Header Ads

LOWASSA EBU TULIA UNYOLEWE



Na Happiness Katabazi

OKTOBA 26 na 28  wiki hii Mgombea urais wa Chama cha Maendeleo ( CHADEMA- UKAWA),  wamefanya mikutano na waandishi Habari wakitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi isiendelee kutangaza Matokeo ya urais kwasababu Taratibu za uchaguzi zilikiukwa.

Lowassa na viongozi wenzake wa UKAWA wamesema pia wanalitakia Jeshi la Polisi kuwaachiria huru vijana wake walikamatwa na Polisi kwasababu amekamatwa isivyohalali.

Itakumbukwa Juzi Mkurugenzi wa Mashitaka aliwafikisha mahakamani vijana Hao ambao wengine ni Raia wa kigeni na wengine ni wataalamu wa Teknolojia ya Habari (IT) na kuwafungulia Kesi Mbalimbali na wengine wameupelekwa gerezani.

Nilipata fursa ya kumsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi ambaye ameshinda Ubunge jimbo la Vunjo, James Mbatia Jana ambaye amesema kwakuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imefuata Matokeo ya kura za Zanzibar basi NEC ni lazima ifute kura za upande wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwasababu eti ni batiri.

Mbatia akaendelea kulalama kuwa eti Mwenyekiti wa NEC,Jaji Mstaafu Damian Lubuva ni boya anatangaza Matokeo batiri ambayo hajui yanatoka wapi aache kuwatangaza.

Mbatia wakati akiongea maneno hayo ambayo Mbele wasomi wa Sheria tunamuona ni kama mtu aliyekwa na akili na asiyejua anachokiongea hajatuonyesha vielezo Vya Kuonyesha Jaji Lubuva ni kama boya na anatangaza Matokeo ya urais yaliyompatikana kwa njia za zisizo halali.

Kwa upande wake mgombea urais  wa Chadema ambaye amevunja rekodi na Kuwa Kituko Mbele ya Jamii na watu wenye uweledi wa kisheria na amevunja rekodi ya kuongoza Kulalamikia utangwazaji wa Matokeo na NEC wakati NEC bado haijamaliza kutangaza Matokeo .

Pia amekuwa ni mgombea urais pekee hapa Tanzania Bara kuvunja rekodi ya Kulalamika kuhusu NEC inavyotangaza Matokeo wakati wagombea wenzake wa urais Saba wakiwemo wa Chama cha CCM,Chauma,ACT na vyama vingine wapo kimya na vyama kama ACT,CHAUMA  kwa mujibu wa Matokeo ya NEC wanaonekana kupata kura chache ukilinganisha na kura anazo endelea kupata Lowassa na Magufuli.

Nirejee kuhusu Madai ya Mbatia, binafsi napenda kumuona Mbatia kupitia kauli zake za Jana Kuwa ni mbumbumbu wa Sheria ambaye anavamia fani hiyo wakati hajawahi kusoma fani hiyo.

Kama mtaalamu wa sheria za Katiba, Dk.Sengondo Mvungi Angekuwa hai ,Mbatia asingethubutu kuongea Utumbo ule aliouongea Jana ambao muda mchache baadae Jaji Damian Lubuva alitoa  ufafanuzi wa kisheria ambao ukilinganisha na Kauli za Mbatia unaona Mbatia amepatoka .

Enzi za Dk.Mvungi alipokuwa hai Mbatia alikuwa akipenda kwenda kumuona Dk.Mvungi Kabla ya kuzungumza na waandishi wa Habari na Dk,Mvungi alikuwa akimuelekeza kisheria na Kikatiba kitu gani aongeee kwa kutumia vifungu mbalimbali Vya Sheria na Katiba na mliokuwa mkifuatilia Mbatia Enzi Dk.Mvungi alipokuwa hai.

Mbatia alipokuwa  Akizungumza na Vyombo Vya Habari alikuwa Akizungumza vitu vyenye mashiko na tangu Dk.Mvungi afariki Mbatia hotuba zake nyingi Hazina mvuto na baadhi ya watu waliokuwa wakipenda kumsikiliza wameacha kumsikiliza.Mungu amrehemu Mume wangu ,Rais Mdhurumiwa ,Baba yangu  Dk.Mvungi.

Nimuulize Kaka yangu Mbatia wakati anatoa tamko lile Jana Kwenye vyombo Vya Habari Kuwa eti uchaguzi wa Tanzania Bara nao ni haramu ,ufutwe alikuwa ametokea wapi Kabla ya kuingia Kwenye mkutano na waandishi wa Habari?

