Header Ads

CHADEMA ACHENI KUVIMBISHA MASHAVU



Na Happiness Katabazi

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, Suleiman Kova  na makamanda wa baadhi ya mikoa nchini wamesema  Jeshi Lao  limepiga marufuku maandamano yasiyo na kikomo yaliyoandaliwa na Chadema yaliyotakiwa yaanze leo na kwamba yoyote atakayekaidi amri hiyo atashughulikiwa.

Binafsi Napongeza amri hiyo ya Jeshi la Polisi la kukataza maandamano hayo kwasababu hayana tija kwa taifa ambayo yanalengo Moja tu ya kutuletea vurugu Kipindi hiki Maandalizi ya Sherehe ya kumuapisha rais wa awamu Ya Tano, Dk.John Magufuli Novemba 5 Mwaka huu, ambapo viongozi wa Mataifa mbalimbali wanakuja nchini kushiriki Katika sherehe hiyo ya kihistoria.

Pia Napongeza katazo Hilo la Jeshi la Polisi kwasababu ni Juzi tu Taifa limemaliza uchaguzi Mkuu, watu wanaitajika kwenda sehemu zao za Kazi kufanya Kazi ya kulitumikia taifa Lao.

Lakini hawa wenzetu wa Chadema ambao ni mabingwa wa kuandaa maandamano ,haya hawayaoni ,fikra zao ni kuleta Hali ya Kuonyesha nchi is itawalike kwa kuanza kutaka kuandaa maandamano ya kipuuzi tu .

Hivi Chadema Kama hamna Kazi za kufanya simu we basi mnakaa majumbani kwenu mnawasaidia wake Zenu ,wa dada wenu wa Kazi kufanya usafi wa ndani iki bidi hata siku Moja Moja basi mjitoleee kuisadia Manispaa kufanya usafi wa kufagia barabara kuzibua mitaro ya Maji machafu ?

Hivi tangu muandamane mmepata nini zaidi kuambulia kufunguliwa Kesi na moshi wa mabomu ya Machozi?

Kweli maandamano ni Haki yenu lakini hivi kwa akili Zenu mnafikiri maandamano kwasasa ni kipaumbele kwa Watanzania? Kwa hiyo mkiandamana ndiyo Rais Magufuli ushindi wake wa Kiti cha urais utatenguliwa na rais ndiyo atakuwa Edward Lowassa? Wajinga sana nyie.

Msiokaa kitako mkajitafakari ni Sababu zipi zilisababisha mgombea wenu wa urais Lowassa,kwanini ameshindwa Kisha mkishapata hizo Sababu mzirekebishe ili uchaguzi wa 2020 muingie kikamilifu Katika uchaguzi .Hilo linawashinda mmeamua kuwaza kufanya maandamano?Mnaakili mbovu.

Chadema msio kaa kitako na wabunge wenu wapya mkaanza kuwafunda jinsi ya kwenda kupeleka hoja Motomoto Katika Bunge lijalo ,Leo hii mmeibuka nakuona kipaumbele chenu ni maandamano yasiyo nakikomo?Hivi mnawazimu?

NEC ilishamtangaza mshindi wa urais  na Ibara ya 74(12) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, inaikataza hata Mahakama kuhoji Utendaji wa NEC.

Nimelazimika kuandika makala hii kwasababu hata kama Jeshi la Polisi limepiga marufuku maandamano hayo, baadhi ya watu Leo wameogopa Kuja mjini kufanya shughuli zao kwa kuhofia lolote laweza tokea yaani hao Chadema wanaweza kuandamana na Kisha Polisi wakaamua Kupambana nao na akaumia asiyeuhusika ,foleni na Kadhia mbalimbali.

Chadema ni Chama cha maandamano maana chini ya serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete ambaye anastaafu rasmi Novemba 5 na kumkabidhi Kijiti rais wa awamu ya tano, Dk.John Magufuli ilivunja rekodi ya kufanya maandamano ya halali na maandamano haramau ambayo maandamano haramu kama Yale ya Arusha, yalisababisha watu kupoteza Maisha kutokana na ghasia zilizojitokeza.

Niwaulize Chadema tangu wafanye maandamano weee,kuna Nishani yoyote waliyowahi kutunukiwa au hata Kombe la Kuwa ni Chama bora ya kuendesha maandamano?

Ieleweke wazi uchaguzi Mkuu umekwisha ,rais amepatikana na Si mwingine ni Dk.Magufuli.Mtake msitake Dk.Magufuli ndiyo rais wenu .Lowassa atabaki Kuwa rais Katika mioyo yenu na Chadema yenu lakini katu kwa sasa Dk.Magufuli ndiyo rais wa Tanzania na Dk.Mohammed Shein ndiyo rais wa Zanzibar.

