KIKWETE,Dk.BILAL KARIBUNI URAIANI
Happiness Katabazi
Dk.Jakaya Kikwete na Dk.Mohammed Gharib Bilal (pichani) ambapo Kikwete alikuwa ni rais na Dk.Bilal alikuwa Makamu wa rais wa serikali ya awamu ya nne ambayo leo ilimalizika muda wake kwa mujibu wa Katiba ya nchi na kupisha serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli na Makamu wa Rais Samilia Hassan Suluhu Leo ikishika madaraka ramsi baada ya Dk.Magufuli na Samia kula Viapo.
Kwa moyo mkunjufu napenda kutoa pongezi Dk.Kikwete,Dk.Bilal " Wanakijiji" kwasababu Katika Uongozi wao waliweza kufanya mambo ya maendeleo waliyoweza kadri ya uwezo wao ikiwa ni pamoja na serikali yao kuruhusu Demokrasia ambayo hata hivyo baadhi ya wananchi walitumia vibaya Demokrasia wakati wakitoa mawazo Yao mbalimbali.Pia ninayofuraha kuona taifa letu Leo viongozi Hao wakikabidhi nchi kwa rais wa awamu ya tano kwa Amani na bila kukataa kung'atuka madarakani,bila ya mmoja wao kupoteza Maisha.
Tumeshuhudia baadhi ya Mataifa mengine Marais wao wakifa Kabla ya kumaliza muda wao na wengine kubadilisha Katiba za Mataifa Yao ili wajiongezee muda wa kuendelea kuyatawala Mataifa Yao lakini Tanzania Hilo halijatikea na hii ni Ishara Marais wetu wanaheshimu Utawala wa Sheria na hawajataliwa na Tamaa ya madaraka.
Nawatakia Afya njema Katika Maisha yenu mapya ya uraiani kwasababu kuanzia Leo 'Mmekuwa Wanakijiji'.Msichoke kutoa ushauri kwa Serikali ya Dk.Magufuli pindi atakapoitaji kutoka kwenu Kwani Tayari mmeishakuwa wazee,nimeona mengi na mmefanya mengi mlipokuwa na vyeo hivyo ambapo Dk.Magufuli,Samia hawajayaona wala kuyafanya.
Rais Mstaafu,Kikwete na Makamu wa Rais Mstaafu,Dk.Bilal karibuni uraiani.Naomba msisahau kufanya mazoezi ya viungo kwaajili ya Afya Zenu na kuzidisha ibada Kwani hiyo ni Moja ya kuimarisha Afya Zenu na Kuwa karibu na Mungu.5/11/2015.
No comments:
Post a Comment