Hivi NCCR Mageuzi sikuhizi imeishiwa Wanasheria wa kumshauri yeye ambaye  ni Mwenyekiti wa NCCR - Mageuzi ni kitu gani azungumze na kipi asizungumze hasa Katika suala Hilo za ZEC Kufuta uchaguzi ambalo ni ukweli uliowazi Kuwa jambo ni la kisheria zaidi hivyo yeye kwa hadhi yake alipaswa kwanza kujipa muda aende ' kudesa' kwa Wanasheria makini wampe 'nondo' za kisheria ili aje kuzungumza kwa Umma?

Mbatia ulifahamu fika huna mamlaka ya kuitaka NEC isimamishe kutangaza Matokeo kisheria, kutoa maagizo kwa NEC .Hivi ni kitu gani kilikusukuma wewe,Lowassa na hao viongozi wengine wa UKAWA kuitaka NEC isiendelee kutangaza Matokeo?

Tupeni uhalali wenu wa kisheria unaowapa mamlaka ya kuitaka NEC isimamishe kutangaza Matokeo ya Urais?Hivi mmeanza kuchanganyikiwa wazee wangu au nini kimewapata?Tuwapeleke makanisani mkafanyiwe maombi?

Na wewe Mzee wangu Lowassa ambaye kwa zaidi ya Mara tano nakushauri achana na Biashara ya urais hutafanikiwa unanipuuza .Hivi ni kwanini lakini Mzee wangu Lowassa unapenda kujishushia heshima Yako Mwenyewe kadri siku zinavyozidi kwenda kwa baadhi ya matendo na matamshi unayoyaongea?

Hivi Lowassa kwanza uoni aibu,Jumatatu ,Jana Kutwa upo Kwenye vyombo ya Habari unailalamikia NEC kuwa kuna hira Katika utangazaji wa Matokeo hayo ambapo hizo hira hazionyeshi kwa vielezo Kuwa zimefanywa nani?lini?kwasababu gani?kwanini hira hizo ufanyiwe wewe tu nasiyo wagombea wengine wa urais toka vyama vingine?

 Ibara ya 74(6) ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano ya Tanzania ya mwaka 1977 , inasomeka hivi ; " Tume ya Taifa ya Uchaguzi ndiyo yenye jukumu kuu la kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura pamoja na uendeshaji wa uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani".

Lowassa Mzee wangu umetumikia serikali kwa muda mrefu unafahamu Utawala wa Sheria ,unafahamu fika Tume ya Taifa ya Uchaguzi ipo huru kwa mujibu wa Ibara ya 74(11) ya Katiba ya nchini ambayo inasomeka hivi; 

"Katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, Tume ya Uchaguzi haitalazimika kufuata amri au maagizo ya mtu yeyote au idara yoyote ya Serikali, au maoni ya chama chochote cha siasa".

Sasa kwanini wewe Lowassa na hao viongozi wenzio wa UKAWA mnatoa amri ,maelekezo kwa NEC kutaka iache kuendelea kutangaza matokeo ya Urais kwasababu madai yenu hayana  kichwa wala miguu wakati Ibara ya 74(11) ya Katiba inawakataza kufanya hivyo? Narudia tena Kuwauliza wewe Lowassa,Mbowe, Saed Kubenea,Fredrick Sumaye mmechanganyikwa?Maana napata Shida kuamini watu wazito kama Nyie kufanya hayo mnayoyafanya dhidi ya NEC.

Lowassa na Mbowe bila aibu wamenukuliwa na vyombo Vya Habari wakitaka Polisi iwaachilie huru wale vijana wa Chadema wataalamu wa IT kwasababu siyo wahalifu.

Wale vijana ni watuhumiwa na wamefunguliwa Kesi mahakamani ,sasa nashangaa Lowassa,Mbowe ambayo ni viongozi wakubwa wanakaa Kwenye vyombo Vya Habari wanashinikiza  hao vijana waachiriwe  huru wakati Tayari Kesi ipo mahakamani.

Hivi Nyie viongozi wa UKAWA hasa wa CHADEMA  nani aliwaambia Mahakama inafanyakazi kwa presha Zenu  huko Kwenye Kumbi Zenu za mikutano na waandishi wa Habari nani?

Hao vijana kama mnavyodai siyo wahalifu, walikuwa wakifanyakazi halali na Nyie ndiyo mliwapa jukumu Hilo ambalo mnadhani halijavunja Sheria za nchi.Kwanini sasa mnapayuka ovyo nje ya Mahakama?