Hivyo hamna budi kukubaliana na hiyo.Lakini misiwashangai Chadema Kwani hata uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 uliomalizika ni hawa hawa Chadema Walisema hawa tambui Rais Jakaya Kikwete Kuwa ni rais wa nchi hii kwasababu Rais Kikwete alimuibia kura aliyekuwa Mgombea urais wa Chadema, Dk.Wilbroad Slaa ambaye naye Enzi akiwa Chadema alisema hamtambui Kikwete kama rais lakini Slaa huyo Huyo ni Mwenyekiti wa Hospitali ya CCBRT .

Hospitali ya CCBRT ikiwa na Kazi zake ,anamualika Yule Yule aliyesema hamtambui Kuwa ni rais yaani Rais Kikwete Kuja Kuwa mgeni rasmi Katika sherehe za CCBRT kwa zaidi ya Mara Moja.

Waliokuwa wabunge wa Chadema siku Kikwete alipoingia kulihutubia Bunge walitonja ya Bunge kwasababu hawa tambui Kikwete Kuwa ni rais wa Tanzania, lakini hao Hao wabunge akiwemo Mwenyekiti wa Chadema, wanakubali Mialiko ya Kikwete ya kwenda Ikulu kujadili mambo mbalimbali.Mhh.!

Ndiyo maana Nasema ndani ya vyama Vya upinzani hasa Chadema kuna baadhi ya watu akili zao hazipo sawa kutokana na matendo wanayo yataenda na matamshi wanayoyataka.

Wakati wa kampeni na baada ya kumalizika kwa kampeni Mwaka huu, tumeshuhudia Chuki ikitamalaki ndani ya Jamii yetu tena ya wazi wazi.

Chuki hii kwa uchunguzi wangu wa muda mrefu sasa inaonyeshwa na watu wanaodai wao ni wafuasi wa UKAWA wa kitokea Chadema. 

Wananchi hao wenzetu huku maofisini, mitaani wameshindwa kuficha Chuki zao hizo pindi wanapoona mtazamo wako wa kisiasa ni tofauti nao. Yaani wakiona umevaa,umetundika Bendera ya CCM, au wa nakwambia ujiunge na Chadema hutaki au Katika maongezi uonekane kupinga aina ya siasa inayofanywa na baadhi ya wana Chadema au useme Magufuli ndiyo mshindi amekuwa rais.

Watu bila aibu wengine ni watu wazima ,wakikusikia ukisema Magufuli ndiyo rais, wanaibuka kwa sauti ya juu ya Ukali wanasema Magufuli kaiba kura Lowassa ndiyo alishinda na kumtaka mtu Yule aliyesema Magufuli ndiyo rais anyamaze watampiga na kwamba uchaguzi Ujao hawatapiga kura na kwamba CCM imezoe a kuiba kura sasa hivi UKAWA Nguvu zao zote wamezielekeza Zanzibar kumsaidia mgombea urais wa CUF, Seif Sharif Hamad ashinde urais kwasababu Rais wa Zanzibar Dk.Shein amemuibia kura Seif Sharrif Hamad.

Mimi napenda sana kuwa enjoy watu wa UKAWA kwasababu wengi wao ni malimbukeni wa siasa na bendera fuata upepo na wasiyojua wanachokishabikia .

 Nawaulizaga kama Magufuli kaiba kura za Lowassa kama wanavyodai  wanieleze Magufuli aliziibaje?Aliiba kura ngapi za Lowassa akaziweka Katika kura zake na Huyo Magufuli awali alikuwa na kura ngapi? Wakati Magufuli anamuibia Lowassa hizo kura wao Chadema walikuwa wapi? Nani alimshuhudia Rais Magufuli akiiba hizo kura?

Nipeni idadi ya kura zilizoibwa?,Mbona Magufuli sio Mjumbe Tume ya Taifa ya Uchaguzi  NEC na Kipindi chote NEC inatangaza Matokeo haijaripotiwa  Kuwa Magufuli alikuwa ndani ya NEC akiiba kura.Na kama Chadema wameshindwa kulinda kura zao ndiyo Leo hii wataweza kulinda mipaka ya nchi ,Siri na Rasilimali ?

Matokeo yake wana Chadema wanashindwa kujibu maswali yangu  hayo Wanaishia Kusema Mimi ni CCM. Minasema hawa baadhi ya Chadema zao mbovu baadhi ya wafuasi wa Chadema.

