Header Ads

POLISI MALIZANENI NA MAJAMBAZI WA AINA HII
POLISI  MALIZANENI' NA MAJAMBAZI WA AINA HII
Na Happiness Katabazi
SEPTEMBA 5 mwaka huu, usiku , watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi walivamia Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Bukombe mkoani Geita huku wakiwa silaha za kivita na kuua askari polisi wawili na kuwajeruhi wengine na kisha kuiba aina mbalimbali silaha zinazomilikiwa na Jeshi la Polisi nchini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Joseph Konyo alithibitisha kutokea kwa tukio Hilo katia Kituo hicho Cha polisi kilichopo mjini Ushirombo. 

Binafsi ni muumini wa Amani wa taifa langu hivyo taarifa za ujambazi huo uliosababisha Askari wetu wasiyokuwa na hatia ambao walikuwa Kazini wakilitumikia taifa wakauwawa  na majambazi Hao na Kisha majambazi Hao wakaiba silaha ambazo zimenunuliwa kodi za wananchi, zimenisikitisha na kunitisha.

Awali ya yote napenda kutolea pole kwa familia za Askari walioouwawa na kujeruhiwa na majambazi hiyo pia natoa pole kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi,  IGP- Ernest Mangu kwa kupoteza vijana wake kutokana na tukio Hilo.

Naweza Kusema hili ni tukio la pili  kwa Mwaka huu,wahalifu kuvamia Vituo Vya polisi Kisha kuua Askari  polisi na Kisha kuondoka na silaha mali ya Jeshi la Polisi. Mara ya kwanza ilikuwa Julai 11 mwaka huu katika Kituo cha Polisi Kimansichana Mkoani Pwani na kuua  Askari polisi aitwaye Joseph Ngonyani na kupora silaha.

Sijui majambazi ndiyo wameamua kutumia mbinu hiyo mpya ya kujipatia silaha bila kutumia Nguvu wala kuzinunua? Maana wao Shida Yao ni kupata kivitendea Kazi va ujambazi ambapo kitendea Kazi Kimoja wapo ni Bunduki.

Aina hii ya ujambazi ya kuvamia Vituo Vya polisi ni ya aina yake Kwani mwisho wa siku itaanza kuwatisha Askari wetu wanaopangiwa Kazi Katika Vituo Vya Polisi.

Sina namna ya kueleza jinsi ninavyochukizwa na matukio ya Uhalifu yanayosababisha binadamu wenzetu kupoteza Uhai kwaajili ya tamaa za watu wa Chache, itoshe kutoa Rai kwa vyombo Vya Ulinzi na Usalama kuakikisha vinatokomeza aina hii ya ujambazi na aina nyingine ya ujambazi.

Aiingii akilini wananchi Wengi wanaogopa kwenda Katika Vituo Vya Polisi iwe kwa kushitakiwa,Kulalamika lakini ndani ya nchi yetu kuna Mashujaa ambao wa nadiriki kwenda kuvamia Vituo Vya Polisi na kuiba silaha.

Ndiyo maana kila siku minasemaga Kuwa hapa Tanzania kuna watu mashujaa na wenye roho katiri kama watu wanaojilipua na mabomu katika nchi za Libya, Iraq,Somalia ila tu Wengi wetu hatuwajui kwa sura. Hatari Sana.

Sina Shaka Jeshi la Polisi pindi liamuapo na litakapokulivalia njuga jambo lake.Hivyo naamini waliofanya tukio hili watapatikana vizuri tu tena wakipatikana polisi wapelekeni Katika ' SALOON ZA JESHI LA POLISI'  mkawapodoe  na mmalizane nao vizuri maana wanakera sana.

Naamini majambazi hayo yakikamatwa na kuwekwa ndani ya 'SALOON'  za jeshi la polisi watataja  ni kwanini wameamua kubuni mbinu  hiyo ya kulifedhehesha Jeshi la Polisi ya kuvamia Vituo Vya polisi na kuiba silaha na Kuua Askari , hizo  silaha nani anaeatuma au wanazipeleka wapi?  Ni hatari sana na majambazi sasa wamevuka mstari.

Chanzo:Facebook: Happy Katabazi
Blog: www.katabazihappy.blogspot.com
Septemba 7 Mwaka 2014
0716 774494

No comments:

Powered by Blogger.