Subirini siku Kesi hiyo ikifikia wakati wa utetezi washitakiwa hao wakianza kujitetea watalazimika kuleta mashahidi wao ambao ni nyinyi basi siku hiyo wewe Mbowe, Profesa Abdallah Safari, Lowassa na viongozi wengine wa Chadema muwe mashahidi wao .

Mfike mahakamani mtoe ushahidi utakaoushawishi Mahakama iamini Kuwa ni kweli washitakiwa hao yaani Hao vijana hawakutenda makosa wanaoshitakiwa na upande wa jamhuri.

Na pia kule gerezani walipo  wapelekeeni vyakula na muwawekee Mawakili wa Kuwatetea msiwatelekeze . Na huo ndiyo utakuwa msaada mmetoa kwa hao vijana ambao naamini hivi sasa Kukamatwa na kufunguliwa kesi  kumeleta Usumbufu mkubwa kwa familia zao na vilio.Nafahamu sana hii hii.

Na kadri siku zinavyozidi kwenda Mbele nazidi kutambua mtu Kuwa na madaraka makubwa au Fedha na Mali sio Kuwa anafahamu kila kitu na kila anacho kufanya ni sahihi na kimetukuka.

Hivi hapa nawatafakari hata wale Marais wa nchini  hii Kipindi kile walipoamua Kumteua Lowassa,Sumaye Kuwa Waziri Mkuu hivi waliwachunguza watu hawa vizuri matendo Yao na uwelewao wa mambo mbalimbali?

Mawaziri Wakuu wastaafu ambao sawa mmeamia  upinzani sio kosa,kwa hadhi yenu mliyonayonayo ,mmeshiriki chaguzi nyingi sana wakati mmpo CCM.

Kabisa hadi Leo hii tuseme mlikuwa hamfahamu matakwa ya hizo Ibara ambazo zinasema NEC ni huru na ni marufuku kwa mtu, Taasisi au mtu yoyote kuingilia Utendaji wa NEC?

 HIvi mmepatwa na Maradhi gani wazee wangu tangu Jumatatu wiki hii yanayowafanya muweweseke na muwe Vituko Mbele ya Jamii ya wasomi wa Sheria na wapenda Demokrasia ya kweli?

Kwanini Lowassa unatapata kiasi hiki tangu Oktoba 26/28 Mwaka huu ,Kutwa kuitisha mikutano na waandishi wa Habari Kulalamikia mchakato wa utangazaji wa Matokeo na kutaka usitishwe?

Hivi wewe Lowassa,Mbatia,Sumaye,Mbowe ni watendaji wa NEC? Nyie siyo watendaji wa NEC.Mmejuaje kura halali ni zipi na zisizo halali ni zipi?Mmetumia vigezo gani kutambua Hilo?

Na kwanini mnashinikiza sana Matokeo ya Urais Tanzania Bara yasimamishwe kutangazwa tu na mbona hamlalamikii Matokeo ya Ubunge na udiwani Katika Majimbo na Kata mlizoshinda Kuwa yana dosari?

Kuna nini hapa kimejificha  nyuma ya hayo malalamiko yenu? Je  hamuoni hayo malalamiko yenu ambayo mnayatoa kwa mashinikizo yanaanza kutulazimisha baadhi ya watu tuanze kuwajea Mashaka  nyie  UKAWA Kuwa Uenda kuna mchezo na Nyie Mlifanya ambalo mlitarajia mgombea urais wenu Lowassa atashinda urais lakini mchezo huo ukabainika na wenyewe ukaharibiwa Ndio maana mmepata kiwewe cha kutoa Kauli za kufunja Ibara ya 74 (11) ya Katiba ya nchi kuingilia Uhuru wa NEC?

Kwanza NEC haijamaliza kutangaza Matokeo ya Urais ,Nyie Viongozi wa UKAWA kitu gani kinawawasha hadi mnabwatabwata ovyo Kwenye vyombo Vya Habari kuhusu NEC ?

Hakuna ubishi Kuwa hadi sasa Katika jumla ya majimbo 195 ambayo NEC imeishatangaza idadi ya kura za Rais ,mgombea urais wa CCM, Dk.John Magufuli amemzidi kwa Mbali sana mgombea urais wa Chadema, Lowassa. 

Lakini NEC bado haijamaliza kutangaza Matokeo ,Leo itaendelea na zoezi lake la kutangaza Matokeo ya urais Katika majimbo 69 yaliyosalia.