Nimalizie kuwaambia wananchi wenzangu ambao ni wanachama wa Chadema na UKAWA kwa ujumla acheni kuvimbisha mashavu yaani kukasirika kwasababu CCM kupitia Dk.Magufuli wameishinda Katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 Mwaka huuu haitowasaidia zaidi zaidi mnazidi kuonekana machizi Mbele za watu wenye akili timamu na Mbele za watu wenye hofu na Mungu kwasababu .

Mimi naamini hadi Dk.Magufuli amefanikiwa  Kuwa rais wa nchi hii Mungu amependa Magufuli awe rais siyo Lowassa au mtu mwingine na kweli imekuwa  hivyo.

 Tuheshimu hilo maana nyie Chadema hata mkiivimbishia mashavu CCM,Magufuli ha itawasaidia zaidi zaidi mnaonekana ni wahuni,uenda mnatumiwa na mabwana zenu kutaka  kuleta vurugu hapa nchini .

 Ninawakikishia hira Zenu chafu hazitafanikiwa   kwasababu Mungu bado analipenda taifa hili na baadhi ya watu kila siku tu naendelea kuliombea  taifa hili liendelee Kuwa na Amani,umoja na mshikamano.

Nawashauri Wataanza wenzangu mlioko huko Chadema, msiandamana kwakuwa msiandamana mtakuwa mmeenda kinyume na agizo Hilo la Polisi.Ila mlijifanya wajuaji mtafanya maandamano  zawadi nono mtakayopata kutoka kwa Polisi msije Kulalamika wala kulia maana mmeishakatazwa.

Niitimishe kwa kulitia moyo Jeshi la Polisi liendelee kukaza Uzi kwa kuyapiga marufuku Maombi ya kufanya maandamano ya kipuuzi kama haya yaliyokuwa yameombwa na wafuasi Hao wa  Chadema kuanzia Leo ili watu wa chape Kazi taifa letu lisonge Mbele.

Kwasabababu tumeshuhudia Katika serikali ya awamu ya nne ,Jeshi la Polisi lililegeza Kamba kwa kutoa vibali Vya maandamano Mara kwa Mara baadhi ya vyama Vya siasa na Katika maandamano hayo baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakitumia kutoa maneno ya mengine ya uzushi yaliyopandikiza Chuki baina ya baadhi ya wananchi kwa serikali Yao .

Ulimi kiungo kidogo lakini matatizo yake ni makubwa sana.Ulimi huu ukitumia vizuri utapata mazuri lakini ukiutumia vibaya utasababisha uhalibifu sana mfano tumeshuhudia familia zikisambaratika,nchi zikiingia vitani,watu wakitoana roho kwasababu ya Ulimi ambao Utumika kutoa Kauli.

Madhara ya Ulimi hapa nchini sasa hivi Tumeyaona Kwani Ulimi ulitumiwa na baadhi ya wanasiasa kupandikiza Chuki Mbaya kwa baadhi ya wananchi wanachama wa Chadema hadi baadhi Yao wanaichukia CCM,serikali Yao na watu wote wanaoipenda CCM wazi wazi na kuwaona ni maadui zao .

Nashauri viongozi wa UKAWA hasa Chadema warudi kwa Wapiga kura wao hata kwa Siri wa washauri waache vinyongo kwa wana CCM na wale wote wanapingana na sera za Chadema,waache Chuki mnatusi ya kiongozi mitaani dhidi ya watu wasiokuwa wanachama wa Chadema ,waondoe fikra Kuwa CCM imeiba kura za Lowassa huku wakijua Utendaji wa NEC hautakiwi  kuhojiwa hata na Mahakama iweje wao wanaipinga na kuhoji?

Niitimishe kwa kuwashauri hasa vijana, msikubali kutumwa na viongozi wenu wa juu wa vyama Vya siasa kuandamana Katika maandamano ambayo ameyapiga marufuku mwisho wa siku mtaumizwa na hao viongozi hawatakuwa nanyie Katika matatizo.

Chadema nendeni  kafanye Kazi za uzalishaji kwasababu hata hivyo kipindi cha kampeni kimepita  .

Chadema mnatakiwa muache kuvimbisha mashavu ili tulijenge sote  taifa letu lakini Chadema inaona Maandamano ni Dili Kumbe Ujinga mtupu Watanzania maandamano siyo kipaumbelee chao wao wanataka Kazi Ifanyike na baadhi ya wawe ,na siyo blablaa   za kufanya maandamano kila kukicha Kwani maandamano yanakwamisha baadhi ya mambo ya maendeleo.

Mungu ibariki Tanzania

Facebiok: Happy Katabazi
3/11/2015 










No comments:

Powered by Blogger.