane na mkono wa Sheria. 

Uhalifu haupaswi kufumbiwa macho na wala wahalifu hawapaswi kuchekewa.

Waswahili wanasema ' Ukicheka na Nyani utavuna mabua'. Sasa vyombo Vya Ulinzi na Usalama iwe ni mwiko sasa kucheka Cheka na wahalifu Kwani mwisho wa siku ndiyo Kama HIvi wahalifu hawa wamevuka mstari na kwenda kuvamia Vituo Vya Polisi.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blog: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Septemba 8 Mwaka 2014

No comments:

Powered by Blogger.