Ambayo Mimi binafsi simfahamu idadi ya kura alizopata Lowassa,Magufuli na wengine Katika majimbo hayo 69 hadi Leo NEC itakapoyatangaza. Lowassa unalalamika utaratibu ni mbovu kutangaza Matokeo basi Ina maana Tayari umeishabaini Kuwa Matokeo yatakayotangazwa Leo Katika majimbo hayo 69 siyo mazuri kwako ndiyo maana unatapatatapa. 

Na kama Umejua,Tueleze umejuaje?Maana UKAWA hamna jukumu la kuhesabu kura kwa mujibu wa Ibara ya 74(6) ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano ya Tanzania inasomeka hivi : " Tume ya Taifa ya Uchaguzi ndiyo yenye jukumu kuu la kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura pamoja na uendeshaji wa uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani".

Lakini  mmenukuliwa kwenye vyombo vya habari mkisema UKAWA mnayomatokeo yenu ambayo kura za mgombea urais wenu Lowassa kuna baadhi ya maeneo zimevurugwa kwa makusudi kwa lengo la kumpendelea mgombea mmoja na Mbatia bila aibu akamtaja Rais Jakaya Kikwete ndiyo katoa maelekezo uchaguzi Zanzibar ufutwe bila kutupa vielezo wakati Yule Mwenyekiti wa ZEC ametaja Sababu ya Kufuta uchaguzi ule.

Nawauliza UKAWA nani aliwapa jukumu la kuhesabu kura na kwa Sheria ipi hadi muwe na jeuri ya Kusema kura Zenu za urais zilizopelekwa NEC siyo zenyewe.Hizo zenyewe mliyonazo zikowapi?

Lowassa  na wana UKAWA wenzako toeni nafasi kwa NEC na msivunje Katiba ya nchi kwa matamshi yenu hayo kwasababu mnatia aibu na mnaibua Mashaka Mashaka katika jamii ambapo sasa baadhi ya watu tumeanza  kujiuliza uenda mlikuwa mmetumia mbinu Fulani chafu kushinda sasa mbinu ile imeshindwa Katika ngazi ya urais ndiyo maana mnatapatapa kutoa matamko wakati NEC haijamaliza kutoa Matokeo yake.

Mnajuaje uenda majimbo 69 ambayo bado Matokeo ya urais yatatangazwa Leo ,idadi ya kura za Lowassa inaweza kuongezeka sana?

Na kwa jinsi mlivyojidhihirisha  baadhi yenu ni  Mambumbumbu  wa Sheria sitoshangaa NEC ikimaliza kutangaza Matokeo ya urais, Kesho yake tukamuona Mmoja wa kiongozi wa UKAWA akienda Mahakama Kuu Kufungua Kesi ya kupinga Matokeo ya urais wakati Matokeo ya urais huwezi kuyapinga mahakaamani.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Lubuva na Tume yake bado hawajamaliza kutangaza Matokeo yote ya urais ambalo majimbo yote kwa Tanzania Bara na Zanzibar ni jumla  264 .

Hadi kufika saa 11 jioni Jana NEC ilikuwa imeishatangaza Matokeo ya urais majimbo 195 na majimbo bado kura za urais halijatangazwa ni majimbo 69. Na Jaji Lubuva akasema Leo NEC inatarajia kumaliza kutangaza Matokeo ya majimbo hayo 69 yaliyosalia na watatoa Vyeti kwa washiriki. 

Na pia Jaji Lubuva Jana alitumia nafasi hiyo kupitia Televisheni ya ITV Kusema uchaguzi Tanzania Bara hautafutwa, kwasababu auna dosari zozote na kwamba NEC itaendelea kutangaza matokeo yote ya Urais .

Jaji Lubuva alisema kura za wagombea ngazi ya urais upande wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano hazijakumbwa na dosari yoyote huko Zanzibar na hapa Tanzania Bara .

Na kuwa NEC inaongozwa na sheria zake mfano Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977,Sheria ya Tume ya Uchaguzi NEC,Sheria ya Uchaguzi sura 343 ya 2015 .

Wakati Zanzibar katika masuala ya uchaguzi  inatawaliwa na Katiba ya Zanzibar ,Sheria ya Tume ya Uchaguzi ya mwaka 1992,Sheria ya uchaguzi ya Zanzibar 1984.

