Header Ads

'WANAOLAMISHA MAANDAMANO NI MAAJENTI WA SHETANI'




'WANAOLAZIMISHA  MAANDAMANO NI MAAJENTI WA SHETANI'

Na Happiness Katabazi

' MUNGU ANAARIBU NA KUVUNJA KAZI ZA SHETANI. Imeandikwa Katika Waraka wa Kwanza wa Yohana Sura ya 3:4,5. '

Binafsi naamini maandamano haramu yanayo lazimishwa kufanywa na Chadema ni Moja ya Kazi ya shetani maana shetani miongoni mwa Kazi zake ni kutumia Maajenti wake kuamasisha vitendo Vya Uvunjifu wa Amani hapa nchini na Duniani, kupandikiza Chuki, Kuzusha uongo na kuwa amasisha wananchi kutoheshimu mamlaka za Duniani wakati Biblia inatutaka sisi waumini wa dini ya Kikristo Kuheshimu mamlaka ya Duniani.
Sasa hawa viongozi  wanaowaamasisha wanachama wao  wasitii amri ya Jeshi la Polisi ambayo imekataza maandamano ya Chadema. Kwa mujibu wa Biblia , Biblia inatutaka  tutii mamlaka ya Dunia.Viongozi Hao wanaomasisha maandamano na migomo isiyo na kikomo ni wazi ni  Maajenti wa shetani kwa  mujibu wa Biblia Takatifu Kwani Jeshi la Polisi ni mamlaka iliyopo  Duniani.
Jana Nabii Kanali Mstaafu wa JWTZ, Bruno Kinunda  wa Kanisa la Eshadai ,Boko Basiaya Dar es Salaam, wakati akituongoza waumini wake Katika ibada alituomba tuombeee tabia hii ya watu waache ambao wanataka kuleta vurugu nchini kwetu kwa kisingizio Cha maandamano Kwani mwisho wa siku watakao uumia ni Hao wananchi wasiyotaka kutii mamlaka ya Duniani na Sheria'. 
HIvyo naamini mungu ataaribu  kazi hiyo hiyo ya shetani inayofanywa na maajenti wa shetani hapa Tanzania ambao maajenti hao ni wale viongozi waliojitokeza adharani kwa wiki nzima sasa kuwataka wafuasi wa Chadema waandamane licha polisi imekataza maandamano hayo. 

Shetani peke yake ndiyo anapenda mambo maovu maouvu, kama vurugu.Sasa na wale wote wasiyotii amri ya jeshi la polisi au wasiyotaka kudai haki zao kwa utaratibu naomba kuanzia sasa Watanzania hasa wakristo wazuri ,wapenda amani wawaone watu hao ni maajenti wa shetani na shetani anawatumia kutaka kuleta vurugu nchini kwetu.Tufunge na kusali ili mungu asambaratishe kazi hiyo inayofanywa na maajenti hao washetani..

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi.
Blog: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Septemba 22 Mwaka 2014.

No comments:

Powered by Blogger.