 Siyo wewe Katika Kampeni za UKAWA ulijitapa utashinda saa nne asubuhi Oktoba 25? Leo Oktoba 29 huo ushindi uliotuahidi uko wapi?Mbona tunachokishuhudia hadi sasa kutoka NEC ni Mgombea wa CCM, Dk.Magufuli anakuzidi sana idadi ya kura wakati Magufuli alifanyaka kampeni nchi nzima kwa Magari huku akiwa ameambata na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa CCM, Abdallah Burembo .

Wakati wewe  Lowassa ulifanyakampeni kwa ufahari kwa kuruka na Helkopta na kuandamana Katika kampeni zako na Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye, mwanasiasa Mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwiru na wengine.

Sio wewe Lowassa ulipoulizwa maswali Kuwa umejiandaaje endapo utaibiwa kura zako Unijibu Kuwa Hilo suala la kuibiwa kura tukuachie wewe?Iweje Leo hii unachukua Lundo la viongozi wa UKAWA unaenda Kulalamika eti Watanzania, Jamuiya za Kimataifa sisi kile kilio Chako cha kwamba eti unataka NEC usimamishe zoezi kuhesabu kura za urais?

Aliyekwambia hizo Jumuiya za Kimataifa na huo umma wa Tanzania unayo mamlaka ya kuingilia Utendaji Kazi na Uhuru wa NEC nani? Mbona Mzee wangu Lowassa unanitia aibu kiasi hiki.

Minakupenda sana Ndio maana Mara zote nakushauri ukweli kupitia makala zangu ila wewe hutaki kunisikia na kunielewa na mwisho wake unagonga ukuta.

Mara Kadhaa kupitia makala zangu mbalimbali zenye vichwa vya habari vifuatavyo (LOWASSA UNATATIZO), (POLEPOLE LOWASSA), (    MAKADA SITA CCM HAMMO KWENYE URAIS!),  ( LOWASSA UEWENDA URAIS UKAUSIKIA REDIO TBC1), (LOWASSA UMEANZA MAPAMBANO NA SERIKALI'. ), (UKIPANDACHO NDICHO UVUNACHO MZEE EDWARD LOWASSA), (LOWASSA TULIA UNYOLEWE).

Nimekuwa nikikuueleza kuna baadhi ya watu wanakushauri vibaya hunielewi .

Wanakutumia wee kwa manufaa Yao Kisha wanakuacha solemba.Na Mifano mizuri ni wale waliokuwa wakijifanya watu wako wa karibu Ulipokuwa CCM wakikupigania  uwe Rais, wamekutafuna wee na wamenyonya Siri zako wee wakazi peleka upande wa pili mwisho wa siku CCM ikakata jina Lako kwasababu hufai kupeperusha bendera ya CCM.

Lowassa akukoma,aliendelea   kusikiliza ushauri wa Hao wanaozidi kumuingiza  mtaroni akaamia  Chadema wakakuaminisha utapata urais eti Ana mvuto na ataleta Mabadiliko.

Nilimuandikia  makala ya kumtahadhalisha Kabla ajaondoka   CCM iliyokuwa na kichwa cha Habari kisemacho ( LOWASSA UMEPIGWA KWENZI NA DOLA LA CCM ,BONYEA), ulipuuza ushauri wangu.

Kumekuwa na taarifa zisizo rasmi Kuwa Chadema walimchukua Lowassa kwasababu wapate ushindi na Lowassa amemwaga Fedha.

Vyovyote Iwavyo, Mzee wangu Lowassa Ifike mahali uamke usingizi na utambue Kuwa ni ukweli ujio wako Chadema uliitikisa CCM kwa kiasi Fulani ,pia   
Umeisaidia Chadema kwa kiasi Fulani kufanyakampeni za kufa na kupona na kwa kweli ujio wako kwa Chadema na ulivyogombea urais ,ulichangamsha kampeni za Mwaka 2015 na pia uwepo wako Chadema pia umesababisha Chadema iongeze idadi ya ushindi wa wagombea udiwani Katika Kata mbalimbali na mmeongeza idadi ya majimbo Dar Es Salaam.Hongereni sana.

Minawashauri viongozi wa UKAWA mjiheshimu, acheni kutoa matamshi ambayo yanapandikiza  Chuki kwa Wapiga kura wenu dhidi ya NEC na serikali kwa ujumla.

Heshimuni Utawala wa Sheria maana NEC imeanzishwa  kwa mujibu wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi.Kimsingi hadi sasa NEC bado haijamtangaza mshindi wa nafasi ya urais na NEC imeishatoa tamko Kuwa uchaguzi wa Tanzania Bara upo kihalali na NEC inaendelea kutangaza Matokeo ya kura za rais.Tuheshimu tamko Hilo la NEC na pia tuheshimu pia Jaji Lubuva.

Hongera NEC chini ya Jaji Lubuva ,mnafanyakazi nzuri licha Changamoto za ndogondogo zilijitokeza .Naiomba NEC iendelee kuvumilia maneno ya kebehi yanayotolewa wanasiasa uchwara ambao ni mambumbumbu wa Sheria dhidi ya NEC.Iendelee pia kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria na NEC hadi sasa inastahili pongezi Kwani makamishna wote wamekuwa kitu Kimoja hatujasikia wameshikana mashati na kutoelewana kama wajumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ambapo wamefanya uhuni uliosababisha Mwenyekiti wa ZEC Kufuta Matokeo.Hatari sana.

Mzee wangu Lowassa tambua kampeni Ndio zimeisha,uliisaidia kwa kadri ya uwezo wako Chadema I kaongeza idadi ya wanachama ambao hadi Mbowe, James Mbatia, Saed Kubenea ,Tundu Lissu na wengine wamefanikiwa kushinda Ubunge.

Hivyo ni wazi wapiganaji wako hao wanakuwa  wabunge,wewe tena sio mbunge .Hivyo nakushauri Kuwa Tayari kuyapokea majibu ya Matokeo yatakayotangazwa na NEC, upuuza ushauri utakaopewa  na hao ambao Tayari wenzako wameishapata Ubunge wewe bado huna hakika kama utapata urais.

Kwasababu kama ni Hao Hao wakati Ulipokuwa Mwana CCM ndiyo walikuwa mstari wa Mbele Kukupaka Kinyesi Kuwa wewe ni fisadi, lakini ghafla uliyojijengea na Chadema Hao Hao wakageuka na kukuona wewe ni mtu msafi na kukupamba ukatoa mchango wako wa Hali na Mali Katika Chadema wameshinda Ubunge.

Sasa akili Kumkichwa Mzee wangu Lowassa.Kama ni Hao Hao Kipindi kile Ulipokuwa CCM walikuchafua kwa maneno chungu mbovu, Mara ulipoingia Kwenye Chama chao wakaachaa kukuchafua nakukuona malaika idi mradi tu wapate wanachokita na wameishakipata kupitia mgongo na Nguvu zako.Kwanini usijiulize watu hao endapo ukikosa urais watakaa Mbali nawe ?

Lowassa zinduka usingizini na utambue sisi Watanzania Wengi ni wanafki sana.Ebu fikiria uliofanya kampeni Dar Es Salaam, Mwanza,Mara ,Mbeya ,Tanga ulivyopata mafuriko ya watu hadi walikudekia barabara,walikesha nje ya Hoteli uliyokuwa umelala ukaamini maelfu yote ya watu wale wangekupigia kura za ndiyo Kumbe Wengi Katika Mikoa hiyo hawakupa kura nyingi Matokeo yake Wameenda Kumpa kura nyingi Magufuli. 

Ndio utujue vizuri Watanzania Wengi tumetawaliwa na unafki, na siku ya kupiga kura Wengi hatuendi licha wengi tulijiandikisha.

Niitimishe kwa kumweleza ukweli Mzee wangu Lowassa Kuwa ,Lowassa huwezi muziki wa mgombea urais wa CCM, Magufuli .Magufuli anarekodi ya utendaji nzuri ambayo haitiwili Mashaka.Labda Mbele ya safari Magufuli aje kujiaribia Mwenyewe rekodi yake ya Utendaji na uadilifu.Na sitosita kumkosoa.

Na wewe pia Lowassa una rekodi ya utendaji nzuri,nimtu wa kuchukua hatua nakufahamu ila tu jina lako limechafuka mno ,uadilifu wako unatiliwa mashaka .Huo Ndio ukweli najua unawaumiza mashabiki wako.

Lowassa usije ukakubari kurubuniwa na baadhi ya Wanasheria  Mara baada ya Matokeo ya urais kutangazwa rasmi uende kuyapinga Mahakamani matokeo hayo,Usikubali Kwani Ibara ya  74   (12) ya Katiba ya nchini inasomeka hivi; 

"Hakuna mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza jambo lolote lililotendwa na Tume ya Uchaguzi katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii". Lowassa ebu Tulia unyolewe.

Mungu Ibariki Tanzania

Facebook: Happy Katabazi
29/10/2015.





















No comments:

Powered by Blogger.